Adharusi
JF-Expert Member
- Jan 22, 2012
- 14,422
- 7,350
^1
Hivi Tanzania ufisadi umefanyika katika swala la Richmond tu?
Halafu kitu ambacho sijapata ufafanuzi wa kutosha ni Richmond (ufisadi wa Lowassa) ilizaa Dowans na Dowans ni mkataba wa kifisadi lakini mpaka sasa serikali inaendelea kulipa Dowans pamoja na kujua kuwa Dowans imetokana na Richmond ambayo ni ufasadi wa Lowassa.. Sasa swali ambalo hata wewe nafikiri utakuwa nalo kichwani Je kwanini serikali iendelee kulipa Dowans hali wanafahamu ni mkataba wa kifisadi na ulitoka kwa fisadi Lowassa? Hiki kigugumizi cha nini?
Swali la pili hivi Tanzania tatizo la ufisadi ni Richmond tu? Kama kuna matatizo mengine ambayo ni makubwa zaidi ya Richmond tena ambayo hata Magufuli anahusishwa, ni kwanini haya hayaongelewi linaloongelewa ni Richmond tu?
Je hatufahamu kuwa katika wizara ya Ujenzi bil.265 zimetoweka bila maelezo yeyote?
Na je tunamaelezo gani kuhusu nyumba za serikali pamoja na kuuzwa kwa bei ya kutupwa lakini nyingine ziligawiwa kwa nyumba ndogo?
Tunapojadili ufisadi wa Lowassa ambaye ni mgombea rais kupita Ukawa, basi tujadili hata ufisadi wa Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM.. hama sivyo tutakuwa tunapendelea upande mmoja na upande wa pili kuufanya kuwa mtakatifu wakati sivyo..
Kweli LOWASA amebadilisha wengi,kwa kisingizio cha mabadiliko.. ETI watu wanauliza eti ufisadi ni RICHMOND tu,kwahiyo ndio nini,ugeugeu ni usaliti