CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

King Suleiman na Alinda hapo juu

Sasa tuna ukweli kuhusu Lipumba. Kuna kitu Tuliitaka kuchangia siku nyingi tukasita, leo tunaangalia na kukiona

Mwaka huu mkutano CUF wa kumchagua mgombea kule Zanzibar umefanyika huko huko na si makao makuu Dar
Tunaposema makao makuu tuna maana hiyo, hata kama uungwaji mkono ni sehemu nyingine
Shughuli za CUF Zanzibar ni tofauti kabisa na CUF bara

Hili tulioana kama 'internal strife ' kwana CUF zanzibar walikuwa na yao kabisa tofauti na bara
Kitendo cha Magdalena kuchukua sehemu kubwa ya kazi za katibu mkuu Maalim, ilikuwa na walakini

Maalim alikuwa pembeni kabisa kuhusu Ukawa, alikuwa anaibia ibia tu, katika ukweli alikuwa mbali kabisa

Kuna hali ya wafuasi wa CUF kutaka mgombea wa chama chao kuwa wa UKAWA.

Prof aliona lina matatizo kwa kuangalia factor nyingi . Kwa mfano, 'nguvu '' ya CUF katika siasa za bara imepungua n.k

Wingi wa wabunge wa CUF unategemea Zanzibar. Hata ukifiuatilia mwenendo wa kisias ni wazi nguvu ya CUF imepungua

Pili, Wafuasi wa CUF wakiamua jambo inakuwa ngumu sana kubadili misimamo yao. Kuna uzuri wa hili na ubaya wake pia

Mfano, Tunakumbuka Mtatiro alipopigwa shinilkizo la kupeleka rasimu mara baada ya kutanganzwa mchakato wa katiba.
Ilikuwa ni shinikizo tu bila kuangalia taratibu katika hali pana. Rasimu ikafikishwa wiki moja!!!

Si Prof Lipumba au Maalim waliokuwepo katika msafara. Ilikuwa ni shinikizo tu la wananchama kwamba lazima itokee

Kwa mtu kama prof ingelikuwa kikwazo kukataa kwa kutumia weledi wake, akaacha wapeleke rasimu akijua si sahihi kufanya hivyo, wala hakukuwa na utaratibu wa kutosha. Ilikuwa shinikizo tu

Tatu, Tunakumbuka wanachama walimwita Lipumba kuhusu majadiliano na UkAWA wakitaka kujua makubaliano yanafanyikaje bila ya wanachama wa CUF kushirikishwa.Ndilo lile tulilosikia, Ukawa wameahirisha kutoa nafasi.

Kulikuwa na shinikizo kali kutoka kwa wanachama kuhusu Ukawa

Duru tuna mtazamo kuwa kujiuzulu kwa Prof kunatokana na matatizo ya ndani ya CUF, haya ya nje ni kichocheo tu cha matatizo ya ndani. Ukimsoma vizuri prof anasema yeye anaonekana kama kikwazo.

Maneno hayo ni mazito kwasababu inaonekana kuna namna anayotofautiana na watu wake kwa mitazamo

Upande mwingine, suala la Dr Slaa linazidi kuchukua sura na ukubwa. Viongozi wana hoji ' moral values' zao , lipo jambo!
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3, Mag3,

..umoja ni jambo la msingi sana wakati ukawa wanaelekea kwenye uchaguzi.

..Prof.Lipumba amesema atashiriki kampeni za ukawa. Jambo la msingi ni kuhakikisha anatumiwa in the most effective way.

..Dr.Slaa naye ni lazima ashawishiwe kushiriki kwa nguvu,moyo, na akili zake zote ktk kampeni. Ukawa must curve a role for Dr.Slaa wakati huu wa kampeni.

..miaka 20+ ni mingi mno kuwa chama cha upinzani. Ukawa lazima wawe sehemu ya utawala kwa kukamata ikulu na bunge, au kukamata bunge peke yake.

Nb:

..halafu wengi tumejielekeza kwenye uraisi.

..tunapaswa kuangalia nini kinaendelea kwenye nafasi za ubunge pia.

..ukawa wakiwa na wabunge wengi maana yake waziri mkuu atateuliwa toka miongoni mwao.
 
Last edited by a moderator:
Sorry "laki 6"
Shukurani!! Nakumbuka hata Freeman Mbowe alishawahi kupata kura laki 3 alivyogombea urais, lakini sasa kati ya wanasiasa wenye ushawishi, hizi kura za NEC wakati mwingine uwa udanganyifu.
 
Tofauti na wengi, Mimi kwa matukio yanayotokea sasa hivi hakuna hata moja linalonishtua wala kunishangaza na badala yake nawashangaa wanaoshangaa. Kwa sasa sitasema mengi kwani natumia simu ila kuwaasa tu wanamageuzi wa kweli kuwa hizi Ni rasha rasha Tu, tusubiri machungu zaidi...Chama ni zaidi ya mtu.

Kuitoa CCM madarakani hakuhitaji Nia Tu na dhamira, kunahitaji na kujitoa mhanga na kuwa tayari kwa lolote lile. Watu waliokaa madarakani kwa muda mtefu kama CCM SI RAHISI kuachia ngazi kirahisi kama wengi tunavyojidanganya. Mpaka watolewe idadi ya majeruhi itaongezeka siku hadi siku.

Wapo waliozaliwa ndani ya CCM, wamelelewa ndani ya CCM, wamekulia ndani ya CCM, wamekomaa ndani ya CCM, wamenenepa ndani ya CCM na wapo wanazeeka ndani ya CGK Wakiapa kufa na kuzikwa ndani ya CCM...hivyo kitendo cha Lowassa ukubali usikubali ni cha kipekee na cha kishujaa. Ingawa si rahisi kuamini kwamba Lowassa Ana Nia njema lakini ukweli ni kwamba kuondoka kwake kumejeruhi watu ndani na nje ya CCM.

Kinachoitwa Collateral damage nje ya CCM itazidi si tu kuwashtua wengi, itawakatisha tamaa ambao walifikiri ngoma inayochezwa ni lelemama. When the going gets tough, only the tough keep going...I am one amongst them. It is now time to separate the men from the boys.

Simu yangu hainiruhusu kuendelea lakini nitarudi...
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3, Mag3,

..umoja ni jambo la msingi sana wakati ukawa wanaelekea kwenye uchaguzi.

..Prof.Lipumba amesema atashiriki kampeni za ukawa. Jambo la msingi ni kuhakikisha anatumiwa in the most effective way.

..Dr.Slaa naye ni lazima ashawishiwe kushiriki kwa nguvu,moyo, na akili zake zote ktk kampeni. Ukawa must curve a role for Dr.Slaa wakati huu wa kampeni.

..miaka 20+ ni mingi mno kuwa chama cha upinzani. Ukawa lazima wawe sehemu ya utawala kwa kukamata ikulu na bunge, au kukamata bunge peke yake.

Nb:

..halafu wengi tumejielekeza kwenye uraisi.

..tunapaswa kuangalia nini kinaendelea kwenye nafasi za ubunge pia.

..ukawa wakiwa na wabunge wengi maana yake waziri mkuu atateuliwa toka miongoni mwao.
Exactly mkuu

Siku nyingi sana hapa duru tulisema, lengo la UKAWA si Plan A or B bali Plan A1 and A2 ulizozieleza

Tulisema, unaweza kuua CCM kwa 'pigo moja' au unaweza kuua kwa kumfunga mikono bungeni

Hata katika mjadala huu unaoendelea, tumeuliza, kama nguvu ya EL ni kubwa vipi nafasi za ubunge?
Je watafanya kura za maoni second round? Kama sivyo, nguvu itafanyaje kazi katika maeneo kama bungeni? Tumehoji

Kuhusu Prof Lipumba na Dr Slaa , hawa ni power broker muhimu sana katika UKAWA

Tulisema pia, lengo si kukubaliana na Dr kama mtu, hata hivyo kuna umuhimu wa kuwa sehemu ya timu
Ukitazama sana maamuzi ya Prof yana reflect kwa kiasi fulani mtazamo wa Dr Slaa

Tunaposikia 'kanyaga twende' tunahoji sana, kuna analysis?.....
 
Nguruvi3,

..wakati mwingine wazazi huwa hawana raha ktk ndoa, lakini huendelea kuishi pamoja just for the sake of their kids.

..kwa hapa tulipofika mimi nadhani ukawa pamoja na ustawi wake ni muhimu kuliko ego/nafsi za Dr.Slaa na Prof.Lipumba.

..wanasema wanaondoka au wanakaa pembeni. lakini wanawaachage wanachama na wapenzi wao ktk ukawa?

cc Mag3, Mzee Mwanakijiji
 
Last edited by a moderator:
Kwa jinsi tulivyosikia kuhusu mgawanyo wa wagombea wa udiwani, Ubunge na Urais. Uwekezaji wa Lowassa kama mwanachama na mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA unainufaisha sana CHADEMA kwa muda mrefu, unamsaidia Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa NLD, Makaidi kutimiza ndoto zao za kuwa wabunge wa kuchaguliwa wa JMT, na unafifisha ukuaji wa CUF Tanzania Bara unaotokana na ruzuku za vyama vya siasa.

Maadam CUF ya Zanzibar iko njia moja na Lowassa, sioni mtafuruku mkubwa ndani ya CUF baada ya kujiengua Prof. Lipumba kama Mwenyekiti hasa ikichukuliwa nguvu kubwa ya CUF iko Zanzibar.

Kuondoka kwa Prof. Lipumba pia kuna ondoka kwa kiwango kikubwa migogoro ya kuachiana majimbo ambayo bado unavinyemelea vyama vilivyoko ndani ya UKAWA kwa sababu CUF kupitia kwa Prof. Lipumba waliachia majimbo mengi kwa CHADEMA wakitegemea nafasi ya Urais watapewa kugombea.

Prof. Lipumba ameachia nafasi ya Uwenyekiti wa CUF kwa sababu alidhani atapewa nafasi ya kugombea Urais kwa tiketi ya UKAWA lakini kikubwa zaidi amekosa nguvu ya ushirikiano ya kutaka awe mgombea wa UKAWA kutoka kwa viongozi wa CUF upande wa Zanzibar baada ya Lowassa kujiunga CHADEMA. Maalim Seif na Lowassa kwa sasa wanaongea lugha moja kwa sababu kati yao hawagusani maslahi!

Ninaamini kabla ya kampeni kuanza Dk. Slaa atarudi ofisini kuendelea na kazi zake kama Katibu Mkuu wa CHADEMA baada ya kukubaliana na ushauri wa wazee na viongozi mbali mbali. Kurudi kwa Dk. Slaa ofisini kutapunguza sana vikwazo ambavyo CHADEMA/UKAWA walikuwa wanaenda kukabiliana navyo katika kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Hata kama CHADEMA haitashinda uchaguzi kwenye kiti cha Rais lakini ninaamini kabisa kitakuwa kimepiga hatua katika ulingo wa kisiasa baada ya ujio wa Lowassa.

Nadhani labda hoja ya msingi ni kujiuliza kama huu uwekezaji utawawezesha CHADEMA kushinda kiti cha Urais wa Tanzania. Bado siamini mpaka sasa kama CHADEMA watashinda kiti cha Urais lakini ninaamini kwa jinsi mvurugano wa kura za maoni ndani ya CCM unavyoendelea, CHADEMA watapata viti vingi vya udiwani na ubunge kutokana na matokeo ya mvurugano ndani ya CCM.
 
Jokakuu;

Nikiyasoma sana maneno ya Lipumba na Mbowe, naona kuwa wana malengo yao. Kwa Lipumba ni kupata mabadiliko ya kikatiba. Kwa Mbowe ni kupata wabunge wengi wa upinzani ambao wanaweza kupunguza nguvu ya CCM. Kwa malengo haya mawili wapo tayari kumkaribisha Lowassa na kuacha principles zao.

Matatizo wanayoyapata ni kuwa wanachama na wapiga kura wengi wanaangalia urais kama mwisho wa matokeo. Vilevile wanakuwa distracted kwa issues ndogo ndogo, zingine zikiwa ni za kishabiki, na kusahau nini ni kiini cha mfumo mbovu wa utawala.

Ukiwa na katiba nzuri na wabunge wa wengi wa upinzani, umemaliza kila kitu. CCM wanaweza kubakia na urais lakini nguvu zake zinategemea ushirikiano na bunge.
 
Tofauti na wengi, Mimi kwa matukio yanayotokea sasa hivi hakuna hata moja linalonishtua wala kunishangaza na badala yake nawashangaa wanaoshangaa. Kwa sasa sitasema mengi kwani natumia simu ila kuwaasa tu wanamageuzi wa kweli kuwa hizi Ni rasha rasha Tu, tusubiri machungu zaidi...Chama ni zaidi ya mtu.

Kuitoa CCM madarakani hakuhitaji Nia Tu na dhamira, kunahitaji na kujitoa mhanga na kuwa tayari kwa lolote lile. Watu waliokaa madarakani kwa muda mtefu kama CCM SI RAHISI kuachia ngazi kirahisi kama wengi tunavyojidanganya. Mpaka watolewe idadi ya majeruhi itaongezeka siku hadi siku.

Wapo waliozaliwa ndani ya CCM, wamelelewa ndani ya CCM, wamekulia ndani ya CCM, wamekomaa ndani ya CCM, wamenenepa ndani ya CCM na wapo wanazeeka ndani ya CGK Wakiapa kufa na kuzikwa ndani ya CCM...hivyo kitendo cha Lowassa ukubali usikubali ni cha kipekee na cha kishujaa. Ingawa si rahisi kuamini kwamba Lowassa Ana Nia njema lakini ukweli ni kwamba kuondoka kwake kumejeruhi watu ndani na nje ya CCM.

Kinachoitwa Collateral damage nje ya CCM itazidi si tu kuwashtua wengi, itawakatisha tamaa ambao walifikiri ngoma inayochezwa ni lelemama. When the going gets tough, only the tough keep going...I am one amongst them. It is now time to separate the men from the boys.

Simu yangu hainiruhusu kuendelea lakini nitarudi...

Mag3:

Wewe kweli umeichoka CCM. Hivi walikupeleka JKT wakati ule wa zamani?
 
Kwa jinsi tulivyosikia kuhusu mgawanyo wa wagombea wa udiwani, Ubunge na Urais. Uwekezaji wa Lowassa kama mwanachama na mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA unainufaisha sana CHADEMA kwa muda mrefu, unamsaidia Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa NLD, Makaidi kutimiza ndoto zao za kuwa wabunge wa kuchaguliwa wa JMT, na unafifisha ukuaji wa CUF Tanzania Bara unaotokana na ruzuku za vyama vya siasa.

Maadam CUF ya Zanzibar iko njia moja na Lowassa, sioni mtafuruku mkubwa ndani ya CUF baada ya kujiengua Prof. Lipumba kama Mwenyekiti hasa ikichukuliwa nguvu kubwa ya CUF iko Zanzibar.

Kuondoka kwa Prof. Lipumba pia kuna ondoka kwa kiwango kikubwa migogoro ya kuachiana majimbo ambayo bado unavinyemelea vyama vilivyoko ndani ya UKAWA kwa sababu CUF kupitia kwa Prof. Lipumba waliachia majimbo mengi kwa CHADEMA wakitegemea nafasi ya Urais watapewa kugombea.

Prof. Lipumba ameachia nafasi ya Uwenyekiti wa CUF kwa sababu alidhani atapewa nafasi ya kugombea Urais kwa tiketi ya UKAWA lakini kikubwa zaidi amekosa nguvu ya ushirikiano ya kutaka awe mgombea wa UKAWA kutoka kwa viongozi wa CUF upande wa Zanzibar baada ya Lowassa kujiunga CHADEMA. Maalim Seif na Lowassa kwa sasa wanaongea lugha moja kwa sababu kati yao hawagusani maslahi!

Ninaamini kabla ya kampeni kuanza Dk. Slaa atarudi ofisini kuendelea na kazi zake kama Katibu Mkuu wa CHADEMA baada ya kukubaliana na ushauri wa wazee na viongozi mbali mbali. Kurudi kwa Dk. Slaa ofisini kutapunguza sana vikwazo ambavyo CHADEMA/UKAWA walikuwa wanaenda kukabiliana navyo katika kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Hata kama CHADEMA haitashinda uchaguzi kwenye kiti cha Rais lakini ninaamini kabisa kitakuwa kimepiga hatua katika ulingo wa kisiasa baada ya ujio wa Lowassa.

Nadhani labda hoja ya msingi ni kujiuliza kama huu uwekezaji utawawezesha CHADEMA kushinda kiti cha Urais wa Tanzania. Bado siamini mpaka sasa kama CHADEMA watashinda kiti cha Urais lakini ninaamini kwa jinsi mvurugano wa kura za maoni ndani ya CCM unavyoendelea, CHADEMA watapata viti vingi vya udiwani na ubunge kutokana na matokeo ya mvurugano ndani ya CCM.

Ng'wamapalala:

Hivi vyama vyote vya kisiasa pamoja na CCM vilitakiwa viwe vya mpito tu. Mpaka pale watanzania watakapozoea demokrasia ya vyama vingine ndipo tunakuwa vyama vya kudumu. Ni katiba na ruzuku ndizo zinazolazimisha kuwepo kwa vyama vya siasa vilivyopo sasa.

Wanachama wengi wa sasa wa CCM hawaelewi kabisa itikadi ya chama hicho. Wanachama wengi wa CDM au CUF hawaelewi itikadi ya vyama vyao. Mpaka pale watu wanapokuwa wanajiunga kwenye vyama kwa kufuata itikadi ndipo tutakaposema vyama vinafaidika.

Kwa sasa tuachia nadharia ya Darwin itumike.
 
Mkuu,
Ninakubaliana na wewe kwa sababu siasa za Tanzania kwa sasa imekuwa kama ushabiki wa vilabu vya mpira.

Nakumbuka kuna wakati nilikuwa ninapitia makabrasha nikakutana na andiko la Mkenya anayeitwa Josh Maiyo ambaye alielezea kuhusu vyama vya siasa katika nchi za Kiafrika na wanachama wake ambapo alisema,
The majority of African political parties are therefore more oligarchic than democratic in practice. Most do not have membership lists and when they do, these are not necessarily exclusive. Voters tend to have multiple party memberships and party loyalty fluctuates significantly. Allegiances are usually to the party leader as opposed the institution of the party. The lack of strong party affiliation and weak institutionalisation promotes a culture of political tourism and party hopping depending on the whims of the party leader or political expediencies.
Kwa sasa kuna uwezekano wa kupata Rais wa Tanzania ambaye anawakirisha andiko la Josh Maiyo!
 
Nimewahi kusema huko nyumba kwamba mabadiliko ya kweli tunayoyataka yana GHARAMA, tena gharama yenyewe ni kubwa sio ndogo. Swali kwetu ni kwamba je, tuko tayari kuingia gharama hiyo? Itakuwa ni kujidanganya kudhani kwamba iko siku kutatokea upinzani ulio PERFECT bila mawaa yoyote ndio uje kutuongoza kwenye mabadiliko yatakayokuja kwa mteremko kiulaini!
 
Mag3, Nguruvi3, Mkandara,

..mimi nadhani nguvu zaidi zingeelekezwa kuwashawishi wana ccm wengi zaidi wahamie ukawa.

..huu ujio wa lowassa utumike kuwahamasisha wana ccm waliochoshwa na chama chao kuja upande wa ukawa.

..uamuzi wa lowassa unatakiwa uwe framed kama uamuzi wa kishujaa unaopaswa kuigwa.

..i guess cdm na ukawa hawana political spinners wanaojua kucheza na saikolojia ya wapiga kura.
 
Mwalimu , ni kweli hakuna 'perfection' si kwa siasa hata kwa rocket science. Kuna nyakati za wax and wane

Pamoja na ukweli huo, lazima kuwe na kipindi cha growth na kingine maturity.

Miaka 20 ni mingi ya kufanya fyongo tena zilizo wazi.
Wewe ni mdau tumewaasa wapinzani kwa kadri ili kumaliza muda wa zimwi linalotafuna taifa. Haionekani kama wanajifunza !

Zakumi kaeleza jambo muhimu hapo juu ya kuw, haukuwa muda wa distractions zisizo na maana
Nikupe mfano mmoja. Wakati EL anaalikwa, kulikuwa na tetesi za baadhi ya viongozi kususa

Hilo likatengeneza tension kwa wanachama wiki 2. Focus ikaondoka na kuishi kwa hisia na tetesi mahasimu wao wakichochea kuni

Ukweli, ilikuwa suala la Mbowe kutoka na kueleza alichosema Baraza kuu mbele ya waandishi wa habari si kusubiri wiki 2.

Ndani ya Baraza kuu alitakiwa kufanya reference ya mkutano na waandishi wa habari kuhusu suala X, kisha kueleza mamb muhimu. Hakufanya hivyo, katumia muda wa baraza kuu kueleza tatizo la katibu mkuu!
Muda wa wiki mbili wanachama wao wapo juu juu kwa kitu cha dk tano

Unakumbuka, tuliwaambia kuwa katika mambo CCM iliyofanikiwa ni mkutano wa Dodoma.

Mkutano ulivuta vyombo vya habari, ukatengeneza vichwa vya magazeti na kuelekeza nchi Dodoma. Ilikuwa ni mkakati mzuri sana

Tukawaambia wapinzani, the best way ni kuhakikisha hiyo 'rythm' inafunikwa kwa kuondoa attention na kuilekeza kwao

Tumewafungulia vitabu, hawataki kusoma. Kinyume, attention ya Dodoma inagubikwa na distractions zikiwa ni weakness za uongozi tu Hivyo, yes we don't expect perfect opposion lakini basi kuwepo na maturity

Huu ni muda wa kuhakikisha dude linaloumiza taifa linavunjwa mgomgo. Tulisema Plan A1 na A2 na siyo plan A au B.
 
Mag3, Nguruvi3, Mkandara,

..mimi nadhani nguvu zaidi zingeelekezwa kuwashawishi wana ccm wengi zaidi wahamie ukawa.

..huu ujio wa lowassa utumike kuwahamasisha wana ccm waliochoshwa na chama chao kuja upande wa ukawa.

..uamuzi wa lowassa unatakiwa uwe framed kama uamuzi wa kishujaa unaopaswa kuigwa.

..i guess cdm na ukawa hawana political spinners wanaojua kucheza na saikolojia ya wapiga kura.
JokaKuu, that is the point. Kabla ya mwaka 1992 tulikuwa na chama kimoja CCM na ni wachache tu kama mimi ambao waliweza kujitenga na kukaa kando bila kujiunga na CCM toka iasisiwe mwaka 1977. Wengi wa wanamageuzi wa mwanzo ama walikuwa ni wana CCM hai au ambao walikuwa CCM mfu ikiwa na maana kwamba ni kwa mwili tu na si kwa moyo. Kujiunga na upinzani kulionekana na kuhesabika kwa baadhi ya watu kama uenda wazimu au usaliti. Wanamageuzi wa mwanzo waliogopwa kama ukoma na sehemu kubwa ya jamii.

Kupigania mabadiliko ya utawala kulitafsiriwa na sehemu kubwa ya jamii kama uroho wa madaraka wakati ukweli ni kwamba waroho wa madaraka ni wale walioyahatamia na kuyang'ang'ania. Ingawa upinzani umefanya kazi kubwa kuuelimisha umma lakini Watu kama hao bado tunao na wengi kama si wote ni wanachama wa CCM. Lakini pia wapo wachache ambao hawaungi mkono CCM kwa mambo mengi lakini wanalazimika kubaki humo kulinda maslahi yao.

Ni hawa ambao kitendo cha Lowassa kinaweza angalau kuwatoa hofu na ama kuwapa ujasiri wa kumfuata huko aliko au kumpigia kura kama atasimama kama mgombea Uraisi. Lakini pia tusisahau kwamba na huko upinzani tunao ambao watauona ujio wa Lowassa kama unahatarisha nafasi zao ndani ya UKAWA. Hapa ndipo natofautiana na wengi kwa sababu naamini kama mtu hasukumwi na ubinafsi, atamkaribisha yeyote na chochote kile mradi kinamuongezea nguvu katika mapambano kama tuliyo nayo kama upinzani.

Tukubali tusikubali ujio wa Lowassa kumeiongezea nguvu UKAWA na pia kuteuliwa kwake kama mgombea kumepunguza kwa kwango fulani sintofahamu (tension) iliyoanza kuota mizizi kuhusu yupi ashike usukani kati ya CUF, Chadema na NCCR. Katika hivi vyama vinavyounda UKAWA, wako wanachama ambao haingekuwa rahisi kwao kuafiki haraka haraka wateule wao wa awali kuenguliwa. Ujio wa mtu mpya ambaye anatoka nje ya watarajiwa kunaleta muafaka na kupunguza munkari ambao wangekuwa nao vinginevyo.

Binafsi nilimpenda Dr. Slaa apeperushe bendera hiyo, lakini ninaye rafiki yangu ambaye alimuona Prof. Lipumba kama anafaa zaidi...kwa bahati sote wawili tumeunga mkono pendekezo la Lowassa kuteuliwa. Nakiri uteuzi wa Lowassa yawezekana umewavunja mioyo watu wengine lakini kwa maslahi mapana ya UKAWA naamini jibu sahihi ni hilo kama lengo ni umoja katika kumuondoa mkoloni CCM. Ningefurahi zaidi kama walengwa wawili hao, Dr. Slaa na Prof. Lipumba wangeunga mkono hayo maamuzi na tusonge mbele.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo ambalo wengi bado hatutaki kulikubali - japo lipo linatukodolea macho - ni kuwa UKAWA siyo entity ambayo unaweza hata kuijadili bila kuonekana ni mtu wa kufikirika. UKAWA siyo chama cha siasa, siyo chombo chochote kinachoongozwa na vitu vinavyoeleweka. UKAWA hata siyo "umoja" kama wengi wanavyodhania - maana nasikia watu wanasema ni 'umoja wa upinzani'. UKAWA hata siyo "Muungano" ni ushirikiano tu. Simply put ni loose association ya watu ambao wana matamanio mamoja. Walikuwa na muda mrefu wa kuunganisha nguvu tangu wakati ule. Kwa mfano, tangu walipotoka kwenye Bunge la Katiba wangeweza kabisa kupanga kuua vyama vyao na kuanzisha chama kimoja chenye nguvu zaidi na chenye mfumo unaoeleweka kabisa kuelekea kuongoza. Lakini wangefanya hivyo bado kungekuwa na mgogoro mkubwa nani awe kiongozi ajaye wa chama hicho? Sidhani kama viongozi wa sasa wa hivi vyama wangekuwa tayari kusalimu amri na kuweka vyeo vyao pembeni ili kupata uongozi mpya wa chama.

Sasa kinachotokea leo na kitakachotokea baada ya uchaguzi ni rahisi sana kutabirika.

1. Kama CDM watashinda Urais (siyo UKAWA kwani siyo chama cha siasa chenye mgombea kwenye Uchaguzi huu) basi mgogoro utakaokuja utakuja kwenye kura za viti maalum. Je CUF ambao mwanachama wao amekubali kuwa makamu wa Rais nao watagiwiwa vipi hivyo viti - Tume ya Uchaguzi itasema imefungwa mikono kwani haiangalii kura za Makamu wa Rais bali za mgombea wa Urais basi viti hivyo vyote vitaenda CDM na kuipa wabunge wengi zaidi Bungeni. Huo mgogoro wa hapo hata kuufikiria naogopa. Makamu akijiuzulu kupinga hilo na kuamua kurudi kwenye chama chake, Lowassa atatakiwa atafute mwenza mwingine kutoka CDM Zanzibar?

2. CDM wakishindwa kura za Urais, ni vipi utawaona kina Duni na Lowassa wanabakia kukijenga chama chao cha kufikia (adopted party) badala ya Duni kurudi zake CUF na Lowassa kuamua kustaafu siasa? Au watu watakubali tena Mbowe aongoze chama kukijenga kuelekea 2020 ambako huko tena watasubiria mgombea mwingine wa CCM kuwasaidia kuing'oa CCM? Hawawezi kuwa na mgombea wao miaka mitano ijayo wakaaminika tena.

Kuna migogoro mingine tu inakuja ambayo sidhani kama tumeifikiria vizuri na maana yake katika demokrasia na siasa za Tanzania kwa miaka mitano ijayo.
 
..mimi ushindi wa ukawa siuangalii kwa kutumia "lens" ya migogoro itakayofuatia.

..naangalia ni mambo gani mazuri yanaweza kutokea.

..kwa mfano, ikiwa ukawa watashinda nategemea sheria inayovikwaza vyama vya siasa kuungana au kuunda coalitions kufutwa mara moja.

..pia sheria inayomzuia mbunge kuhama chama bila kupoteza ubunge wake nayo nategemea itafutiliwa mbali

Cc Mkandara, Nguruvi3 Alinda Mwalimu
 
Jokakuu, huwezi kukaa na kutegemea tu kuwa kitu fulani kitatokea. Msingi aa kutegemea huko ni nini? Isipofutwa utalalamika? Kama watu hawatatataka kujua wanataka kufanya nini wasi poo ofanya wasichotakiwa tutaanza vipi kuwauliza? Hii pragmatism should have some basis.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom