CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Ni matokeo ya kutowafikiria wananchi ila tu Ikulu, anayekomolewa ni mwananchi si CCM. Yalishaonekana.
Anaita sasa!
Swali linalokuja, je, hicho ndicho wananchi wanataka?
Je, hiyo itakuwa suluhu ya kudumu itakayojenga misingi imara ya taifa, utaifa na maendeleo?
 
TIFU LA CHADEMA
Dr Slaa akaa kando


Timbwili la CDM limechukua sura mpya , Mbowe kuliambia baraza kuu kuhusu ‘kukaa kando'kwa Dr Slaa

Ukweli umejulikana,Dr Slaa ameonekana kukinzana na maamuzi ima akishiriki au yakipelekwa puta.
Duru tunaamini kukaa pembeni ni sifa ya kusimama kwa anachoamini ni sahihi


Slaa alisimamia ukweli, CCM ikamtosa. Akasimamia ukweli upinzani, nao wamemtosa
Hata pale alipohitajika, Slaa aliamini hivyo na kuacha fursa zake ili atumkie umma

Slaa ni alama ya ukweli ndani ya upinzani. Hana mvuto mkali kisiasa(Charisma) kama inavyodhaniwa, ana kitu kisicho cha kawaida, anasimama katika ukweli, mwingi wa busara na mvumilivu

Sifa hizo zimeteka nyoyo za watu akiwa alama ya maridhiano,ukweli na haki dhidi ya uhuni wa watawala.
CDM ipo moyoni mwa watu kupitiaSlaa.


Kauli zake zimekuwa majibu ya matatizo au mitafaruku iliyorindima ndani ya CDM
Kukaa pembeni ni katika kuamini kuwa nchi inataka mabadiliko ya dhati.


Mabadiliko lazima yawe ya kweli na yanahitajika,lakini,ni lazima yaakisi hali ya baadaye ya nchi na siyo ‘cosmetic changes'

Duru tumesema , wananchi wasimame katika ukweli,utaifa, maono na mitazamo mipana na ya muda mrefu .

Haitoshi tu kuiondoa CCM kama mabadiliko ya muda mfupi, ni muhimu kuangalia mabadiliko yatajengaje nchi kwa muda mrefu?

Dr Slaa amesimama na kile anachoamini ni kweli kwa mujibuwake. Alichoeleza na kile asichoweza kukikana

Uamuzi wake ni ishara ya busara, haku ufanya nyuma ya pazia wala kuhujumu CDM

Amesimama mchana na kusema hakubaliani na hawezi kuwa katika safari asiyoiamini.

Hili linamjengea heshima mbele ya jamii. Watu kama Slaa wanatoa mifano ya kuwajibika kwa heshima na uadilifu

Hawasubiri kuzikirihisha nafsi zao pembeni au kusimamia wasichokiamini.

Kwa wale wanaosema tofauti kati ya Slaa na Zitto, hiki ndicho tumekuwa tunasema

Kiongozi asiyeridhika na maamuzi anasema wazi, si kuunda magenge ya uhujumu akiwa ndani.

Dr Slaa amejenga heshima sana na mfano mzuri


Uamuzi

Uamuzi wa Slaa si uasi au uhalifu, ni uungwana. Wasiokubaliana naye, wakubali jambo moja, uamuzi wake uheshimiwe, umefanyika mchana bila kificho,majungu au hujuma

Ni mfano kwa wanasiasa, penye kuhitilifiana, awaye, asimame na kuhesabiwa

Tuheshimu maamuzi yaliyogusa kazi, nafsi,nafasi,maisha, na mtazamo wake mbele ya jamii.

Ni mambo magumu yaliyohusisha uhai na si busara kuyafanyia dhihaka au kejeli


Slaa anaujua vema ukweli kwasababu ameishi' live' nao

Inaendelea sehemu ya II
 
Sehemu ya II

BARAZA KUU NA MBOWE

Tulisema, Mbowe anawajibika kueleza sintofahamu iliyotawalamuda mrefu. Ukimya umeleta madhara tukijua aliujua .

Habari za mitandao zimevuruga taswira wanachama kuhitilifiana, na mahasimu kuingiza fitna, uongo na uchaonganishi

Maelezo yake ndani ya baraza kuu yanaacha ukakasi midomoni.

Mbowe anasema, uamuzi ulizingatia tafiti za kisayansi na kuwamuda si mshiriki mzuri ' ‘time and tide awaits no body'

Maelezo yanatafoutiana na Kauli ya Lissu. Akihojiwana AyoTV Lissu alisema suala la kuvizia makapi ya CCM ilikuwa mkakati wakijua lolote linaweza kutokea https://www.youtube.com/watch?v=EL5eo9bWOHw

Hili linajibu hoja za FJM na Mzee Mwanakijiji, haikuwa suala la tukio bali kupanga.

Wakati Mbowe anasema ' muda na wimbi' havimsubiri mtu,ilikuwaje waliweza kusubiri muda wote huo CCM wakiparurana?

Tena walisubiri CUF wafanye mikutano yao. Na muda wote Mbowe aliaminisha umma majadiliano ya UKAWA yalikuwa yanaendelea vema

Mbowe anasema, ni uamuzi wa wengi, hawawezi kumsubiri mtu.

Hoja, je ni suala la wingi au busara? Kama ni wingi, vipi alilalamika CCM walipotumia wingi bungeni?

Hatudhani ni suala la wingi, kama wingi ungekuwa ni suluhu, chama alichokijenga Slaa kwa haiba yake kingalikuwa mbali kwa kutumia wingi huo si kusubiri makapi. Wapi haiba ya wingi ilipo?

Maamuzi magumu hayapimwi kwa wingi, yanapimwa kwa uzito wahoja.

Hoja ya Mbowe inashaaria kutokuwa na hoja ya msingi yakutengua hoja za Slaa

Mbowe anasema, chama hakiwezi kuongelea ya jana, lazima kiongelee maendeleo ya kesho,akimaanisha hakuna haja ya kuongelea ufisadi tu bila maendeleo.

Inasikitisha, huwezi kuongelea maendeleo kama hujaongelea vikwazo vya maendeleo.

Na hakuna anayezuia CDM wasiongelee maendeleo na hiyo haiwezi kuwa sababu ya kukubali team EL au kumtosa Dr Slaa

Mbowe. amesahau agenda ya ufisadi ndiyo imewafikisha CCM katika kingo

Ni agenda mbele ya wananchi ya kuizungumza ,CCM iendelee kujitetea wapinzani wakishambulia hoja na sera.

Kucheza na hoja ya maendeleo ni kucheza ngoma yaCCM. Mbowe anajua mapigo yake au anatamani mirindimo ?


Kuiacha hoja iliyo kama ‘theme' ya chama kwa kukumbatia hoja ya CCM ni kauli isiyozingatia hali halisi

Anasema,tafiti za wataalam wa Poll zinaonyesha ilikuwamuhimu kukubali ujio wa EL.

Hakutueleza tafiti zilizingatia kushinda uchaguzi au hali yakisiasa nchini. Kushinda uchaguzi ni suala moja, namna ya kushinda ni sualajingine. Je, tafiti zilizingatia mambo kama tume ya uchaguizi navyombo vya dola

Je, tafiti zilizingatia matarajio, matamanio, kiu na adha yawananchi wa Tanzania?

Tatizo la tafiti za nje ni kutoelewa hali ya kisiasa nchi.

Nchi yetu huwezi kuilinganisha na nchi zingine ambazo chaguzi hutawaliwa na itikadi, rekodi na na mipango mezani

Hii ‘Kanyaga' twende ni ya kwenda wapi, kwa lengo gani na nini end goal yake.

Mbele ya safari hoja zinazoipambanua CDM na CCM kama mfumo mbaya, ufujaji na wizi zitakataliwa kwa hoja gani?

Ni maendeleo yapi anayotegemea kuongelea mbele ya CCM?

Je, hilo si kutoa unafuu kwa CCM kunoa mapanga na kumaliza upinzani?


Inaendelea III
 
Sehemu ya III

Ujio wa EL ulijadiliwa kwa hoja za nguvu na si nguvu ya hoja. Kutegemea tafiti za nje badala ya hali halisi kuna shaka.

Matatizo ya wananchi ni mengi, rushwa na ufisadi vinaongoza. Hoja ya rushwa na ufisadi ndiyo iliyoitetemesha CCM na kuifikisha ukingoni. Hiyo ni slogan ya wapinzani kuelekea uchaguzi Mbowe hawezi kuibeza

Kuiacha hoja hiyo kwa sababu tu kuna nguvu nyingine ni kujikana. Leo CDM/UKAWA wanarudi mtaani kwa slogan ipi?

Slogan (kibwagizo) cha rushwa na ufisadi kilibeba ujumbe wa maadili, uadilifu haki na usawa.
Kilibeba ujumbe na si mada kamili.


Ni kipi kimetokea tofauti hadi kupiga U-turn? Je, waaminiwe kwa principle gani wanazosimamia na kuzitetea?

Kuelekea uchaguzi, CDM/UKAWA wana changamoto watakazokumbana nazo nje ya tafiti zao

1 Wananchi wanataka mabadiliko. Je, mabadiliko ni kubadili watu au mfumo?

2 Kwa muda uliobaki, ni hoja gani watakayobeba mbele ya mahakama ya wananchi.

3 Mbowe na CDM wataamshaje ari ya ‘base' yao wakiwa katika sintofahamu iliyopo?

4 Mbowe anakabiliana vipi na ujio wenye nguvu unaotishia uwepo wa chama chake

Mwisho,maamuzi yaliyofikiwa hayakufanyiwa kazi kikamilifu wala kuwa shirikishi.

Morali ya wananchi imeshuka na kuchanganyikiwa. Katika muda mfupi ujao,CDM/UKAWA wanaenda mbele ya wananchi wakiwa na ujumbe gani,na wanaamini nini katika kuibadili nchi

Huu uwekezaji ni hatari kwa mustakabali wa demokrasia na maendeleo.

Taasisi haiwezi kuwa mtu na wala haijengwi kwa matofali ya barafu.

Tunarudia ,wekezaji haukuwa sahihi na tafiti haziuzngatia uhlisia. Haikufanyiwka tathmini kwa kuzingatia hali halisi.

Waliodhani CCM imebanwa, kwa hili inapumua. Hakukuwa na sababu za wapinzani kununua ugomvi wala uharaka wa kwenda bila uhakika.

Kama wapinzani hawakuweza kujipanga kwa miaka 10 na leo wanasubiri kupangwa, hali ya nchi kubadilika inatia shaka.

Uamuzi wa CDM/UKAWA unashaka zaidi ya matumaini. Wanaokataa wekezaji huo wana hoja! wasibezwe

Tusemezane
 
Nakumbuka mara tu ya mchakato wa uteuzi mgombea uraisi wa CCM ulipomalizika na Dr Magufuli kuibuka kidedea reaction ya wachache niliobahatika kukumbana nao ilikuwa kama vile upinzani hauna chance ya kushinda... Nilisikia baadhi wakisema "kwa kweli mimi naunga mkono upinzani lakini kwenye uraisi nampa kura yangu Magufuli"!

Inawezekana hii isiwe majority ya mtazamo wa wanaopenda upinzani lakini inatoa picha fulani juu yetu sisi watanzania msimamo wetu uko vipi. Tunaweza kuwajadili viongozi wa CHADEMA/UKAWA na kuwapima kwa vigezo vya uadilifu, msimamo usioyumba n.k. lakini kuna wakati huwa najiuliza kama hivi ni vigezo ambavyo sisi kama wananchi wa kawaida tunaviishi? Yapo mengi ambayo upinzani ulipaswa kufanya ambayo hayajafanyika lakini najiuliza pia kuhusu nini nafasi yetu sisi wananchi wa kawaida kwenye kuleta mabadiliko?

Endapo Lowassa angeamua kubaki CCM baada ya kuenguliwa na akamunga mkono Magufuli nafasi ya CDM/UKAWA kushinda ilikuwa vipi? Endapo Lowassa angeshinda uteuzi wa mgombea urais kupitia CCM nafasi ya CDM/UKAWA kushinda ilikuwa vipi?

Leo hii CCM kwa kuondoka Lowassa imetakasika na kuwa ni safi inayostahili kupewa ridhaa ya kutawaka miaka mingine 5?
 
Mwalimu,

..lowassa amejieleza kuwa richmond ilikuwa ni amri ya ikulu.

..mpaka sasa hivi sijasikia ikulu ikikanusha. Mara nyingi huwa wako very quick kukanusha.

..kwa hiyo hali hiyo inaacha maswali kama lowassa kweli ana hatia kuhusu kashfa ya richmond.

..wakati huo huo mafisadi wengine kama chenge, tibaijuka, na ngeleja, wameshinda ktk kura za maoni za ccm. Hiyo nayo sijui inakupa picha gani kuhusu wana-CCM na waTz kwa ujumla.

cc Zakumi, Ritz, Mkandara, Nguruvi3, Alinda
 
Last edited by a moderator:
Mwalimu,

..lowassa amejieleza kuwa richmond ilikuwa ni amri ya ikulu.

..mpaka sasa hivi sijasikia ikulu ikikanusha. Mara nyingi huwa wako very quick kukanusha.

..kwa hiyo hali hiyo inaacha maswali kama lowassa kweli ana hatia kuhusu kashfa ya richmond.

..wakati huo huo mafisadi wengine kama chenge, tibaijuka, na ngeleja, wameshinda ktk kura za maoni za ccm. Hiyo nayo sijui inakupa picha gani kuhusu wana-CCM na waTz kwa ujumla.

cc Zakumi, Ritz, Mkandara, Nguruvi3, Alinda

Kwa kuondoka kwa Lowassa watanzania watasahau kabisa kuhusu hawa wengine waliobaki na isitoshe watawapigia kura kuwarudisha mjengoni.
 
Mwalimu,

..lowassa amejieleza kuwa richmond ilikuwa ni amri ya ikulu.

..mpaka sasa hivi sijasikia ikulu ikikanusha. Mara nyingi huwa wako very quick kukanusha.

..kwa hiyo hali hiyo inaacha maswali kama lowassa kweli ana hatia kuhusu kashfa ya richmond.

..wakati huo huo mafisadi wengine kama chenge, tibaijuka, na ngeleja, wameshinda ktk kura za maoni za ccm. Hiyo nayo sijui inakupa picha gani kuhusu wana-CCM na waTz kwa ujumla.

cc Zakumi, Ritz, Mkandara, Nguruvi3, Alinda
Mkuu JokaKuu , tatizo si ushiriki wa Lowassa moja kwa moja.

Tatizo linalomkabili ni kushindwa kusimama na umma wakati hujuma inaendelea.

Kwa mfano, alipoita kikao cha makatibu wakuu, ni wazi alijua kuna jambo lisilo sawa sawa.

Wabunge walipotaka uchunguzi ufanyike, ni yeye kama kiongozi wa serikali alikuwa mstari wa mbele kutaka kuzuia hoja

PCCB walipokwenda na uchunguzi feki, Lowassa alisimama na kutetea uchunguzi huo akisema suala limefika mwisho

Shelukindo aliposema kuna jambo, Lowassa hakusimama na kusema' wait a minute' inawezekana. Alisimama na serikali

Tume ya Mwakyembe iliptoa taarifa, yeye hakueleza tatizo, kasema ilikuwa ni uwaziri mkuu

Ukiangalia kwa undani, yeye kama kiongozi alijua lipo lisilo sahihi.

Je alisimama katika ukweli au alisimama kutetea ukweli wa masilahi ya nafasi yake?

Hapa ndipo ndipo tunahoji 'moral authority' yake

Na tunahoji ziko wapi zile values Cdm ilizosimama nazo kuhusu masilahi ya taifa
 
Mwalimu,

..lowassa amejieleza kuwa richmond ilikuwa ni amri ya ikulu.

..mpaka sasa hivi sijasikia ikulu ikikanusha. Mara nyingi huwa wako very quick kukanusha.

..kwa hiyo hali hiyo inaacha maswali kama lowassa kweli ana hatia kuhusu kashfa ya richmond.

..wakati huo huo mafisadi wengine kama chenge, tibaijuka, na ngeleja, wameshinda ktk kura za maoni za ccm. Hiyo nayo sijui inakupa picha gani kuhusu wana-CCM na waTz kwa ujumla.

cc Zakumi, Ritz, Mkandara, Nguruvi3, Alinda

Jokakuu;

Katika mlolongo wa maisha binadamu wanafanya makosa. Kuhusiana na kashfa ya Richmond, ngoja tumkubalie Lowassa kuwa Ikulu ilifanya makosa. Au kwa kuongezea watanzania wote tulifanya makosa. Kwa maana nyingine tumsafishe kutoka kwenye kashfa hiyo.


Lakini tukirudi kwenye masuala ya tabia za bnadamu ziwe mbaya au nzuri kuna kitu kimoja kinajionyesha pattern. Au kwa maneno mengine kujirudiarudia kwa tabia. Watu wanaoshutumiwa kuwa ni mafisadi hawajafanya vitendo vyao mara moja na kuacha. Wamefanya mara nyingi na zipo patterns za kuthibitisha.

Swali je tukimsafisha Lowassa kutoka kwenye Richmond, bado atakuwa mtu safi? Kama sio mtu safi, basi kuhusika kwake au kutohusika kwake hakumpi sifa zozote ubora wa uongozi.

Kwanini Nyerere alimzuia 1995 asiwe rais? Au alimuonea tu? Mwishoni mwa 2005 baada ya JK kuchaguliwa kuwa rais alifanya ziara Marekani. Kwenye mkutano wake na watanzania waliopo DC, kijana mmoja kwa hasira aliuliza bila kupewa nafasi, kwanini umemteua Lowassa kuwa waziri mkuu wakati ni mla rushwa. Wakati huo hata neno fisadi ilikuwa halijapamba moto Tanzania.

cc Alinda, Mkandara, Ritz, Kichuguu, Mzee Mwanakijiji, Jasusi, Mag3, Nguruvi3,
 
Mwalimu,

...kwa mtizamo wangu wa-tz wako too busy na matatizo yao.

..hoja ya ufisadi peke yake haiwezi kuwapa ushindi wapinzani.

..wapinzani waingie ikulu au bungeni kwa mbinu zkzote zile. Wakifika huko ndiyo watakuwa na ubavu wa kutokomeza ufisadi.

..upinzani ukishindwa safari hii basi ujue ccm itatawala miaka mingi ijayo. Yaani itakuwa ni sawa na kurudi mwaka 92.
 
Last edited by a moderator:
Mwalimu,

...kwa mtizamo wangu wa-tz wako too busy na matatizo yao.

..hoja ya ufisadi peke yake haiwezi kuwapa ushindi wapinzani.

..wapinzani waingie ikulu au bungeni kwa mbinu zkzote zile. Wakifika huko ndiyo watakuwa na ubavu wa kutokomeza ufisadi.

..upinzani ukishindwa safari hii basi ujue ccm itatawala miaka mingi ijayo. Yaani itakuwa ni sawa na kurudi mwaka 92.
Mwalimu, hivi ndivyo nilivyomjibu Mzee Mwanakijiji huko jukwaa la siasa; naomba nisikie na maoni yenu wengine kwa sababu nimejikuta natofautiana sana na msimamo wa colleagues ambao tumekuwa pamoja sana kwa mambo mengi. Mimi naamini tatizi letu kubwa kama taifa ni CCM. Everything else takes second place, could I be wrong?

Mag3 said:
Nina maswali mawili tu kwako Mzee Mwanakijiji;


  1. Kwa nini umewataja tu wana Chadema kuongoza kampeni hali unajua wazi kwamba Lowassa akiteuliwa kugombea Uraisi, atakuwa atakuwa ameridhiwa na UKAWA na si Chadema peke yake?
  2. Hivi Dr. Slaa alitayarishwa kwa muda mrefu kugombea Uraisi kupitia Chadema au UKAWA?

Nimeuliza haya maswali nikiwa na sababu kubwa moja, kupata mgombea muafaka kupitia UKAWA kulihitaji maridhiano na si vinginevyo. Kwangu niliamini maridhiano hayo yangetakiwa yazingatie mambo mawili;


  1. Nguvu aliyonayo mteuliwa ndani na nje ya UKAWA
  2. Uwezo wa kuibua sintofahamu ndani ya Chama tawala.

Mwisho naomba niweke jambo moja linalosahaulika kila wakati UFISADI wa Lowassa unapotajwa. Orodha ya mwaka 2007 pale Mwembeyanga ulitaja watu wanane waliohusika moja kwa moja (directly) na ufisadi na watatu ambao uhusika wao ulitokana na nafasi walizokuwa nazo (indirectly). Pamoja na hilo the bottomline, nakiri, walitajwa na jumla yao walikuwa mafisadi kumi na moja.

Hata hivyo kinachonipa taabu zaidi ni namna tunavyofanya hizi hesabu zetu...kumi na moja ukitoa moja jibu sahihi ni kumi, lakini kulingana na mjadala unavyoendelea humu ndani napata hisia tofauti kabisa. Kwamba maadam fisadi moja katoka kwenye hilo bonde la kashfa, ufisadi wote umehamia huko na kuliacha bonde likiwa safi. Ukimtoa Lowassa, timu iko pale pale na benchi lake la akiba.

Jamani tuwe wakweli, tukilinganisha mapendekezo ya maridhiano aliyogusia Mzee Mwanakijiji, ujasiri wa tendo alilofanya Lowassa la kuikana CCM mchana kweupe unafunika mengi katika hayo. Wapo wengi tu ambao wameshindwa kuupata ujasiri kama huo kwa woga wa kushughulikiwa na system...wako wafanya biashara wakubwa wanaamini kabisa kwamba kuhama CCM ni sawa na kujitia kitanzi.

It had to start from somewhere and Lowassa has had the courage to lead the way, kwamba CCM si baba wala mama, there is also life outside CCM. Kama ndoto yako na matamanio yako hayawezi kufikiwa ndani ya CCM, utayatafuta nje ya CCM kama alivyotuasa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. CCM ilianza kupoteza dira kitambo na kama si matumizi ya nguvu za dola tayari ingebakia historia.

Na mwisho naomba niseme machache kuhusu nafasi ya Dr. Slaa. Mojawapo ya makubaliano yaliyofikiwa ndani ya UKAWA ni kwamba yeyote yule ambaye angeteuliwa wote wangemuunga mkono. Swali langu ni ingekuwaje kama Chadema baada kumpendekeza Dr. Slaa, washiriki wengine wa UKAWA wakashindwa kufikia muafaka na tuseme mgombea kutoka CUF au NLD akakubalika zaidi, Chadema wangejitoa?

Wengine wetu wakati Chadema inawatema Zitto & company, tulisisitiza kwamba Chadema ni zaidi ya mtu binafsi; si Zitto tu bali hata Mbowe na Dr. Slaa anaweza kutoka na Chadema ikaendelea. Kwa nini leo tuwe tayari kuivunja chama kwa sababu tu wako watu wawili watatu hawakubaliani na maamuzi ya wengi? Nampenda sana Dr. Slaa na naamini bado anayo nafasi tena kubwa tu ndani ya Chadema.

Kwangu kuiondoa CCM madarakani takes first place ahead of everything else na ninaelewa msimamo wangu huu haukubaliki kwa baadhi ya wana mageuzi but then toka lini watu wote wakakubaliana? Ukikuta watu wote wanakubaliana kwa kila jambo wakati wote, there is something very wrong somewhere, somehow, somewhat. Asante Mzee Mwanakijiji ila naomba nisikubaliane nawe kwa mengi uliyopendekeza.
 
Jokakuu;

Katika mlolongo wa maisha binadamu wanafanya makosa. Kuhusiana na kashfa ya Richmond, ngoja tumkubalie Lowassa kuwa Ikulu ilifanya makosa. Au kwa kuongezea watanzania wote tulifanya makosa. Kwa maana nyingine tumsafishe kutoka kwenye kashfa hiyo.


Lakini tukirudi kwenye masuala ya tabia za bnadamu ziwe mbaya au nzuri kuna kitu kimoja kinajionyesha pattern. Au kwa maneno mengine kujirudiarudia kwa tabia. Watu wanaoshutumiwa kuwa ni mafisadi hawajafanya vitendo vyao mara moja na kuacha. Wamefanya mara nyingi na zipo patterns za kuthibitisha.

Swali je tukimsafisha Lowassa kutoka kwenye Richmond, bado atakuwa mtu safi? Kama sio mtu safi, basi kuhusika kwake au kutohusika kwake hakumpi sifa zozote ubora wa uongozi.

Kwanini Nyerere alimzuia 1995 asiwe rais? Au alimuonea tu? Mwishoni mwa 2005 baada ya JK kuchaguliwa kuwa rais alifanya ziara Marekani. Kwenye mkutano wake na watanzania waliopo DC, kijana mmoja kwa hasira aliuliza bila kupewa nafasi, kwanini umemteua Lowassa kuwa waziri mkuu wakati ni mla rushwa. Wakati huo hata neno fisadi ilikuwa halijapamba moto Tanzania.

cc Alinda, Mkandara, Ritz, Kichuguu, Mzee Mwanakijiji, Jasusi, Mag3, Nguruvi3,

Niliwahi kusema huko nyuma kabla ya Lowassa hajajiunga Ukawa kuwa tatizo la CCM ni kutaka kutuaminisha kuwa ndani mwa CCM fisadi na mla rushwa, ni Lowassa tu, CCM wanataka tuamini kuwa kwa kujiondoa Lowassa ndani ya CCM basi CCM imekuwa safi kama theruji.

Sasa swali kwa kila mtanzania anayesoma hapa hivi ni kweli ndani ya CCM fisadi ni Lowassa tu? Je tunamsamaje Kinana nyara za serikali? Sitta na chenji ya katiba mpya je? Chenge?Mwakyembe na mabehewa hewa? Pinda na vibari vya sukari? Magufuli na upoteaji wa bil.265? Kikwete na mikataba 16 ya gesi? Kwa hiyo ukiangalia utaona kuwa CCM hakuna msafi kuanzia kwa Mwenyekiti wao mpaka kwa balozi wa nyumba kumi kumi.

Je watanzani wanaelewa dhana nzima ya ufisadi?

Pamoja na shule nzuri iliyotolewa na Chadema kupitia Katibu kwake mkuu Dr. Slaa, lakini unaona mwitikio wa kuchukia ufisadi kwa wananchi walio wengi ni mdogo. Watanzania wengi waishio vijijini ambao wao ndio wanaamua nani awe rais, mbuge na diwani hawana habari na ufisadi tena usherekea wakati wa uchaguzi kwani ndio wakati wa mafuno ya shilingi 500 mpaka 10000 kutegemea na mtu na mtu. Watanzania hawa hawafahamu kuwa matatizo yao yanaletewa na hizo 500 wanazoongwa bali wao wanaamini ni "mapenzi ya Mungu"

Kila mbunge au diwani awe ni mpinzani au CCM atakubaliana nami kuwa katika vijiji vingi kushinda uchanguzi si swala la sera tena au kuimba ufisadi ni swala la mikakati na hongo. Maana katika akili za kawaida huwezi kuhubiri ufisadi hali mgombea mwenzako akigawa rushwa ukategemea utashinda. Hiki kitu wabunge wa upinzani na CCM wanakielewa. Mwanakijiji wa kawaida haamini kuwa mbunge anawakilisha matatizo yake maana wakisha changuliwa uhamia Dar na kwenda vijijini kwa ajili ya uchanguzi, na hii umfanya wananchi kuona ubunge ni sehemu ya kuula sasa huwezi kupewa ulaji bila wewe kutoa kitu kidogo.


Ushuhuda wa kuwa ufisadi na sera nzuri si hoja wa watuchagulio viongozi (wananchi wa vijijini)

Mwaka 2010 wakati swala la Richmond bado likiwa nimeshika kasi, wakati swala la Epa liko kwenye chat tulitegemea kuwa watanzania watakasirika na kutowachagua mafisadi au wala rushwa lakini kilichotokea wote tunakifahamu. Mh. Chenge alirudi tena alishinda kwa kishindo, Mh. Lowassa alishinda kwa kishindo, Rostam alishinda kwa kishindo na hata ninavyoandika hivi sasa wale watuhumiwa wa Escrow wameshinda wote kwa kishindo katika kura za maoni. (nii masikitiko lakini ndio hali halisi)

Vyama vya upinzani wafanye nini? ili ndilo swali ninajiuliza na sipati jibu je maadamu watanzania hawatishwi tena na ufisadi, hawajali kama Lowassa ni fisadi au la, basi waende kiccm na watakapo bahatika kupata uongozi basi warudishe nchi yetu katika msingi? au waendelee kuhubiri wanachokiamini hata kama itawakuchua miaka mingine 20 kuchukua nchi ambayo itakuwa imeshaliwa vya kutosha na miktaba hewa? Nafkiri jibu kila mtu analo kichwa.

....
 
Kwanza, niwashukuru na kuwapongeza sana wachangiaji kwa 'civil debate'. Wachangiaji wameonyesha 'insightful' katika suala zima.

Na hakika, Mag3 kahitimisha vizuri sana, kama hakuna mitazamo tofauti, something is wrong.

Mtazamo wangu umejawa na shaka zaidi ya matumaini. Shaka inajengwa na historia ya wapinzani.
Kama mtakumbuka wakati wa BMLK, tuliwaonya wapinzani kunywa juisi Ikulu (uzi wa juice ya maembe).
Kwa mshango, ni Mbowe huyu wa leo ndiyo aliyeongoza feilia ile hadi nguvu ya umma ilipowalazimisha kutoka. Tulikuwa sahihi!

Pili, sina tatizo na ujio wa Lowassa, ni haki yake kama raia mwingine. Ninashaka, suala lilivyokuwa handled kama kulikuwa na busara , maafikiano na uchambuzi wa kina. Tulishangaa tu Mbowe anakabidhi hiki na kile ilimradi kila mtu kaduwaa kwa hii 'voda fasta'

Tatu, CDM kuchukua hatua dhidi ya kiongozi kwasababu Chama si mtu ni hatu nzuri, nimeipigia debe sana.
Wakati tetesi zinavuma, niliandika bandiko la kuwaasa Mbowe, Slaa na CDM dhidi ya haraka wanayoifanya.
Hivyo, suala si mtu, suala ni hoja za mtu, tunaangalia hoja zaidi ya mtu au watu

Nne, kama ipo njia ya mkato ya kuiondoa CCM basi na iwe. Njia lazima iwe katika mkakati mzuri, isi compromize values nyingine

Njia hiyo iongozwe ili kufikia mabadiliko ya kweli na si ya rangi.Tatizo si CCM kama chama, ni watu wanaounda CCM kama chama.
Lazima tujiulize, hawa wanaokuja, wanakuja kwa dhati au wanakuja kwasababu ya.

Tano, kilio cha watu siku zote ni CCM kutekwa nyara na matajiri. Umiliki wa chama umekuwa suala la kundi na si wanachama.
Je, athari hizo zimeangaliwa kwa upana na marefu yake?

Sita, kama lengo ni kubomoa mfumo mchafu, tunabomoa mfumo huo kwa kutumia nini?
Alinda kasema mafisadi wameshinda kura za maoni. Wanafahamu mfumo ulivyo na wanavyoweza kuutumia katika 'survival' kama si manupalation. Hawa wanaokuja lini wameacha mfumo huo ghafla na kukumbatia mabadiliko?

Saba, Ujio wa EL umefungamaniishwa na nguvu kubwa kisiasa kiasi cha kuonekana UKAWA imejiunga na EL na si kinyume chake.
Mbele ya safari, nini hatima ya UKAWA kama chombo kinachosimamia mabadiliko?
Again, kwanini watu waamini mtu kama taasisi ikiwa tunaamini hakuna mkubwa zaidi ya chama?

Nane,ujio wa EL umepelekea viongozi kusema 'asiyetaka aondoke'. Well, tunathamini vipi mchango wa watu waliojitolea roho zao katika kupigania mabadiliko ya nchi hii. Kwanini mtu anaweza kuingia na kukigawa chama kiasi hicho. Hii ni dalili njema kweli!

Tisa, Ni hesabu zipi zinazoonyesha ujio utanufaisha Ukawa? kura za maoni zimekamilika, nini kinategemewa zaidi ya hapo?
Kama ni wananchi nani ataongoza mapambano ikiwa ujio upo nje ya 'system mpya'?
Ongezeko la wabunge linatoka wapi? Je, wale wa Ukawa waenguliwe kupisha nguvu kubwa ya kisiasa?

Kumi, endapo tunaamini katika demokrasia, ni kwanini demokrasia haikuachwa ichukue mkondo wake kwa kuweka wagombea bali inaonekana kama EL amekuja kwa 'mission' hiyo. Hakuna aliyezuiliwa kuchukua fomu, lakini mazingira yaliyojionyesha ni wazi huyu ni chaguo tayari. Je, lini wanachama walipima nguvu yake na kuridhika itawavusha?

Kumi na moja, Ujio wa EL utaambatana na marafiki zake wengi. Kuna uhakika gani kuwa marafiki zake walioko kimya wataendelea kuwa nje ya sytem pindi na ikitokea akafanikiwa? Na hao kama mzee wa vijisenti wataachaje influence yao hata kama wapo nje ya Ukawa? Nani atakuwa na upper hand, ukawa au marafiki wa safarini?

Kumi na mbili, kipi kilipaswa kutangulia kama alivyosema Mzee Mwanakijiji katika uzi wake. Je, ni hawa kukiri mapungufu na kujiunga na mbadiliko, au ni wapenda mabadiliko kushangilia wajao?

Na mwisho, endapo suala hili ni rahisi, iweje linavuruga viongozi? Je, huko kwa wananchi kukoje!

Kwanini kunakuwa na 'mixed feelings' ikiwa lengo ni moja, kuondoa CCM. Kwanini kuna hofu iliyotanda isiyojulikana inatokana na nini?
Je, si vema kuondoa shaka hiyo kuliko kuiacha watu wakaiondoa wakiwa wenyewe katika sanduku la kura!

Nikiangalia, kijamii, moral perceptive, aina ya mabadiliko tunayohitaji,historia ya uongozi wa Ukawa katika nyakati za crisis, mkakati uliopo, namba n.k. ninabaki na maswali mengi kuliko majibu.

Najaribu kusoma kwa umakini kama nitashawishika zaidi na hoja nikijishauri nipo wrong side of the history.

Until then nabaki kusema huu ni uwekezaji hatari na wenye risk! I hope I'm wrong!
 
Nguruvi3, naomba nikuulize kaswali kamoja tu, inavyoonekana baadhi ya watu wanaonekana wamemvalia njuga Lowassa kwa kiwango cha kutisha, si ndani ya upinzani na si ndani ya CCM. Wote wako tayari kusahau tofauti zao kiungo kikuu kikiwa ni chuki yao dhidi ya mtu moja tu Edward Ngoyai Lowassa. Kwa baadhi ya watu kuondoka kwa Lowassa kunadaiwa kumeitakasa CCM, na kujiunga na Chadema kunadaiwa kumeitia najisi UKAWA. Ufisadi wa Lowassa ukitajwa, watu huamini mara moja lakini ufisadi wa mtu kama Magufuli ukitajwa, miguno inasikika aah wapi bwana mnataka tu kumchafua Bwana Pombe. CCM ilipotufikisha, ufisadi si tena jambo la kushtua, ufisadi umekuwa ni kitu cha kawaida, ufisadi umekuwa kama sehemu tu ya maisha. Asiye fisadi ndiye watu wanashangaa, huyu vipi, kama hataki kula shauri yake asituletee nuksi hapa! Hapo ndipo CCM ilipotufikisha.

Ndugu yangu Nguruvi3, swali langu ni hili...kweli unaamini kwa dhati kwamba katika taifa hili Lowassa ndiye kinara wa ufisadi? Kwamba Lowassa ndiye sura ta ufisadi? Kwamba Lowassa ndiye mwanzilishi wa ufisadi? Kwamba awe serikalini ama nje ya serikali, ufisadi wake ni kama ugonjwa wa kansa, dawa ni moja tu kumkata Lowassa.

Unakumbuka hii orodha aliyoitaja Dr. Slaa viwanja vya chipukizi Tabora kama muendelezo wa orodha ya Mwembeyanga?

Dr.Wilbrod-Slaa.jpg


Sunday, April 17, 2011

Dr SLAA ATAJA ORODHA MPYA YA MAFISADI, WAFIKIA 17


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ametaja orodha mpya ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotuhumiwa kwa ufisadi.
Vigogo hao ni;



  1. [*=left]John Pombe Magufuli, Waziri wa Ujenzi,
    [*=left]John Samwel Malecela, aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu Mwenyekiti wa CCM,
    [*=left]Fredrick Sumaye, aliyekuwa Waziri Mkuu,
    [*=left]Philip Mangula, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM

kwa kuhusika na wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kupitia Benki Kuu. Dk. Slaa alitangaza majina hayo jana mjini Tabora alipokuwa akiwahutubia wanachama na wananchi waliofurika kwenye viwanja vya Chipukizi.

Alisema majina hayo ni muendelezo wa yale ya vigogo wanaotuhumiwa kwa ufisadi aliyoyataja Septemba 15, 2007 katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam ambayo ni 11 akiwemo Rais Jakaya Kikwete.

Katika orodha ya mwaka 2007, Dk. Slaa aliwataja aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), ambaye sasa ni marehemu, Dk. Daudi Balali, Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM) na Basil Mramba aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Rombo (CCM). Wengine ni Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, kada wa CCM, Nazir Karamagi, Mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono (CCM), Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM), Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, na Rais Jakaya Kikwete

Ni Mafisadi 17 aliowataja Dr. Slaa na kati ya hawa wote ni Lowassa tu ameweza kuwa na ujasiri wa kuvua gamba na kuvaa gwanda. Walobaki bado wamo humo humo lakini twaambiwa baada ya kutoka moja na kubaki 16 ndani ya CCM, ufisadi nao umehamia huko huko alikokwenda Lowassa, does this make any sense to anybody?


Ingekuwa ni hivyo CCM wangekuwa wanapiga vigelegele lakini wote tunashuhudia jinsi walivyopigwa butwaa...wanajiuliza huyu mwenzetu kapatwa na nini mpaka anatuacha? Je ni kitu gani wanakililia...je ni kuondokewa na fisadi? Au kuvuliwa kwa gamba? UKAWA naomba mzidi tu kukaza buti, msibweteke na machozi ya samaki ya CCM.


 
Nguruvi3,

..mimi kinachonitisha zaidi ni hatima ya upinzani huku Magufuli amekamata ikulu na wakati huohuo ni mwenyekiti wa ccm.
Kuna mtu anasema mwenye ushahidi wa ufisadi wake aende mahakamani, analeta siasa kasahau kwamba vikaratasi alivyowaandikia kina Msabaha kuwashinikiza na richmond yake watu wanavyo. Natamani Magufuli aliswage mahakamani fisadi hili kwani anao ushahidi.
 
Kuna mtu anasema mwenye ushahidi wa ufisadi wake aende mahakamani, analeta siasa kasahau kwamba vikaratasi alivyowaandikia kina Msabaha kuwashinikiza na richmond yake watu wanavyo. Natamani Magufuli aliswage mahakamani fisadi hili kwani anao ushahidi.

Kabla Magufuli hajamswaga Mahakamani, ni bora Magufuli atwambie zile nyumba alizouzia familia yake aliziuza kwa msingi ipi? je Kabula aliwahi kufanya kazi serikalini? Na pia tunaomba ufafanuzi wa Bil. 265 zilizokosa maelezo katika wizara yake rejea GAC na hasisahau ubofu na ufinyu wa barabara alizojenga kwa gharama kubwa ambazo zimekuwa chinja chinja kwa watanzania. Akimaliza hapo aende kwa Mweyekiti wake na swala la Epa, Meremeta, Escrow na vifuruji vya fedha na mikataba ya Gesi. Akimaliza hapo aende kwa Kinana na nyara za serikali akimalizwa ndio ampeleke Lowassa Mahakamani kinyume cha hapo ni kumkomoa Lowassa kisa amehama chama.
 
Kuna mtu anasema mwenye ushahidi wa ufisadi wake aende mahakamani, analeta siasa kasahau kwamba vikaratasi alivyowaandikia kina Msabaha kuwashinikiza na richmond yake watu wanavyo. Natamani Magufuli aliswage mahakamani fisadi hili kwani anao ushahidi.
Thubutu, mbona yeye Magufuli vikaratasi vyake vimeenea kila mahali kama ilivyo tabia ya mkurupukaji siku zote, subiri kampeni ianze...vikaratasi vyake ndivyo vimezagaa hovyo kama anavyokurupuka hovyo.
 
Mkuu Mag3 nadhani utakumbuka si mara moja au mbili ni zaidi ya mara 20 nipo katika rekodi ya kusema hakuna msafi ndani ya CCM. Hilo ndilo hasa linasukuma zaidi ari ya mabadiliko tukijua miaka 50 na hasa 10 ya mwisho nchi imekuwa hohe hae
Ndani ya CCM ni ufisadi tu, hakuna, narudia hakuna msafi hata mmoja

Ufisadi wa EL unaosema ninaungalaia katika mtazamo tofauti. Baada ya kusikia utetezi na baada ya yeye kutueleza nani mhusika, hilo lilikuwa sehemu moja tu ya mbili zilizokuwa zinamkabili

1. Tuhuma za ufisadi kwa namna moja au nyingine , ambazo sasa anazipangua
2. Kushiriki kuficha maouvu hata kama hakushiriki katika dili

Hili la pili, nimemjibu Mkuu JokaKuu hapo juu kuwa

Lowassa alipoita kikao cha makatibu wakuu alijua lipo tatizo

Aliwezaje kupokea maagizo ya katibu mkuu naye akiwa 'right hand man' na kushindwa kumuuliza bosi kulikoni?

Alisimama mbele ya bunge kutetea kile alichojua si kweli. Taarifa zikafanyiwa usanii wa PCCB naye kasimama nao

Taarifa ya Shelukindo ilipotoka kuwa ipo namna, hakusimama kusema ngoja tufuatailie, alisimama kutetea hakuna tatizo

Taarifa ya Mwakyembe ilipotoka, hakusema nini kimetokea bali uwaziri mkuu

Long story short, hayo yote ilikuwa katika kulinda mfumo wa ufisadi. Alipostaafu bado alikaa kimya akijua maneno yanaweza kumwengua mapema. Sasa hatima imefikia ndiyo tunapata inside info. Hakuna tatizo hadi hapo

Tatizo lililopo, lini tunaweza kuamini ndio umekuwa mwisho wake wa kutetea mfumo kama tulivyoona hapo juu?
Ni kwa namna gani tunaweza kusema, ujio wake na pengine mafanikio yatokanayo, yatabadilisha hali ya sasa?
Ni vipi tuamini hataweza kuwageuka wenzake ili hali bado 'timu' yake imemzunguka kuanzia nia hadi kutangaza?

Upande mwingine, hawa ukawa wamejiridhishaje kuwa ujio wake utakuwa na manufaa bila athari katika maeneo tofauti?
Je, wamewasiliana na hadhra yao tofauti na tunavyosikia au kuona mambo yakienda kasi?

Je, ile nguvu iliyoteka CCM na ambayo inapigiwa upatu sasa inadhibitiwaje?
Kwa jinsi ilivyo, mtu anageuka kuwa taasisi, ni sawa sawa hiyo?

Sina tatizo na uanachama wake huko upinzani, nina shaka sana na wapinzani kama wameliangalia jambo hili kutoka kona zote. Kama wamekaa chini kwanza na kutafakari kwa kina leo na kesho.

Haitoshi kusema tu ana nguvu, ni lazima ionekane nguvu hiyo inaongezwaje katika iliyopo ili kuleta maana iliyokusudiwa

Nasema hayo kwasababu ujio huo ume compromize values nyingi na umeduwaza

Nina shaka, isije kuwa handling ni poor tukaishia na 'bubble burst' kati kati safari , meli ikazama na mzigo, CCM wakaendelea nayo.

The fact that kuna mixed feelings, doubt etc ina translate alot
 
Back
Top Bottom