Pre GE2025 CHADEMA na vyama vingine chukueni mwelekeo huu haraka kabla ya uchaguzi, mtanishukuru baadaye!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Desprospero

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
1,015
Reaction score
2,493
Nchi hii ni yetu sote. Kwa mantiki hiyo kila mmoja anao uhuru wa kutoa maoni bila kuingiliwa maadamu havunji sheria. Nazungumza na Chadema kama mwakilishi wa vyama vingine vya upinzani nchini Tanzania.

Kila chama kinatamani kushinda uchaguzi na kuunda Serikali. Zitto Kabwe ametoa wazo la vyama kuunganisha nguvu kukiondoa CCM katika chaguzi kadhaa. Hata hivyo amebezwa japo utaratibu huu umeviondoa vyama vingi madarakani na mifano iko mingi barani Afrika.

Wazo hili nimewapa upinzani toka 2010 lakini uroho wa madaraka, kutokuaminiana, kujiuza na kununulika kwa kupigwa bei kama mbuzi wa shughuli mnadani imeshindikana bila kujua kuwa hakuna chama oga na mwepesi kama CCM.

Leo nakazia tena hoja niliyowahi kuwapa mara kadhaa. Kaeni kitako. Pitieni nyakati mlizopitia hadi sasa. Ni INJILI gani mliyohubiri ikawaingia Watanzania? Sasa ninawaambia. Haya ya kudai Tanganyika, kudai kuuawa kwa kutekwa, kuteswa, kuuawa na kutupwa hayagusi moja kwa moja wapiga kura hasa wa vijijini wasio na smartphone. Huko ndiko kwenye kura.

Hivi mnakumbuka mlivyokonga nyoyo za Watanzania mlipotangazac LIST OF SHAME pale Mwembe Yanga? Mnajua ni kwa kiasi gani mligusa maisha ya watu? Political Science inafafanua kuwa mwambie mtu nini chanzo cha ugonjwa wake, umasikini wake na kwa namna gani anaweza kuondokana na maisha hayo dhalili? Unajua kwa nini watu masikini wamejazana kwa kina Mwamposa, Kiboko ya Wachawi nakadhalika? Ni kwa sababu watu hawa wamekata tamaa na hawaoni wapi wakimbilie zaidi kwa "mungu" na si vinginevyo.

Na mkumbuke serikali ya CCM inavilea sana dini na made madhehebu haya maana ni chaka la kuficha udhalimu wao usijulikane na wanakondoo wanaojazana kwa Mwamposa huku wakihubiriwa, "tafuteni ufalme wa mbinguni maana mali za dunia ni za kupita tu". Falsafa hii ilianzia Ghana sasa ni Afrika nzima Tanzania ikiwa kinara ambapo idadi ya makanisa ni mengi kuliko viwanda. Umeona mafisadi waking wakianguka kwa Mwamposa? Ushahidi amewaambia Kiboko ya Wachawi majuzi akiwa Lubumbashi, "Watanzania ni wajinga kweli, nimekula hizo hela zenu laki 5 tano dah".

Nataka kuwaambia nini Chadema na upinzani kwa ujumla. Hubirini injili hii wasiyotaka CCM kusikia. Nayo ni rushwa na ufisadi uliotamalaki. Mawaziri wanashindana kwa utajiri. Upigaji sqsa ni wa kutisha. Waambieni watu haya ili akilala njaa anajua aliyesababisha ni fisadi fulani. Wakipita mijini na vijijini watatemewa mate na kupopolewa mawe. Hii ni hoja inayoeleweka kirahisi kuliko kuwaambia Ally Kibao kauliwa. Nani na wangapi kwa idadi ya kura walimfahamu? Na katika muktadha upi?

Nawaambia haya ili ku-win kura kutoka huko huko CCM na kwa wasio na vyama. Umasikini unawatesa Wwatanzania kuliko kutekwa. Na CCM inafurahi mno mnaposhadadia mambo haya ya mauaji ambayo polical milage yake si kubxwa. Mama yangu hata hhajui kuna Ubalozi wa. USA ililaani. Anajua balozi wake wa nyumba kumi tu.

Mnakumbuka ishu ya uuzwaji wa Bandar na Ngorongoro ilivyowagusa masikini hata bila kuandamana? Waambieni shida zao na wasababishi kwa majina yao na vyeo vyao. Safari hii mnaweza kuja na list of shame ya karne maana mpaka mtoto wa rais atakuwepo. Vaeni ujasiri kama kweli nia yenu ni kuleta mabadiliko. Kataeni kunywa chai Ikulu mnakolegezwa.

Mwisho, mitandao ya kijamii ni muhimu lakini fanyeni utafiti. Ni wapiga kura wangapi wana smartphone? Kama wapo sawa, hao waacheni. Mnawapataje wanavijiji wasiojua hata nini maana ya Facebook akiwemo mama yangu? Kama mliweza kumiliki magazeti (Tanzania Daima), milikini pia na redio na TV? Hivi kama Kiboko ya Wachawi anaweza kuhubiri utapeli wake kupitia redio tena usiku wa manani (si manane) leo Chadema inaweza kushindwa kuhubiri chama kila siku siku 7 kwa mwezi bila kuchoka na wasikilizaji kuchangia gharama? Guseni maisha ya watu. Mbowe mnakwama wapi?

Kura ziko kijijini. Juzi mmeona Samia anashukuru wananchi Tunduru kwa mapokezi lakini mita 215 kutoka alikokuwa akihubiri walikuwepo wagonjwa waliopakiwa kwenye tenga la nyanya kupelekwa hospitalini. Semeni haya si tu kwenye WhatsApp. Yule mgonjwa hajui WhatsApp. Sasa misitu yote Tanzania imeuzwa kwa Wamarekani chini ya mpango wa biashara ya carbon. Waambieni wananchi haya nyie vipi?

Kifupi mkitaka kukishika CCM sehemu nyeti hubirini ufisadi. Hata wao huitumia sana kupata wagombea wao. Rejeeni ya Lowassa na Membe. Ufisadi vs Uadilifu hata kama wote walikuwa na madhambi yao. UFISADI UNAWAGUSANA MASIKINI, MTASHINDA.

Ahsanteni sana.
Mkipenda mchukue, kinyume chake mpuuze CCM ishangilie.
Ova!
 
Chadema na Mbowe hawana uhalali wa umma kukemea ufisadi tangu walipokubali kumkaribisha Lowassa katika wa kilele cha kuaminika kwao na umma.
 
Wahesabu kura ndio wanaoamua mshindi awe nani ma sio hizo kura za hao wanavijiji. Kwa taarifa yako hao wenye smartphone wanatosha sana kufanya hata bunge lisiweze kufanya maamuzi watakavyo ccm. Kwa tume hii ya uchaguzi, ni wendawazimu kuongelea kura za vijijini eti hawana smartphone.
 
Wewe Gen Z bila shaka. Huna uzoefu na uchaguzi wa Tanzania kama mimi toka 2010
 
Chadema wana muda mzuri wa kijiandaa wakiamua kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu 2025.

Wahitaji mikakati imara ambayo ni ya aina yake, wahitaji stratejia, wahitaji jarida lenye kuonyesha sera zao au manifesto na wahitaji kuwandaa wananchi wapiga kura kisaikolojia.

Ila kwa namna wanavyobamizwa kisaikolojia sidhani kama watakuwa na "momentum" yoyote ukizingatia Tundu Lissu yeye kaanza na kushughulikia kesi yake huko London.
 
Sure
 
Elimu elimu elimu elimu, kwa sasa chadema haina hajenda.
 
Back
Top Bottom