Uchaguzi 2020 CHADEMA na vyama Vingine pinzani mmekubali kuingia kwenye Uchaguzi kwa Tume hii ya Uchaguzi? Baada ya Uchaguzi tusisikie mnalia

Kadoda nguku

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2019
Posts
332
Reaction score
475
Huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu, kwa jinsi hali ilivyo ukiachilia maneno ya wanaccm ,vyama vya upinzani vina nafasi kubwa ya kupata ushindi kwenye majimbo mengi

Nimejaribu kufanya observation maeneo mengi, wananchi wamekata tamaa na hali ya maisha yamekuwa ya uwoga msingi kitu ambacho kinaashiria kama vyama vya upinzani wangeanza kushughurikia tume huru kwanza kabla ya kukubali kuingia kwenye uchaguzi wangeweza pata matokeo makubwa kuliko uchaguzi wa 2015

Ila kwa tume hii wagombea wengi wataanza kuwekewa zengwe na kuondolewa kwenye hatua za awali tu, na hicho ndicho ninachokiona
Sasa kama vyama pinzani vimekubali (hapa nazungumzia vyama pinzani vinavyojitambua kama ACT nana kuingia kwenye uchaguzi na tume hii ya CCM kitakachowapata hatutaki kusikia vilio vyenu

Sisi wanachama tungefurahi kama mngeanza kushughurikia time huru kwanza, huu utawala hauna hata chembe ya aibu, na tunalo la kujifunza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, watendaji wa kata walio waondoa wagombea wa upinzani ndio hao hao watakao waondoa wagombea wa upinzani mwaka huu
 
Nakubaliana na wewe. Kama wamekubali ujinga kama huo, wanyamaze yatakayowapata. Tusiunge mkono ubatili kwa kushiriki, wacha wachaguane dunia ijue!
 
Ni majmbo gani na mangapi uliyofanyia utafiti ukaona vyama vya upinzani vitachukua? hebu yataje yote uliyoyaona yataenda upinzani!
 
Kwa tume hii ya ccm vyama vya upinzani vitakuwa na agenda elekezi na siyo upinzani tunaoutaka wa kuchukua nchi na kuifutilia mbali ccm
 
Ni majmbo gani na mangapi uliyofanyia utafiti ukaona vyama vya upinzani vitachukua? hebu yataje yote uliyoyaona yataenda upinzani!
Mengi sana, kuyataja nitasababisha Yesu wa CCM apate kihoro
 
Nakubaliana na wewe. Kama wamekubali ujinga kama huo, wanyamaze yatakayowapata. Tusiunge mkono ubatili kwa kushiriki, wacha wachaguane dunia ijue!
Na Mimi naona hakuna sababu ya kwenda kushindana wakati unajua unakwenda kushindwa,ni bora kuwaachia
 
Unajisumbua tu...
Hao wote lao ni moja
Kwa sasa wamepanga waingie kwenye uchaguzi ile hali wanajuwa kabisa kamisaa ni mwizi, refa mwizi, na mshika kibendera ni mwizi.
Kisha baada ya hapo watakuja na sarakasi ya kulialia na kuomba huruma kwa raia.

Siasa ya Bongo ni series kama series nyingine tu
 
Hata wakimpa Mbowe uwenyekiti wa NEC Magufuli atashinda kwa zaidi ya 95%, mjue kusoma alama za nyakati, matusi ya mitandaoni ya multiple accounts za vyeti feki na mafisadi yalosomeshwa namba zisikudanganye, huku field watu huwaambii kitu kuhusu Magufuli.
 
Hivi Kuna uchaguzi mwaka Huu?
 
Ungeweka hapa ushauri unaoeleweka. Wafanye nini ili kupata hiyo tume huru?? Na hiyo inatakiwa kuwa jukumu la wananchi wote, siyo vyama pekee.

Kwa uzoefu tu, yeyote akianza kudai hiyo tume atabambikiziwa kesi feki za uhujumu uchumi akae ndani hadi uchaguzi upite.. chezea sisiemu ww?!

Mabadiliko ya kweli yatapatikana siku wananchi wenyewe wakizinduka usingizini.

Kususa shamba na kuachia tumbili kula mahindi siyo suluhisho. Waliposusia uchaguzi wa serikali za mitaa wali-achieve nini??
 
Tatizo upinzani halisi ukigomea uchaguzi Kuna kikundi cha upinzani feki kitaibuka kusema watashiriki uchaguzi Kama kawaida.
 
Naunga hoja kweli kabisa yaani kwa kweli ni upuuzi mkubwa kuingia kwenye uchaguzi kwa tume hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…