Mikutano ya vyama ni kipimo kizuri kwa mwenye macho kupima nguvu za chama. Hii ni mahsusi kwa chama chenyewe na washindani pia.
Labda hatua hii ilikuwa ni kwenye kuzindua mikutano zaidi. Hata hivyo upepo umeshaonekana na muda wa kwenda kwenye core business ni sasa.
Core business - Katiba Mpya.
Ninakazia bila mpanga mikakati mkuu wa maana, kufika tutafika lakini tukiwa tumepoteza muda mwingi au Kwa taabu zaidi.
Mkuu 'brazaj', nikubali, kuna mambo mengi sana yanawekwa hapa JF kiasi kwamba ni vigumu kila mara kukumbushana yaliyokwishasemwa huko nyuma.
Ni hivi: Swala la Katiba Mpya kabla ya 2025 hilo sahau.
Utakuwa unawaonea tu CHADEMA, ambao kwa kweli hawana njia tena ya kulifanikisha katika muda huu. Hili tulishalijadili humu kwa kina.
Lakini usije ukadhani kwamba Katiba Mpya siyo swala muhimu, ila 'logistics' zake ndiyo tayari zimegota, na Bi mkubwa alishawaweka mfukoni vizuri sana juu ya jambo hilo.
Kwa hiyo, usidhani CHADEMA hawatambui hali hiyo, na pasi shaka ndiyo sababu swala hilo halizungumziwi tena kwenye mikutano hii.
Nitakuelewa vizuri sana ukishikia bango jekundu kabisa lenye kutafuta njia sahihi kabisa za kuhakikisha kwamba uchaguzi 2025, na ule wa serikali za mitaa, hapa mwakani tu; ni lazima uwe wa HAKI na HURU kabisa. Pasiwepo na kura yoyote ya mwananchi inayochezewa kama ilivyokuwa kwenye chaguzi zote zilizokwishafanywa huko miaka iliyopita.
CHADEMA wasipokuwa waangalifu, hata hili watajikuta Bi mkubwa akiwalisha vumbi bila ya wao kujitambua.
Habari ya Katiba Mpya kabla ya 2025, sahau, ila ni wajibu kuhakikisha chaguzi zote zitakazofanyika ni lazima zifuate taratibu za HAKI. Muda wa kutosha upo kuhakikisha hili linawezekana.
Mengi ya haya nilishayaandika humu humu JF.