Alinda
Platinum Member
- Jun 26, 2008
- 1,695
- 2,149
Kaka yangu Nguvuri3 hayo maswali unayojiuliza ni maswali anayojiuliza kila mtanzania, kila mtanzania hasiyetaka kuburuzwa, kila mtanzania ambaye amefundishwa na kulelewa katika mazingira ya kuhoji na kuhoji kwa nia nzuri tu ya kupata maelezo ya kuridhisha kwa swala husika.
Watanzania tumezoea kutohoji, tumezoea na kulelewa kuwa mkubwa akisha sema jambo basi wewe unatekeleza, tumefundishwa kuwa kiongozi akisema kitu basi ni sahihi, na huu udhaifu wetu wanautumia sana viongozi wetu kutuamulia mambo hata kwa maswala ambayo hatutaki. (rejea katiba mpya, sheria mbali mbali na hili swala la Lowassa) na kibaya zaidi ukiwauliza maswali wanajibu kwa kejeli na dharau, (rejea Lowassa na Richmond.)
Kama Taifa tunabidi tuwe taifa la kuhoji, taifa la kuwakosoa viongozi pindi pale tunapoona wanakwenda nje ya makubaliano yetu, tuwakatalie pale tunapoona wameweka masilahi yao mbele kuliko maslahi ya nchi. Inawezekana kabisa Lowassa amehojiwa na kamati kuu na kutoa maelezo ya kuwaridhisha lakini hayo maelezo ndo tunataka sisi wananchi wa kawaida kuyasikia kwani waamuzi ni sisi, tutakao kwenda kupiga kura ni mimi na wewe, ni sisi tunahoji lakini kwa bahati mbaya sana viongozi (hawa miungu watu wametia pamba masikioni) kwani vichwani vyao kumejaa zile dhana za kizamani kuwa kiongozi hakakosei, kuwa kiongozi analohamua ndilo na sisi tumekuwa kama watoto yatima hatupatizi sauti zetu kuwambia kuwa "hapana stop" huu mstari havuki maana huu ni mpaka wetu.
Ndugu watanzani wezangu tunahitaji kufahamu tena kwa maelezo ya kina ni kwanini achaguliwe Lowassa ni kwanini Dr. Slaa yuko nje ya uwanja. Ni maswali na yanaeleweka hayahitaji kuwa na degree ili uweze kuyajibu, lakini majibu yake yana mantiki kubwa kwetu sisi, majibu ya haya maswali ndio yatatufanya kuona kuwa viongozi ni waajiri wetu, kuwa viongozi wanathamini mchango wetu, kwamba na sisi tunathaminiwa, kwamba tunaweza kuwakatalia viongozi na nk.
Hivyo basi Mbowe, John Mnyika , Tumaini Makene , Salum Mwalimu Tundu Lissu, Lowassa na wengineo huu si wakati wa kuburuzana si wakati wa kutufanya watoto yatima, si wakati wa nyie kuwa miungu watu, ni wakati wa kujibu maswali yetu na kutuondoa wasiwasi,
Tunataka kujua nini hatima ya Dr. Slaa? Mchango wa mzee huyu katika kujenga chama unaeleweka, nakumbuka picha nilizoziona wakati yuko Kigoma mzee wa watu wakimpopoa mawe kwa ajiri ya Chadema hivi leo hii huyu mtu hana maana tena mwenye maana ni Lowassa? Na kibaya zaidi tukihoji hatupati jibu..
Huyu mzee ni mtu mwenye busara sana, mtu mwenye maono na kama hasingekuwa anapenda chama chake alichokijenga kwa mikono yake miwili tena kuliko kiongozi yeyoye yule ndani ya Chadema angekuwa ameishaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutangaza kujihudhuru lakini kwa busara zake, kwa upendo kwa chama chake ameamua kukaa kimya ili hasiharibu hata alichojenga. Tumpeni heshima yake msikilizeni Mzee wetu anataka nini kwa chama chake alichojenga kwa jasho lake hali Mbowe na viongozi wengine wakipaa na angani.
Leo hii rudhuku ya Chadema ambayo imefanya mambo makubwa, ambayo imeibua viongozi wa serikali za mitaa ni mchango wake, angekuwa mtu mwingine wakati wanamkurupusha kwenda kugombea urais basi angekataa maana alifahamu kabisa kuwa hawezi kushinda urais, lakini aliamua kuachana na ubunge, kuhama kutoka katika jimbo lake na kuhamia Dar ili ajenge chama. Tunafahamu kuwa Chama kilimpangishia nyumba lakini kwa kuona kuwa hela inayolipwa na chama kwa pango lake ni kubwa aliamua kujenga nyumba yake tena kwa mkopo. Kiongozi wa jinsi hii hawapatikani kirahisi nchini Tanzania
Pamoja na kuumizwa sana na uamuzi wa Chadema kuhusu Lowassa, lakini kinachoniuma zaidi zaidi kuona mzee wangu Dr. Slaa yuko nje ya uwanja na mtanitia faraja kidogo walau nirudishe imani kwa Chadema kidogo pale nitapomuona Dr. Slaa ofisi si lazima aende kumnadi Lowassa lakini kwangu mie walau nimuone ofisini tu.
Hilo ndilo ombi langu kwa viongozi wote wa Chadema.
Salum Mwalimu leo umetuhaidi kuwa mwenye ushauri atoe na nyie mtaufanyia kazi, kwenye swali aulize na mtajibu hivyo basi maswali yetu yako katika thread hii na katika ile thread iliyoanzishwa leo na Mwanakijiji.

Last edited by a moderator: