CHADEMA sasa itakuwa na kadi za aina 5 za uanachama zitakazolipiwa viwango tofauti kwa mwaka

This is fine idea
 
Mbowe kaishia kununua Jumba Dubai.

Makamanda wamebaki kupiga miayo tu.
 
Ila tuache kujidanganya kwa maneno. Yaani wa 2500/= awe na thamani sawa na wa 200,000/= ktk maamuzi ya chama?. Labda sio weusi sisi.
 
Chama Cha kibaguzi sana hiki

Hayo madaraja ya Nini kama wote ni binadamu??

Huku CCM wote tunalipa ada moja, uwe Rais au Mkulima ada ni Moja.

Haya Watanzania nendeni Chadema mkabaguliwe.
Kwamba mwenye kadi ya Almasi atakuwa anapata upendeleo gani kulingajisha na mwenye ya fedha?
 
Amefeli wapi huyu jamaa.
Kadi ziwe uniform
Lakini michango watu watoe kulingana na kile wanacho

Huyu wa kadi buku 2 na jero hata tu ukaaji kwenye kikao yuko mbali achilia mawazo sisi wengine sio washabiki wa siasa ila tunaona mgawanyiko UNAKUJA

Sembuse tu watu wavisha cover ya Iphone simu ya Techno . Hili la kadi hata kuonyesha ile ya blue mbele ya platinum au Diamond utaona aibu.

Hii ni dalili chama kinakuwa si cha wanyonge tena.

Mkuu hayo mawazo ni ya mtu mmoja au?
 
upumbavu, ndio wachaga wahini kuchukua hizo kadi,chama la kikabila hilo nani ajiunge nalo ushenzi tu
 
Wahini mkajenge chama lenu lililojaa ukabila 100%
 
Pamoja na kuwa wazo zuri la kuingizia pato kwenye chama, lakini hizi ni 'Hisa" kwenye chama. Wenye hisa kubwa watadai sauti kubwa zaidi ndani ya chama, hili haliepukiki.

Huku ni kuweka matabaka ndani ya chama, ambako kutawasababishia matatizo tu mbele ya safari.

Yeyote mwenye mapenzi mema ya chama, hahitaji kuwa na kadi maalum kukichangia chama.
 
Tumefanya utafiti mnene sana na tumejiridhisha kwamba mfumo huu ni mzuri na hakuna hata mmoja atakayekuwa na hisa , Kamati kuu ilichambua mambo yote hayo , na labda nikustue , wajumbe wengi wa Kamati kuu wana kadi ya Bluu
 
Tumefanya utafiti mnene sana na tumejiridhisha kwamba mfumo huu ni mzuri na hakuna hata mmoja atakayekuwa na hisa , Kamati kuu ilichambua mambo yote hayo , na labda nikustue , wajumbe wengi wa Kamati kuu wana kadi ya Bluu
Haijalishi mkuu Erythro.

Kuwa na kadi za wanachama za aina hiyo, hayo ni matabaka tayari ndani ya chama, tuache masihara pembeni kabisa!
Kuchangia chama hakuhusiani kabisa na kuwa na kadi hizo za utambulisho. Anayekijali chama na anajua umuhimu wa kutatua tatizo linalokihusu chama, hahitaji kuwa na kadi ya utambulisho wa kipekee wa aina hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…