Kwa taarifa yako hata CCM sio chama makini, kipo madarakani hadi hii leo sio kwasababu ya umakini wake, bali ni kwa sababu za kihistoria, katiba ya mfumo wa chama kimoja, tume isiyo huru ya uchaguzi, na uoga wa wananchi. Hiyo migogoro michache unayoiona ndani ya vyama vya upinzani, hata CCM ipo, ila kwakuwa CCM inafaidika na uwepo wake madarakani ndio maana unataka kudhani CCM ni chama makini. Siku CCM ikitoka madarakani pamoja na ukubwa wake, itakufa kirahisi mno kama ilivyokufa KANU ya Kenya. Unapoona chama kimekaa madarakani zaidi ya miaka 50, lakini inategemea tu nguvu ya dola kukaa madarakani, basi ujue hicho sio chama.