CHADEMA si chama cha wananchi, ni kikundi tu cha watu wanaotaka kushika madaraka

UPUUZI MTUPU!!!

 
Si bi kikundi tu cha watu !!. Sasa matumizi makubwa ya PT ya nini ?!

Pili hicho kikundi si ni wananchi ?! Au ni mbuzi !!
 
Reactions: BAK
Hiki si chama tawala bali ni genge la wahuni, majizi na wauaji. Unatawala nchi yenye utajiri mkubwa na pia imepewa misaada na mikopo ya trillions kwa miaka chungu nzima halafu hakuna chochote kile cha KUJIVUNIA!!!
Hakuna chama cha siasa Tanzania kilichojipanga na kuweza kuchukua nchi kwasasa

Na kwa hizi mbinu za CHADEMA kwasasa ndio sioni any posibility



CCM bado itaendelea kutawala.
 
Chama kinachotaka madaraka lazima kionyeshe kuwa kina sera bora kwa maneno na vitendo. Ukipata madaraka unaweza usizitende, lakini anayetaka madaraka hayo ni muhimu sana.
 
Akili za kushikiwa hizi au akili za ZWAZWA. Watanzania kama wewe ni hasara kubwa sana kwa Taifa. Chadema haijui shida za Watanzania lakini hao walio madarakani wanaozijua shida za Watanzania wapo madarakani kwa miaka 60 lakini shida za Watanzania zinazidi kukithiri kila kukicha. Elimu ya hovyo, huduma muhimu maji, umeme na afya ni za hovyo na ajira hakuna kabisa wenye ajira mishahara haiendani na gharama za maisha.

ACHA KUKURUPUKA NA KUANDIKA UPUMBAVU.

Na watu wa hivi hufikiri kuwa tatizo la nchi ni wao kutoshika madaraka. Kama vile wakishika madaraka kila shida itaondoka. Hawajui shida ya mwananchi wa kawaida.
 
Kama hakina sera bora kwanini maccm WANAHOFIA uchaguzi huru naweza haki? Acha kuonyesha ujuha wako hadharani!!!
Chama kinachotaka madaraka lazima kionyeshe kuwa kina sera bora kwa maneno na vitendo. Ukipata madaraka unaweza usizitende, lakini anayetaka madaraka hayo ni muhimu sana.
 
Hiki si chama tawala ni genge la wahuni, majizi na wauaji ambao wanapora chaguzi kwa mtutu wa bunduki kwa kujua fika kwenye uchaguzi huru na wa haki HAWATAAMBULIA chochote kwa jinsi wanavyochukiwa na Watanzania. Ni chama kinabebwa na polisiccm na mahakama ili kung’ang’ania madarakani.

Hakuna chama cha siasa Tanzania kilichojipanga na kuweza kuchukua nchi kwasasa

Na kwa hizi mbinu za CHADEMA kwasasa ndio sioni any posibility



CCM bado itaendelea kutawala.
 
Chadema ni chama cha siasa sio chama cha wakulima au wafanyakazi na lengo la chama cha siasa ni kushika dola.

Hao wafanyakazi na wakulima watatetewa na vyama vyao.
 
Bull crap!! Mleta mada, maadamu umetoa vipimo na mizani ya kuwa chama cha wananchi - hebu tupe mifano ya vyama vya wananchi kwa kuonesha matendo kama maandamano kwa ajili ya jambo lolote la wananchi. Kwa ufupi, nipe mambo ya CCM na UDP!

Nikukumbushe kuwa una haki ya uhuru wa mawazo lakini mawazo binafsi hayawezi kuwa ni kipimo kwa umma. Nikukumbushe tu kuwa UDP, ADC, CCM na wengine vimeandikishwa kisheria kama vyama vya siasa na vina hadhi sawa kisheria - tofauti ni kuwa CCM ndio inaongoza serikali na CCM inapenda madaraka sawa sawa na walio nje ya madaraka!! Madaraka ni lengo kuu la chama cha siasa! Ni kwa sababu, utekelezaji wa mrengo wowote wa chama cha siasa hutokana na madaraka!!! Sioni ukiweza kujifunza hata hili. Ndio ninyi mnasema “ni wanaharakati”. Ukiamini dhana au jambo na kulipigania - unafanya harakati. Harakati ni jambo muhimu kwa yeyote asiye na madaraka. Harakati ni kutaka kuibua jambo na kutaka lisikilizwe na kufanyiwa kazi na walio na mamlaka au madaraka!! Bila hatakati - mwenye mamlaka au madaraka anakosa kusimamiwa!!

Jamii Forum imeishiwa great thinkers. Haki ya kutoa taarifa inaanza kuwa haki ya kusema lolote kwa msingi wa uhuru wa kupata au kutoa taarifa na sio tena ueledi, ukweli!!

So sad!!
 
Chadema ni chama cha siasa sio chama cha wakulima au wafanyakazi na lengo la chama cha siasa ni kushika dola.

Hao wafanyakazi na wakulima watatetewa na vyama vyao.
Kwani walipokuwa wanapambana na mafisadi walikuwa ni TAKUKURU?
 
Kwani walipokuwa wanapambana na mafisadi walikuwa ni TAKUKURU?
Hiyo ilikuwa njia ya kuwashawishi wapiga kura kuwa wakichaguliwa watapambana na hilo jinamizi.

Kasome kazi ya vyama vya siasa acha kuwatwisha majukumu yasiyowahusu.
 
Huo ni mtazamo wa Little Red , ninauheshimu mtazamo wako. 😂
 
Tuache ujinga sasa.
Kama CHADEMA siyo chama cha siasa kwa nini Msajili hajakifuta?

CCM tujipange kurejesha matumaini ya wananchi tuache visingizio kwamba tunakwama kwa sababu ya hao CHADEMA


Neno Utawala Bora kwa tafsiri ya Tanzania maana yake ni ulinzi wa Rais awapo madarakani. Tunahitaji reforms tujenge taasisi imara tena tujenge utamaduni wa ukuu wa sheria hapo tunaweza kusema we have a country inayoendana na haiba ya demokrasia.

Vita vya kusaka madaraka ndani ya CCM imetuletea majanga na ukatili mkubwa kidemokrasia
 
Hivi maana halisi ya chama cha siasa ni ipi? Kuna mahali katika ufafanuzi wa maana ya kinachoitwa chama cha siasa utakosa kugusa kitu kinaitwa "kikundi?"

Hivi CCM sio kikundi cha watu kinachounda dola? Mbona uko mweupe sana kichwani? Tuna safari ndefu sana kukomboa fikra zetu.

Nikurudishe shule kidogo: "Define what is a political party."
 
Chama cha Siasa sio NGO ya kupigania Haki za wafugaji au wavuvi, wajibu namba moja wa Chama cha Siasa ni kushinda chaguzi na kuingia madarakani ili kikatekeleze Sera zake, na kwenye Sera ndio utakuta utetezi wa hayo makundi yote katika jamii.

Ukiona MTU anafikra kuwa CHADEMA kikawe kikundi cha kutetea wauza vitumbua ,hajui wajibu wa Chama cha Siasa, huyu washauri CCM !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…