CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Tuanze na kwenye red: Unaamini kwa sasa Wapinzani wana nguvu? Ndani ya week mbili Lowassa kabadili karibu kila kitu - unchallenged! Huoni kama sasa ni mfalme?

Kwenye blue: Ni kweli hatumii gharama yoyote CDM/UKAWA?

Hawana nguvu. Wangekuwa na nguvu wangetangaza mgombea wao kabla ya CCM. Lakini wakasubiri makapi (Iwapo Lowassa atashindwa) au Jiwe la pembeni walilokaa wajenzi (iwapo atashinda).

Atakuwa ametumia gharama. Lakini ni ndogo sana ukilinganisha na zile alizotumia akiwa CCM. Toka 1995 mpaka alipojiunga CDM ametumia kiasi gani?
 
Katika sakata hili la Lowassa kuhamia Chadema kuna vitu vya kuzingatia;

1. Mpaka sasa hakuna yeyote anayejadili sera ya kilimo, elimu , afya , miundombinu, uwekezaji , mambo ya nje, ulizi na usalama, michezo na utamaduni, hali ya hewa, nishati na madini, muungano na mambo mengine muhimu kwa taifa.
Hili ni kosa, lakini si kubwa sana kwa vile ilani za uchaguzi hazijaanza kutangazwa.
Hata hivyo, hapa tunajifunza kuwa ratiba ya kuchagua mgombea kabla ya kuwa na ilani sio sahihi. Inafanya mijadala ijikite kwenye personalities rather than real issues.

2. Kila upande unaweza kuathirika au kunufaika na maamuzi ya Lowassa kwenda Chadema kama ifuatavyo;
i) CCM
Faida
a) Kupunguza lawama za kuitwa chama cha mafisadi. Chadema wameshaanza kuondoa neno ufisadi na mafisadi kwenye kauli zao. Kauli yao mpya ni kubadili mfumo. Hata hivyo bado Chadema wana kibarua cha kuelezea wataubadili vipi mfumo kwa sababu mfumo sio chama cha siasa.

b) Kutoa fursa kwa wanasiasa wasio waaminifu kwa chama kukikimbia na kuacha wale walio tayari kukipigania chama. Rafiki wa kweli hujulikana kipindi cha changamoto.

c) Kupata fursa ya kuingiza wimbi kubwa la mamluki ndani ya upinzani kwa kisingizio cha kumfuata Lowassa. Hawa watapewa hero's welcome na kuaminiwa kirahisi.

Hasara
a) Siri zake za maandilizi ya uchaguzi zitafahamika kwa upinzani. CCM italazimika kufanya mabadiliko makubwa kwenye mikakati jambo ambalo litakigharimu chama.

b) Kupoteza baadhi ya watu ambao fundamentally wanaamini Lowassa ndio mtu pekee nchini mwenye uwezo na haki wa kuongoza. Ingawa kundi hili ni la watu wasielewa maana ya chama lakini lipo. Hawa wstamfuata Lowassa kokote anakoenda, wanasema "ulipo, tupo". Mrema alikuwa na watu wapatao 200,000 kwenye kundi kama hili. Lowassa anaclaim kuwa anao milioni moja. Hata hivyo inahitajika utafiti zaidi kuthibitisha idadi hii.

i) Chadema
Faida
a) Kupata mgombea tajiri ambaye ni high profile politician.

b) Kupewa siri za CCM.

c) Kupokea wafuasi wa Lowassa.

d) Kuongeza uhalali wake wa kuwa chama kikuu cha upinzani na kuweza kupata nguvu ya kusikilizwa Zanzibar. Lowassa ana wafuasi Zanzibar ambako Chadema hushindwa kuwa hata nafasi ya tatu kwenye uchaguzi.

Hasara
a) Kujenga sura ya kuthamini umaarufu na pesa kuliko misingi ya Chama.

b) Kukiri de facto kuwa hawakuwa na uwezo wa kuishinda CCM. Hapa watahojiwa je mtu mmoja ndio amewaletea uwezo? Je , kama mtu huyo ana nguvu kubwa kuliko Chama, mtamdhibiti vipi akiwageuka huko mbeleni?

c) Kuwakatisha tamaa wanaojitolea kwa ajili ya Chama. Kitendo cha Slaa kukatwa na kutokusikilizwa kitawafanya watu kama kamanda Mawazo wakae chini na kutafakari kazi wanayojitolea inalenga kubadili nini? Wengi wa wanaojitolea kwa nia njema huongozwa na misingi na itikadi ya Chama. Chama kinapotoka nje ya misingi , kinahatarisha kupoteza au kuwavunja nguvu watu hawa.

d) Kupunguza kuaminiwa na wananchi. Sura iliyojengeka ni kuwa Chadema inacheza tu mchezo wa siasa na hailengi hasa kuboresha maisha ya mtanzania. Mtu yeyote anayewapa pesa za uchaguzi watamtukuza ilimradi tu washinde. Kauli hizi za Mbowe hazijapokelewa vizuri na watanzania.

e) Kutumia nguvu kubwa kusambaza ujumbe mpya. Siku zote inafahamika ujumbe wa chadema ni kupinga mafisadi. Sasa kuna mabadiliko, tatizo sio mafisadi ila mfumo. Hii itahitaji resources nyingi kuwaeleza watu mpaka waikubali. Kwahiyo muda wa kuzungumzia masuala mengine ya maisha ya kila siku utakuwa mdogo kuliko wa kufafanua mabadiliko haya ya msimamo. Hii inaatarisha Chadema kuonekana Chama kinachotafuta madaraka bila kuwa na mkakati wa kuongoza nchi na kuboresha maisha.

f) Iwapo Chama hakitashinda uchaguzi kitakosa misingi ya kukiendeleza. Kitabaki kuonekana chama cha wajanjawajanja. Watu wa Lowassa ambao wameahidiwa vyeo serikalini itabidi watake vyeo kwenye Chama. Chama kitachukuliwa na watu wasiokijua wala kukijali kwa dhati.

Pamoja na kwamba watu hudhani siasa ni mchezo, lakini siasa ni taaluma. Katika haya yanayoendelea, mwenye taaluma zaidi ndiye atayejipatia faida zaidi kuliko hasara.

Sisi kama watanzania tunachotakiwa kuomba ni Mungu aendelee kuilinda nchi yetu iwe na amani na umoja kama taifa.
 
IMG-20150731-WA0009.jpg
Kiukweli kabisa Lowassa ni risk sana kwenye kuwapasua CDM hasa kama swala la Dr.Slaa halijawa handled with care, na linaweza kuhatarisha zaidi kuliko faida, mm naomba nichangie mambo yafuatayo kwa mtazamo wangu,

1. Mm kimsingi nilipinga kabisa Lowassa kuhamia CDM na kugombea, nikipenda zaidi ahamie na kuwa nomarl part member na kuwasaidia UKAWA kwenye mapambano, lakini kama mnavyojua wengi wa viongozi waliona Lowassa ni fursa kwao japo ni fursa yenye mashaka makubwa wakaamua kugamble na kuitumia.
Kiukweli hakuna yyt ambae haoni impact iliyotokea CCM kwa kuondoka huyu Bwana, na ninadhani kama UKAWA wakishikamana angalau Bunge wanawezq kukamata, na ninadhani hiyo ndio target yao kubwa.

2. Dr.Slaa, huyu alitakiwa from begining ya makubaliano na EL awe clear na akubaliane na wenzake wote kama kweli wanasema walifanya vikao kadhaa kabla ya kumualika rasmi, na kama alikubali au kushawishiwa kwenye vikao mpaka akakubali basi sioni kama kutakua kuna shida yyt zaidi ya hizi porojo za kila siku kumuhus. kimsingi yeye ndio devide Factor kubwa ambayo ndio naiona kwa sasa, wakimuhandle kwa busara na yeye kuamua kufunika kombe mwanaharamu apite angalau tunaweza kuona matunda kidogo kwenye uwekezaji huu wa wenye risk kubwa waliofanya Ukawa.

Laah, akishupaza shingo na kukomalia msimamo wake kwamba hamtaki EL na kwamba hawezi kula matapishi yake, basi kutatokea na anguko kubwa sana kwa UKAWA nawatakua wameharibu hata kidogo walichokijenga, mpaka sasa mm sijajua standing yake baada ya EL kujoin kwamba ataendelea au ataachana na siasa, maana yeye yupo kimya kabisa, zaidi tunasikia tu vurumai za kwenye mitandao na magazeti kuhusu future yake after El envision.

3. Kwa sisi tunaopinga Kuhusu Lowassa, lazima pia tutafakari kwa kina na kwa mapana yake, hawa viongozi wa UKAWA ndio wameshakosea sana kwa kumkaribisha huyu mtu na muda umekwisha, je bora kukosa kabisa mabadiliko hata kama machache kuliko kumtumia EL kufanikisha hili jambo ambalo kwa utashi wao wao wanaona anaweza kuwavusha. Au kuendelea kukomaa na mabadiliko, kwamba mtoto ndio Kanyea Mkono (viongozi wa UKAWA kwa kumkaribisha EL kwenye uraisi) tuusafishe na kusonga mbele kuliko kuukata au kumpiga mtoto, maana ndio keshakosea. Ni fikra tatanishi sana ila ndio hali tuliyopo.

mwisho, mm nadhani ni busara UKAWA kuelewana mapema na kukubaliana katika kutokukubaliana, muda si rafiki tena na jamaa ndio huyo keshapewa bendera ya UKAWA so wayamalize na kusonga mbele, japo wamekosea njia, ila kikubwa kufika hata kama kupita kwa njia ya Pori.

So far sijajua msimamo wa Dr.Slaa maana sijamsikia exactly yeye binafsi akionge, ila kwa minong'ono iloyopo yeye ndio jabari linalogoma Fisadi kuongoza mapambano ya watakatifu kuwatoa mafisadi, kama ni kweli, muda hautoshi nayeye inabidi kwa kipindi kifupi hiki ajitafakari kama sisi (hoja namba 3) kwamba aendelee na msimamo wake ambao principally ni sahihi kabisa na kudhoofisha upinzaji kwenye uchaguzi huu kwa makosa ya wenzake, au apige moyo konde na kuwaunga mkono kibishi kufanikisha angalau kwa uchache kile amekua akikipigania siku zote. Japo sina uhakika kama nilivyosema juu ya msimamo wake juu ya hili jambo maana ni rumours tu ambazo zinazagaa bila uthibitisho wa moja kwa moja wa muhuika.

Hayo ndio maoni yangu wadau, tujadili kwa mustakabali wa taifa letu pendwaTz
 
Mkuu bado kabisa hujanisoma ukanielewa miye? nilishasema wazi wala sii mara moja ya kwamba mimi natazama REALITY na ndicho nachoandika siwezi kuwa OBJECTIVE katika mambo ambayo najua haiwezekani.. Na kama unajua yote hayo uloandika hapo juu, utajengaje matumaini kwa mtu mmoja ambaye ni sehemu ya waloikwamisha nchi hii. Utapandaje mbegu bora juu ya magugu ukategemea kuvuna mavuno bora?

Unamkumbuka Lowassa alivyotupa matumaini juu ya swala la UMEME na MAJI mwaka 2006 ati itakuwa historia tukajenga watu matumaini! Halafu mtu huyu huyu akatuletea Richmond kwa walokuwa wakimfahamu walijua toka mwanzo kuwa tumeliwa! Leo mnakuja jenga tumaini, kumwita yeye ndiye Messi, jamani ushabiki mwingine basi hata uwe na maana. Bacelona hawawezi kumwachia Messi wala kumuuza akachezee Real Madrid lakini wameweza kumwachia Xavi akacheze Arabuni...
 
Mkuu,
Kwenye post zako nyingi hapo nyuma ulicoment kwa reality zako kwamba bora Prof. Lipumba agombee UKAWA sio Dr. Slaa kwamba angalau watafanya vizuri kiasi ( maana ulishawatabiria kushindwa),na ukasem iwapo UKAWA wakimsimamisha Dr.Slaa badala ya pro.Lipumba watapoza zaidi, sasa can u give us a rivised comment based on reality ambae anaweza kuwapatia UKAWA anafuu japo kidogo hawa jamaa kati ya Dr.Slaa, pro.Lipumba na mvamizi Lowassa? Na je based on reality Lipumba au Slaa wanaweza kweli kushindana na kupata ushindi bila Edo kuwaingili??
 
whyareyousosad.gif

I'm soooo sad...!

Wana jukwaa, mimi niliunga mkono Lowassa kujiunga Chadema kwa sababu moja kuu nalo ni kwamba ujio wake utapelekea kudhoofika kwa CCM na kuongezea nguvu upinzani. Niliamini kwa dhati kwamba kabla ya kupokelewa Chadema, viongozi wote wa UKAWA watakuwa wamekaa, wameafiki na kuridhia ujio wake huo. Niliamini na bado ninaamini, pengine kwa makosa, kwamba kama ana nia ya kupeperusha bendera ya UKAWA itabidi apambanishwe kwanza ndani ya Chadema na wagombea wengine. Hii habari ya yeye pekee kuteuliwa, kama ni kweli, imenishtua kidogo.
 
Ni kweli na ndiyo ilikuwa sharti lake la kuhamia na kutoa kale kabilioni 10 ..
 
Ni kweli na ndiyo ilikuwa sharti lake la kuhamia na kutoa kale kabilioni 10 ..
Hapana Susuviri, hilo la kabilioni kumi peleka jukwaa lileee, utapata like nyingi tu. Humu watu hawajadili umbea. Kidogo kidogo naanza kuelewa what is happening, nikipata data kamili sitakuwa mchoyo.
 
Last edited by a moderator:
whyareyousosad.gif

I'm soooo sad...!

Wana jukwaa, mimi niliunga mkono Lowassa kujiunga Chadema kwa sababu moja kuu nalo ni kwamba ujio wake utapelekea kudhoofika kwa CCM na kuongezea nguvu upinzani. Niliamini kwa dhati kwamba kabla ya kupokelewa Chadema, viongozi wote wa UKAWA watakuwa wamekaa, wameafiki na kuridhia ujio wake huo. Niliamini na bado ninaamini, pengine kwa makosa, kwamba kama ana nia ya kupeperusha bendera ya UKAWA itabidi apambanishwe kwanza ndani ya Chadema na wagombea wengine. Hii habari ya yeye pekee kuteuliwa, kama ni kweli, imenishtua kidogo.

Process nzima imeawaliwa na ubabe bila maandalizi ya kutosha.

Ukifuatilia maoni ya wafuasi wa Chadema kwenye itandao utaona Slaa anaemwa kwa kejeli na dharau. Lakini wanaofanya hivyo wanaweza kuwa ni wale mashabiki wa Lowassa ambao amekuja nao. Hawa tangu mwanzo hawakumuunga mkono Slaa.

Pamoja na kwamba kuondoka kwa Lowassa kunaweza kutafsiriwa kama kuigawa CCM, madhara yake ya kuigawa Chadema yameshaanza kuonekana...
 
‘WAFANYAKAZI ULIOSEMA NI HAWA'

WAMEMALIZA KAZI, WANA MKANA MCHANA KWEUPE

LILE KUNDI KUBWA NI LIPI?

Habari hii ni kwa hisani yagazeti la Habari Mwananchi CCM Zanzibar ‘wamteta’ Lowassa - Kitaifa | Mwananchi

Mnaotufutilia hapa duru, tumesema mara nyingi, kundi linalosemwa ni kubwa la Lowassa lipo kweli.
Hata hivyo, si kundi la waumini wa itikadi au falasafa yake, ni wafanyakazi wanaopata mafao auwatarajia

Mmoja wa watu maarufu ndani yaCCM ni mwenyekiti Borafya wa Zanzibar aliyedaiwa kuwakilisha makundi ya wanyeviti watano, Arusha, wakati wa uzinduzi wa mtia nia Lowassa

LEO BORAFYA ANASEMA NINI
Anasema, ''wameachana na Lowassa kwasababu anataka madaraka. Walimpekendekeza kwasababu alifanya kazi nzuriya chama na wameachana naye kwasababu anataka madaraka na hadhani kama kuna mwana CCM atamfuata''

Wakati Borafya anakwendaArusha, alifanya hivyo ili kumpendekeza awe chaguo la CCM na pengine Rais.
Alikwenda kumpa ‘madaraka' leo anasema Lowassa anataka madaraka sana.

Hapa tupanaonyesha uwepo wake Arusha ulikuwa kikazi na si katika kuamini yale ya Lowassa. Hivi huyu si mfanayakazi?

Mwenyekiti wa Geita, Msukuma,alifika kwa helikopta ndani ya uwanja kuanza safari ya matumaini.
Baada ya Dodoma ameonekana akimpokea Magufuli kwa shangwe. Huyu hakuwa mfanyakazi?

Wapi Mgana Msindai, Mgheja nawengine?

Ikumbukwe, wenyeviti ndiyo waliokuwa na ushawishi ndani ya Halamashauri kuu. Kitendo cha jina kutowafikia ni kikubwa.

Wenyeviti wana kikao chao peke yao. Hadi leo hatujasikia wakionyesha kutoridhishwa na mwenendo mzima, kinyume chake ni timu Magufuli

Wenyeviti walichukuliwa na team Lowassa kutokana na ushawishi wao. Kuondoka kwao kungeashiria kuondoka na kundi kubwa.

Leo wapo kimya hakuna aliyejaribu kuzungumza achilia mbali kujiuzulu au kumfuata. Maana yake,wamebaki na kundi lao huko wakiwa na manung'uniko

WAKATI WA KAMPENI
Haijulikani wenyeviti hao watamponda mtu wao au wataugulia maumivu kimya. Hapa napo tuna swali, nani atashawishikundi lile kubwa linalosemwa kumjali mtu wao aliyevuka barabara?

Wako wapi walioongoza safari ya matumaini huko nyuma?

Kundi linalosemwa hata kufikia UKAWA kubadili mwelekeolipo wapi?

Tusemezane
 
Process nzima imeawaliwa na ubabe bila maandalizi ya kutosha.

Ukifuatilia maoni ya wafuasi wa Chadema kwenye itandao utaona Slaa anaemwa kwa kejeli na dharau. Lakini wanaofanya hivyo wanaweza kuwa ni wale mashabiki wa Lowassa ambao amekuja nao. Hawa tangu mwanzo hawakumuunga mkono Slaa.

Pamoja na kwamba kuondoka kwa Lowassa kunaweza kutafsiriwa kama kuigawa CCM, madhara yake ya kuigawa Chadema yameshaanza kuonekana...
Wanachama wa CDM wanamwaminisana Dr Slaa. Hata pale alipokosea , walikuwa tayari kumpa ‘benefit of doubt'

Upo uzi mmoja wengine tulipingana naye kwa jibu lake moja kutoka kwa mtua liyekuwa na hoja ya msingi.
Hapo ndipo tuliamini wanachama wanampenda. Tulishambuliwa kwa maneno

Ulichosema ni sahihi kabisa.Ujio wa Lowassa una watu wake ambao ni wazuri sana wa kutumia mitandao.
Ndio waliomjenga hadi kufikia mahali CCM ikatetereka.

Hao wasingependa kingine zaidi ya kuhakikisha hakuna kikwazo. Na ndio wanafanya kazi

Tuliwahi kusema kuwa. je, ujio wake utakuwa wa kwake mwenyewe au utaambatana na mizigo.

Na lini mgeni akaambiwa aache mizigo nje aingie ndani
!!

Mvua ni neema, lakini pia hujana mafuriko ikiwa ni pamoja na upepo unaoezua mapaa

CCM wapo salama sana, tatizo walililokuwa nao wamefanikiwa kulihamishia Chadema kwa upole na unyenyekevu.

Hali ndani ya CDM si shwari hata kama kuna ‘denial'
 
whyareyousosad.gif

I'm soooo sad...!

Wana jukwaa, mimi niliunga mkono Lowassa kujiunga Chadema kwa sababu moja kuu nalo ni kwamba ujio wake utapelekea kudhoofika kwa CCM na kuongezea nguvu upinzani. Niliamini kwa dhati kwamba kabla ya kupokelewa Chadema, viongozi wote wa UKAWA watakuwa wamekaa, wameafiki na kuridhia ujio wake huo. Niliamini na bado ninaamini, pengine kwa makosa, kwamba kama ana nia ya kupeperusha bendera ya UKAWA itabidi apambanishwe kwanza ndani ya Chadema na wagombea wengine. Hii habari ya yeye pekee kuteuliwa, kama ni kweli, imenishtua kidogo.

Mag3:

There we go. Lowassa anasema CCM ilimnyima haki kwa kundi la viongozi kumteua Magufuli. Lakini process hiyo hiyo imetumika CDM/UKAWA. Hapa na mimi naona something is fishy.

Vilevile kama Dr. Slaa hakuwa na ridhaa kwa process hiyo, na mimi nitaanza kupunguza support zangu za hatua yake kwenda CDM.
 
Lowassa ni risk kwa CDM, kama swala la Dr.Slaa halijawa handled with care, linaweza kuhatarisha kuliko faida

1. Mm kimsingi nilipinga kabisa Lowassa kuhamia CDM na kugombea, nikipenda zaidi ahamie na kuwa nomarl part member na kuwasaidia UKAWA kwenye mapambano, lakini kama mnavyojua wengi wa viongozi waliona Lowassa ni fursa kwao japo ni fursa yenye mashaka makubwa wakaamua kugamble na kuitumia.

Kiukweli hakuna yyt ambae haoni impact iliyotokea CCM kwa kuondoka huyu Bwana, na ninadhani kama UKAWA wakishikamana angalau Bunge wanawezq kukamata, na ninadhani hiyo ndio target yao kubwa.
Mkuu suala la Dr Slaa halinanamna ya ku-handle isipokuwa busara zake.
Na wala hakuna jibu atakalotoa halina makosa kutokana na hali ilivyo

Hoja zako
1 Viongozi wa UKAWAhawakukosea bali walibofoa. Kulikuwa na kila funzo la kuwatahadharisha.

Walichokifanya ni kuongozwa na hisia badala ya elimu. Siasa ni taaluma kama tulivyofafanua katika ule uzi ‘sayansi ya jamii
'

Tuliwahi kuwa na mjadala na Mchambuzina gfsonwin na wengine kuhusu uongozi.
Wenzangu walisema taasisi zinawezakujengwa kutoka juu kwenda chini ‘top-bottom'

Msimamo wangu ulikuwa kujengataasisi kuanzia chini kwenda juu ‘bottom-top'

Madhara ya top-bottom ndiyo haya wanayokabiliana nayo

Viongozi wa UKAWA wamekuwa na tabia ya kutoa maamuzi wakitegemea kila mara wataungwa mkono.

Mbatia hana chakupoteza katika chama kama Lipumba.
Mbowe ana cha kupoteza kama kiongozi wa upinzani, na chama kilichompokea Lowassa

Maamuzi ya Mbowe yalipaswa kuzingatia hali ilivyokuwa, na nafasi ya chama chake

Baada ya tetesi za Lowassakuhamia , Dr Slaa alikwenda Mwanza katika ziara ya kichama iliyokuwaya kihistoria.
Ile tu ilikuwa vote of no confidence kwa hatua zinazoandaliwa

lakini pia kupeleka message kuhusiana na hilo. Mbowe alisoma alama za nyakati?

MBOWE KAKOMAA BILA KUANGALIAWADAU WAKE

Hali iliyopo ambayo si nzuri hata kama haisemwi inatishia sana umoja na ustawi wa CDM.

Katika hali yakawaida, wanachama wa CDM wangemtaka Dr Slaa atoe tamko. Ndivyo ilivyokuwa kila mara.

Kinyume chake kuna vijineno kama kasusa. Iwe kweli au si kweli tunajua kuna tatizo

Mbowe anakomalia hatua zakumkaribisha Lowassa. Akiwa kiongozi wa CDM, kazi kubwa nikuweka mustakabali wa chama sawa . Kakaa kimya akiendelea na mipango huku wanachama wake wakiwa confused, mesmerized and bewilderd.

Hili ni tatizo kubwa kuliko ujio. Mbowe ana kila sababu zinazomtaka ajitokeze aeleze anachosimamiaiwe sahihi au la, kuzungumza si option kwake ni lazima, vinginevyo anakuza tatizo na litamgharimu sana kisiasa. Nitty gritty

Uwezekano uliopo ni kupotezameli na mzigo. Nafasi waliyokuwa nayo ni ima kupoteza meli kubaki na mzigo, aumzigo kubaki na meli.

Hawakuhitaji personality, walihitaji message, strategyand execution.

Sasa wana dili na personality katika wakati mbaya wakiwa na ''parastake holders na kuacha stake holder wanaoujua infrastructure wakiwa wameduwaa

2. Dr.Slaa, huyu alitakiwa from begining ya makubaliano na EL awe clear na akubaliane na wenzake wote kama kweli wanasema walifanya vikao kadhaa kabla ya kumualika rasmi, na kama alikubali au kushawishiwa kwenye vikao mpaka akakubali basi sioni kama kutakua kuna shida yyt zaidi ya hizi porojo za kila siku kumuhus. kimsingi yeye ndio devide Factor kubwa ambayo ndio naiona kwa sasa, wakimuhandle kwa busara na yeye kuamua kufunika kombe mwanaharamu apite angalau tunaweza kuona matunda kidogo kwenye uwekezaji huu wa wenye risk kubwa waliofanya Ukawa.

Laah, akishupaza shingo na kukomalia msimamo wake kwamba hamtaki EL na kwamba hawezi kula matapishi yake, basi kutatokea na anguko kubwa sana kwa UKAWA nawatakua wameharibu hata kidogo walichokijenga, mpaka sasa mm sijajua standing yake baada ya EL kujoin kwamba ataendelea au ataachana na siasa, maana yeye yupo kimya kabisa, zaidi tunasikia tu vurumai za kwenye mitandao na magazeti kuhusu future yake after El envision.
Hili suala halikuwa namaandalizi wala maridhiano.

Tumeeleza safari ya Dr Slaa Mwanza kama isiyokuwaya kawaida.
Kipindi kirefu kimepitaUKAWA wakatafuta mgombea.
Tumesikia CUF walikataa mpakaABCD zikubaliwe n.k.

Ghafla likaja hili tenalikinzia kamati kuu bila vikao vingine

Ndio maana tunasema,kinachotakiwa ni busara na hekma za Dr Slaa peke yake, si ku handle with care kwasababu the whole process is flawed ab initio
.

Mbowe should come out to address the situation. Kuacha mambo ya ''hang'' namna hii ni kulikuza tatizo ambalo kwa maoni yangu binafsi Mbowe is at the centre of the whole fiasco kama mwenyekiti na KUB
 
3. Kwa sisi tunaopinga Kuhusu Lowassa, lazima pia tutafakari kwa kina na kwa mapana yake, hawa viongozi wa UKAWA ndio wameshakosea sana kwa kumkaribisha huyu mtu na muda umekwisha, je bora kukosa kabisa mabadiliko hata kama machache kuliko kumtumia EL kufanikisha hili jambo ambalo kwa utashi wao wao wanaona anaweza kuwavusha. Au kuendelea kukomaa na mabadiliko, kwamba mtoto ndio Kanyea Mkono (viongozi wa UKAWA kwa kumkaribisha EL kwenye uraisi) tuusafishe na kusonga mbele kuliko kuukata au kumpiga mtoto, maana ndio keshakosea. Ni fikra tatanishi sana ila ndio hali tuliyopo
Hili ni suala la wadau kulitafakari. Ni hoja nzito

Duru tumeandika wazi ‘UKAWA hofuhii ilikuwa na ulazima wowote?'

Wana jukwaa, mimi niliunga mkono Lowassa kujiunga Chadema kwa sababu moja kuu nalo ni kwamba ujio wake utapelekea kudhoofika kwa CCM na kuongezea nguvu upinzani. Niliamini kwa dhati kwamba kabla ya kupokelewa Chadema, viongozi wote wa UKAWA watakuwa wamekaa, wameafiki na kuridhia ujio wake huo. Niliamini na bado ninaamini, pengine kwa makosa, kwamba kama ana nia ya kupeperusha bendera ya UKAWA itabidi apambanishwe kwanza ndani ya Chadema na wagombea wengine. Hii habari ya yeye pekee kuteuliwa, kama ni kweli, imenishtua kidogo.
Mkuu kama ingelikuwa anapigania mabadiliko, mbona tungeshaona siku nyingi!!!

Hii ni kukamilisha safari iliyoanza ikakumbwa na dhoruba. Na amesema mwenyewe, anakuja kuendeleza safari

Utakumbuka tuliwaambia UKAWA kama wanaona kwa mtazamo wao ni vema kumpokea basi awe kama Mtanzania mwingine. Kuanzia hapo naye angekuwa mwanachama na haki za kugombea.

Leo wange ongelea ushindani kwa vipimo.

Walimkaribisha kwasababu ana watu nyuma na nguvu. Nani wa kuhoji nguvu walizozitolea ‘hukmu' tayari?

Kwasasa kama wangeniuliza ningewashauri wahangaike na tembochumbani (elephant in the room) tu.

Wasijaribu kabisa kwasababu ‘the house is crumbling'
 
Mag3:

There we go. Lowassa anasema CCM ilimnyima haki kwa kundi la viongozi kumteua Magufuli. Lakini process hiyo hiyo imetumika CDM/UKAWA. Hapa na mimi naona something is fishy.

Vilevile kama Dr. Slaa hakuwa na ridhaa kwa process hiyo, na mimi nitaanza kupunguza support zangu za hatua yake kwenda CDM.
Mkuu,

Kwenye ilani yauchaguzi ya Chadema ya 2010 wameandika kuwa hawataweza kuingia madarakani mwaka 2015 iwapo hawatashinda 2010. Sijajua sababu au umuhimu wa wao kuandika vile kwenye ilani.

2015 ndio hii. Chadema hawaamini kama wataingia madarakani. Hata ukisikiliza hotuba ya Mbowe ya kumpokea Lowassa anakiri kuwa hawakuwa na uwezo huo na wanadhani labda Lowassa atauleta uwezo wa kuingia madarakani. Lakini ukisoma saikolojia ya Mbowe na body language, Mbowe yuko more comfortable around Lowassa than with Slaa.
Kwahiyo Mbowe anachoangalia ni ile brand ya kuwa na Lowassa ambaye ni high profile politician kwa vipimo vyote. Sio kweli kwamba Mbowe anachotaka ni kushinda Urais kwa gharama yoyote, kwa sababu alishajiandaa kisaikolojia tangu 2010 kuwa hawatashinda 2015.

Kwa wepesi na juu juu anachofanya Mbowe na Mtei kinaweza kutafsiriwa kama ubinafsi
 
Hili suala halikuwa namaandalizi wala maridhiano.

Tumeeleza safari ya Dr Slaa Mwanza kama isiyokuwaya kawaida.
Kipindi kirefu kimepitaUKAWA wakatafuta mgombea.
Tumesikia CUF walikataa mpakaABCD zikubaliwe n.k.

Ghafla likaja hili tenalikinzia kamati kuu bila vikao vingine

Ndio maana tunasema,kinachotakiwa ni busara na hekma za Dr Slaa peke yake, si ku handle with care kwasababu the whole process is flawed ab initio
.

Mbowe should come out to address the situation. Kuacha mambo ya ''hang'' namna hii ni kulikuza tatizo ambalo kwa maoni yangu binafsi Mbowe is at the centre of the whole fiasco kama mwenyekiti na KUB

umeeleweka mkuu,
Na mm nadhani the best option kwa Mr.Mbowe ni kuadress tatizo kuliko kulifumbia macho, maana kukaa kwake kimya anazidi kuaharibu na kuongeza sintofahm zaidi, hakuna cha kuficha tena kilq mwenye akili timamu anajua UKAWA hususai CDM mambo hayajakaa sawa, hii ku hang bila kuadress ni mbaya zaidi kuliko wanavyofikiri.

kuhusu mzee Slaa nadhani ni kama ulivyoshauri hakuna cha kuhandle, kinachohitajika hapa ni busara zake tu basi, yeye anaona mtazamo utakuaje ili aweze kuserve situation kliyoharibika. Let us wait and c watafanya nn kwa muda huu mchache mno uliobaki.
 
..Dr.Slaa ha kuchukua fomu.

..inasemekana cc ya cdm ilimpendekeza.

..sasa cc ya cdm imempendekeza Lowassa badala ya Dr.Slaa.

..pia inaelekea nccr na cuf wamemkubali Lowassa kuliko ambavyo cdm wamemkubali.

..halafu kuna zile tetesi kwamba cuf hawamtaki Dr.Slaa. Huenda ni ukweli. Labda tujiulize fomu aliyochukua Prof. Lipumba imepotelea wapi? Je, Prof wakati anachukua fomu hakujua kwamba anayepaswa kugombea kupitisha ukawa ni Dr.Slaa?

..inawezekana Lowassa anawaunganisha Ukawa kuliko ambavyo Dr.Slaa angewaunganisha.

. Mkandara, Susuviri, Nguruvi3, Mag3, King Suleiman
..
 
Mkuu maneno haya sio kweli, Ofisi ya Chadema ilifungwa baada tu ya Lowassa kuchukua fomu na hakuruhusiwa mtu mwingine yeyote kuchukua fomu ya Urais, hivyo kupendekezwa kwa Dr.Slaa wakati uchukuaji fomu bado haujatangazwa rasmi haina maana yoyote. Chadema wametuonyesha mfumo mbovu kuliko hata ule wa CCM kuengua watu na kamati ya maadili jambo ambalo mimi naona CCM wameboresha mfumo wao zaidi ili kupata viongozi wenye sifa, zamani hapakuwa na sifa isipokuwa mwenye umaarufu na uwezo wa ku deal na matatizo!.

Mimi naomba tuutazame ukweli nao ni kwamba Dr.Slaa alihama CCM kwa sababu ya kundi hili hili la Mtandao mwaka 2005. hawa walichagua watu wao na kuwasimamisha hivyo yeyote ambaye hakuwa nao walimtosa kwa sababu walikuja kuchuma na wamechuma kweli kweli. Na ikumbukwe pia kwamba kama mwaka 2005 jina la JK lingeenguliwa kundi hili lingekuja CHadema na hivyo utawala mzima wa JK na ubovu wake ungekuwa wa Chadema sio CCM. na hii ndio hali halisi.i

Sasa leo, Chadema inayotaka kupambana na kundi hili ambalo kwa miaka 10, Chadema imejenga hoja nzito kwa wananchi juu ya utawala huu, mara ghafla wanabadilika na kuwapokea Mtandao kwa sababu wanataka CCM iondoke madarakani lakini kisera mtawaambia nini wananchi ikiwa Mtandao ule ule mloupiga vita miaka yote ndio wamekuja kwenu?..Walichokifanya Chadema ni kuvua gwanda na kuvaa gamba..

Ni kweli CUF hawamtaki Dr.Slaa kwa sababu za Udini ambao mimi naamini Upo nchini (Uhalisia) lakini Chadema kama chama cha Demokrasia kinatakiwa wawe mfano bora maana anayechaguliwa na wanaChadema ndiye mgombea wa Chadema sio wa CUF na anakubalika na wananch wengi. Swala hapa ni nani mgombea anakubalika na wananchi wengi, hivyo vyama vingine havina budi kumwachia kama ilivyo katika Ubunge. Sio wabunge wote wa Chadema wanapendwa na wafuasi wa CUF wala wa CUF kupendwa na WanaChadema isipokuwa maridhiano yao waliamini kuwa wananchi wataunga mkono yeyote atakaye wakilisha UKAWA.

Hivyo wangeendelea na hiyo pata potea japo mimi nilisema wazi kuwa UKAWA kwa njia hiyo hawawezi kushinda uchaguzi huu nadhani hili unalikumbuka vizuri. Walitakiwa kuunda chama kimoja na kuondoa hizi hisia za U - Chadema na U - CUF. Lakini naambiwa hakuna kiongozi ndani ya UKAWA anayekubali kuwa chini ya mwingine hivyo muungano huu ni utapeli mtupu kushushana ili kuanzia mwaka 2016 vyama vyote hivi vya Upinzani viwe na nguvu sawa..
 
Back
Top Bottom