CHADEMA na Wanaharakati kuonesha chuki dhidi ya Diamond ni ukosefu wa ajenda

Your browser is not able to display this video.
 
Kwa kuongezea tu watanzania waonyeshe uzalendo nchi jirani wanamkubali why not us pili hii ni zile roho mbaya za ktz hata kwenye kusaidiana kupasiana ajira kimataifa hawataki kama nchi zingine
 
Unaposema hajihusishi na siasa wakati alipanda majukwaani kuwanadi na kuwaimbia sifa, hapo hajihusishi na siasa?
 
Usiwapangie watu huo ni Uhuru wao wewe mpigie kura.
Acha hizo jombaa!!
 
Kauli gani rasmi imetolewa na chadema kumpiga vita?
 
Wew ndugu kuwa muelewa. Ni lini Chadema imetangaza hayo unayoyasema? Ni kikao gani kilikaa na kuamua kama madai yako hapa?
Chadema ni taasisi na inaongozwa na sheria na taratibu ikiwemo katiba. Mwanachama na hata viongozi ni raia wa nchi na wanahaki ya kutoa maoni yao juu ya jambo lolote na yasiwe maoni ya chama. Kauli ya chama hutolewa na msemaji wa Chama na kauli hutolewa baada ya vikao vya kikatiba vya chama kuamua. Hivyo brother acha kukihusisha chama na hili suala la Diamond.
 
Chama kikemee viongozi wake wanaoharibu taswira ya chama kwa kujihusisha na vitu vidogo. Viongozi waandamizi zaidi ya mmoja wanapojitokeza kuongelea tuzo ya BET ni dalili ya uongozi mbovu na kushusha hadhi ya chama. Mambo kama haya ni aibu kwa mtu kama Lissu, Msigwa na Lem kuyaongelea. Wangewaachia kina Malisa, Yeriko, Nanyaro na vijana wengine machachari wa CHADEMA.
 
Hawa wanaharakati wajinga kweli wenyewe wapo nyumba ya keyboard kukosoa serikali afu wanataka diamond Stoke front huu ujinga wa wapi huu
 
Huyu unayempigia debe ndiyo mwenye ule wimbo wa "magu baba lao?"

Yawezekana unaowashutumu leo hawana haja ya haramu na yote yahusikanayo na haramu hiyo.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Kwani alkiba hana wimbo wa magufuli, au hamonize hana wimbo wa CCM? Ni msanii gani mkubwa ambae hajawahi kushiriki shughuli za kisiasa hapa nchini?
 
Huyu unayempigia debe ndiyo mwenye ule wimbo wa "magu baba lao?"

Yawezekana unaowashutumu leo hawana haja ya haramu na yote yahusikanayo na haramu hiyo.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Unasema uongo,ndg yangu.
 
Ukisikia chama Cha matahila tupu,ndo hawa Sasa chadema.walitaka daimondi afanyaje !?,au walitaka naye awe mwanasiasa aachane na kazi yake ya muziki!? Yule ni musician ,na yuko ki biashara na yupo chini ya Management,ili afanye kazi na mtu/kampuni fulani anaangalia Kama mkataba unaompa ausaini je unamlipa kulingana na soko alilonalo kwenye kiwanda Cha muziki.sasa chadema ni wapumbavu na matahila tupu ,walitaka akubaliane na nao,kusaini mkataba nao azunguke nao kwenye kampeni,na awatungue nyimbo za kampeni,hata Kama Wana mpa mkataba wa hasara!?,ambao hauna faida kwake!?,mbowe ni mfanya biashara je yeye hukubali kufanya biashara za loss!? Ni matahila Sana hawa!,muziki ni biashara Kama biashara zingine!
 

Ila mkuu si unaifaham ile ngoma yake aliyo imba WACHA NIKAE KIMYA nadhani tutaelewana kidogo kidogo.
 
Unasema uongo,ndg yangu.

Uongo kuwa hakuimba "magu baba lao?"

Uongo kuwa unaowashutumu leo hawana haja ya haramu wala yote yatokanayo na haramu hiyo?

Kweli mmevurugwa kiasi kwamba mambo yote yanawaendea lukumba lukumba.

Hiiiiii bagosha!
 
Kwani alkiba hana wimbo wa magufuli, au hamonize hana wimbo wa CCM? Ni msanii gani mkubwa ambae hajawahi kushiriki shughuli za kisiasa hapa nchini?
Tatizo ni wimbi wa Magufuli? Elewa swali - hili lilikuwa na maana halisi tu ya kumtambua mpigiwa chapuo nothing more nothing less.

Kumbe wewe unadhani shida ni wimbo wa mwendazake? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚:


Kama hujajua shida ilipo bado sema uelewe. Kuuliza haijawahi kuwa ujinga.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…