CHADEMA Njombe yapiga marufuku waliobwagwa kura za maoni kugombea kupitia chama hicho

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,138
Reaction score
288,731
_Nimepata taarifa kuwa kuna wagombea Udiwani wa @ccm_tanzania walioshughulikiwa  ( 359 X 640 ).jpg

Hayo yamesemwa na kamanda Rose Mayemba ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Njombe alipokuwa anaongea na waandishi wa habari.

Amesema kwamba wale mamluki waliobwagwa kwenye kura za maoni wanaoomba na kubembeleza ili wapewe nafasi ya kugombea udiwani na ubunge kupitia Chadema hawana nafasi hiyo, hii ni kwa sababu wengi hawaaminiki na wakifanikiwa hawachelewi kujiuza kwa bei ya kutupwa.

Binafsi naunga mkono msimamo huo wa kikakamavu
 
Safi sana kamanda Rosse Mayemba...hatuhitaji mamluki ndani ya chadema aisee ..yaliyotukuta kwenye hama hama hii ni fundisho tosha ...alafu kwa sasa chadema tunajitosheleza kiukweli ndo maana tumeanza sisi ndo ccm wakafuatia ..miaka hiyo ndo tulikuwa tunasubiria waliokataliwa ccm tunawaona lulu lkn kwa sasa tuko gado ..waende Nccr Mageuzi
 
Nani mlisikia atakuja Chadema hii ya kilevilevi?
 
View attachment 1520722

Hayo yamesemwa na kamanda Rose Mayemba ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Njombe alipokuwa anaongea na waandishi wa habari.

Amesema kwamba wale mamluki waliobwagwa kwenye kura za maoni wanaoomba na kubembeleza ili wapewe nafasi ya kugombea udiwani na ubunge kupitia Chadema hawana nafasi hiyo, hii ni kwa sababu wengi hawaaminiki na wakifanikiwa hawachelewi kujiuza kwa bei ya kutupwa.

Binafsi naunga mkono msimamo huo wa kikakamavu
Dah wamama wanaibeba chadema vema kabisa. Wamama ni watu wenye misimamo thabiti hadi raha.
 
Sio mtolea tu wa Temeke hata huyu Mtulia wa Kinondoni kaomba arudi cuf ...nasikia wako kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho ili warejee cuf
Kama vidume kweli waombe kwenda ACT ndo tujue kuwa weshawehuka kabisa. Hao ndo "Masaka tonge" kweli kweli
 
View attachment 1520722

Hayo yamesemwa na kamanda Rose Mayemba ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Njombe alipokuwa anaongea na waandishi wa habari.

Amesema kwamba wale mamluki waliobwagwa kwenye kura za maoni wanaoomba na kubembeleza ili wapewe nafasi ya kugombea udiwani na ubunge kupitia Chadema hawana nafasi hiyo, hii ni kwa sababu wengi hawaaminiki na wakifanikiwa hawachelewi kujiuza kwa bei ya kutupwa.

Binafsi naunga mkono msimamo huo wa kikakamavu

Yaani hapa cdm wametembea na matamanio yangu kwa 100%. Hapa ndio najua kweli cdm ni wasikivu. Tena inatakiwa ipitishwe sheria kwenye katiba kabisa, kuwa hairuhusiwi kugombea nafasi yoyote ndani ya cdm bila kukaa ndani ya chama kwa miaka mitano mfululizo. Hao matapeli waende vyama vinavyotegemea mbeleko ya ccm.
 
Back
Top Bottom