Chadema na dharau kwa amri ya mahakama.

Chadema na dharau kwa amri ya mahakama.

Binafsi sikuona sababu ya kutangaza uamuzi huu leo hii badala ya kusubiri suala la mahakamani kwa sababu masuala yote yanawahusu wote watatu. Ingekuwa ni hekima tu kusubiri suala la mahakamani li play out kabla ya kuchukua uamuzi wowote.
 
Hiyo 'gag order' kama ipo, inasemaje?

Kama kuna mtu anayo basi nitashukuru akiniwekea hapa verbatim.

Niliuliza hili swali sijajibiwa mpaka sasa. Watu wameenda mahakamani ku liveblog, Kurugenzi za habari zimeripoti hapa, ukiuliza the genuine article hupati.
 
Niliuliza hili swali sijajibiwa mpaka sasa. Watu wameenda mahakamani ku liveblog, Kurugenzi za habari zimeripoti hapa, ukiuliza the genuine article hupati.

Ndugu yangu siku zote mhuni hataki kuambiwa unavunja sheria...yeye anavyofanya ni sahihi lkn wengine sio sahihi
 
Unapomzuia zitto kufanya mikutano unaongelea suala lake binafsi au uanachama wake?
Kutokufanya mikutano tafsiri yake ni kutokufanya moja kati ya shughuli za chama, uanachama wake kwa maana ya "status" haijaguswa wala kubadilishwa kwa namna yoyote. Na ndicho mahakama ilichoelekeza. Kujadili uanachama tafsiri yake ni kuhoji awe mwanachama au asiwe? uanachama wake ni halali au sio halali? Sidhani kama hili liliguswa na kikao hicho. Huu ni mtazamo wangu, lete wa kwako kwa hoja tuwekane sawa.
 
Lissu anasema kuwa Zitto anaendelea kuwa Mwanachama na Mbunge wa CHADEMA kwasababu ya Mahakama tu na sio kwasababu ya mapenzi ya CHADEMA.

Hii kauli ya Tundu Lissu ukiisome vyema utagundua kuwa anasema wao kama chadema wamesha ujadili uanachama wa zitto kinyume na amri ya mahakama na walisha mfukuza uanachama.

hivyo tukubaliane kuwa ukiungasha kauli za Dr.W.Slaa na Tundu Lissu unapata kosa walio lifanya dhidi ya zuio la mahakama.
 
Last edited by a moderator:
Kutokufanya mikutano tafsiri yake ni kutokufanya moja kati ya shughuli za chama, uanachama wake kwa maana ya "status" haijaguswa wala kubadilishwa kwa namna yoyote. Na ndicho mahakama ilichoelekeza. Kujadili uanachama tafsiri yake ni kuhoji awe mwanachama au asiwe? uanachama wake ni halali au sio halali? Sidhani kama hili liliguswa na kikao hicho. Huu ni mtazamo wangu, lete wa kwako kwa hoja tuwekane sawa.

Hicho ndicho nilichoelewa.

CHADEMA inaweza kuzuia mwanachama wake yeyote kufanya mikutano kwa jina la chama, lakini hilo halimaanishi kwamba kufanya hivyo ni kumvua uanachama.

Kizungumkuti kinakuja akitaka kwenda kufanya mikutano ya kibunge jimboni kwake.

Kwa sababu yeye ni mbunge wa CHADEMA, mkutano wowote wa kibunge utafanyika chini ya mwamvuli wa chama.

Na kwa kumkataza kufanya mikutano kwa jina la chama, CHADEMA kimemzuia mbunge wake kufanya kazi za kibunge zinazohusisha kufanya mikutano na wananchi wa jimbo lake.
 
Sijui Lissu alisoma cho gani.kitendo cha kuelezea hatima ya Zitto CHADEMA katika taarifa yake ya leo kitabadilisha maamuzi ya jaji.

lisu ni mlevi wa sheria na ameharibu mlengo wa kesi.

usiku mwema.

Mambo ya chadema hayakuhusu. Nenda kalalamike mahakamani na wewe.

Unakumbuka point yangu hii ua ukumbuki? ndugu foshizzle
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom