CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Kaka yangu Nguvuri3 hayo maswali unayojiuliza ni maswali anayojiuliza kila mtanzania, kila mtanzania hasiyetaka kuburuzwa, kila mtanzania ambaye amefundishwa na kulelewa katika mazingira ya kuhoji na kuhoji kwa nia nzuri tu ya kupata maelezo ya kuridhisha kwa swala husika.

Watanzania tumezoea kutohoji, tumezoea na kulelewa kuwa mkubwa akisha sema jambo basi wewe unatekeleza, tumefundishwa kuwa kiongozi akisema kitu basi ni sahihi, na huu udhaifu wetu wanautumia sana viongozi wetu kutuamulia mambo hata kwa maswala ambayo hatutaki. (rejea katiba mpya, sheria mbali mbali na hili swala la Lowassa) na kibaya zaidi ukiwauliza maswali wanajibu kwa kejeli na dharau, (rejea Lowassa na Richmond.)

Kama Taifa tunabidi tuwe taifa la kuhoji, taifa la kuwakosoa viongozi pindi pale tunapoona wanakwenda nje ya makubaliano yetu, tuwakatalie pale tunapoona wameweka masilahi yao mbele kuliko maslahi ya nchi. Inawezekana kabisa Lowassa amehojiwa na kamati kuu na kutoa maelezo ya kuwaridhisha lakini hayo maelezo ndo tunataka sisi wananchi wa kawaida kuyasikia kwani waamuzi ni sisi, tutakao kwenda kupiga kura ni mimi na wewe, ni sisi tunahoji lakini kwa bahati mbaya sana viongozi (hawa miungu watu wametia pamba masikioni) kwani vichwani vyao kumejaa zile dhana za kizamani kuwa kiongozi hakakosei, kuwa kiongozi analohamua ndilo na sisi tumekuwa kama watoto yatima hatupatizi sauti zetu kuwambia kuwa "hapana stop" huu mstari havuki maana huu ni mpaka wetu.

Ndugu watanzani wezangu tunahitaji kufahamu tena kwa maelezo ya kina ni kwanini achaguliwe Lowassa ni kwanini Dr. Slaa yuko nje ya uwanja. Ni maswali na yanaeleweka hayahitaji kuwa na degree ili uweze kuyajibu, lakini majibu yake yana mantiki kubwa kwetu sisi, majibu ya haya maswali ndio yatatufanya kuona kuwa viongozi ni waajiri wetu, kuwa viongozi wanathamini mchango wetu, kwamba na sisi tunathaminiwa, kwamba tunaweza kuwakatalia viongozi na nk.

Hivyo basi Mbowe, John Mnyika , Tumaini Makene , Salum Mwalimu Tundu Lissu, Lowassa na wengineo huu si wakati wa kuburuzana si wakati wa kutufanya watoto yatima, si wakati wa nyie kuwa miungu watu, ni wakati wa kujibu maswali yetu na kutuondoa wasiwasi,

Tunataka kujua nini hatima ya Dr. Slaa? Mchango wa mzee huyu katika kujenga chama unaeleweka, nakumbuka picha nilizoziona wakati yuko Kigoma mzee wa watu wakimpopoa mawe kwa ajiri ya Chadema hivi leo hii huyu mtu hana maana tena mwenye maana ni Lowassa? Na kibaya zaidi tukihoji hatupati jibu..

Huyu mzee ni mtu mwenye busara sana, mtu mwenye maono na kama hasingekuwa anapenda chama chake alichokijenga kwa mikono yake miwili tena kuliko kiongozi yeyoye yule ndani ya Chadema angekuwa ameishaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutangaza kujihudhuru lakini kwa busara zake, kwa upendo kwa chama chake ameamua kukaa kimya ili hasiharibu hata alichojenga. Tumpeni heshima yake msikilizeni Mzee wetu anataka nini kwa chama chake alichojenga kwa jasho lake hali Mbowe na viongozi wengine wakipaa na angani.

Leo hii rudhuku ya Chadema ambayo imefanya mambo makubwa, ambayo imeibua viongozi wa serikali za mitaa ni mchango wake, angekuwa mtu mwingine wakati wanamkurupusha kwenda kugombea urais basi angekataa maana alifahamu kabisa kuwa hawezi kushinda urais, lakini aliamua kuachana na ubunge, kuhama kutoka katika jimbo lake na kuhamia Dar ili ajenge chama. Tunafahamu kuwa Chama kilimpangishia nyumba lakini kwa kuona kuwa hela inayolipwa na chama kwa pango lake ni kubwa aliamua kujenga nyumba yake tena kwa mkopo. Kiongozi wa jinsi hii hawapatikani kirahisi nchini Tanzania

Pamoja na kuumizwa sana na uamuzi wa Chadema kuhusu Lowassa, lakini kinachoniuma zaidi zaidi kuona mzee wangu Dr. Slaa yuko nje ya uwanja na mtanitia faraja kidogo walau nirudishe imani kwa Chadema kidogo pale nitapomuona Dr. Slaa ofisi si lazima aende kumnadi Lowassa lakini kwangu mie walau nimuone ofisini tu.

Hilo ndilo ombi langu kwa viongozi wote wa Chadema.

Salum Mwalimu leo umetuhaidi kuwa mwenye ushauri atoe na nyie mtaufanyia kazi, kwenye swali aulize na mtajibu hivyo basi maswali yetu yako katika thread hii na katika ile thread iliyoanzishwa leo na Mwanakijiji.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3, Lowassa katamka kwa mdomo wake na kwa wazi kabisa kwamba kaamua kwa mapenzi yake kuvua gamba na kuvaa gwanda. Yuko aliyekuwa pacha wake Andrew Chenge aka vijisenti aka nyoka wa makengeza, huyu bado yuko CCM na kashinda kwa mbali kura ya maoni jimboni kwake Bariadi kupitia CCM hiyo hiyo inayodaiwa imejitakasa kwa kuondokana eti na fisadi Lowassa. Sina hakika kama ufisadi wa huyu mtu Chenge unalinganishwa vipi na wa Lowassa lakini lilo dhahiri kabisa ni kwamba hakuna ufisadi ulioweza kufanyika nchini usiomhusisha Chenge kwa namna moja ama nyingine kuanzia IPTL wakati wa Mwinyi hadi huu wa juzi wa ESCROW. Ajabu ni kwamba huko CCM hakuna hata mtu anayemsema Chenge, wote ni kama wamepagawa na kitendo cha Lowassa kuwaacha kwenye mataa.

Lowassa katoa maelezo ambayo yawezekana kwa wengine wakayachukulia kama vile hayana ukweli, hilo sawa lakini la muhimu kaongea na kataja kwa nini aliamua kujiuzulu. Wapo watu wanaouliza kwa nini alikaa kimya muda wote...mimi nasema better late than never. Labda alitaka kugombea Uraisi kupitia CCM ili aweze kupata nafasi ya kuuelezea umma ukweli wa kilichojiri na hakuna wakati mzuri kama wakati wa kampeni. Yawezekana hata hao waliokata jina lake walifanya hivyo kwa hofu baada ya kuona alivyochangamkiwa na wananchi wakati anatafuta wadhamini. Yawezekana pia waliamini hawezi kupata ujasiri wa kuchukua hatua kama hiyo aliochukua na hivyo tendo hilo limewafanya wakose amani kabisa mioyoni mwao.

Mpaka sasa hatujui aliwaeleza nini viongozi wa Chadema hadi wakafikia uamuzi wa kumpendekeza awe mgombea wao na ikikubalika wa UKAWA. Bila shaka ndani ya Chadema wako walioafiki na waliopinga na sababu zao lakini mwisho wa siku uamuzi wa wengi uliheshimiwa. Kwamba walihongwa mabilioni ni hoja mufilisi zinazotolewa na watu wasioitakia Chadema/Ukawa mema...dai la mtu kama Tundu Lissu aliyekataa mabilioni ya CCM kumrubuni miaka yote leo hii aje apokee kutoka kwa (fisadi) Lowassa, siamini kama linaweza kuwa kweli. Katika kufuatilia mijadala inayoendelea nimegundua kwamba wengi waliovalia njuga hizo shutuma za Chadema kununuliwa hawajawahi kuwa wapenzi wa kweli wa mabadiliko.

Kama itatokea kwamba lengo hasa la Lowassa kujiunga na upinzani si kama ninavyofikiria, basi natanguliza samahani kwa wote ambao msimamo wangu utakuwa umewakwaza. Lakini kama ameungana na Chadema kwa nia safi baada ya kuuona mwanga mkali kama Saulo na akawa Paulo, namwambia karibu sana kamanda. Ni wachache wetu hapa nchini ambao hata siku moja hatukuwahi kuwa wanachama wa CCM maishani, tulijiondoa kabisa katika siasa hadi pale upepo wa mageuzi ulipofunua kamwanga ka tumaini mwaka 1992. Ujasiri wa Lowassa umenirudisha nyuma hadi mwaka 1989 Mabere Nyaucho Marando alipotamka Baba wa Taifa kafilisika kisiasa.

Wengi tulishtuka na ujasiri aliouchukua na wapo ndugu na marafiki hawakutaka hata kukaa karibu naye; aliogopwa kama ukoma. Muda mfupi baadaye alimkatalia Raisi Mwinyi uteuzi wa kuwa mjumbe katika kamati iliyotafuna mamilioni ya kodi za wananchi kuwauliza kama wanataka uhuru zaidi. Huo ndio nauita ujasiri. Lowassa naye kaonesha ujasiri kwa kiwango chake...mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Zakumi wala sikutaka kulizungumzia tena kwasababu Alinda aliweka ukweli
Hoja si kuchukua fomu , ni kauli za fitna. Kuna tofauti kati ya '' Zakumi nitakupiga na silaha '' na Zakumi nitakupiga na silaha

Mkandara alichoandikaHakuweka alama '' '' bali sentensi kama ilivyo. Kwa sisi wengine hilo lilitosha sana kuona uhuni uliofanyika.

Kufunga ofisi fomu zisichukuliwe ni uhuni wa kulaani. Tulipohitaji ufafanuzi, kaja na kauli , aah ni lugha ya mjini.

Huwezi kuandika uchochezi ukasema ni lugha ya mjini, huo ni uongo na ndiyo fitna.
Hakuzingatia alau kanuni za uandishi, aliongozwa na fitna

Hizi alama '' '' zina maana kwa msomaji. Ukweli ni kuwa hakuna ofisi iliyofungwa

Alipulizwa kwa fomu zipo chini ya mamlaka ya nani. Hakujibu, anachosema Dr Slaa amezuiwa.

Hoja kuu hapa si nani kachukua nani hakuchukua. Ni fitna ya uandishi kwa lengo la fitna.

Tuendelee na mambo mengine ya maana
Sasa wewe ikiwa meza ya kutoa fomu ya Urais imefunguliwa na kufungwa mara baada ya mtu mmoja kuchukua fomu hiyo utasemaje?..Kiswahili gani nunachotaka wewe uambiwe ili uelewe..Kila napojadili na wewe siku zote hukosi kugeuza mjadala ili uwe wangu wakati inaeleweka nilichoandika na kama kisingeeleweka basi wachangiaji wengine wangeendelea kuhoji isipokuwa wewe ukishika jambo basi hata kama umeshindwa hutaki kukubali na ukiona umeshindwa unakimbia mada! nakujua sana. Hukubali kufahamishwa ila kwa lugha yako.

Mbona sisi tunakusoma na kukuelewa na tunachangia kwa hoja zako sio wewe mtu wa aina gani! Hivi nikianza kuzungumzia navyokuchukulia tutafika kweli? Ama unafikiri mimi sijakusoma vizuri na sina la kuzungumzia juu yako wewe..Fitna unayo wewe na wapuuzi wenzako juu ya Zitto na yeyote anayechambua chama chako! na kila mara ukweli huwaponza katika maneno yenu wenyewe maana matokeo huwa tofauti na kile ulichopigania. Anyway nakuacha kama ulivyo!

Zakumi,
Mimi nakuelewa sana na naelewa mfumo wa Chadema toka enzi ya Mbowe na ndicho watu wengi wamekuwa wakijadili kwa miaka. Mimi sikutatizwa na hilo wakati ule kwa sababu jina la mgombea lilitokana na mapendekezo ya vikao vya chama toka halmashauri kuu hadi Kamati kuu hupitia majina kwa sifa na vigezo walivyoweka. Haijawahi kutokea jina la mtu mmoja kutoka nje kuchukua fomu na ndiye akawa mgombea pekee kwa masharti yake. Huyu nguruvi anapenda ubishi wakati wote na mwepesi sana kutukana watu japo tunamvumilia sana, lakini ana mdomo mchafu bado ujana unamsumbua. Busara haziuzwi dukani ajifunze kuheshimu watu kama anavyoheshimiwa laa sivyo hapatakalika humu..
 
Mwalimu,

..lowassa amejieleza kuwa richmond ilikuwa ni amri ya ikulu.

..mpaka sasa hivi sijasikia ikulu ikikanusha. Mara nyingi huwa wako very quick kukanusha.

..kwa hiyo hali hiyo inaacha maswali kama lowassa kweli ana hatia kuhusu kashfa ya richmond.

..wakati huo huo mafisadi wengine kama chenge, tibaijuka, na ngeleja, wameshinda ktk kura za maoni za ccm. Hiyo nayo sijui inakupa picha gani kuhusu wana-CCM na waTz kwa ujumla.

cc Zakumi, Ritz, Mkandara, Nguruvi3, Alinda
Mkuu swala la UFISADI kwa CCM halijawahi kuwa issue isipokuwa kwa vyama vya Upinzani sasa maadam nao wamelikumbatia ina maana gani kwako unapopiga kura mwaka huu? Kwa yeyote yule somo lilipo - Fahamu ya kwamba Ufisadi ni RUKSA! na watu Wadanganyika wameanza kulikubali mengine mtajaza wenyewe...Ila kesho wasije kulia lia hapa na kura zeo wenyewe..
 
Nguruvi3, naomba nikuulize kaswali kamoja tu, inavyoonekana baadhi ya watu wanaonekana wamemvalia njuga Lowassa kwa kiwango cha kutisha, si ndani ya upinzani na si ndani ya CCM. Wote wako tayari kusahau tofauti zao kiungo kikuu kikiwa ni chuki yao dhidi ya mtu moja tu Edward Ngoyai Lowassa. Kwa baadhi ya watu kuondoka kwa Lowassa kunadaiwa kumeitakasa CCM, na kujiunga na Chadema kunadaiwa kumeitia najisi UKAWA. Ufisadi wa Lowassa ukitajwa, watu huamini mara moja lakini ufisadi wa mtu kama Magufuli ukitajwa, miguno inasikika aah wapi bwana mnataka tu kumchafua Bwana Pombe. CCM ilipotufikisha, ufisadi si tena jambo la kushtua, ufisadi umekuwa ni kitu cha kawaida, ufisadi umekuwa kama sehemu tu ya maisha. Asiye fisadi ndiye watu wanashangaa, huyu vipi, kama hataki kula shauri yake asituletee nuksi hapa! Hapo ndipo CCM ilipotufikisha.

Ndugu yangu Nguruvi3, swali langu ni hili...kweli unaamini kwa dhati kwamba katika taifa hili Lowassa ndiye kinara wa ufisadi? Kwamba Lowassa ndiye sura ta ufisadi? Kwamba Lowassa ndiye mwanzilishi wa ufisadi? Kwamba awe serikalini ama nje ya serikali, ufisadi wake ni kama ugonjwa wa kansa, dawa ni moja tu kumkata Lowassa.

Unakumbuka hii orodha aliyoitaja Dr. Slaa viwanja vya chipukizi Tabora kama muendelezo wa orodha ya Mwembeyanga?

Dr.Wilbrod-Slaa.jpg

Sunday, April 17, 2011

Dr SLAA ATAJA ORODHA MPYA YA MAFISADI, WAFIKIA 17

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ametaja orodha mpya ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotuhumiwa kwa ufisadi.
Vigogo hao ni;

  1. [*=left]John Pombe Magufuli, Waziri wa Ujenzi,
    [*=left]John Samwel Malecela, aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu Mwenyekiti wa CCM,
    [*=left]Fredrick Sumaye, aliyekuwa Waziri Mkuu,
    [*=left]Philip Mangula, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM

kwa kuhusika na wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kupitia Benki Kuu. Dk. Slaa alitangaza majina hayo jana mjini Tabora alipokuwa akiwahutubia wanachama na wananchi waliofurika kwenye viwanja vya Chipukizi.

Alisema majina hayo ni muendelezo wa yale ya vigogo wanaotuhumiwa kwa ufisadi aliyoyataja Septemba 15, 2007 katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam ambayo ni 11 akiwemo Rais Jakaya Kikwete.

Katika orodha ya mwaka 2007, Dk. Slaa aliwataja aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), ambaye sasa ni marehemu, Dk. Daudi Balali, Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM) na Basil Mramba aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Rombo (CCM). Wengine ni Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, kada wa CCM, Nazir Karamagi, Mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono (CCM), Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM), Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, na Rais Jakaya Kikwete

Ni Mafisadi 17 aliowataja Dr. Slaa na kati ya hawa wote ni Lowassa tu ameweza kuwa na ujasiri wa kuvua gamba na kuvaa gwanda. Walobaki bado wamo humo humo lakini twaambiwa baada ya kutoka moja na kubaki 16 ndani ya CCM, ufisadi nao umehamia huko huko alikokwenda Lowassa, does this make any sense to anybody?

Ingekuwa ni hivyo CCM wangekuwa wanapiga vigelegele lakini wote tunashuhudia jinsi walivyopigwa butwaa...wanajiuliza huyu mwenzetu kapatwa na nini mpaka anatuacha? Je ni kitu gani wanakililia...je ni kuondokewa na fisadi? Au kuvuliwa kwa gamba? UKAWA naomba mzidi tu kukaza buti, msibweteke na machozi ya samaki ya CCM.

Mag3;

CCM wanajijua vizuri kuwa wao ni mafisadi. Hivyo kwao tatizo sio kujitambua. Wao wanachotaka ufisadi usiwe issue katika uchaguzi. Wanachotaka ni ku-frame uchaguzi huu kuwa wa kumpata rais atakayepigania maendeleo ya mtanzania. Hawataki kampeni iingiliane na mambo ya ufisadi.

Lowassa hawakumkataa siokwa sababu hawampendi. Wanampenda na kawanufaisha sana. Wamemkataa kwa sababu kama angepata nafasi suala zima la ufisadi lingekuwepo. Kwa maoni yangu kama Lowassa angesimama kupitia CCM na Dr. Slaa CDM, Dr. Slaa alikuwa na nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwa sababu alikuwa na ammunitions zote.

Mgombea wa urais ni lazima asimame na kujipigia kampeni. Kitendo cha Lowassa kuwania urais kwa kupitia CDM kutamfanya asizungumze baadhi ya mambo wa kampeni, hususa ni ufisadi. Na hili wanaogombea nafasi mbalimbali kupitia CDM wasimuaibishe Lowassa, nao itabidi wafumbie macho suala zima la ufisadi.

Ukweli wa mambo kuimarika kwa CDM kutategemea sana na matokeo ya uchaguzi. CDM ikishinda urais, kamari ya kumkaribisha Lowassa itakuwa ni mtaji mzuri. Iwapo CDM itashindwa, CDM haitatumia tena karata ya ufisadi kujenga Chama.
 
Niliwahi kusema huko nyuma kabla ya Lowassa hajajiunga Ukawa kuwa tatizo la CCM ni kutaka kutuaminisha kuwa ndani mwa CCM fisadi na mla rushwa, ni Lowassa tu, CCM wanataka tuamini kuwa kwa kujiondoa Lowassa ndani ya CCM basi CCM imekuwa safi kama theruji.

Sasa swali kwa kila mtanzania anayesoma hapa hivi ni kweli ndani ya CCM fisadi ni Lowassa tu? Je tunamsamaje Kinana nyara za serikali? Sitta na chenji ya katiba mpya je? Chenge?Mwakyembe na mabehewa hewa? Pinda na vibari vya sukari? Magufuli na upoteaji wa bil.265? Kikwete na mikataba 16 ya gesi? Kwa hiyo ukiangalia utaona kuwa CCM hakuna msafi kuanzia kwa Mwenyekiti wao mpaka kwa balozi wa nyumba kumi kumi.

Je watanzani wanaelewa dhana nzima ya ufisadi?

Pamoja na shule nzuri iliyotolewa na Chadema kupitia Katibu kwake mkuu Dr. Slaa, lakini unaona mwitikio wa kuchukia ufisadi kwa wananchi walio wengi ni mdogo. Watanzania wengi waishio vijijini ambao wao ndio wanaamua nani awe rais, mbuge na diwani hawana habari na ufisadi tena usherekea wakati wa uchaguzi kwani ndio wakati wa mafuno ya shilingi 500 mpaka 10000 kutegemea na mtu na mtu. Watanzania hawa hawafahamu kuwa matatizo yao yanaletewa na hizo 500 wanazoongwa bali wao wanaamini ni "mapenzi ya Mungu"

Kila mbunge au diwani awe ni mpinzani au CCM atakubaliana nami kuwa katika vijiji vingi kushinda uchanguzi si swala la sera tena au kuimba ufisadi ni swala la mikakati na hongo. Maana katika akili za kawaida huwezi kuhubiri ufisadi hali mgombea mwenzako akigawa rushwa ukategemea utashinda. Hiki kitu wabunge wa upinzani na CCM wanakielewa. Mwanakijiji wa kawaida haamini kuwa mbunge anawakilisha matatizo yake maana wakisha changuliwa uhamia Dar na kwenda vijijini kwa ajili ya uchanguzi, na hii umfanya wananchi kuona ubunge ni sehemu ya kuula sasa huwezi kupewa ulaji bila wewe kutoa kitu kidogo.

Ushuhuda wa kuwa ufisadi na sera nzuri si hoja wa watuchagulio viongozi (wananchi wa vijijini)

Mwaka 2010 wakati swala la Richmond bado likiwa nimeshika kasi, wakati swala la Epa liko kwenye chat tulitegemea kuwa watanzania watakasirika na kutowachagua mafisadi au wala rushwa lakini kilichotokea wote tunakifahamu. Mh. Chenge alirudi tena alishinda kwa kishindo, Mh. Lowassa alishinda kwa kishindo, Rostam alishinda kwa kishindo na hata ninavyoandika hivi sasa wale watuhumiwa wa Escrow wameshinda wote kwa kishindo katika kura za maoni. (nii masikitiko lakini ndio hali halisi)

Vyama vya upinzani wafanye nini? ili ndilo swali ninajiuliza na sipati jibu je maadamu watanzania hawatishwi tena na ufisadi, hawajali kama Lowassa ni fisadi au la, basi waende kiccm na watakapo bahatika kupata uongozi basi warudishe nchi yetu katika msingi? au waendelee kuhubiri wanachokiamini hata kama itawakuchua miaka mingine 20 kuchukua nchi ambayo itakuwa imeshaliwa vya kutosha na miktaba hewa? Nafkiri jibu kila mtu analo kichwa.

....

Alinda:

Unamkumbuka babu wa Loliondo na kikombe chake? Kwa kifupi hiyo ndio siasa ya Tanzania. Kuna watu waliacha madaktari waliowasaidia kwa miaka mingi kukimbia kikombe cha babu ili wapone kabisa. Waliposhindwa kupona waliambiwa hawakuwa na imani na babu hakuwajibika kwa matatizo yao.
 
Kuna mtu anasema mwenye ushahidi wa ufisadi wake aende mahakamani, analeta siasa kasahau kwamba vikaratasi alivyowaandikia kina Msabaha kuwashinikiza na richmond yake watu wanavyo. Natamani Magufuli aliswage mahakamani fisadi hili kwani anao ushahidi.

..hii ngoma inagonga mpaka ikulu.

..umesahau Jk alidai hamjui mmiliki wa dowans lakini watu wakatoa "vizibiti" walivyomuumbua Jk?

..kuna kikao cha halmashauri kuu au kamati kuu Lowassa alianza kumwaga mtama kwenye kuku wengi ikabidi Nkapa aingilie kati kuokoa jahazi.

Cc TUJITEGEMEE
 
Last edited by a moderator:
..hii ngoma inagonga mpaka ikulu.

..kuna kikao cha halmashauri kuu au kamati kuu Lowassa alianza kumwaga mtama kwenye kuku wengi ikabidi Nkapa aingilie kati kuokoa jahazi.

Cc TUJITEGEMEE
JokaKuu, na mimi nakumbuka pale mwanzo kabisa baada ya Lowassa kujiuzulu, kuna siku baada ya kuchoshwa na shutuma zilizoelekezwa kwake alitaka kuwaita waandishi wa habari aeleze kilichojiri kuhusu Richmond, lakini dakika za mwisho akapigwa stop. Leo wapo watu wanauliza kwa nini alikuwa kimya siku zote, wamesahau serikali yetu hii ilivyomfunga luku asiongee. Halafu hapo hapo wanadai serikalini hakukuwepo na mtu wa kuweza kumdhibiti!
Zakumi said:
Unamkumbuka babu wa Loliondo na kikombe chake? Kwa kifupi hiyo ndio siasa ya Tanzania. Kuna watu waliacha madaktari waliowasaidia kwa miaka mingi kukimbia kikombe cha babu ili wapone kabisa. Waliposhindwa kupona waliambiwa hawakuwa na imani na babu hakuwajibika kwa matatizo yao.
Je ni haki kuwalaumu hao wananchi? Wengi walikuwa ni watu waliopoteza tumaini la kupona na mbaya zaidi waliwaona viongozi wao wenye fursa za kupata matibabu popote pale kwa gharama zozote zile wakibugia kikombe. Moja wa hao viongozi hivi sasa kateuliwa kuwa mgombea Uraisi kupitia CCM na kwa wadhifa wake alihakikisha serikali inatenga kiasi kikubwa cha fedha kujenga barabara nzuri hadi kijiji cha Samunge kwa babu.
 
Last edited by a moderator:
JokaKuu, na mimi nakumbuka pale mwanzo kabisa baada ya Lowassa kujiuzulu, kuna siku baada ya kuchoshwa na shutuma zilizoelekezwa kwake alitaka kuwaita waandishi wa habari aeleze kilichojiri kuhusu Richmond, lakini dakika za mwisho akapigwa stop. Leo wapo watu wanauliza kwa nini alikuwa kimya siku zote, wamesahau serikali yetu hii ilivyomfunga luku asiongee. Halafu hapo hapo wanadai serikalini hakukuwepo na mtu wa kuweza kumdhibiti!

Je ni haki kuwalaumu hao wananchi? Wengi walikuwa ni watu waliopoteza tumaini la kupona na mbaya zaidi waliwaona viongozi wao wenye fursa za kupata matibabu popote pale kwa gharama zozote zile wakibugia kikombe. Moja wa hao viongozi hivi sasa kateuliwa kuwa mgombea Uraisi kupitia CCM na kwa wadhifa wake alihakikisha serikali inatenga kiasi kikubwa cha fedha kujenga barabara nzuri hadi kijiji cha Samunge kwa babu.

Mag3;

Kwikwikwi, kweli Tanzania ina mambo. Hata Dr. Magufuli (PhD chemistry) kanywa kikombe. Sasa hao watu wa kawaida wafanye nini?

Tukirudi kwenye mada, naona umefafanua vizuri mfano wangu wa Babu wa Loliondo. Toka nchi imepata inaendeshwa kwa matumaini. Hatujahamua kuvuka na kujaribu ku-think rationally.

Kwa upande wangu mzimu wa matatizo ni CCM na mfumo wake wa utawala. Wasiwasi nilionao ni kuwa hata hivyo vyama vya upinzani vina-behave kama CCM. Simuoni Lowassa kama ni game changer. Atakuwa game changer iwapo ataweza kudhoofisha CCM.

Mimi sio CCM na ningependa upinzani ushinde kwa kishindo kikubwa. Japokuwa simpendi Lowassa, ningependa ujio wake CDM ulete mafanikio. Lakini kwa News ninazozipata ujio wake tayari umewafaidisha baadhi ya watu na kuwadhulumu wengine. Kwa sasa naomba mnishawishi sio kwa kutumia kikombe cha babu bali fikra maendeleo ya upinzani baada ya uchaguzi iwapo hawatafanikiwa kuing'oa CCM.
 
Wadau naomba muangalie video hii mumsikilize Tundu Lissu akihojiwa kuhusu ujio wa Lowassa Chadema;
Gonga hapa chini...

[video]https://youtu.be/EL5eo9bWOHw?t=13[/video]
 
Mkuu swala la UFISADI kwa CCM halijawahi kuwa issue isipokuwa kwa vyama vya Upinzani sasa maadam nao wamelikumbatia ina maana gani kwako unapopiga kura mwaka huu? Kwa yeyote yule somo lilipo - Fahamu ya kwamba Ufisadi ni RUKSA! na watu Wadanganyika wameanza kulikubali mengine mtajaza wenyewe...Ila kesho wasije kulia lia hapa na kura zeo wenyewe..
Ndio hao mimi naposema defender wetu mbowe badala ya kuzuia mipira inayoelekea golini kwetu, ameisukumia kwenye nyavu zetu. Mpaka sasa mbowe ana 2 own goals. Baada ya mechi Novemba tutakuwa tumefungwa dazeni za magoli.
 
Kaka yangu Nguvuri3 hayo maswali unayojiuliza ni maswali anayojiuliza kila mtanzania, kila mtanzania hasiyetaka kuburuzwa, kila mtanzania ambaye amefundishwa na kulelewa katika mazingira ya kuhoji na kuhoji kwa nia nzuri tu ya kupata maelezo ya kuridhisha kwa swala husika.

Watanzania tumezoea kutohoji, tumezoea na kulelewa kuwa mkubwa akisha sema jambo basi wewe unatekeleza, tumefundishwa kuwa kiongozi akisema kitu basi ni sahihi, na huu udhaifu wetu wanautumia sana viongozi wetu kutuamulia mambo hata kwa maswala ambayo hatutaki. (rejea katiba mpya, sheria mbali mbali na hili swala la Lowassa) na kibaya zaidi ukiwauliza maswali wanajibu kwa kejeli na dharau, (rejea Lowassa na Richmond.)

Kama Taifa tunabidi tuwe taifa la kuhoji, taifa la kuwakosoa viongozi pindi pale tunapoona wanakwenda nje ya makubaliano yetu, tuwakatalie pale tunapoona wameweka masilahi yao mbele kuliko maslahi ya nchi. Inawezekana kabisa Lowassa amehojiwa na kamati kuu na kutoa maelezo ya kuwaridhisha lakini hayo maelezo ndo tunataka sisi wananchi wa kawaida kuyasikia kwani waamuzi ni sisi, tutakao kwenda kupiga kura ni mimi na wewe, ni sisi tunahoji lakini kwa bahati mbaya sana viongozi (hawa miungu watu wametia pamba masikioni) kwani vichwani vyao kumejaa zile dhana za kizamani kuwa kiongozi hakakosei, kuwa kiongozi analohamua ndilo na sisi tumekuwa kama watoto yatima hatupatizi sauti zetu kuwambia kuwa "hapana stop" huu mstari havuki maana huu ni mpaka wetu.

.
Kuhoji kuna maana nyingi, kutaka kupata ufafanuzi kabla ya maamuzi, kuwafanya viongozi accountable na kutaka kujua bila kuburuzwa kwa namna yoyote

Huu uwe utamaduni kuliko ilivyo sasa ambako watu hawakubali kuhoji au kuhoji ni tatizo

Mfano, kuna maswali mengi sana nyuma ya huu mpango wao wa EL.

Ukimsikiliza Lissu ni kama walikuwa wanasubiri tatizo ili kutoka hapo wapate fursa.

Ukimsikiliza Mbowe ni kama opportunity presents itself. Ukimsililiza Wenje, ni kama hakuwa informed nini kinaendelea huko kamati kuu

Maamuzi mazito yanahitaji ushiriki wa pamoja. Siyo suala la kanyaga twende.

Lazima wajue wanakwenda wapi na kwa njia gani.

Ukisimkiliza Mbowe anaposema 'si kuzungumzia ya jana tu lazima watu wazungumzie maendeleo' inashangaza.

Hoja si maendeleo ni namna gani watambana CCM mbele ya wananchi, namna gani wanatwaa dola.

Ataongeleaje maendeleo audience yake ikiwa katika 'confusion' na base ikiwa paralyzed.
Hivi Mbowe anayaona haya au ni kanyaga twende. Zipo hoja anatakiwa azijibu na hizo atahojiwa nazo

Pili, hoja zote lazima ziwe mezani. Hii ya ufisadi imetetemesha sana CCM, si lazima iwe hoja kuu, Mbowe hawezi kuibeza leo kwasababu kuna nguvu mpya. Lengo la nguvu anayosema si kuua nguvu iliyopo

Kwa wenzetu kuna kitu wanaita 'attacking dog'' katika uchaguzi.
Unampeleka anayehusika katika kujilinda wakati unashambulia kutoka kona nyingine

Hapa ndipo tunasema, team nzima ingekuwa kamili wangekuwa na fursa sana.

Let wanao ongelea ufisadi wazungumzie na wanaoongelea maendeleo waseme.
Muhimu ni kujipanga na kuhakikisha ujumbe unafika na unasikika

Si suala la kanyaga twende, ni muhimu watu wakajua kila hatua, si suala la kusikia tu huku wakiambiwa picha feki za kuunga, hakuwepo katika kikao which later on tunajua ilikuwa kweli. Handling ya ujio pekee ina maswali!!

Kuna vacuum katika suala zima na haionekani Mbowe kama ana address suala hilo!
 
HILI LA PROF LIPUMBA LINATUELEZA NINI?

Taharuki iliyozuka Buguruni makao makuu ya CUF pengineinahitaji fikra kidogo
Hatuna uhakika kama kuna eneo ambalo Prof ametolea maelezozaidi ya tunayojua.

Zipo tetesi prof aliitisha mkutano wa habariambao haukufanyika kwavile alikuwa na kikao na wazee wa CUF

Tetesi zilizoleta kiwewe ni zile za Prof kutaka kuachana nasiasa. Zipo kauli kuwa prof amewataka wanachama kuisoma katiba na kuielewakwasababu chama si mtu ni taasisi
Lipumba ni mwenyekiti mwenza wa UKAWA akishirikiana naMbowe, Mbatia na Makaidi.
Wamekuwa pamoja kuanzia bunge la katiba hadi kutangaza ujio wa EL

Prof hakuwepo mkutano mkuu wa CDM uliomteuamgombea Urais, jambo lisilo la kawaida kwa UKAWA

Hatujui prof alitaka kuongelea nini, kinachoonekana, mkutanona waandishi wa habari ulikuwa uwe na uzito , mazungumzo na wazee yana uzito nahamaki ya wanachama ina uzito. Lipo jambo linaloendelea tusilo lijua

Kauli ya Lipumba alipoongea kwa ufupi na wanachama,aliwataka wasome katiba na kuielewa na kwamba CUF ni taasisi kubwa na si mtu

NI KIPI KINAMSUKUMA PROF ?
Upo uwezekano mkubwa wa Prof kuachia nafasi yake. Kama hilolitatokea( nadharia tu hatuna uhakika) lazima kutakuwa na sababu zinazomsukumakatika wakati huu anapohitajika zaidi
Wanachama wa CUF waliwahi kumbana kuhusu maafikiano naUkawa.

Ndicho kimetumika kama sababu za Ukawa kuchelewa kupata mgombea. Halindani ya CUF haikuwa nzuri

Je, Prof anataka kuondoka kutokana na mashinikizo anaiopatakutoka CUF?

Je, prof anaondoka kufuatia ujio wa mh EL, nakwanini! ikiwa alikuwa bega kwa bega na wenzake katika vikao

Je, prof ameona ndoto yake ya kuwania tena imezimwa? Je,anahisia za kuburuzwa?
Je, ni mkakati wa Ukawa pengine wamtumie kwa njia nyingine?
Je, ni katika kumpa Duni Haji majukumu kama mgombea mwenzana makamu mwenyekiti?
Kwa namna yoyote, hali ya sintofahamu iliyoikumba Chademainaonekana kuhamia CUF.

Ni mwendelezo wa homa iliyoanzia CCM. Kwa uapnde waUKAWA hili ni moja kati ya mambo ya hatari sana. Kambi zinapokuwa zimeduwaa na muda ukikatika ni jambo la kufikirisha

Wanachama wanaweza kugawanyika kutokana na tafsiri yoyoteanayoweza kutoa Prof kama atajiuzulu.

Hali ya ukinzani ‘tensio' katika kambi ya upinzani inazidi kushika kasi

Ikitokea kuwa EL ni sehemu ya tatizo, watu watahitajimaelezo zaidi.

Iweje viongozi wawili maarufu wawe nje ya mchakato? Ni nani hasaatakuwa nyuma ya mpango mzima?

Tusemezane
 
Mkuu mimi binafsi nimebaki nikiduwaa sana, nahisi swala la EL envision kwenye UKAWA limechangia kuwavuruga hasa kwa CDM, ila kwa CUF ni balaa zaidi maana inachanganya sana kwani nadhani hata kama EL asingekuja CUF bado walikua na mgogoro na UKAWA hasa suala la mgombea Urasi, wafuasi wengi wa CUF walimkataa Dr.Slaa na wakamtaka Prof . Lipumba ndo asimame, hivyo kwao sidhani kama Lowassa ni tatizo, bali wana matatizo yao ambayo hata sijajua nini, labda haswa ni mgongano wa kimaslahi.

Ukiangalia kwa makini, pro.Lipumba alishiriki kwenye hatua zote za kumkaribisha Lowassa UKAWA na hata kumsafisha siku moja kabla hajajiunga rasmi CDM na hata siku ya kupewa kadi Lowassa alimsafisha sana na kumtetea, so kujiuzulu kwake kwa kimantimi itakua ni mgongano na viongozi wenzake zaidi ya uvamizi wa Lowassa UKAWA, Prof. Lipumba ameshabikia sana ujio wa Lowassa UKAWA sasa iweje leo aseme anajitoa?? Kuna jambo nyuma yake ambalo ni sintofaham, na ninadhani wanaoombea hawa watu wafarakanesasa wanaelekea kufanikiwa.

Tulionya muda mrefu kuhusu hili jambo kwenye nyuzi za duru la siasa, na akina Nguruvi3 mlipiga kelele sana kwamba wasipokua makinj na hasa kipindi hiki walichompokea EL watavurugana na ndio tunayaona sasa, let us wait and c hw they will change the situation facing them.
 
Wanaukumbi.

Profesa Lipumba ajiuzulu rasmi uongozi CUF.

Nawaomba radhi sana Wanachama na Wananchi walioniamini na kuonesha mapenzi makubwa ktk Uongozi wangu'

'Najua hili litawashtusha, litawakasirisha, litawafadhaisha. Ndani ya Chama mimi naonekana ni kikwazo'

Naonekana siwezi kuwa na mchango kama Kiongozi ktk Mapambano ya kudai haki sawa'

Nimeona niachie ngazi lakini niendelee kushiriki shughuli nyingine zinazohusu Maendeleo ya Chama Kiuchumi'

'Ninaendelea kuwa Mwanachama wa CUF na nimelipia Kadi ya Uanachama mpaka 2020, sina mpango wa Kujiunga ACT'

Taarifa ya kung'atuka niliitoa August 01 2015, nilisubiri kukamilisha masuala ya UKAWA ndio nitoke'

'Naubariki Umoja wa UKAWA ili tusimamie kupata Katiba iliyopendekezwa na Wananchi'

'Ni kweli nilishiriki kumkaribisha Lowassa UKAWA lakini dhamira na nafsi yangu inanisuta'-

'Tumekaribisha watu wa CCM ambao waliipinga Rasimu ya Katiba, najiuliza tutaweza kusimamia malengo ya UKAWA'

'Nimeona nijikite kwenye kufanya Utafiti wa Ushauri wa masuala ya Uchumi ili kuinua Uchumi wa nchi'

Sijashawishiwa na mtu yoyote kuachia ngazi,ni dhamira na nafsi yangu.. asisingiziwe mtu kwamba amenishauri'

'CUF bado imo ndani ya UKAWA, nitashiriki Kampeni za Uchaguzi kama mwanachama wa kawaida wa CUF'
 
Kuhusu kujiuzulu prof.Lipumba CUF na mgogoro mpya UKAWA,
Mwanakijiji Uliona mbali sana kupinga huu umoja, ni bora kila chama kingesimama chenyewe na hasa CDM maana walijiandaa muda mrefu sana, kwa mtazamo wangu kujiuzulu Prof. Lipumba ni kuibuka mgogoro mpya kabisa ndani ya CUFna hatiame UKAWA na CDM, maana zitaanza sintofam nyingine apart fro Lowassa incoming.

kweli nimeamini siasa ni ngumu mno na akina sisi wenye moyo mwepesi bora tukae mbali kabisa na siasa maana mahesabu yake ni magumu sana na hayatabiriki kirahisi, mtu ambae siku mbili alikua anakusifia na kukupongeza anaweza kukugeuka ndani ya muda mfupi na usiamini kabisa kwamba kakugeuka.

Hili la UKAWA Kusabisha mogogoro kwenye vyama shiriki nililiona muda mrefu sana nikafikiri ni hofu na hisia zangu, kumbe kweli. Kumbe kurubuniwa kwenye siasa ni very possible, let us wait if the game can change.

Kama alivyotabiri Nguruvi3 na wadau wengine, migogoro iliyokuwa CCM sasa imehamia rasmi UKAWA na kuwavuruga, na mbaya zaidi kwao muda sio rafiki kabisa kuelekea Uchaguzi na hawajaota mizizi kupambana na migogoro hasa kipindi hiki, sijui nini kitatokea kuwanusuru ila naona maadui zao UKAWA wanakaribia kushinda, labda game changer itokee maana siasa haitabiriki, bt so far UKAWA are looser
 
Mkuu mimi binafsi nimebaki nikiduwaa sana, nahisi swala la EL envision kwenye UKAWA limechangia kuwavuruga hasa kwa CDM, ila kwa CUF ni balaa zaidi maana inachanganya sana kwani nadhani hata kama EL asingekuja CUF bado walikua na mgogoro na UKAWA hasa suala la mgombea Urasi, wafuasi wengi wa CUF walimkataa Dr.Slaa na wakamtaka Prof . Lipumba ndo asimame, hivyo kwao sidhani kama Lowassa ni tatizo, bali wana matatizo yao ambayo hata sijajua nini, labda haswa ni mgongano wa kimaslahi.

Ukiangalia kwa makini, pro.Lipumba alishiriki kwenye hatua zote za kumkaribisha Lowassa UKAWA na hata kumsafisha siku moja kabla hajajiunga rasmi CDM na hata siku ya kupewa kadi Lowassa alimsafisha sana na kumtetea, so kujiuzulu kwake kwa kimantimi itakua ni mgongano na viongozi wenzake zaidi ya uvamizi wa Lowassa UKAWA, Prof. Lipumba ameshabikia sana ujio wa Lowassa UKAWA sasa iweje leo aseme anajitoa?? Kuna jambo nyuma yake ambalo ni sintofaham, na ninadhani wanaoombea hawa watu wafarakanesasa wanaelekea kufanikiwa.

Tulionya muda mrefu kuhusu hili jambo kwenye nyuzi za duru la siasa, na akina Nguruvi3 mlipiga kelele sana kwamba wasipokua makinj na hasa kipindi hiki walichompokea EL watavurugana na ndio tunayaona sasa, let us wait and c hw they will change the situation facing them.
Hivyo hivyo hata wafuasi wengi wa Chadema pia walikuwa hawamtaki Prof Lipumba.

Lakini hatuwezi kuhukumu kitu ambacho akijatokea.

Tuangalie hali ya sasa ya UKAWA bado inabakia kuwa tumaini la wataka mageuzi?
 
Nilitegemea CUF kujiondoa Ukawa kuliko Pro. Lipumba kuondoka CUF. Maana dalili za Cuf kujiondoa Ukawa zilishaanza hata kabla ya Lowassa hajaingia Ukawa.

Siasa za Tanzania ni mgumu, watanzania na viongozi wa vyama vya ni wapenda pesa na hii ndo imekuwa kete ya chama cha mapinduzi siku zote. Nasema hivyo kwa sababu mwaka 2010 Prof. Lipumba aliongoza kampeni ya kupigia kura chama cha mapinduzi na kuwacha chama chake kikiibuka na kura laki 6. Kwa akili za kawaida kiongozi gani wa chama cha upinzani aliye "serious" na kujenga chama chake, kutaka kukuza chama chake anaweza kupingia kampeni chama tawala bila yeye binafsi kufaidika?

Nimekuwa nikijiuliza ni faida gani kiongozi wa chama cha siasa kuwa mgombea wa kudumu cha chama cha siasa lakini baadaye nilikuja kugundua hii ni biashara kama biashara nyingine na wakati wa uchaguzi ndio wakati wa mavuno.

Siwezi kusema kuwa Pro. Lipumba kahongwa kama ilivyokuwa mwaka 2010 alipotosa chama chake ila kwangu mimi ninapata ugumu wa kushawishiwa kuwa Pro. Lipumba ameachia ngazi kwa faida ya watanzania na wanacuf kwa ujumla.
 
Nilitegemea CUF kujiondoa Ukawa kuliko Pro. Lipumba kuondoka CUF. Maana dalili za Cuf kujiondoa Ukawa zilishaanza hata kabla ya Lowassa hajaingia Ukawa.

Siasa za Tanzania ni mgumu, watanzania na viongozi wa vyama vya ni wapenda pesa na hii ndo imekuwa kete ya chama cha mapinduzi siku zote. Nasema hivyo kwa sababu mwaka 2010 Prof. Lipumba aliongoza kampeni ya kupigia kura chama cha mapinduzi na kuwacha chama chake kikiibuka na kura 600. Kwa akili za kawaida kiongozi gani wa chama cha upinzani aliye "serious" na kujenga chama chake, kutaka kukuza chama chake anaweza kupingia kampeni chama tawala bila yeye binafsi kufaidika?

Nimekuwa nikijiuliza ni faida gani kiongozi wa chama cha siasa kuwa mgombea wa kudumu cha chama cha siasa lakini baadaye nilikuja kugundua hii ni biashara kama biashara nyingine na wakati wa uchaguzi ndio wakati wa mavuno.

Siwezi kusema kuwa Pro. Lipumba kahongwa kama ilivyokuwa mwaka 2010 alipotosa chama chake ila kwangu mimi ninapata ugumu wa kushawishiwa kuwa Pro. Lipumba ameachia ngazi kwa faida ya watanzania na wanacuf kwa ujumla.
Samahani naomba ufafanuzi kidogo Prof Lipumba, alipata kura 600 kwenye kwenye uchaguzi gani?
 
Mkuu mimi binafsi nimebaki nikiduwaa sana, nahisi swala la EL envision kwenye UKAWA limechangia kuwavuruga hasa kwa CDM, ila kwa CUF ni balaa zaidi maana inachanganya sana kwani nadhani hata kama EL asingekuja CUF bado walikua na mgogoro na UKAWA hasa suala la mgombea Urasi, wafuasi wengi wa CUF walimkataa Dr.Slaa na wakamtaka Prof . Lipumba ndo asimame, hivyo kwao sidhani kama Lowassa ni tatizo, bali wana matatizo yao ambayo hata sijajua nini, labda haswa ni mgongano wa kimaslahi.

Ukiangalia kwa makini, pro.Lipumba alishiriki kwenye hatua zote za kumkaribisha Lowassa UKAWA na hata kumsafisha siku moja kabla hajajiunga rasmi CDM na hata siku ya kupewa kadi Lowassa alimsafisha sana na kumtetea, so kujiuzulu kwake kwa kimantimi itakua ni mgongano na viongozi wenzake zaidi ya uvamizi wa Lowassa UKAWA, Prof. Lipumba ameshabikia sana ujio wa Lowassa UKAWA sasa iweje leo aseme anajitoa?? Kuna jambo nyuma yake ambalo ni sintofaham, na ninadhani wanaoombea hawa watu wafarakanesasa wanaelekea kufanikiwa.

Tulionya muda mrefu kuhusu hili jambo kwenye nyuzi za duru la siasa, na akina Nguruvi3 mlipiga kelele sana kwamba wasipokua makinj na hasa kipindi hiki walichompokea EL watavurugana na ndio tunayaona sasa, let us wait and c hw they will change the situation facing them.

KS:

Mpaka sasa hivi ni CCM ndio wanaoongoza wanao-control utaratibu wa uchaguzi. Vyama vingine vinafanya improvisation kutokana na matukio muhimu ya CCM. Kwa maneno mengine vyama vingine vimelazimishwa au vimejilamisha kuwa Askari wa Zima moto.

Kutokana na mtaji huu, viongozi wa juu wa CDM na CUF walifanya maamuzi magumu kutokana na muda uliopo. Katika kipindi cha wiki moja au mbili huwezi kuwashawishi wanachama wote kuwa Lowassa ni mtu mzuri.

Kutokana na maamuzi hayo magumu, Lipumba amekuwa majeruhi. CDM wasipofanya vizuri kwenye uchaguzi, Mbowe atakuwa majeruhi mwingine.
 
Back
Top Bottom