CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Mkandara,

..Dr alitakiwa awe na fomu yake tayari.

..nini kilikuwa kinampa kigugumizi asichukue fomu?

..sasa hata haieleweki kama alikuwa anataka kugombea au alikuwa anasubiri aombwe na chama chake.

..je, tatizo ni kwamba hamtaki Lowassa? Au, tatizo ni kwamba amedhulumiwa nafasi hiyo?

..Je, Mbowe angeleta mtu asiye na tuhuma bado kungekuwa na sintofahamu tuliyonayo sasa hivi?

Cc Nguruvi3, Zakumi

Kwa maelezo ya Tindu Lissu (alikuwa anaongea na vyombo vya habari) ni kwamba mchakato wa kupata 'mabaki' toka CCM kugombea CHADEMA yalianza muda mrefu. Walikuwa wanasubiri mchakato wa CCM umalizike ili wapate mgombea wao.

Lissu pia anatutaarifu kuwa wamefanya tafiti nyingi kupitia kwa makampuni makubwa dunia (makampuni ya polls), na walipewa majibu yanayoonesha nguvu ya Lowassa. Maswali ya kujiuliza ni haya:

- Ni lini CHADEMA walianza mchakato wa kumpata Lowassa, ni baada ya kukatwa huko Dodoma, au wakati wa tafiti?
- Ni watu gani walihusishwa kuandaa hizo tafiti? Dr Slaa alikuwa miongoni mwa watu waliojua kuhusu hizo tafiti? Hadidu rejea zilikuwaje?

- Nini lengo la CHADEMA kutaka kujua (kupitia tafiti) faida watakayopata kama wataungana na Lowassa kwenye uchaguzi?

--Kama walikubaliana Lowassa aje CHADEMA, walikubali aje kama mwanachama wa kawaida au mgombea urais kupitia CHADEMA?
- Kama jibu ilikuwa aje kama mwanachama wa kawaida, nani alibadilisha na kupitia kikao gani na kwa sababu zipi?
- Mpaka sasa hivi (niko tayari kusahihishwa) Pro. Lipumba bado ni mgombea urais kupitia CUF. Sikumbuki kusikia kuwa amejitoa rasmi kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais kupitia CUF!
 
Jokakuu;

Nimerudi kutoka bongo. Sehemu ninayotoka ilikuwa ni strong hold ya CCM. Na katika uchaguzi wa madiwani na serikali za mitaa, CDM walichukua baadhi ya viti. Na walichukua kwa sababu ya kuwaadhibu wadiwani wa CCM na viongozi wa mitaa ambao hawakufanya chochote zaidi ya kuwa wala rushwa. Na baadhi ya CDM waliochaguliwa, hawana exprience and qualifications zozote.

Kwa maoni yangu kampeni za CDM zimefanya watu kukielewa chama hicho hata katika sehemu ambazo hakikuwa maarufu. Ukienda kwenye jimbo ninalotoka bendera za CDM zipo. Tatizo kubwa linalokuja CDM inaendeshwa na local guys. Ambao hawana exposure kubwa, wengi ni small traders, bodaboda and n.k. Kwa maneno mengine inategemea watu wenye kufanya shughuli zao ndogo ndogo za hapa na pale. Kwa wao kuingia kwenye siasa hakuna liability yoyote.

Kwa kutumia mtaji wa sehemu niliyotoka, naamini kuwa siasa za personality bado zinatawala. Pamoja na kuwa wa CDM ameshaanza kuweka mizizi, ni lazima personality ambazo zinaweza kuleta mabadiliko katika majimbo zianze kuwepo. Kumchagua kijana wa bodaboda kuwa diwani au kiongozi wa serikali za mitaa ni kitu kimoja, kumchagua mtu kwenye ubunge au urais ni kitu kingine kabisa.

Sababu ya Lowassa kukubali CDM/UKAWA ni personality yake. Ingekuwa ujio wake ungesababisha watu wenye pesonalities nyingi (kama 200) kujiunga na CDM au CUF kugombea ubunge, mabadiliko makubwa yangefanyika mwaka huu.

Kwa maoni yangu binafsi, kama watu tunataka kuwasaidia upinzani, itabidi tuanze kujiunga nao hili kuongeza profiles za watu wenye degrees, exposures, na mambo mengi katika local politics. Upinzani unahitaji personality.
 
Mkuu ikiwa fomu hazikutolewa ulitaka mimi nithibitishe vipi?.. Labda wewe unayejua zaidi nambie, au nipe mfano ikiwa wewe ungejua ofisi haikutoa fomu za mgombea urais utathibitisha vipi? mathlan..wakati mwingine mnabisha tu ili mradi kubisha mtu utathibitisha vipi kuwa fomu hazikutolewa!..kama ningesema zilitolewa, ningekuonyesha fomu hii hapa sasa hazikutolewa nikuonyeshe nini..
Mkuu,
Hizi hoja zenu kuhusu uamuzi wa CHADEMA kusimamisha mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA zilishajibiwa na Mbunge wa Nyamagana, Wenje katika video hii,

 
Last edited by a moderator:
Una point kubwa kwenye connection. Miaka iliyopita tulikuwa tunawanukuu wamarekani hapa: all politics is local. Uchaguzi wa ubunge Tanzania is very localized. Nilipokuwa natembelea wazee wa jimboni, walichokuwa wanasema: mbona mtu huyu hatumjuhi. Kwa majina ya watia nia ya ubunge, kulikuwa hakuna mtenganisho mkubwa sana wa huyu CCM au huyu CDM.

Cha kushangaza zaidi, maneno makali yaliokuwa yanatolewa na baadhi ya wabunge wa CDM kwa spika au mawaziri kwa kutumia lugha ya kejeli turned people off, in particular the older generation. Unaweza kuwa machachari bungeni au kwenye mikutano, lakini matumizi ya lugha yanaweza kuleta mtazamo mwingine tofauti japokuwa unaongea kitu kizito na cha maana. Unapokuwa DSM,Arusha au kwenye miji mingine mikubwa unaweza kusema kuwa Wassira mzee sana na anasahau kufunga koti na watu wakakubali. Lakini wazee wa vijijini will no be amuzed. Kwao adabu ni kitu cha kwanza.
 


Alinda: Hivi umesoma ulichokiandika au unataka kubishana na bibie Alinda? Hizo fomu zitatokaje kama hakuna mtu aliyekwenda kuziomba/kuzichukua? Tangazo lilitolewa, hakuna mtu ambaye alikwenda kuchukua fomu, sasa wewe unataka nikuonyeshe watu waliokwenda kuchukua fomu?????????? kweli?

Unataka Dr. Slaa aombwe na nani kuchukua fomu? Na Dr. Slaa ana cheo gani ndani ya Chadema? Au unachotaka kutwambia kuwa Mbowe alimficha Dr. Slaa fomu? (kama ni hivyo hizi ndizo fitina nilizosema?

Nilichokwambia kama wewe unakosea, kama binadamu je na wengine wasikosee?https://www.jamiiforums.com/member.php?u=11140
Alinda , nadhani hoja hii imeisha baada ya fitna na uongokuonyeshwa.

Mkandara alianza na fitna ya ofisi kufungwa. Tumemuonyesha fitna hiyo si kweli. Sasa anazungumzia fomu.

Nilipomuuliza suala la fomu lipo chini ya madaraka ya nani,hakujibu akijua ni jibu sahihi la fitna na uongo.

Anachotaka kufanya nikuingiza fitna kati ya Mbowe na Slaa.

Huyo ndiye Mkandara, ambaye kama hana fitna za ukabila,ataleta fitna za udini.

Watu wanapuuza hoja zake wanajua fitna ni sehemu ya hulka na utamaduni wake.

Nadhani kuna hoja za muhimu, hii muachie maana jamvilinaona.

Karaha ni kuvuruga mada na hoja zisizolingana na exposure yake achilia mbali mengine

I hate to say this, lakini inafika wakati jukwaa liwe naheshima, siyo mtambo wa fitna.

Naomba radhi wanajmavi, tuendelee na hoja zenye sense
 
Tatizo ni lipo sehemu moja, kwamba kila mtu anadhani ni Orator

Katika mikutano lazima kuwe na kujipanga. Wapo wahamasishaji, watoa facts na Orator

Orator ni mtu mwenye uwezo wa kuunganisha mambo kadhaa akiangalia hadhra anayoongea nayo.

Njia rahisi ya kuwafikia wananchi ni kujenga hoja zikielezwa katika muktadha wa pale walipo na nchi kwa ujumla

Haitoshi tu kueleza ufisadi. Vipi kama unaeleza tatizo linalowakabili wananchi pale walipo, ukalitoea suluhu yake na kuonyesha limitations zake zinazotokana na ufisadi.

Ufisadi unakuwa sehemu ya, lakini si hoja muhimu kwamwanakijiji.

Umuhimu wake ni pale utakapoonyesha tatizo la mwanachi katika uhusiano na ufisadi in a simple language


Lakini pia hoja ni lazima zijengwe kutokana na mazingira.Hivyo, ni muhimu sana kusoma eneo mtu analokwenda kuhutubia ili kuyaelewa mazingira kikamilifu, si suala la msafara kwenda kuzungumzia GDP, FDI n.k. Hayo yana maeneo yake
 
-Mkuu FJM endapo uliyoandika ndiyo Lissu aliyosema, inatia shaka sana na maandalizi ya wapinzani. Kuna habari pia , alisema yapo maeneo wapinzani ni dhaifu

-Hoja ya kujiuliza, kwa miaka 10 wapinzani wamejijenga kiasi gani? Huo udhaifu wanaosema ulikuwa hauna ‘tiba'

-Kusubiri makapi ya CCM ni kielelezo cha kushindwa kujitanua. Kushinda uchaguzi ni jambo moja, kujitanua ni jambo jingine. Je, walishindwa yote?

Dilly dally za kupata mgombea wa CDM/UKAWA ni ushahidi mzuri wa kusubiri makapi


Hakukuwa na tafiti, hayo ni maneno tu. Kama tafiti zilikuwepo iweje leo wasitoke kama timu mmoja.
Je, tafiti zililenga watu ndani ya CDM au makapi yanayosubiriwa?


-Walimpata EL baada ya kukatwa. Haiwezekani tafiti zije na matokeo ya kukatwa kabla ya kutokea.
Kilichofanyika ni kusubiri nini kitatokea CCM


-Kama tafiti ilikuwepo, mtendaji mkuu wa chama ni katibu mkuu. Tena ndiye mratibu kama hilo limetokea.

-Lengo la tafiti watakuwa wanalijua wao, hatujui kama ni kupata mwelekeo wa uchaguzi, kubaini maeneo dhaifu, kutathmini nguvu waliyonayo au kutafuta nguvu kutoka nje

-Hakuna anayejua makubaliano yalikuwa uanachama au kugombea. Tunachojua, suala hilo limezuka kutoka UKAWA na kamati kuu ya CDM imeonekana kushiriki dakika za mwisho. Video ya Wenje inaonyesha kutokuwa ‘aware' na ujio wa EL

-Hatudhani EL ange sacrifice uanachama wake CCM bila kuwa na mafao huko aendako.
Inavyoonekana kulikuwa na vikao, sasa mwanachama mpya anachukua kadi na kupata haki zote.
Majadiliano yalihusu nini?
 
Last edited by a moderator:
Ukiangalia sana ndugu zangu, tatizo la Lowassa kujiunga CHADEMA siyo kubwa sana kulinganisha na tatizo la jinsi gani amejiunga na kuibadilisha CHADEMA. Tuliofuatilia siasa hizi kwa muda tulikuwa na uhakika mkubwa tu kuwa Lowassa akikatwa jina lake CCM hatosalimu amri tu yakaisha; atatafuta njia nyingine ya kuingilia. Kati ya njia zote sidhani kama CDM ilikuwa ni njia iliyokuwa wazi zaidi (the path of least resistance). Tulitarajia labda angeenda ACT au chama kingine hivi; japo kulikuwa na tetesi za kuwa angeweza kwenda CDM. Dalili za yeye kwenda CDM ni jinsi gani CDM ilionekana kujing'ata ng'ata meno katika kupanga kalenda yake ya Uchaguzi; ni kama waliangalia sana kalenda ya CCM. Sijui kwa mfano ni kwanini CDM hawakuanza mchakato wao wa kupata wagombea miezi hata sita kabla na kumalizana na hilo na kuwaacha CCM waumane meno wenyewe. Leo hata kina Makanga wanatoka CCM kwa mbwembwe wakitarajia njia hii ya CDM. Of course, kuna dudu jingine kabisa linaitwa UKAWA; mwisho wa siku ninaamini hukumu itapitishwa vikali sana kwa viongozi wa CDM kufuatia uchaguzi huu mkuu kwani sasa hivi wamejenga imani kuwa wataiangusha CCM kabisa; kama walivyofanya kwenye Serikali za Mitaa mwaka jana au imani iliyojengeka mwaka 2010. Wanasahau CCM inachogombea ni 50% tu.
 
Ahsante Alinda

Mkuu Mkandara , Alinda kaja na hoja hizo. Ni wakati utuambie kama uliyosema bado unasimama nayo na kwasababu zipi


Kumbuka madai yako ni mazito ima kwa uongozi au wanachama.Kuyaacha tu kama yalivyo ni fitna.
Tuondoe fitna kwa wewe kutueleza ukweli
au kufuta


Mkuu tatizo la kaka Mkandara ni chuki zaidi kwa CDM kuliko uhalisia,
Ni kweli CDM wamekosea sana swala la Lowassa na wanastahili lawama, lakini huyu mkuu ukimfuatilia analeta hasira za Supreme leader na genge lake kufukuzwa CDM, so anaongozwa sana na hasira kiasi cha kuyakana maneno yake au ukweli uliopo.

ukimfuatilia kwa siku za nyuma kabla ya mgogoro wa Lowassa kuingi, alikua anawapigia sana chapuo CUF kuongoza ukawa na kuwaponda CDM and specifically Dr.Slaa kwamba hafai kuongoza, leo anageuka mtetezi wake mkuu kisa tu inawapa advantage ya CDM kubomoka na automatic kuipa nguvu ACT, jambo ambalo mm binafsi naliona sio sawa.

Mm nadhani kwenye jukwaa hili tuwe objective and realistic kwenye kujadili mada humu, na wakati mwingine kumeza ukweli mchungu hata kama haupendi hilo jambo, na ndio uungwana, mfano kuna watu wameumizwa sana na Lowassa kuhamia upinzani na kuuvuruga, pamoja na kuwapenda na kuwakubali viongozi wa UKAWA kwa baadhi ya juhudi zao, lakini hawaachi kuwapiga mawe kwa upuuzi waliofanya.
 
Mkuu upo sawa,
hili suala tukifuatilia trend EL asingeweza kugiveup so easily so ilikua lazima atafute stage ya kufanyia siasa, hatukutegemea kabisa kama atakimbilia CDM, bt ndio huyoo keshaingia ndani ya nyumba.

maswali yanayoniumiza sana kichwa sana na kunisumbua, je viongozi wote wa UKAWA including katibu mkuu wao walishirikishwa na kimsingi kukubaliana ( hata katika kutokukubaliana ) ujiao wa huyu mtu, na je waliforseen risk ya huyu jamaa kuja na kuwavuruga, na je walijipanga kuzuia machafuko yyt yatakayoletwa na huyu Bwana. Sijui hawa viongozi walijiandaaje.

kuhusu UKAWA hili ni Dubwana ambalo kimsingi linabidi liwe handled very careful maana ni kama vile wamejiingiza kwenye migogoro from outside, nadhani kuna umuhimu sana baada ya uchaguzi new blood to come and riveve their harakati maana hawa waliopo mchango wao ni mkubwa sana na unathaminiwa ila kwa sasa wamechoka na wanahitaji kupumzika, waachie wengine. Let us wait and c what will happen kwa uwekezaji wao huu hatari.
 
Hamna namna tena itabidi muungane na Lowassa kwenye safari yake ya matumani.

CHADEMA kwa sasa hawana ubavu wa kumnyoshea kidole Lowassa na timu zake.

Lowassa kwa sasa ni chama ndani ya CHADEMA.

Hukumuona Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mbowe, anavyo mnyenyekea Lowassa mpaka anamsindikiza Lowassa kwenye gari yake wakati yeye ni mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, kama mwenyekiti yupo kwenye hali hiyo wafuasi watakuwa kwenye hali gani.

Kiitifaki, Lowassa inabidi amsindikize mwenyekiti wa chama taifa kwa sababu Lowassa ndani ya CHADEMA ni mwanachama tu na hana cheo chochote. Kwa sasa ni kinyume chake!

Pesa na umaarufu wake ndiyo unawafanya viongozi wakuu wa CHADEMA wajishushe chini yake.

Money talks and money alone sets the entire world in.
 
Wanaukumbi.

Haya ndiyo majibu ya Mbowe kuhusu Dr.Slaa.


Mbowe-Tumekubaliana na Katibu Mkuu apumzike kwa muda, kwamba sis tuendelee na atakapokuwa tayari ataungana nasi mbele ya safari.

Mbowe-Chama hiki hatukiendeshi kwa siri, tunakiendesha kwa mikakati.

Mbowe-Tulilazimika kutumia kila mbinu halali ambayo inakiwezesha chama chetu kusaka matumaini na matarajio ya wananchi.

Mbowe-Tuliridhika pasipo shaka kwamba ugeni wa Edward Lowassa katika chama chetu ni mpango wa Mungu.

Mbowe-Umoja wetu ndio ushindi, fursa iliyojitokeza ni nadra.

Mbowe-Mtikisiko huu umekuja kwa CCM kipindi ambacho Watanzania wanamatamanio ya mabadiliko

Mbowe-Hatuwezi kuwa chama cha kuendelea kuhubiri mabaya ya jana tukashindwa kuhubiri maendeleo ya kesho

Mbowe- Kipigo wanachopata CCM, hawajawahi kukipata tangu tuanze siasa za vyama vingi

Mbowe-Kila tunayeweza kumpokea kutoka vyama vilivyo nje ya UKAWA tutamchukua

Mbowe-Mungu ameamua kutumia chama chetu kujeruhi na kuangusha CCM.

Mbowe-CHADEMA ni chama cha siasa, ni chama makini, chama makinI ni chama cha watu, chama kisichokuwa makini ni chama cha viongozi.
 
Wanajamvi hayo ni marejeo ya nyuma.

Kutokana na hali ilivyokambi ya upinzani, tutakuwa na mabandiko kueleza yaaymhusu Dr Slaa ,kauli tata za Mbowe na hatma ya upinzani
katka uchaguzi

Jambo moja la wazi, kwamba, political base ya CDM si kuwaipo paralyzed bali sasa ime collapse

Itaendelea....



 
Wanajamvi hayo ni marejeo ya nyuma.

Kutokana na hali ilivyokambi ya upinzani, tutakuwa na mabandiko kueleza yaaymhusu Dr Slaa ,kauli tata za Mbowe na hatma ya upinzani
katka uchaguzi

Jambo moja la wazi, kwamba, political base ya CDM si kuwaipo paralyzed bali sasa ime collapse

Itaendelea....

Tunasubiria mkuu tuweze kuchangia, maana hata mm nawaona sasa wanaweweseka tu, na kwa hakika kwa ushindi wowote watakaopata ni dhahiri hautakuwa wao bali ni wa EL na genge lake na kimsingi naona taasisi kama vile iko disolved na inahitajika kujipanga upya kwa sasa wameshashindwa
 
Ni matokeo ya kutowafikiria wananchi ila tu Ikulu, anayekomolewa ni mwananchi si CCM. Yalishaonekana.
Anaita sasa!
 
Wanaukumbi.

Mskilizeni Mwenyekiti wa Chadema hapa chini anatumia mfumo wa spika wa bunge Anna Makinda, kwenye mkutano wa Chadema...

https://www.youtube.com/watch?v=MbhVG64TRGM&feature=youtube_gdata_player.

Wakati akihutubia wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA, Mbowe anukuliwa akisema chama hakiwezi kumsubiri mtu katika kufanya maamuzi yake kwa sababu maamuzi ya wengi ni maamuzi ya Mungu.

Ameenda mbali zaidi na kudai, kuna falsafa inayosema, wakati wa kufanya maamuzi magumu lazima kila mwanamke na mwanamme asimame ahesabiwe.

Mbowe akamalizia kwa kusema, kuna msemo unaosema, ''time and tide wait nobody''.

Kwa tafsiri yangu, Mbowe alikuwa ana maana kuwa, No one is so powerful that they can stop the march of time!
 
Nguruvi3, mkuu muda wote mimi hujadili na wewe kama kulazimika maana huna adabu na mtovu wa heshima. Kwa hiyio usione watu tunajadili nawe ukajiona cake sana kumbe unaweza kuwa mwanangu maana mimi nagonga ngoma 6 na nina wajukuu zangu.. Hakuna mahala mimi hukuzungumzia wewe isipokuwa issue iliyopo ubaoni lakini mara zote lazima wewe utoke kwenye Issue na mimi ndiye niwe habari yako usivyoheshimu watu wengine.

Ni mada zipi ambazo wewe kweli umeona mimi nataka kuwagombanisha Mbowe na Dr.Slaa ama nazungumzia hali halisi iliyopo? Sasa kama wewe unayajua majibu kwa nini huyatoi, isipokuwa unataka kuuliza swali ambalo halina jibu? Halafu unauliza maswali meigine ya kipuuzi kwa sababu Chadema walipokuwa wakitoa fomu kila mtu kaona picha zake,na majuzi tu tumemuona Lowassa akikabidhiwa fomu unataka mimi niseme huko Chadema, hilo jukumu liko kwa nani wakati tunazungumzia kwamba fomu hazikutoka. Haya wee nambie huko CCM swala la fomu nani mwenye madaraka na itasaidia kitu gani ikiwa kuna mtu hakupewa ama hakuchukua.

Huyu mwenye madaraka hayo anahusika vipi? Kama ni wewe sema na utuambie nani alochukua fomu ya Urais Chadema kabla na baada ya Lowassa. Simple as that! usizungushe maana unataka kuikata kauli yangu kuwa ni uongo, sasa wewe sema ukweli ili watu wakusome na wachuje ukweli upi na uongo upi, kisha subiri maelezo kutoka kwangu. Unazungusha kwa nini? bila shaka huna hoja ila unatafuta pa kutokea kama kawaida yako.

Hii habari ya kuniita mimi Mkabila, Mfitini, mdini wakati wewe ndiye kinara uloanzisha hoja ya Ukabila wa Zitto na ACT. Wewe ndiye kinara mkuu JF wa kufitinisha Mbowe na Zitto, ukidanganya Umma mkwamba ACT ni CCM B kumbe ni Chadema! Nimekukamata kwa mangapi? na mangapi ulokuja jikuta kwamba nilichoandika miye ndio ukweli baada ya marumbano marefu! Na kwa nini wewe hutaki watu wayaseme makosa ya Chadema na viongozi wake, mbona ya JK na Lowassa tunayasema na husemi tunawachonganisha? Halafu hizi ni Events zilizokwisha tokea na migogoro ipo kweli sio uzushi..Chadema mna laana gani haswa!

Tafadhali sana mkuu nakuomba kwa mara nyingine, Unataka kujadili na mimi acha hii tabia yako ya kuita watu majina na matusi maana tunakuvumilia sana sisi wengine na hakuna wakati nakufanya wewe kuwa ndio hoja yangu ila unalazimisha watu waseme yasiyofaa kuandika. Mada umeianzisha mwenyewe na kuiita - CDM/UKAWA UWEKEZAJI USIOTABIRIKA... Sasa pengine wewe unafanya utabiri lakini miye nafahamu Uhalisia wake na ndicho nachoandika humu unataka kunikosoa elezea ukweli ni upi sio kuuliza swali lisilojibika. Unaposema watu wanapuuza hoja zangu ati mimi FITNA ndio hulka na utmaduni wangu haya matusi yanatokana na nini..Nilikufitini wewe na nani - Mkeo?

Mimi ndiye niliyemfukuza Dr.Slaa au tunaandika baada ya Dr.Slaa kupinga maamuzi yenu na hata kamsuta Yericko humu JF..Ugonvi wenu wenyewe kwa nini unataka kuuleta kwangu wakati sina mawasiliano na Mbowe wala Dr.Slaa niwafitinishe vipi!.Mkuu tafadhali fanya heshima kama wewe waona ukumbi huu ndio utauheshimu kuliko binadamu basi una matatizo ya akili...
- Thanks anyway..
 
Nguruvi3 na Mkandara:

Kwa vyama kama CDM na CUF kuchukua fomu ni formalities na msije mkagombana kwa suala hili. Kwa CDM Slaa alikuwa anapitwa bila kupingwa na kwa CUF, Lipumba alikuwa anapitwa bila kupingwa. Kama kuchukua fomu, walikuwa wanafanya hivyo hili kutimiza masharti ya kikatiba ya vyama vyao.

Kwa miaka 10 iliyopita CDM ilijitangaza kuwa ni Chama kinachojijenga kwa kutumia principles na moral values. Na kuna watu mlivutiwa na jitihada zao. Na mliamini wanachosema wholeheartedly. Katika uchaguzi huu, CDM imehamua kuachana kwa kiasi fulani na principles na moral values na kujaribu kutumia mikakati. Na mikakati mingine imewataka kuwakubali maadui wenu.

Miaka ya zamani, CDM kilikuwa ni chama cha mkondo wa kulia. Kimoyo nilikuwa karibu nao. Lakini walishindwa kuziuza siasa hizi kwa mtanzania wa kawaida. Na kimikakati walianza kuimba siasa za zamani za CCM: serikali kumiliki viwanda, elimu bure n.k bila kueleza tofauti yao na siasa za mwalimu Nyerere. Hapa mimi niliachana nao. Hivyo kwa maoni yangu CDM ni chama cha mikakati ambacho kinajaribu kutafuta sauti. Ukisoma falsafa yao ya vitabu na yale wanayolonga majukwaani unapata vitu viwil tofauti.

Tukirudi kwa Mbowe na Slaa. Kutokana backgrounds zao, kinadharia hawa ni viongozi wawili tofauti. Kama mfanyabiashara, Mbowe anaangalia maendeleo ya chama kimikakati. Wakati Slaa anaweza kuangalia maendeleo ya chama kwa kupitia darubini ya vile anavyoamini kuwa sahihi. Hivyo katika kipindi hiki cha mpito na uchaguzi, maendeleo ya baadaye ya CDM yanategemea sana uvumilivu wa Dr. Slaa kukubali yanayotokea kama mtu mzima, na vilevile kufanikiwa kwa mikakati ya bahati nasibu ya kumkubali Lowassa.
 
Mkuu Zakumi wala sikutaka kulizungumzia tena kwasababu Alinda aliweka ukweli
Hoja si kuchukua fomu , ni kauli za fitna. Kuna tofauti kati ya '' Zakumi nitakupiga na silaha '' na Zakumi nitakupiga na silaha

Mkandara alichoandika
Mkuu maneno haya sio kweli, Ofisi ya Chadema ilifungwa baada tu ya Lowassa kuchukua fomu na hakuruhusiwa mtu mwingine yeyote kuchukua fomu ya Urais, hivyo kupendekezwa kwa Dr.Slaa wakati uchukuaji fomu bado haujatangazwa rasmi haina maana yoyote. Chadema wametuonyesha mfumo mbovu kuliko hata ule wa CCM kuengua watu na kamati ya maadili jambo ambalo mimi naona CCM wameboresha mfumo wao zaidi ili kupata viongozi wenye sifa, zamani hapakuwa na sifa isipokuwa mwenye umaarufu na uwezo wa ku deal na matatizo!.

..
Hakuweka alama '' '' bali sentensi kama ilivyo. Kwa sisi wengine hilo lilitosha sana kuona uhuni uliofanyika.

Kufunga ofisi fomu zisichukuliwe ni uhuni wa kulaani. Tulipohitaji ufafanuzi, kaja na kauli , aah ni lugha ya mjini.


Huwezi kuandika uchochezi ukasema ni lugha ya mjini, huo ni uongo na ndiyo fitna.
Hakuzingatia alau kanuni za uandishi, aliongozwa na fitna


Hizi alama '' '' zina maana kwa msomaji. Ukweli ni kuwa hakuna ofisi iliyofungwa

Alipulizwa kwa fomu zipo chini ya mamlaka ya nani. Hakujibu, anachosema Dr Slaa amezuiwa.

Hoja kuu hapa si nani kachukua nani hakuchukua. Ni fitna ya uandishi kwa lengo la fitna.

Tuendelee na mambo mengine ya maana
 
Back
Top Bottom