Kwanza, niwashukuru na kuwapongeza sana wachangiaji kwa 'civil debate'. Wachangiaji wameonyesha 'insightful' katika suala zima.
Na hakika,
Mag3 kahitimisha vizuri sana, kama hakuna mitazamo tofauti, something is wrong.
Mtazamo wangu umejawa na shaka zaidi ya matumaini. Shaka inajengwa na historia ya wapinzani.
Kama mtakumbuka wakati wa BMLK, tuliwaonya wapinzani kunywa juisi Ikulu (uzi wa juice ya maembe).
Kwa mshango, ni Mbowe huyu wa leo ndiyo aliyeongoza feilia ile hadi nguvu ya umma ilipowalazimisha kutoka. Tulikuwa sahihi!
Pili, sina tatizo na ujio wa Lowassa, ni haki yake kama raia mwingine. Ninashaka, suala lilivyokuwa handled kama kulikuwa na busara , maafikiano na uchambuzi wa kina. Tulishangaa tu Mbowe anakabidhi hiki na kile ilimradi kila mtu kaduwaa kwa hii 'voda fasta'
Tatu, CDM kuchukua hatua dhidi ya kiongozi kwasababu Chama si mtu ni hatu nzuri, nimeipigia debe sana.
Wakati tetesi zinavuma, niliandika bandiko la kuwaasa Mbowe, Slaa na CDM dhidi ya haraka wanayoifanya.
Hivyo, suala si mtu, suala ni hoja za mtu, tunaangalia hoja zaidi ya mtu au watu
Nne, kama ipo njia ya mkato ya kuiondoa CCM basi na iwe. Njia lazima iwe katika mkakati mzuri, isi compromize values nyingine
Njia hiyo iongozwe ili kufikia mabadiliko ya kweli na si ya rangi.Tatizo si CCM kama chama, ni watu wanaounda CCM kama chama.
Lazima tujiulize, hawa wanaokuja, wanakuja kwa dhati au wanakuja kwasababu ya.
Tano, kilio cha watu siku zote ni CCM kutekwa nyara na matajiri. Umiliki wa chama umekuwa suala la kundi na si wanachama.
Je, athari hizo zimeangaliwa kwa upana na marefu yake?
Sita, kama lengo ni kubomoa mfumo mchafu, tunabomoa mfumo huo kwa kutumia nini?
Alinda kasema mafisadi wameshinda kura za maoni. Wanafahamu mfumo ulivyo na wanavyoweza kuutumia katika 'survival' kama si manupalation. Hawa wanaokuja lini wameacha mfumo huo ghafla na kukumbatia mabadiliko?
Saba, Ujio wa EL umefungamaniishwa na nguvu kubwa kisiasa kiasi cha kuonekana UKAWA imejiunga na EL na si kinyume chake.
Mbele ya safari, nini hatima ya UKAWA kama chombo kinachosimamia mabadiliko?
Again, kwanini watu waamini mtu kama taasisi ikiwa tunaamini hakuna mkubwa zaidi ya chama?
Nane,ujio wa EL umepelekea viongozi kusema 'asiyetaka aondoke'. Well, tunathamini vipi mchango wa watu waliojitolea roho zao katika kupigania mabadiliko ya nchi hii. Kwanini mtu anaweza kuingia na kukigawa chama kiasi hicho. Hii ni dalili njema kweli!
Tisa, Ni hesabu zipi zinazoonyesha ujio utanufaisha Ukawa? kura za maoni zimekamilika, nini kinategemewa zaidi ya hapo?
Kama ni wananchi nani ataongoza mapambano ikiwa ujio upo nje ya 'system mpya'?
Ongezeko la wabunge linatoka wapi? Je, wale wa Ukawa waenguliwe kupisha nguvu kubwa ya kisiasa?
Kumi, endapo tunaamini katika demokrasia, ni kwanini demokrasia haikuachwa ichukue mkondo wake kwa kuweka wagombea bali inaonekana kama EL amekuja kwa 'mission' hiyo. Hakuna aliyezuiliwa kuchukua fomu, lakini mazingira yaliyojionyesha ni wazi huyu ni chaguo tayari. Je, lini wanachama walipima nguvu yake na kuridhika itawavusha?
Kumi na moja, Ujio wa EL utaambatana na marafiki zake wengi. Kuna uhakika gani kuwa marafiki zake walioko kimya wataendelea kuwa nje ya sytem pindi na ikitokea akafanikiwa? Na hao kama mzee wa vijisenti wataachaje influence yao hata kama wapo nje ya Ukawa? Nani atakuwa na upper hand, ukawa au marafiki wa safarini?
Kumi na mbili, kipi kilipaswa kutangulia kama alivyosema Mzee Mwanakijiji katika uzi wake. Je, ni hawa kukiri mapungufu na kujiunga na mbadiliko, au ni wapenda mabadiliko kushangilia wajao?
Na mwisho, endapo suala hili ni rahisi, iweje linavuruga viongozi? Je, huko kwa wananchi kukoje!
Kwanini kunakuwa na 'mixed feelings' ikiwa lengo ni moja, kuondoa CCM. Kwanini kuna hofu iliyotanda isiyojulikana inatokana na nini?
Je, si vema kuondoa shaka hiyo kuliko kuiacha watu wakaiondoa wakiwa wenyewe katika sanduku la kura!
Nikiangalia, kijamii, moral perceptive, aina ya mabadiliko tunayohitaji,historia ya uongozi wa Ukawa katika nyakati za crisis, mkakati uliopo, namba n.k. ninabaki na maswali mengi kuliko majibu.
Najaribu kusoma kwa umakini kama nitashawishika zaidi na hoja nikijishauri nipo wrong side of the history.
Until then nabaki kusema huu ni uwekezaji hatari na wenye risk! I hope I'm wrong!