Waberoya, najua sana unakotaka kwenda na usijali sina tatizo na hilo, feel free kunikosoa pale utakapoona napotosha jambo ila naomba nikutoe hofu, mimi naamini chama ni zaidi ya mtu. Chama kama nilivyowahi kusema zamani na sijabadilika, Chadema ni zaidi ya Mbowe, zaidi ya Slaa na mpaka dakika hii naamini unless otherwise ni zaidi ya Lowassa kama ilivyokuwa zaidi ya Zitto.
Tofauti yangu na wewe labda iko kwenye tafsiri ya matakwa na malengo. Naamini kwa mfano wana CCM ni watu tu wa kawaida kama mimi na wewe, kinachotutofautisha ni UCCM wao, period. Mkapa alipokuwa akinadiwa na Mwalimu, tulishuhudia Mwalimu akizunguka kila pembe ya nchi akituaminisha kuwa ndani ya CCM kwa wakati huo hakuna kama Mkapa, bila shaka utawala wa kishkaji wa Mwinyi ulichangia kwa kiasi kikubwa.
Lakini Mkapa kama ilivyokuja kutokea, hakuweza kuwa juu ya Chama, huo uwezo labda alikuwa nao Mwalimu tu na sababu ni kwamba wakati wake mfumo wetu ulikuwa wa chama kimoja na kuiasi CCM wakati huo kulitafsiriwa kama uhaini dhidi ya taifa. Wakati tunaingia katika mfumo wa vyama vingi tayari CCM ilishatekwa haikuwa tena chama cha wakulima na wafanyakazi...kuliongezeka kundi la mabepari, wafanya biashara.
Mr Clean Mkapa hangeweza kubaki msafi kama kila anapogeuka kazungukwa na wachafu na hivyo ili aendelee kuwa moja wao lazima akubali kuchafuka. Mwalimu aligutuka na akaanza kupingana wazi wazi na aliyekuwa kipenzi chake kitendo ambacho kilisababisha asiushuhudie uchaguzi uliofuata mwaka 2000. Watu wanapodai ndani ya CCM wako watu wasafi, mimi huwauliza usafi wa Mkapa uliishia wapi?
Ndani ya CCM kuna ndugu zetu, rafiki zetu, wazazi wetu, watoto wetu, babu zetu na wajukuu zetu lakini kitu kinachowaunga pamoja na kuwa na mshikamano wa pamoja ni UCCM. Ukiwavua UCCM wanabaki binadamu tu kama sisi wengine...jiulize ni kitu gani kinamtuma polisi ampige ndugu yake wa kuzaliwa kama mbwa mwizi kwa kudai tu haki mbele ya sheria? Hapana
Waberoya adui wetu nambari one ni CCM.
Mtu yeyote atakayeongeza nguvu katika kumshinda huyu adui CCM kwangu ni rukhsa na mtu yeyote atakayehusishwa na njama za kudhoofisha nguvu hizo dhidi ya adui CCM kwangu si rukhsa. Nafikiri kwa kiasi fulani utakuwa umenielewa ndugu yangu; adui wa adui yangu ni rafiki na vivyo hivyo rafiki wa adui yangu ni adui na hapo sina mjadala. Chama ni zaidi ya mtu na ninachopiga vita ni mfumo unaonifitini na ndugu yangu...basi.