Kitu cha heri, hata siku moja hakishawishiwi kwa rushwa. Kama ni jambo la heri, kwa nini mwekezaji awahonge wabunge na waandishi wa habari?
Hakuna mtu yeyote mwenye akili nzuri na dhamira njema anayeweza kupinga partnership ya aina yoyote yenye manufaa kwa pande zote.
Lakini hii proposed partnership ya bandari, hata bila ya kuangalia content yake, imeanza vibaya kwa kutanguliza rushwa kwa wafanya maamuzi. Kama dhamira ni njema, kabla ya lolote, kwa upande wa Tanzania, wabunge wote waliopokea rushwa wakamatwe na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria. Kwa upabde wa nchi mwekezaji, wote waliohusika na utoaji rushwa wakamatwe na ithibitike wazi wamechukuliwa hatua na wasihusike kwa lolote kwenye mkataba. Baada ya hapo ndipo mazungumzo yaanze upya.