
Kiukweli kabisa Lowassa ni risk sana kwenye kuwapasua CDM hasa kama swala la Dr.Slaa halijawa handled with care, na linaweza kuhatarisha zaidi kuliko faida, mm naomba nichangie mambo yafuatayo kwa mtazamo wangu,
1. Mm kimsingi nilipinga kabisa Lowassa kuhamia CDM na kugombea, nikipenda zaidi ahamie na kuwa nomarl part member na kuwasaidia UKAWA kwenye mapambano, lakini kama mnavyojua wengi wa viongozi waliona Lowassa ni fursa kwao japo ni fursa yenye mashaka makubwa wakaamua kugamble na kuitumia.
Kiukweli hakuna yyt ambae haoni impact iliyotokea CCM kwa kuondoka huyu Bwana, na ninadhani kama UKAWA wakishikamana angalau Bunge wanawezq kukamata, na ninadhani hiyo ndio target yao kubwa.
2. Dr.Slaa, huyu alitakiwa from begining ya makubaliano na EL awe clear na akubaliane na wenzake wote kama kweli wanasema walifanya vikao kadhaa kabla ya kumualika rasmi, na kama alikubali au kushawishiwa kwenye vikao mpaka akakubali basi sioni kama kutakua kuna shida yyt zaidi ya hizi porojo za kila siku kumuhus. kimsingi yeye ndio devide Factor kubwa ambayo ndio naiona kwa sasa, wakimuhandle kwa busara na yeye kuamua kufunika kombe mwanaharamu apite angalau tunaweza kuona matunda kidogo kwenye uwekezaji huu wa wenye risk kubwa waliofanya Ukawa.
Laah, akishupaza shingo na kukomalia msimamo wake kwamba hamtaki EL na kwamba hawezi kula matapishi yake, basi kutatokea na anguko kubwa sana kwa UKAWA nawatakua wameharibu hata kidogo walichokijenga, mpaka sasa mm sijajua standing yake baada ya EL kujoin kwamba ataendelea au ataachana na siasa, maana yeye yupo kimya kabisa, zaidi tunasikia tu vurumai za kwenye mitandao na magazeti kuhusu future yake after El envision.
3. Kwa sisi tunaopinga Kuhusu Lowassa, lazima pia tutafakari kwa kina na kwa mapana yake, hawa viongozi wa UKAWA ndio wameshakosea sana kwa kumkaribisha huyu mtu na muda umekwisha, je bora kukosa kabisa mabadiliko hata kama machache kuliko kumtumia EL kufanikisha hili jambo ambalo kwa utashi wao wao wanaona anaweza kuwavusha. Au kuendelea kukomaa na mabadiliko, kwamba mtoto ndio Kanyea Mkono (viongozi wa UKAWA kwa kumkaribisha EL kwenye uraisi) tuusafishe na kusonga mbele kuliko kuukata au kumpiga mtoto, maana ndio keshakosea. Ni fikra tatanishi sana ila ndio hali tuliyopo.
mwisho, mm nadhani ni busara UKAWA kuelewana mapema na kukubaliana katika kutokukubaliana, muda si rafiki tena na jamaa ndio huyo keshapewa bendera ya UKAWA so wayamalize na kusonga mbele, japo wamekosea njia, ila kikubwa kufika hata kama kupita kwa njia ya Pori.
So far sijajua msimamo wa Dr.Slaa maana sijamsikia exactly yeye binafsi akionge, ila kwa minong'ono iloyopo yeye ndio jabari linalogoma Fisadi kuongoza mapambano ya watakatifu kuwatoa mafisadi, kama ni kweli, muda hautoshi nayeye inabidi kwa kipindi kifupi hiki ajitafakari kama sisi (hoja namba 3) kwamba aendelee na msimamo wake ambao principally ni sahihi kabisa na kudhoofisha upinzaji kwenye uchaguzi huu kwa makosa ya wenzake, au apige moyo konde na kuwaunga mkono kibishi kufanikisha angalau kwa uchache kile amekua akikipigania siku zote. Japo sina uhakika kama nilivyosema juu ya msimamo wake juu ya hili jambo maana ni rumours tu ambazo zinazagaa bila uthibitisho wa moja kwa moja wa muhuika.
Hayo ndio maoni yangu wadau, tujadili kwa mustakabali wa taifa letu pendwaTz