CHADEMA mwendo mdundo

kwani Rais alie mfukuza kazi alikua Mkristo, jadili hoja ilio muhusisha, kwani Kikwete akiwa waziri hazina aligundua nini, umesahau maafisa kumi n mbili makamishna alifukuzwa nao......mfumo wa kulindana ndio umeua nchi hii.
 

- Huwa sio kawaida yangu kuingilia ishus za ndani za vyama vya siasa, tatizo langu hapa ni kwa nini huyu mkuu hakusema haya kabla hajafukuzwa? Na yeye anakuwa kama majaji wakuu wa Tanzania, mpaka saa ya ku-retire ndio tunajua kuwa hata kama walikuwepo!

Respect.


FMEs!
 
Nimeaga nimerudi tena kidogo tu nitoe jibu la sentensi moja: NAAMINI WAZEE WALIMSHAURI ZITTO AJITOE NA ZITTO AKAKUBALI KWA SABABU CHADEMA NI ZAIDI YA MBOWE NA ZITTO. Alamsiki, siku nyingine Kituko.
JJ

pamoja na kuwa ndani ya CHADEMA kama kiongozi, Pamoja na kupewa mamlaka ya kuandika huo waraka ulioubandika hapo kwenye website yenu, still hujuhi kinachoendelea unaishi humo kwa IMANI TU, mi nadhani majibu yako yanapaswa kuwa ya uhakika na sio mambo ya imani, siku zote ukiwa mtu wa kuaminiamini tu thinking yako lazima iwe zero, na kama wewe unaishi kwa imani ndani ya CHADEMA je sisi wa nje?
SWALI KWA NINI WAZEE WALIMSHAURI ZITTO AJITOE kama hilo ni gumu hebu jibu hili KWA NINI WAZEE HAWAKUMSHAURI MBOWE AMBAYE KAKAA MUDA MREFU AJITOE,
naomba majibu ya uhakika sio ya IMANI
 

Dogo JK siyo role model wa kiongozi wa siasa ninaye admire...what a joke?

Ungeniuliza ni kiongozi gani wa chama cha siasa una-appreaciate uongozi wake so far ningesema..ni "Ibrahimu Lipumba" wa CUF

Kwanini, chama kimelaumiwa sana kuwa na cha kidini lakini kila siku wanajitahidi na unaona viongozi wanafanya hivyo kwa vitendo...kuwa chama cha kitaifa...inapenetrate sehemu na kona zote za nchi.. hajalaumiwa uadilifu wake iwe katika kuonea mwanchama au kufisadi fedha za chama, hana njaa na ni msomi muadilifu..that is my take.

on the other hand, chadema wanaendeleza nepotism na ubabe usio na maana...kwa wanachama wake eti kisingizio tunalinda heshima

kulazimisha heshima au kuheshimwa wakati wewe huna heshima ni ugonjwa mbaya sana ambao chadema itakufa kifo cha mende kwa uongozi wa kina slaa na mbowe
 
[/COLOR]

Ha ha haa! Kuna ngoma inaitwa mduara.

Ulishaharibu mkuu, mbaya zaidi wewe ni injinia wa forums

Forum; A public facility to meet for open discussion-SAGE

Ulichofanya mara ya kwanza hakikuwa 'forum' ila ushabiki.kama wewe unaonyesha mfano huu, mkuu tutegemee nini kuja humu?

Hata kama una ushabiki weka kando, kwa nafasi yako ndani ya JF..wewe uwe kama mwenyekiti wa 'debate' kama mtu hajatukanwa whats wrong?

I am dissaponted!

Na usije kwa mamlaka yako ukanifungia au kunizushia mambo ya ajabu
 
Ungeniuliza ni kiongozi gani wa chama cha siasa una-appreaciate uongozi wake so far ningesema..ni "Ibrahimu Lipumba" wa CUF
mimi najiepusha kuzungumzia CUF, kwasababu zangu binafsi, ila swala la UDINI linawatafuna sana, watajuana na CCM, ila siioni falsafa maridhawa ndani ya ya chama hiko, ndo maana niko CHADEMA. kwanza CUF sio tishio kwetu, ni kama TLP tu, sisi tuwaza kupambana na CCM ALIE Madarakani, anaetuletea unasikini....nyinyi mnapambana na asie na mamlaka....ama dola, ama kweli.
kwangu issue sio kua Muislamu , mpagani , mpare , mpemba au Mmasai, cha muhimu ni namna gani unaweza kuongoza na kuleta mambo mema kwa nnchi yako....
 

Sababu zako binafsi ni "UDINI" kama kawaida unajificha sehemu tambarare

CUF siyo tishio..kwako..lol unafurahisha baraza au?...CUF ni wa pili kwenye uchaguzi wa serikali za mitaani uliopita...tlp sijui ni ya ngapi wapi na wapi?

Ibrahimu hajalaumiwa na wanachama for nepotism, kuonea wanachama wa CUF na ubadirifu wa fedha...lakini huyo jamaa yako mbowe na slaa kila siku wanachama wanalalamika je wakipewa dola..

Namna gani gani unaweza kuongoza na kuleta mambo kwa nchi yako ha ha ha ..hayo ni matokeo ya uadilifu wako binafsi na uadilifu wa taasisi yako..kusimamia hayo..tumeshuhudia CCM na Chadema kwenye swala la kusimamia uadilifu....wanaboa...long way to go for chadema as an institution.
 
Kesho tutakuwa na Kongamano la Vijana, halafu kuanzia tarehe 30 Novemba, 2009 mpaka tarehe 3 Disemba 2009 tutakuwa kwenye mfululizo wa vikao vya juu vya chama tukiutathmini mwaka 2009 na kupanga mwelekeo wa chama kwenda mwaka 2010.

Ndugu Mnyika maswali yangu utayajibu , japo sidhani kama nitaweza kusoma kwa sasa. Ila ondoeni huo wingu unaotanda mkijua kuwa ndio mtaji wa wapinzani wenu kuwakosesha kura.

Pili, sijajua ile sera ya nyumba tano imeishia wapi na ni kwa kiasi gani inakuwa reinforced that was brilliant idea, na inawezekana

Tatu kitengo chenu cha siasa bado kiko poor katika vyama hicho kitengo ni kama ;department ya marketing kwenye makampuni kama Tigo. Tatizo sijaona kama mnachukua opportunity zilizopo kwa kiasi gani.Mathalan Sofia Simba alisema CCM mafisadi-mnaweza kuweka postal kubwa ya Sofia simba na kuandika maneno yake chini ''CCM wote mafisadi' na kuisambaza. Sijajua kama kuna kitengo kama hiki na sijajua kiko efficiency kiasi gani

Nne chukulieni kuwa Changamoto hizi ni kwa ajili ya nyie kukomaa na kukua.Forum hizi zinasaidia sana kuona watu wanawaza nini.Kupata kura ni ishu nyingine mkuu, hata ukijibu tuhuma zote na watu wote JF wakaelewa lakini kupata Kura is another art Kumbuka,

"The ballot is stronger than bullet" J.A.Schumpeter.

Tunataka mpate kura, THATS ALL

Kazi njema
 
ni wapi nimezungumzia udini, wewe na CUF wako mtajuana kama vikao vya kuhamasishana mnafanyia misikitini ama laah, ila nijuacho mimi moja ya malengo ya CHADEMA nikushika dola, kwa maendeleo ya Taifa, lengo letu sikupambana na vyama visivyo na dola.......
CCM wenyewe wanajua nani ni adui yao kwanza, maana wanapambana kwa nguvu zao zote.
 
Ngoja awaudhi wenye chama ndio atajua unachooongea..dogo bado anabebwa kwa nepi...

Awaudhi wenye chama kwa kukubali kununuliwa na RA ili awe anawapigia ndogondogo -- kumtetea kujananja katika ufisadi wake na kujaribu kuibomoa Chadema. Na kila mara huwa ni Mbowe dikteta, Mbowe anatafuna ruzuku -- hivi hakuna hoja nyingine? Hoja hii inachosha sana -- imeshatumika huko nyuma na wengi tu viongozi waliotimuliwa kutoka vyama vingine vya siasa kama NCCR, TLP, CUF etc.Halafu naunga mkono akina kafulia na huyu dandi ni sisimizi tu -- na nawahakikishia RA hatawajali tena, kwani hawawezi kumsaidia wakiwa katika chama ambacho kimepoteza kabisa mwelekeo -- yaani NCCR. Mbatia aliaibika Tarime kutokana na kukubali kuwa wakala wa CCM kujaribu kuizuia Chadema.mbatia aliweza kufanikiwa Pemba miaka kadha iliyopita alipoisaidia CCM kuchukua viti kule alikopiga kambi -- huku hao hao CCM wakimnyang'sanya kiti katika jimbo Kigoma. Akina Dandi wawe tayari kufanya hiyo kazi ya UWAKALA -- kwa RA na CCM!!!
 

Wewe na chadema mtajua kama vikao vyenu vya kuhamasishana ni kanisani au laah,! au uchagani

Malengo yenu si kupambana na vyama visivyo na dola...recall sherehe mliyofanya baada ya kumchukua Lwakatare! lol

CCM wenyewe wanajua nani adui yao wa kwanza! joking! CCM iwaogope viongozi ambao si waadilifu ambao bei yao ni kununua muasisis moja kutoka kilimanjaro na kubadilisha uamuzi mzima...wa chama kwa faida yake na familia yake...

CCM haina shida na mtu ambaye ni fisadi mwenzao kama mbowe ambaye anaweza kununuliwa kwa kufunguliwa biashara ya kuuza pombe...etc..get your record right..na inajua chadema hai-function kitaasisi (family show institution)
 
CHADEMA, HALI NI SHWARI...........
Kesho tutakuwa na Kongamano la Vijana, halafu kuanzia tarehe 30 Novemba, 2009 mpaka tarehe 3 Disemba 2009 tutakuwa kwenye mfululizo wa vikao vya juu vya chama tukiutathmini mwaka 2009 na kupanga mwelekeo wa chama kwenda mwaka 2010.
Vijana wote wapenda mabadiliko haya shime tuungane, maana adui yetu CCM ametangaza vita tayari kuelekea uchaguzi mkuu, tukutane kesho.
 

Si kweli kelele ni sauti zisizo na mpangilio maalum.

Kelele ni sauti yoyote iliyo ktk frequency(masafa) ambayo hupendelei kusafiri nayo na hayo masafa (frequency).

Mfano sauti yako inasikika na unapendelea kuisikia ikiwa ktk frequency(masafa) ya 40 Hz, hivo ikija sauti nyingine iliyo ktk mpangilio mzuri na sauti ya kuvutia na murua na iko ktk frequency (masafa) ya 100Hz,hii itakuwa kelele ktk bandwidth yako.

Kwa hiyo angalia unapoita sauti iliyo ktk frequency nyingine ni sauti isiyo ktk mpangilio unakosea sana maana unajilimit sana.

Na kwa kukushaurini fanyeni mpango wa kuzi intergrate pamoja hizo sauti zilizo ktk frequency tofauti.
 

Umenena ndugu yangu -- ingawa huyo dandi bado hajaenda NCCR. Labda ataenda CUF -- lakini kule pia RA ana mkono. Tumeliona hilo.Lakini kuondoka kwa kiongozi/mwanachama kutoka chama cha siasa ni hiari ya mtu, na hakuna haja ya kuondoka kwa maneno, matusi nk. Hii imekuwa ndiyo utamaduni wa siku hizi, hawezi kiongozi kuondoka kimyakimya kutoka katika chama bila kuwabwatukia viongozi wa juu.Itakumbukwa huko nyuma guninita alitimuliwa Chadema na alibwatuka hayo hayo -- utafunaji wa ruzuku. Kumbe alikuwa kihiyo wa kutupa! Mwingine ramadhani Mzee alitimuliwa CUF na akataja hayo hayo ya kutafuna ruzuku. Hivi yuko wapi huyu?Ninachotaka kusema ni kwamba hao na wengine waliondoka hakukutokea kukuzwa au maneno mengi magazetini nk na masuala yalisahauliwa kwa siku chache tu. Siku hizi "sisimizi" (nami nakubali ni sisimizi) akiondoka Chadema, basi linakuwa jambo kubwa kweli kweli -- magazeti ya RA yanaliendeleza mpaka vichwa vya habari vinasikitisha na kutia doa katika fani ya uandishi. lakini sababu ya hii inajulikana -- ufisadi tu.
 
Siyo vibaya kijipa moyo...endelee

Je unaonaje ukianzia kanisani na uchagani kuhamasisha watu kuja huko ..lol just curious
 
kumbe kuna mafungamano , sasa naanza kuelewa haya mambo.....
 

chadema pambaneni sana maana hizi gharika ni vitu vya kawaida. Kwani katika kondoo kuna na mbuzi hivyo hivyo kujua kondoo ni yupi na mbuzi ni yupi ni kazi kubwa. Cha muhimu wekeni misingi bora itakayowezesha kondoo kuchujwa kwa urahisi. Upinzani ni kawaida ila upatapo upinzani unajua jinsi ya kujipanga kwani huwa unaonyesha mapungufu yako na ya adui.
 
Hivi kwanini watu wapenda sana ushabiki? Issue ya mbowe kuwa fisadi ilishaongelewa hapa jamvini sasa watu wanarudia ili kubadilisha mada au? Wewe ukisema kuwa CHADEMA mfano wanachama wake wanalalamika kuwa mbowe, slaa ni wadini, mafisadi, wanatumia hela la ruzuku vibaya. Je wanachama kwanini wanawapigia kura? Kwanini hawaambiwi haya kwenye vikao tena vya wazi siyo vya siri kama vya chama fulani? CUF huwezi kuilinganisha na Chadema kwani inanguvu sehemu zenye waislamu wengi hilo halina ubishi. Mifano michache zanzibar, kondoa, rufiji, temeke, mikoa ya kusini. Huwezi kukuta CUF imefanya vizuri mikoa ya kaskazini labda mtu awe anakubalika hivyo watu wamchague. Hata Lwakatale kushinda mwaka 2000 ni kwasababu kulikuwa na support ya chadema pia.

Tumezoea sasa kila chama kinapojaribu kusimama kinashambuliwa plus kuplant mamruki ili kiyumbe kife cheki NCCR, TLP, CUF na sasa wanafanya kwa CHADEMA. Lakini for information chama hiki kiko makini hivyo sidhani kama kitayumba.
 
Alisema ndani ya Chadema kuna makundi mawili, kundi la Mbowe lenye maisha mazuri na magari ya kifahari na lile la Zitto lenye wanachama wanaomuunga mkono mwanasiasa huyo.


Huyu Ms Nsanzugwanko anajua anachosema? Kundi la Mbowe lina maisha mazuri na magari ya kifahari halafu la Zitto lina wanachama wanaomuunga mkono.

Jamani! Mambo ya Chini Ya Muti School of Journalism.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…