MwK,
Hebu punguza jazba kidogo na kusoma tena ujumbe wangu kwa uangalifu ili ujibu hoja badala ya kuendeleza mayowe. Mimi ni Mdanganyika, sishabikii chama chochote kama mwenzangu ambaye umemchagua Mrema. Kama uteuzi wenye ratio ya 4 out of 6 kiukabila sio controversial basi tunaweza ku-ignore wanaolalamika, otherwise Chadema ni vema wakarekebisha hiyo hali. Halafu narudia tena kuwa, matumizi yaliyotangazwa na Chadema ni ya mwaka 2005 tu. Kingine cha muhimu ni kuangalia statement ya mwisho kabisa kwenye hiyo page ya matumizi, kuhusu CCM, ili uelewe kwa nini matumizi hayo yaliwekwa na pengine kwa nini mengine hayajawekwa wazi hadi leo ambapo wanachama mikoani wanalalamika.
Gharama za Kampeni Uchaguzi Mkuu 2005 - Chadema
http://www.chadema.net/uchaguzi/gharama.php
Mapato
1. Ruzuku kutoka Serikalini 22,770,712
Agosti mpaka Novemba
2. Michango ya Wanachama na Wapenzi wa Ndani 246,723,543
3. Michango ya Wahisani wa Nje ya Nchi 83,500,000
Conservative Party
4. Mikopo ya Wanachama na Wapenzi wa Ndani 399,574,543
Jumla 752,568,798
Matumizi
1. Gharama za Helikopta 223,030,726
Kukodisha helikopta 186,500,800
Mafuta ya helikopta 31,057,786
Vibali, Kodi viwanja vya ndege, Uendeshaji n.k. 5,472,140
2. Kampeni kupitia vyombo vya habari 60,576,450
Malazi, chakula na posho za waandishi wa habari 21,186,050
Matangazo kwenye luninga, radio na magazeti 39,390,400
3. Nyenzo za Kampeni 61,363,660
Machapisho - mabango, vipeperushi 51,113,500
Nyenzo za kampeni - bendera, fulana 8,580,000
Gharama za uchapishaji Makao Makuu 1,670,160
4. Gharama za Vikao vya Uteuzi 87,386,659
Kura za awali (Primaries) 43,490,959
Kamati Kuu, Baraza Kuu & Mkutano Mkuu 43,895,700
5. Misaada ya fedha taslim kwa Wagombea Ubunge 59,250,000
6. Gharama za Usafiri 160,558,084
Kukodisha magari 35,580,000
Kununua magari 79,200,000
Matengenezo ya magari 15,867,850
Mafuta ya magari 26,725,234
Usafiri wa ndege 3,185,000
7. Uendeshaji wa Makao Makuu kipindi cha Kampeni 17,500,000
8. Gharama za kuendesha mikutano 68,615,000
Kukodisha vipaza sauti 44,095,000
Kununua Majenereta kwa ajili ya mikutano 17,720,000
Kununua vipaza sauti kwa Wagombea Ubunge 6,800,000
9. Gharama za Simu/Mawasiliano 1,112,000
10. Gharama za Mazishi 1,300,000
11. Posho za Watendaji wa Kampeni 7,780,000
12. Malazi na chakula kwa Watendaji wa kampeni 5,021,826
13. Gharama nyinginezo 292,100
Jumla 753,786,505
Chama cha Mapinduzi kimepata kigugumizi na kimeshindwa kukanusha tuhuma kwamba kilitumia zaidi ya shilingi bilioni 40 (40,000,000,000,000) katika kampeni za Uchaguzi wa 2005. Aidha, Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikipinga kwa nguvu zake zote mabadiliko yeyote kwenye sheria za uchaguzi ambayo yataweka ukomo wa matumizi ya fedha katika kampeni.
Huu ni mkakati wa makusudi kabisa wa chama hiki cha mafisadi wakuendelea kung'ang'ania madaraka kwa kuhakikisha uchaguzi hauwi wa huru na haki.
http://www.chadema.net/uchaguzi/gharama.php