Hii ni muhimu unapoongelea alternative kwa wananchi lazima uwe na uhakika kuwa hiyo alternative ni safi ndo maana kama kuna lolote baya au zuri kwenye vyama vya upinzania lazima lijadiliwe sambamba na mabaya na mazuri ya CCM
Jambo moja ambalo Jaco na Kubwajinga wanapotosha ni hili:
1. Hawakosoi Chadema kusaidia taifa au kuatafuta alternative. Kama wangekuwa na nia hiyo wasingeiandama Chadema tu, bali wangezijadili TLP, CUF, NCCR-Mageuzi, UDP na vyama vingine. Sisi tunaijua kinachoendelea ndani ya system tunajua kazi wanayofanya hawa vijana. Kwa kujua au bila kujua, wanafanya KAZI CHAFU!!!!
2. Kwa kuwasoma vizuri (between the lines), mtu yeyote atagundua kwamba wana UKABILA ndani yao, ila wanaufunua kwa kushambulia makabila ya wengine. Ni bahati mbaya kwao kwamba Chadema kina NGUVU kubwa Kilimanjaro, Tarime, Karatu, Kigoma na Mpanda Kati. Ni bahati nzuri kwa CCM kwamba Chadema kina jimbo MOJA tu Uchagani - Moshi Mjini!
Jaco na Kubwajinga hawatazami personal charisma ya viongozi wa chama, wanatazama makabila yao. Hawaoni mweleko wa chaka kukua na kusambaa nchi nzima, wao wanaona kinajifinya tu kwenye Uchaga. Kikubwa kwao ni zile nafasi chache za uongozi zinazoshikiliwa na viongozi waliozaliwa (kwa mapenzi ya Mungu) Wachagga.
3. Sijui Kubwajinga ana maslahi gani na 'viti maalumu' vya Chadema, maana wanawake wenyewe waliokuwa wanavilalamikia (kina Chiku Abwao) walishanyamaza baada ya hasira za kukosa ubunge kuisha, hasa baada ya maelezo.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa maelezo hayo yalishatolewa na Mnyika hapa hapa JF. Huyu anayelileta hili sasa na matatizo yake na malengo yake.
Hebu tuwajadili wabunge hao:
1. Ndesamburo alishinda kwenye kura. Tulitaka awe Mzaramo?
2. Zitto alishinda kwenye kura. Naye Mchagga?
3. Wangwe alishinda kwenye kura. Si Mkurya huku?
4. Said Arfi alishinda kwa kura. Naye ni Mchagga?
5. Dk. Slaa alishinda kwa kura. Mchagga?
VITI MAALUMU (kwa nafasi zao)
6.
Grace Kiwelu. Aliteuliwa na mkutano mkuu wa Chadema kwa sifa moja. Alikuwa mbunge pekee wa kike wa chama hicho (2000-2005) ambaye alitoa mchango mkubwa wa muda na raslimali kukikuza chama na kukieneza nchi nzima. Hata kalbaya uchaguzi Mkuu, wajumbe wa mkutano mkuu waliahidi kwamba iwapo ingetokea mnafasi moja tu ya viti maalumu APEWE GRACE. Uchagga wake unaingiaje hapa?
7.
Anna Komu: Alikuwa mgombea mwenza wa urais. Busara pekee inatosha kueleza kwa nini alipata ubunge. Uchagga uko wapi hapa? Tulitarajia kama tungekuwa na katiba ya maana, hata wagombea urais wote na wenyeviti wa vyama vyenye wabunge wangepaswa kuwa automatically bungeni. Walio wengi bungeni na wenye madaraka hawataki. Chadema waliona busara kumpa mgombea mwenza nafasi hiyo. Kuna ubaya gani?
VITI MAALUM (kwa kugombea).
Hapa ilitegemea idadi ya kura za jumla kutoka kila mkoa.
8. Kilimanjaro ilitoa kura nyingi zaidi: Mgombea alikuwa
Lucy, akapata Ubunge. Ana kosa gani?
9. Mkoa uliofuata ulikuwa Kigoma. Mgombea aliyeshinda alikuwa
Mhonga; akapa ubunge. Ana kosa gani?
10. Dar es Salaam ikafuata kwa wingi wa kura. Mgombea mshindi alikuwa
Halima Mdee. Ana kosa gani?
11. Katika taasisi: Elimu ya Juu alikuwa
Susan lyimo. Akapita.
Hii inaonyesha kwamba tunajua kinachoendelea. Tazama michango ya wabunge hawa Bungeni. Wanajadili na kuibua hoja za kitaifa au za kikabila?
Sasa wanaozungumzia ukabila, watuambie wabunge hawa waliletwa tu na kupewa au waliondolewa dada zao waliostahili wakapewa wao kwa sababu ya ukabila? Halafu ni vema ieleweke kwamba Chadema tunayoijadili leo haikuwa hivi kabla ya uchaguzi mkuu. Wakati watu walikuwa wakikimbilia kugombea CCM kwa sababu ya ukubwa wa chama, wengi walivikimbia vyama vidogo. Hawa waliojitokeza kugombea na kupata ni mashujaa ambao hata huko nyumba waliamua kuwekeza katika kuvijenga vyama hivi vidogo.
Kubwajinga acha spinning. Ina maslahi gani ya taifa kuharibu hata hicho kidogo kilichopatikana katika
kuchek nguvu za CCM. Unawabomoa Chadema kwa faida ya nani? Eti tunaangalia alternative kwa spinning? Acga hizo! Mkubwa wewe!