Haya Sumaye huyoo ndani ya nyumba! Alafu anasema ukaskazini
Hawa jamaa wameshavurugana! Ila safari hii ndo wanaishia. Sikonge na Bunda ni tip of the iceberg. Bado sasa mvurugano wa CUF bara!
Lack of long term strategy and vetting of some of these folks! They are going for short term gains and even awed with some sensational 15 seconds of fame rather than clear conscious and strategy.
Hapakuwa na haja kumharakisha Bulaya au Nkumba wagombee, tayari kulikuwa na watu waliojijenga kwa muda mrefu ndani ya chama...same rule applies to EL when it comes to Slaa.
Sasa hivi with Mngeja, Guninita and others party stalwarts crossing the river, Chadema kitabadilika sana in 2-3 years. Ile Upinzani makini kutoka ndani ya CCM will now starting shaping up maana ndani ya CCM kuna vita kubwa ya kiitikadi, maslahi, generational difference na hata personalities.
Hii dhana na kulazimishana "Umoja ni Ushindi" will not survive for that long especially kama Mkapa na Kikwete still have significant say ndani ya Chama.
Kuna majeruhi wa Kichama na Kiitikadi na hata walionyimwa fursa kutokana na mizengwe.
Hopefully Magufuli will stand by his first promise "Umoja wa Kitaifa" na aanze aggressively kusafisha Chama Sekretarieti na Kamati Kuu ambazo ndio kidogo anaweza kuwa na nguvu kuleta msukumo na mabadiliko ya kweli anayoyataka yatokee katika Serikali yakisukumwa na kuhakikiwa na Chama.
CCM sasa ni lazima iendelee kumeguka (si suala la ufisadi tuu au kigezo cha ufisadi), fursa hii imeanza na Lowassa, wenyeviti wa mikoa wabunge wachache na sasa Sumaye.
Kuna makapi wanaokimbilia uchaguzi, lakini pia kuna wanaoondoka kwa hiari wakijua mfumo wa sasa wa Chama haufai au unahitaji marekebisho na hasa tofauti za kiitikadi na dira ya Chama.
CCM haiewezi kuwa na dira au uimara kama kuna mgongano wa kiitikadi ndani ya chama.
CCM ilianzishwa kusimamia haki za wanyonge, kusimamia utu na kupiga vita utajiri wa kupita kiasi hasa kutokana na viongozi wake.
Azimio la Zanzibar, liliruhusu viongozi kuwa matajiri kupindukia na msuguano kati ya wananchama na wananchi wanaoamini ujamaa na viongozi wanaoamini ubepari, umezaa chuki na ufisadi.
Chadema ni chama cha mabepari, wanaokihama CCM kwa kudiriki leo iwe ni fursa (au tamaa) ya kupata mamlaka na uongozi au ni mvuto wa kuchoka CCM na ni watu wenye mwelekeo wa Kiubepari, watakuwa salama Chadema na huko ndiko itabidi waingize nguvu zao na kushindana na wajamaa (Dr. Slaa na wenzake) ambao waliamini kutumia itikadi za ujamaa walipoanza wimbi la kuing'oa CCM kupiga kelele za Ufisadi (UTAJIRI).
Yetu macho.