Mkandara,
..Dr alitakiwa awe na fomu yake tayari.
..nini kilikuwa kinampa kigugumizi asichukue fomu?
..sasa hata haieleweki kama alikuwa anataka kugombea au alikuwa anasubiri aombwe na chama chake.
..je, tatizo ni kwamba hamtaki Lowassa? Au, tatizo ni kwamba amedhulumiwa nafasi hiyo?
..Je, Mbowe angeleta mtu asiye na tuhuma bado kungekuwa na sintofahamu tuliyonayo sasa hivi?
Cc Nguruvi3, Zakumi
Kwa maelezo ya Tindu Lissu (alikuwa anaongea na vyombo vya habari) ni kwamba mchakato wa kupata 'mabaki' toka CCM kugombea CHADEMA yalianza muda mrefu. Walikuwa wanasubiri mchakato wa CCM umalizike ili wapate mgombea wao.
Lissu pia anatutaarifu kuwa wamefanya tafiti nyingi kupitia kwa makampuni makubwa dunia (makampuni ya polls), na walipewa majibu yanayoonesha nguvu ya Lowassa. Maswali ya kujiuliza ni haya:
- Ni lini CHADEMA walianza mchakato wa kumpata Lowassa, ni baada ya kukatwa huko Dodoma, au wakati wa tafiti?
- Ni watu gani walihusishwa kuandaa hizo tafiti? Dr Slaa alikuwa miongoni mwa watu waliojua kuhusu hizo tafiti? Hadidu rejea zilikuwaje?
- Nini lengo la CHADEMA kutaka kujua (kupitia tafiti) faida watakayopata kama wataungana na Lowassa kwenye uchaguzi?
--Kama walikubaliana Lowassa aje CHADEMA, walikubali aje kama mwanachama wa kawaida au mgombea urais kupitia CHADEMA?
- Kama jibu ilikuwa aje kama mwanachama wa kawaida, nani alibadilisha na kupitia kikao gani na kwa sababu zipi?
- Mpaka sasa hivi (niko tayari kusahihishwa) Pro. Lipumba bado ni mgombea urais kupitia CUF. Sikumbuki kusikia kuwa amejitoa rasmi kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais kupitia CUF!