CHADEMA Nyomi si Habari Tena, Tujidhatiti kumaliza Mchecho

CHADEMA Nyomi si Habari Tena, Tujidhatiti kumaliza Mchecho

Picha imepigwa kihuni mno eto nyomi au mnadanganywa na hiyo horizontal oblique
Nyomi si habari tena, tunajizatiti kumaliza mchezo.

Ya kizenji, chenga twawala imetosha.
 
Efforts zinatakiwa ziwekwe kwenye last step, serious efforts I mean, tusiendelee kuridhika na hii nyomi ambayo imekuwepo kwa miaka mingi, mipango iwekwe hasa kwenye Katiba Mpya na Tume Huru.

So Hiyo ni Nyomi? Na hao Ni wanachama wa CDM?
 
Hivi ni kwa nn eti huitaki katiba mpya?
Sio siitaki, mie naongelea fact,, chadema wanataka majimbo, yaani mkuu wa mkoa apigiwe kura na wananchi,, ACT wanataka serikali tatu,, ccm wanataka muundo uliopo uendelee,, katiba mpya itapatikana hapo?
 
So Hiyo ni Nyomi? Na hao Ni wanachama wa CDM?

Nyomi si lazima wawe wanachama. Wanachama wako kwenye orodha Nyomi ya hao inajulikana.

Hawa ni wanachama, well wishers, sympathizers, supporters, wanachama nk wakiwamo chawa wa mama.

Wote hao kwenye mapambano tunawahitaji Kwa umuhimu wao.
 
Mikutano ya vyama ni kipimo kizuri kwa mwenye macho kupima nguvu za chama. Hii ni mahsusi kwa chama chenyewe na washindani pia.

Labda hatua hii ilikuwa ni kwenye kuzindua mikutano zaidi. Hata hivyo upepo umeshaonekana na muda wa kwenda kwenye core business ni sasa.

Core business - Katiba Mpya.

Ninakazia bila mpanga mikakati mkuu wa maana, kufika tutafika lakini tukiwa tumepoteza muda mwingi au Kwa taabu zaidi.
Mkuu 'brazaj', nikubali, kuna mambo mengi sana yanawekwa hapa JF kiasi kwamba ni vigumu kila mara kukumbushana yaliyokwishasemwa huko nyuma.

Ni hivi: Swala la Katiba Mpya kabla ya 2025 hilo sahau.

Utakuwa unawaonea tu CHADEMA, ambao kwa kweli hawana njia tena ya kulifanikisha katika muda huu. Hili tulishalijadili humu kwa kina.
Lakini usije ukadhani kwamba Katiba Mpya siyo swala muhimu, ila 'logistics' zake ndiyo tayari zimegota, na Bi mkubwa alishawaweka mfukoni vizuri sana juu ya jambo hilo.

Kwa hiyo, usidhani CHADEMA hawatambui hali hiyo, na pasi shaka ndiyo sababu swala hilo halizungumziwi tena kwenye mikutano hii.

Nitakuelewa vizuri sana ukishikia bango jekundu kabisa lenye kutafuta njia sahihi kabisa za kuhakikisha kwamba uchaguzi 2025, na ule wa serikali za mitaa, hapa mwakani tu; ni lazima uwe wa HAKI na HURU kabisa. Pasiwepo na kura yoyote ya mwananchi inayochezewa kama ilivyokuwa kwenye chaguzi zote zilizokwishafanywa huko miaka iliyopita.
CHADEMA wasipokuwa waangalifu, hata hili watajikuta Bi mkubwa akiwalisha vumbi bila ya wao kujitambua.

Habari ya Katiba Mpya kabla ya 2025, sahau, ila ni wajibu kuhakikisha chaguzi zote zitakazofanyika ni lazima zifuate taratibu za HAKI. Muda wa kutosha upo kuhakikisha hili linawezekana.

Mengi ya haya nilishayaandika humu humu JF.
 
Back
Top Bottom