CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika


Kweli LOWASA amebadilisha wengi,kwa kisingizio cha mabadiliko.. ETI watu wanauliza eti ufisadi ni RICHMOND tu,kwahiyo ndio nini,ugeugeu ni usaliti
 

Unafikiri mahali muafaka pa kujisafisha dhidi ya tuhuma za ufisadi ni jukwaani na sio kwenye vyombo vya sheria?

Na hii ndio shida tuliyo nayo watanzania. Kashfa ya Richmond imekuwa ni gumzo kwa miaka 8 kwa sababu tumekuwa ni watu wa kupiga makelele tu majukwaani halafu inaishia hapo! Vyombo vya dola (DPP, Polisi, TAKUKURU, etc..) hawajachukua hatua yoyote kwa miaka 8 huku watu wakiendelea kupiga kelele mtaani kuwa na "nyaraka" za ufisadi za Lowasa! Yeye mwenyewe ameshasema mwenye ushahidi dhidi yake aende mahakamani mbona mpaka sasa hakuna aliyekwenda ikiwamo Dr Slaa mwenyewe?

Leo hii naweza kwenda kwenye press nikakutuhumu wewe Galaxy S3 kwamba ni mwizi na nina nyaraka, halafu nakwambia kama unabisha njoo ukanushe ili niibue madudu zaidi (tishia nyau). Vyombo vya dola vinafanya kazi gani?
Na huu ndio utamaduni wa hovyo tuliojijengea kuwa ni watu wa kupiga kelele majukwaani huku wenye wajibu wa kuchunguza na kushitaki wakiwa likizo ndio tunapaswa kuupiga vita kabisa.
 
Kweli LOWASA amebadilisha wengi,kwa kisingizio cha mabadiliko.. ETI watu wanauliza eti ufisadi ni RICHMOND tu,kwahiyo ndio nini,ugeugeu ni usaliti
Nadhani hujawaelewa hao wanaosema hivyo.

Hoja yao ni kuwa , je, tukizungumzia Richmond hilo ndilo tatizo pekee la ufisadi lililopo nchini?


Hawajasema Richmond si tatizo, wameuliza, je, hilo ndilo tatizo pekee la ufisadi tunalodhani ndilo taifa linapaswa kupigana nalo?

Wengine wameuliza vile viporo vingine vipoje?

Hapa unapaswa kuelewa dhana na maana ya swali bilakuwahukumu hao unaowasema kabla ya kuwaelewa

Nadhani hili tumeshaiongelea hapo juu kwa undani ili listuondoe katika kiini cha mada kama alvyosema GalaxyS3
 
Last edited by a moderator:
Bavaria,

Ukipata bunge jingine ya "Wanaokubali, waseme Ndio" NDIYOOOOOOOO , ukaja kulalamika hapa. Ntakuja kukumbusha uhai ukiwepo mungu akipenda. It begins with you.

GalaxyS3
Nadhani hujanielewa ninacho maanisha.
Mimi binafsi napenda mfumo kama unaosema. Ila kwa Tanzania ninayoiona sidhani kama itatokea kwasababu mtu hawezi kusema anamchagua Lowasa kuwa rais na masabauri kuwa mbunge. Hilo haliwezekani kabisa.
Watanzania wanachagua chama hawachagui mtu, hata huyo mtu ameleta hoja kubwa kiasi gani.
 

Nimesema hivi kama Richmond ilizaa Dowans kwa maana hiyo Richmond na Dowans ni mikataba ya kifisadi, na haya maneno yanasemwa na serikali (Serikali nikiwa na maana ya Dr. Mwakyembe na Sitta ambao ni mawaziri tena ni wanasheria)

Sasa swali langu kwako au kwa mtu yeyote yule ni kama Richmond ni Lowassa ambayo ilizaa Dowans, Dowans inalipwa mamilion ya shilingi je ni kwanini serikali isisitishe mkataba wa Dowans na kuwachukulia hatua viongozi wote waliohusika na mikataba hewa hiki kigugumizi ni cha nini?

Ningeomba kupata ufafanuzi kutoka kwako....

Swala la Magufuli na nyumba, halihitaji mpaka Magufuli aibuke na kusema hivi au vile kunahitaji mimi na wewe kuhoji ni kwanini aliuza nyumba kwa bei ya kupwa na ni kwanini walihonga nyumba hizo kwa wake zake na wadogo zake? na si nyumba tu kuna hata bil 265 zimepotea katika wizara ya ujenzi, kuna kivuko kibofu cha bil.8 haya ni mambo ambayo hatuwezi kusubiri mpaka Magufuli kuibuka na sema maaana hawezi kuyasema bali ni wajibu wangu mimi na wewe kuhoji na kupata majibu kutoka kwake.

Na kama ndvyo kwa tusubiri mtu mpaka ibuke ndio tumuweke kikaangoni, Je kama Lowassa angekaa kimya inamaana hili Richmond lingepita tu bila kuhojiwa?
 

Labda iwe chaguzi zijazo mkuu.

Mawaziri wakuu kuondolewa madarakani ni sehemu ya kuwajibishwa na bunge.

Je, hao wabunge kwanin hawakumuwajibisha rais wa nchi kwa tuhuma za ufisadi?
 

..msamehe tu.

..kama uliweza kumsamehe Lukuvi, why not Lowassa?

..Magufuli naye ana rekodi ya kuongea kilugha kwenye shughuli za kiserekali. Je, hakuna mushkeli hapo?

..ushauri wangu ni kwamba tujikite kwenye sera na ilani za wagombea.
 
Last edited by a moderator:
..msamehe tu.

..kama uliweza kumsamehe Lukuvi, why not Lowassa?

..Magufuli naye ana rekodi ya kuongea kilugha kwenye shughuli za kiserekali. Je, hakuna mushkeli hapo?

..ushauri wangu ni kwamba tujikite kwenye sera na ilani za wagombea.
Wapi na lini nilimshamehe Lukuvi? najua sasa hivi hamuwezi kuona makosa ya Lowassa kwa mahaba nadhani baada ya uchaguzi tutakumbushana hizi kauli za kuomba kura Kanisani.
 
Wapi na lini nilimshamehe Lukuvi? najua sasa hivi hamuwezi kuona makosa ya Lowassa kwa mahaba nadhani baada ya uchaguzi tutakumbushana hizi kauli za kuomba kura Kanisani.

..mbona Magufuli naye amesema aombewe?

..tangu anachukua fomu Magufuli amekuwa akisema aombewe.

..kwanini hukulalamika wakati huo, unalalamika sasa hivi?
 
Mkuu mnashangaa nyie lakini mimi hainishangazi kabisa. Na najua watu watasema mimi mdini lakini ndio hali halisi (Reality) na ndivyo Edo alivyo. Hakuomba aombewe tu ila kasema ni zamu ya Warutheli na ndio kauli yake!..Wengi wanamsikia tu hawajui ya Nigeria na Ujarumani..

Kama aliweza kurudisha shule na Hospital zilizojengwa na Mkoloni Mjarumani mikononi mwa kanisa lake atashindwa nini? Yeye Mrutheli, Mbowe sijui, Mtei sijui, Wakaskazini wengi sijui...kwa nini anapewa support kubwa hivyo sijui!. Panapofuka moshi kuna moto! Mimi ningependa tu kujua huyu Gwajima Askofu mzima ameingiaje katika uongozi wa Chadema au UKAWA hadi awe mshauri na msemaji wao?

- Unategema nini kitaandaliwa hapo? Nimeandika haya najua yatakuja mashambulizi ya hali ya juu kwa sababu watu hawatazami reality, wanataka kudanganyana na bikra ya ndimu! Udini upo mkuu wangu na hautakwisha kirahisi...
 

Nimesikiliza clip yote sijaona alipoomba kura, nimesikia anaomba aombewe, labda kama nime miss habari kamili
 
..mbona Magufuli naye amesema aombewe?

..tangu anachukua fomu Magufuli amekuwa akisema aombewe.

..kwanini hukulalamika wakati huo, unalalamika sasa hivi?

Jokakuu;

Hayo mambo ya kuombewa ni kitu cha kawaida. Kwenye clip hii hapa anasema toka nchi iundwe nchi haijawai kuwa na rais mrutheri. Anasema Nyerere alikuwa mkatoliki, Mkapa alikuwa mkatoliki. Awe wanahusiana vipi na yeye kuombewa?

https://igcdn-videos-b-5-a.akamaihd...6-16/11936206_512395512258265_863362784_n.mp4




https://igcdn-videos-b-5-a.akamaihd...6-16/11936206_512395512258265_863362784_n.mp4
 
..mbona Magufuli naye amesema aombewe?

..tangu anachukua fomu Magufuli amekuwa akisema aombewe.

..kwanini hukulalamika wakati huo, unalalamika sasa hivi?
Kwa faida ya Wanaukumbi unaweza kutuwekea audio au video clip ya Magufuli akiomba kuombewa Kanisani ili ashinde urais kama Mkatoliki?

Halafu mimi silalamiki naeleza hali halisi na video clip hiyo hapo.

Mkuu naona unafunika kombe.....
 
Nimesikiliza clip yote sijaona alipoomba kura, nimesikia anaomba aombewe, labda kama nime miss habari kamili
Hamna tatizo mtu yeyote kuombewa haya maneno mbona ujayasema.

Anasema toka nchi iundwe nchi haijawai kuwa na rais MRUTHERI, Anasema Nyerere alikuwa mkatoliki, Mkapa alikuwa mkatoliki, mkuu hayo ndiyo maombi?

Kama mgombea urais anakwenda Kanisani na kuomba aombewe awe rais na kusema sasa hivi zamu ya MRUTHERI halafu watu wanakaa kimya daah!! Sijui zamu ya Wasabato lini.
 

Twende taratibu ni sek. ya ngapi anasema hayo maneno yaani hapo kwenye nyekundu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…