CHADEMA sasa itakuwa na kadi za aina 5 za uanachama zitakazolipiwa viwango tofauti kwa mwaka

CHADEMA sasa itakuwa na kadi za aina 5 za uanachama zitakazolipiwa viwango tofauti kwa mwaka

1.Kadi ya bluu (2500) kwa mwaka

2. Kadi ya fedha (25,000) kwa mwaka

3. Kadi ya dhahabu (50,000) kwa mwaka

4. Kadi ya Platnum (100,000) kwa mwaka

5. Kadi ya Almasi (200,000) kwa mwaka

Huu ndio mpango mpya utaowezesha chama kujiendesha kwa mapato yake chenyewe badala ya pesa za ruzuku ambazo CHADEMA ilishazikataa kitambo kwa vile hazikuwa za halali.

MUHIMU SANA : Pamoja na kadi hizo kuwa na viwango tofauti lakini hadhi ya wanachama wote ni sawa , viwango tofauti vimewekwa kwa ubunifu tu ili kuongeza mapato ya Chama yatayowezesha kijiendeshe bila kukwama .

Ombi : Chadema ituwekee utaratibu sisi wengine tulio na uwezo wa kulipa zaidi ya hivyo viwango vyao hata kwa kutuandalia risiti maalum bila hata kubadilisha viwango vilivyowekwa , Kwa mfano naweza kulipa milioni 3 lakini nikaomba nipewe kadi ya bluu ambayo ada yake kwa mwaka ni 2500/= tu

View attachment 1800416
This is fine idea
 
Kwa muda wa miaka 5 chadema imekuwa ikipokea ruzuku ya zaidi ya sh million 400 kila mwezi na kuwakata wabunge wake wapatao zaidi ya 70 kila mmoja sh 1.5 million kila mwezi kutoka kwenye posho zao za ubunge. Pia ilikuwa ikitembeza bakuli la michango mara kwa mara kwa wanachama wake. Pesa zote hizo hazikuweza kuifanya chadema kuweza kujitegemea. Ilibaki masikini wa kutupwa hadi kushindwa kujenga nyumba ya makao makiu yake na kubaki kupanga kwenye kijumba kinachofanana na kakibanda ka kuku wa kienyeji.

Huo mpango wake wa ada ya kila mwaka kwa wanachama wake itakayokuwa ikilipwa kidijitali aka mpesa, tigopesa na airtel money, makusanyo yake kwa mwaka nina uhakika hayatazidi posho ya miezi miwili ya ubunge wa Mh. Halima Mdee! Subiri tutaona. Acheni kujidanganya.
Mbowe kaishia kununua Jumba Dubai.

Makamanda wamebaki kupiga miayo tu.
 
Ila tuache kujidanganya kwa maneno. Yaani wa 2500/= awe na thamani sawa na wa 200,000/= ktk maamuzi ya chama?. Labda sio weusi sisi.
 
Chama Cha kibaguzi sana hiki

Hayo madaraja ya Nini kama wote ni binadamu??

Huku CCM wote tunalipa ada moja, uwe Rais au Mkulima ada ni Moja.

Haya Watanzania nendeni Chadema mkabaguliwe.
Kwamba mwenye kadi ya Almasi atakuwa anapata upendeleo gani kulingajisha na mwenye ya fedha?
 
Amefeli wapi huyu jamaa.
Kadi ziwe uniform
Lakini michango watu watoe kulingana na kile wanacho

Huyu wa kadi buku 2 na jero hata tu ukaaji kwenye kikao yuko mbali achilia mawazo sisi wengine sio washabiki wa siasa ila tunaona mgawanyiko UNAKUJA

Sembuse tu watu wavisha cover ya Iphone simu ya Techno . Hili la kadi hata kuonyesha ile ya blue mbele ya platinum au Diamond utaona aibu.

Hii ni dalili chama kinakuwa si cha wanyonge tena.

Mkuu hayo mawazo ni ya mtu mmoja au?
 
upumbavu, ndio wachaga wahini kuchukua hizo kadi,chama la kikabila hilo nani ajiunge nalo ushenzi tu
 
Amefeli wapi huyu jamaa.
Kadi ziwe uniform
Lakini michango watu watoe kulingana na kile wanacho

Huyu wa kadi buku 2 na jero hata tu ukaaji kwenye kikao yuko mbali achilia mawazo sisi wengine sio washabiki wa siasa ila tunaona mgawanyiko UNAKUJA

Sembuse tu watu wavisha cover ya Iphone simu ya Techno . Hili la kadi hata kuonyesha ile ya blue mbele ya platinum au Diamond utaona aibu.

Hii ni dalili chama kinakuwa si cha wanyonge tena.

Mkuu hayo mawazo ni ya mtu mmoja au?
Wahini mkajenge chama lenu lililojaa ukabila 100%
 
1.Kadi ya bluu (2500) kwa mwaka

2. Kadi ya fedha (25,000) kwa mwaka

3. Kadi ya dhahabu (50,000) kwa mwaka

4. Kadi ya Platnum (100,000) kwa mwaka

5. Kadi ya Almasi (200,000) kwa mwaka

Huu ndio mpango mpya utaowezesha chama kujiendesha kwa mapato yake chenyewe badala ya pesa za ruzuku ambazo CHADEMA ilishazikataa kitambo kwa vile hazikuwa za halali.

MUHIMU SANA : Pamoja na kadi hizo kuwa na viwango tofauti lakini hadhi ya wanachama wote ni sawa , viwango tofauti vimewekwa kwa ubunifu tu ili kuongeza mapato ya Chama yatayowezesha kijiendeshe bila kukwama .

Ombi : Chadema ituwekee utaratibu sisi wengine tulio na uwezo wa kulipa zaidi ya hivyo viwango vyao hata kwa kutuandalia risiti maalum bila hata kubadilisha viwango vilivyowekwa , Kwa mfano naweza kulipa milioni 3 lakini nikaomba nipewe kadi ya bluu ambayo ada yake kwa mwaka ni 2500/= tu

View attachment 1800416
Pamoja na kuwa wazo zuri la kuingizia pato kwenye chama, lakini hizi ni 'Hisa" kwenye chama. Wenye hisa kubwa watadai sauti kubwa zaidi ndani ya chama, hili haliepukiki.

Huku ni kuweka matabaka ndani ya chama, ambako kutawasababishia matatizo tu mbele ya safari.

Yeyote mwenye mapenzi mema ya chama, hahitaji kuwa na kadi maalum kukichangia chama.
 
Tumefanya utafiti mnene sana na tumejiridhisha kwamba mfumo huu ni mzuri na hakuna hata mmoja atakayekuwa na hisa , Kamati kuu ilichambua mambo yote hayo , na labda nikustue , wajumbe wengi wa Kamati kuu wana kadi ya Bluu
 
Haijalishi mkuu Erythro.

Kuwa na kadi za wanachama za aina hiyo, hayo ni matabaka tayari ndani ya chama, tuache masihara pembeni kabisa!
Kuchangia chama hakuhusiani kabisa na kuwa na kadi hizo za utambulisho. Anayekijali chama na anajua umuhimu wa kutatua tatizo linalokihusu chama, hahitaji kuwa na kadi ya utambulisho wa kipekee wa aina hiyo.
 
Back
Top Bottom