Alinda
Platinum Member
- Jun 26, 2008
- 1,695
- 2,149
Samahani naomba ufafanuzi kidogo Prof Lipumba, alipata kura 600 kwenye kwenye uchaguzi gani?
Sorry "laki 6"
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Samahani naomba ufafanuzi kidogo Prof Lipumba, alipata kura 600 kwenye kwenye uchaguzi gani?
Shukurani!! Nakumbuka hata Freeman Mbowe alishawahi kupata kura laki 3 alivyogombea urais, lakini sasa kati ya wanasiasa wenye ushawishi, hizi kura za NEC wakati mwingine uwa udanganyifu.Sorry "laki 6"
Exactly mkuuNguruvi3, Mag3,
..umoja ni jambo la msingi sana wakati ukawa wanaelekea kwenye uchaguzi.
..Prof.Lipumba amesema atashiriki kampeni za ukawa. Jambo la msingi ni kuhakikisha anatumiwa in the most effective way.
..Dr.Slaa naye ni lazima ashawishiwe kushiriki kwa nguvu,moyo, na akili zake zote ktk kampeni. Ukawa must curve a role for Dr.Slaa wakati huu wa kampeni.
..miaka 20+ ni mingi mno kuwa chama cha upinzani. Ukawa lazima wawe sehemu ya utawala kwa kukamata ikulu na bunge, au kukamata bunge peke yake.
Nb:
..halafu wengi tumejielekeza kwenye uraisi.
..tunapaswa kuangalia nini kinaendelea kwenye nafasi za ubunge pia.
..ukawa wakiwa na wabunge wengi maana yake waziri mkuu atateuliwa toka miongoni mwao.
Nguruvi3,
..wakati mwingine wazazi huwa hawana raha ktk ndoa, lakini huendelea kuishi pamoja just for the sake of their kids.
..kwa hapa tulipofika mimi nadhani ukawa pamoja na ustawi wake ni muhimu kuliko ego/nafsi za Dr.Slaa na Prof.Lipumba.
..wanasema wanaondoka au wanakaa pembeni. lakini wanawaachage wanachama na wapenzi wao ktk ukawa?
cc Mag3, Mzee Mwanakijiji
Tofauti na wengi, Mimi kwa matukio yanayotokea sasa hivi hakuna hata moja linalonishtua wala kunishangaza na badala yake nawashangaa wanaoshangaa. Kwa sasa sitasema mengi kwani natumia simu ila kuwaasa tu wanamageuzi wa kweli kuwa hizi Ni rasha rasha Tu, tusubiri machungu zaidi...Chama ni zaidi ya mtu.
Kuitoa CCM madarakani hakuhitaji Nia Tu na dhamira, kunahitaji na kujitoa mhanga na kuwa tayari kwa lolote lile. Watu waliokaa madarakani kwa muda mtefu kama CCM SI RAHISI kuachia ngazi kirahisi kama wengi tunavyojidanganya. Mpaka watolewe idadi ya majeruhi itaongezeka siku hadi siku.
Wapo waliozaliwa ndani ya CCM, wamelelewa ndani ya CCM, wamekulia ndani ya CCM, wamekomaa ndani ya CCM, wamenenepa ndani ya CCM na wapo wanazeeka ndani ya CGK Wakiapa kufa na kuzikwa ndani ya CCM...hivyo kitendo cha Lowassa ukubali usikubali ni cha kipekee na cha kishujaa. Ingawa si rahisi kuamini kwamba Lowassa Ana Nia njema lakini ukweli ni kwamba kuondoka kwake kumejeruhi watu ndani na nje ya CCM.
Kinachoitwa Collateral damage nje ya CCM itazidi si tu kuwashtua wengi, itawakatisha tamaa ambao walifikiri ngoma inayochezwa ni lelemama. When the going gets tough, only the tough keep going...I am one amongst them. It is now time to separate the men from the boys.
Simu yangu hainiruhusu kuendelea lakini nitarudi...
Kwa jinsi tulivyosikia kuhusu mgawanyo wa wagombea wa udiwani, Ubunge na Urais. Uwekezaji wa Lowassa kama mwanachama na mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA unainufaisha sana CHADEMA kwa muda mrefu, unamsaidia Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa NLD, Makaidi kutimiza ndoto zao za kuwa wabunge wa kuchaguliwa wa JMT, na unafifisha ukuaji wa CUF Tanzania Bara unaotokana na ruzuku za vyama vya siasa.
Maadam CUF ya Zanzibar iko njia moja na Lowassa, sioni mtafuruku mkubwa ndani ya CUF baada ya kujiengua Prof. Lipumba kama Mwenyekiti hasa ikichukuliwa nguvu kubwa ya CUF iko Zanzibar.
Kuondoka kwa Prof. Lipumba pia kuna ondoka kwa kiwango kikubwa migogoro ya kuachiana majimbo ambayo bado unavinyemelea vyama vilivyoko ndani ya UKAWA kwa sababu CUF kupitia kwa Prof. Lipumba waliachia majimbo mengi kwa CHADEMA wakitegemea nafasi ya Urais watapewa kugombea.
Prof. Lipumba ameachia nafasi ya Uwenyekiti wa CUF kwa sababu alidhani atapewa nafasi ya kugombea Urais kwa tiketi ya UKAWA lakini kikubwa zaidi amekosa nguvu ya ushirikiano ya kutaka awe mgombea wa UKAWA kutoka kwa viongozi wa CUF upande wa Zanzibar baada ya Lowassa kujiunga CHADEMA. Maalim Seif na Lowassa kwa sasa wanaongea lugha moja kwa sababu kati yao hawagusani maslahi!
Ninaamini kabla ya kampeni kuanza Dk. Slaa atarudi ofisini kuendelea na kazi zake kama Katibu Mkuu wa CHADEMA baada ya kukubaliana na ushauri wa wazee na viongozi mbali mbali. Kurudi kwa Dk. Slaa ofisini kutapunguza sana vikwazo ambavyo CHADEMA/UKAWA walikuwa wanaenda kukabiliana navyo katika kampeni za Uchaguzi Mkuu.
Hata kama CHADEMA haitashinda uchaguzi kwenye kiti cha Rais lakini ninaamini kabisa kitakuwa kimepiga hatua katika ulingo wa kisiasa baada ya ujio wa Lowassa.
Nadhani labda hoja ya msingi ni kujiuliza kama huu uwekezaji utawawezesha CHADEMA kushinda kiti cha Urais wa Tanzania. Bado siamini mpaka sasa kama CHADEMA watashinda kiti cha Urais lakini ninaamini kwa jinsi mvurugano wa kura za maoni ndani ya CCM unavyoendelea, CHADEMA watapata viti vingi vya udiwani na ubunge kutokana na matokeo ya mvurugano ndani ya CCM.
Mkuu,Ng'wamapalala:
Hivi vyama vyote vya kisiasa pamoja na CCM vilitakiwa viwe vya mpito tu. Mpaka pale watanzania watakapozoea demokrasia ya vyama vingine ndipo tunakuwa vyama vya kudumu. Ni katiba na ruzuku ndizo zinazolazimisha kuwepo kwa vyama vya siasa vilivyopo sasa.
Wanachama wengi wa sasa wa CCM hawaelewi kabisa itikadi ya chama hicho. Wanachama wengi wa CDM au CUF hawaelewi itikadi ya vyama vyao. Mpaka pale watu wanapokuwa wanajiunga kwenye vyama kwa kufuata itikadi ndipo tutakaposema vyama vinafaidika.
Kwa sasa tuachia nadharia ya Darwin itumike.
Kwa sasa kuna uwezekano wa kupata Rais wa Tanzania ambaye anawakirisha andiko la Josh Maiyo!The majority of African political parties are therefore more oligarchic than democratic in practice. Most do not have membership lists and when they do, these are not necessarily exclusive. Voters tend to have multiple party memberships and party loyalty fluctuates significantly. Allegiances are usually to the party leader as opposed the institution of the party. The lack of strong party affiliation and weak institutionalisation promotes a culture of political tourism and party hopping depending on the whims of the party leader or political expediencies.
Mwalimu , ni kweli hakuna 'perfection' si kwa siasa hata kwa rocket science. Kuna nyakati za wax and waneNimewahi kusema huko nyumba kwamba mabadiliko ya kweli tunayoyataka yana GHARAMA, tena gharama yenyewe ni kubwa sio ndogo. Swali kwetu ni kwamba je, tuko tayari kuingia gharama hiyo? Itakuwa ni kujidanganya kudhani kwamba iko siku kutatokea upinzani ulio PERFECT bila mawaa yoyote ndio uje kutuongoza kwenye mabadiliko yatakayokuja kwa mteremko kiulaini!
JokaKuu, that is the point. Kabla ya mwaka 1992 tulikuwa na chama kimoja CCM na ni wachache tu kama mimi ambao waliweza kujitenga na kukaa kando bila kujiunga na CCM toka iasisiwe mwaka 1977. Wengi wa wanamageuzi wa mwanzo ama walikuwa ni wana CCM hai au ambao walikuwa CCM mfu ikiwa na maana kwamba ni kwa mwili tu na si kwa moyo. Kujiunga na upinzani kulionekana na kuhesabika kwa baadhi ya watu kama uenda wazimu au usaliti. Wanamageuzi wa mwanzo waliogopwa kama ukoma na sehemu kubwa ya jamii.Mag3, Nguruvi3, Mkandara,
..mimi nadhani nguvu zaidi zingeelekezwa kuwashawishi wana ccm wengi zaidi wahamie ukawa.
..huu ujio wa lowassa utumike kuwahamasisha wana ccm waliochoshwa na chama chao kuja upande wa ukawa.
..uamuzi wa lowassa unatakiwa uwe framed kama uamuzi wa kishujaa unaopaswa kuigwa.
..i guess cdm na ukawa hawana political spinners wanaojua kucheza na saikolojia ya wapiga kura.
..mimi ushindi wa ukawa siuangalii kwa kutumia "lens" ya migogoro itakayofuatia.
..naangalia ni mambo gani mazuri yanaweza kutokea.
..kwa mfano, ikiwa ukawa watashinda nategemea sheria inayovikwaza vyama vya siasa kuungana au kuunda coalitions kufutwa mara moja.
..pia sheria inayomzuia mbunge kuhama chama bila kupoteza ubunge wake nayo nategemea itafutiliwa mbali
Cc Mkandara, Nguruvi3 Alinda Mwalimu