Pre GE2025 Chadema na CCM msituhamishie kwenye Muungano Tunahitaji Tume huru ya Uchaguzi

Pre GE2025 Chadema na CCM msituhamishie kwenye Muungano Tunahitaji Tume huru ya Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Hayo malumbano yamekaa kimarekani mmetutoa Ukrane mkatupeleka gaza na sasa mnatuelkeza Iran.

Muungano uwepo usiwepo tunahitaji tume huru ya Uchaguzi,mmetutoa kwenye Katiba mkatupeleka kwenye bandari sasa dira inaonyesha mnatupekecha kwenye Muungano.

Uchaguzi umebakia miezi tu ,hatuoni fununu za kutaka au kudai Tume huru za Uchaguzi ,
Naviuliza vyama vya siasa kwa nini agenda hii hamuivalii njuga ?
Natoa mwezi mmoja kama hamkuipa kipau mbele nitaipigia kura CCm na kushajihisha waTanzania walio wengi wafanye hivyo.

Kwani inaonekana kukaa kwenu kwenye vyama vya upinzani kuna faida mnaipata nyinyi viongozi tu ,wananchi wanabaki kuburuzwa na sasa wanaburuzwa kwenye viunga vya muungano.
 
Umeona,ila la katiba linamtiririko wa muda,Shee uchaguzi upo kizingizitni unapiga hodi ,hivi Tume ni ile ile unahisi vyama vya maandamano vitavuka ?
Timu zile zile refa yuleyule aliewazimisha 2020 ,wanabaki kulalaimika uchaguzi sio huru wakiulizwa sababu wanajibu tume sio huru.
Suali watakaloshindwa kulijibu
Je kabla ya uchaguzi mliwahi kulivalia njuga ,watajibu tulikuwa tunashugulikia bandari ,mwaka huu watakuwa na dalaja la Masaki .

Kesho kutwa CCM wataanza kuimba CCM ni ile ilee.

Vyama vya upinzani mambo ya uchaguzi na mchaguliwa ndani ya CCM hayawahu ,lakini utwaona upinzani nao wanahemukwa na mambo ya ndani ya ccm.
Yaani kama si wezi ni manyang'au ,hakuna kama Marehemu Maalim Seif amepigana hadi Chama chake kimeweka mguu ikulu.
 
Back
Top Bottom