Hivi kwanini watu wapenda sana ushabiki? Issue ya mbowe kuwa fisadi ilishaongelewa hapa jamvini sasa watu wanarudia ili kubadilisha mada au? Wewe ukisema kuwa CHADEMA mfano wanachama wake wanalalamika kuwa mbowe, slaa ni wadini, mafisadi, wanatumia hela la ruzuku vibaya. Je wanachama kwanini wanawapigia kura? Kwanini hawaambiwi haya kwenye vikao tena vya wazi siyo vya siri kama vya chama fulani? CUF huwezi kuilinganisha na Chadema kwani inanguvu sehemu zenye waislamu wengi hilo halina ubishi. Mifano michache zanzibar, kondoa, rufiji, temeke, mikoa ya kusini. Huwezi kukuta CUF imefanya vizuri mikoa ya kaskazini labda mtu awe anakubalika hivyo watu wamchague. Hata Lwakatale kushinda mwaka 2000 ni kwasababu kulikuwa na support ya chadema pia.
Tumezoea sasa kila chama kinapojaribu kusimama kinashambuliwa plus kuplant mamruki ili kiyumbe kife cheki NCCR, TLP, CUF na sasa wanafanya kwa CHADEMA. Lakini for information chama hiki kiko makini hivyo sidhani kama kitayumba.
Michango hii inafurahisha sana.
Kwanini RA anapigiwa kura? kwanini wananchi hawaambiwi ktk vikao vya wazi??