Alinda na Jokakuu;
Posti zenu zilinifanya nisome sifa za Dr. Slaa na kumkubali. Ghafla bin vuu, naona mmemwacha mzee wa watu na kumbeba Lowassa. Hakika siasa hazina marafiki na maadui wa kudumu.
Sijakuelewa unakata sek ya nini wakati unatakiwa kumuelewa msemaji! Hii hapa rudia kusikiliza
Mwalimu,
Katika mazungumzo au majadiliano kuna kitu kinaitwa context. Ni muhimu sana katika kufikia muafaka.
FACT: Richmond ilifanyika chini ya serikali ya CCM, na kwa jinsi serikali ya CCM inavyoendeshwa hakukuwa na hatua za kisheria zilizochukuliwa.
CDM kwa kujua hiyo fact hapo juu, wakaenda kushitaki kwa wananchi. Ndio maana leo unaona yanayoitwa mafuriko kwenye mikutano ya CDM kuelekea uchaguzi mkuu. Ambaye alishtakiwa kwa wananchi na CMD akitaka kujibu mashtaka yake (kwa kipindi hiki ambacho bado CCM inaongoza), inabidi akajibu hayo mashitaka kwa wananchi ambako alishtakiwa. Sasa ukisema kuwa jukwaani sio sehemu ya kujisafisha bali ni kwenye vyombo vya sheria (which is true) katika muktadha huu tunaouongelea unakuwa out of context. Ni kama vile hujui hili suala lilianzia wapi na lipo katika mazingira gani. Hizo kauli za mwenye ushahidi aende mahakamani ni kauli za ki CCM CCM tu. Wewe unazisema kwa kebehi kelele za mitaani juu ya ufisadi kwa miaka 8 lakini najua unajua kuwa umaarufu wa kisiasa ambao upinzani unafaidi sasa hivi umetokana na hizo unazo ziita kelele za mitaani. Na sitaki kuamini kuwa katika all seriousness unahoji vyombo vya dola vinafanya kazi gani katika zama hizi za CCM katika kujenga hoja zako.
Na ili tusiende nje ya maada kidogo, naomba niseme nukta tunaizungumzia hapa, ni hoja yangu hapa ni kuwa Lowasa alipaswa sio kujieleza kwa kamati kuu peke yake, bali ilipaswa aidha akajieleza kwa wananchi ambao kwa miaka 8 waliambiwa taarifa ya uvundo wa Lowasa au kamati kuu ieleze Lowasa alitoa vielezo gani vilivyo fanya ushahidi waliotangaza kwa miaka 8 kuwa wanao juu yake uwe hauna msingi tena.
Na ili kuondoa kujirudia rudia kwa maswali na hoja zile zile, mimi ukinipa mjadala unaosema kwa nini CCM haiwezi kufanya mabadiliko yanayotangazwa na Magufuli katika kampeni zake, nitazungumza na kuzungumza kila ufisadi uliowahi kutokea katika serikali za CCM zilizopita kujenga hoja zangu. Katika mjadala huo sitakaa hata sehemu moja kwenye hoja zangu nikamtaja Lowasa eti alihusika na Richmondi. Kwa sababu hicho kitu japo ni kweli, kitakuwa kiko nje ya mada husika.
Alinda na Jokakuu;
Posti zenu zilinifanya nisome sifa za Dr. Slaa na kumkubali. Ghafla bin vuu, naona mmemwacha mzee wa watu na kumbeba Lowassa. Hakika siasa hazina marafiki na maadui wa kudumu.
Kuhusu mchango wa Dr katika upinzani hasa CDM , hakuna shaka na hilo. Kazi yake kama katibu mkuu ilikuwa nzuri , fair to say...hata mimi aliyenivutia kuipenda CDM ni Dr.Slaa.
..pamoja na mapungufu yake ya kibinadamu naamini CDM isingefika hapo ilipo bila mchango wa Dr.Slaa.
..binafsi I wish CDM na Dr.Slaa wangemaliza tofauti zao ktk namna tofauti na ya kistaarabu kuliko hivi walivyofanya.
..pamoja na kumpenda Dr.Slaa, wako wana-CDM wengine ambao wamenivutia; watu kama Tundu Lissu, John Mnyika, Halima Mdee, Benson Kigaila, Godbless Lema, Mohamed Mtoi, Tumaini Makene, etc etc. Hatuwezi kuwatupa mkono wote hao kwasababu tu Dr.Slaa ameamua kubwaga manyanga.
..kama wanavyosema ktk siasa hakuna maadui wa kudumu, I hope and pray kwamba Dr.Slaa atarudishwa kundini wakati CDM na UKAWA wameingia madarakani.
NB:
..Particularly nachukizwa sana na mashambulizi yanayoelekezwa kwa mke wa Dr.Slaa. Mimi naamini kumshambulia mke wa mtu, au watoto wake, ni kuvuka mpaka wa siasa za kistaarabu.
Kwamba ikiwa EL ni fisadi mbona serikali haikumchukulia hatua ni hoja ya ajabu kwa kweli na ni hoja ambayo hivi sasa imepata mashiko ile mbaya! Kimsingi hoja ya kwamba mbona serikali haikumchukulia hatua ni hoja isiyo na mashiko unless kama unataka kusema nchi haina mafisadi! Ni nani miongoni mwa wengi waliotuhumiwa ufisadi wamechukuliwa hatua? Itoshe tu kusema kwamba hoja ya kwamba mbona hakuchukuliwa hatua wala haiwezi kumfanya mtuhumiwa wa ufisadi kuwa hana hatia unless kama tunataka kusema wale wote wanaotuhumiwa ufisadi nao ni wasafi!!!
Swali langu kwako ni rahisi sana nalo ni kama Serikali inafahamu kuwa Lowassa ni fisadi ni kwanini hamuchukulii hatua? tatizo liko wapi?
Richmond ni Mkataba wa kifisadi, na Richmond ndio ilizaa Dowans, ambayo serikali wanatuhaminisha kuwa ni Lowassa, na mpaka leo hii serikali hii inayolia na ufisadi wa Lowassa inaendelea kuilipa Dowans. (ambayo ni ya Lowassa fisadi). Kwa akili zetu za kawaida kwanini tusiamini maneno ya Lowassa kuwa Richmond ni kampuni ya mkubwa?
Na tatu Serikali wanatulilia kuhusu ufisadi wa Lowassa wanataka sisi tufanye nini?
Wananchi hawana shida ya ufisadi... anyway, am speechless! Binafsi mara zote nimekuwa nikisimamia jambo moja kwamba jamii yetu ni ya hovyo, imeoza kila mahali! Hata hivyo sikutarajia kama hali ni mbaya kiasi hiki cha kufikia kusema wananchi hawana shida ya ufisadi! Are you serious? Au ili mradi tu tunayemtaka ashinde urais! Lakini kwa upande mwingine unashangaza unaposema wananchi hawana shida ya ufisadi na wanachotaka ni ajira na huduma bora za kijamii!! Hizo ajira na huduma bora za kijamii zitatoka wapi ikiwa no body cares about corruptions?
Hivi vijana kukosa ajira ni kwa vile ni ufisadi wa Lowassa? Viongozi kutibiwa nje hali hospitali zetu hazina dawa nao ni ufisadi wa Lowassa?, nimeuliza swali moja kuwa hivi Tanzania kama taifa uchumi wetu unategemea nini? au nalo ni tatizo la Lowassa? mashule kukosa chaki, madawati, walimu kutolipwa mishahara inayokidhi mahitaji yao hali viongozi wakijilipa mamilioni na rais akipokea mshahara wa mil.192 nao ni ufisadi wa Lowassa?, Vifo wa watoto, wazazi kujifungulia chini, wajawazito kulazimishwa kupelekeka ndoo za maji wakati wa kujifungua hali wake wa viongozi wakienda kujifungulia Marekani nao ni ufisadi wa Lowassa? Tanzania tuna ardhi ya kutosha tena nyenye rutuba, tuna vijana hivi kama taifa tunashindwa kuwekeza kwenye kilimo hali soko lipo kuanzia hapa Afrika mpaka Ulaya and US au huo nao ni ufisadi wa Lowassa? Wakati vijana wetu wakitafuta ajira serikali inaorder samani za maofisi ya serikali kutoka China nao ni ufisadi wa Lowassa?
Mwaka 2010 hoja ya ufisadi ilikuwa moto moto lakini pamoja ya hayo watuhumiwa wote wa ufisadi akiwemo Kikwete walishinda kwa kishindo sasa labda nikuulize wewe je unafikiri ni kwanini hawa watu walishinda pamoja na tuhuma za ufisadi?
Kwamba ukiniuliza nitajibu nini kuhusu uchumi wa Tanzania unategemea nini zaidi ya madini na gesi; labda nikuulize wewe hiyo gesi ni gesi ipi unayoisema wewe? Tangu lini Tanzania imeanza kutegemea uchumi wa gesi? Hiyo gesi inauzwa nchi zipi? Na hata hayo madini unayosema wewe mapato yake hayafikii ya mapato kutoka sekta ya utalii
Nimekuuliza kama Taifa uchumi wetu unategemea nini?
Wakati wewe hutegemei chochote kutoka kwa Magufuri, mimi sitegemei chochote kutoka kwa yeyote kati ya hao mafahari wawili! Na kama umenisoma vizuri tangu mwanzo, ingawaje wengi wenu huwa mnajishitukia sana; mara zote hoja yangu imejikita kwenye suala la EL na kauli mbio ya mabadiliko! Mimi si leo wala si jana; mara zote msimamo wangu haujabadilika kwamba CCM na upinzani wote ni wale wale tu...!! Na sio CCM na upinzani tu, bali sehemu kubwa ya jamii ya Kitanzania ni corrupt community na ndio maana hata wakati wa mchakato wa katiba maoni yangu ilikuwa ni kuachana na what's the so called good governance... ingawaje lengo na misingi ya mfumo wa utawala bora ni mzuri lakini huwezi ku-practice good governance kwenye corrupt community! Na viongozi wetu wamekua wakiupigia chapuo sana huu mfumo coz' unasaidia kuficha uovu wao... ni sawa tu na ulivyosema wewe; kama EL ni fisadi mbona hajafikishwa mahakamani...
Hivi wewe kweli unataka kusema kila mtu humu ataandika neno kwa neno la mtu alosema au unaandika ulichoelewa? Watu wote wamemuelewa hivyo, na hata viongozi wa dini wamekemea kwa hilo iweje wewe ulielewa tofauti?NasDaz Si kweli kuwa ninatetea mgombea wangu, kwa kweli nitasema uongo kama nitasema nina mahaba na Lowassa..rejea maandishi yangu ya nyuma. Lakini nashindwa kuelewa mtu anapomwanga petrol kwenye nyumba inayowaka moto unategemea nini..
Sipendi kujadili mambo ya dini, kwenye mjadala ya dini huwa ninakuwa na kigugumizi gafla lakini hapo hapo sipendi kuona mtu anamtia maneno binadamu mwenzake ili akidhi haja zake.. Alichokifanya Lowassa ni kosa na ameona hilo na kuomba msamaha...
Bado ninafahamu kuwa nina deni la kujibu hoja zako..
Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste nchini, Askofu David Batenzi, akizungumzia suala hilo pamoja na kuipongeza NEC, alisema kitendo cha Lowassa kuwaomba Walutheri kumchagua si sahihi, kwa vile kiutaratibu kama taifa, hakuna zamu za dini katika urais.
Mkuu samahani kuingilia hoja yako.. kama tunautaka ukweli haswaa, Chadema lazima wakubali kupotosha watu ama wameteleza kisiasa wataeleweka lakini CCM kwangu mimi sidhani kama kuna kuomba radhi kwa sababu wao ndio walokuwa madarakani, hawakuteleza bali walikusudia.
Kitu kingine ambacho UKAWA wamebugi ni kwamba there is no way katika serikali yao iwapo watashinda wanaweza Kuiweka nje ya madaraka CCM moja kwa moja.
Ukawa walifanya Mistake ya Kugawana majimbo kwa misingi ya Vyama, Matokeo yake hakuna chama cha Ukawa chenye guarantee ya Kupata Majority ya Wabunge ili Kiweze Kutoa Waziri Mkuu kama katiba inavyosema.
Chadema wameachiwa na UKAWA Majimbo 139,
Wanahitaji kushinda majimbo hayo kwa zaidi ya Asilimia 90 ili waweze kuwa na Majority bungeni, Kitu ambacho ni ndoto!
Matokeo yake ni dhahiri Kuna Chance Kubwa kwa CCM iliyosimamisha Wagombea wengi kupata Wabunge wengi zaidi na Hivyo kutoa Waziri Mkuu.
Matokeo yake Ni kuundwa kwa Serikali ya Pamoja ya Ukawa na CCM, na hivyo lengo la Kuing'oa CCM madarakani lisifanikiwe moja kwa moja.
Je Iwapo, Ukawa watashindwa kupata Jumla ya Theluthi mbili ya Wabunge wa Bara na Visiwani, Hiyo Katiba ya Warioba watairudishaje?, Tusidanganyane, Muungano w Sasa wa Ukawa is a big Joke, na Watajikuta wanaumia Zaidi baada ya Uchaguzi huu kwa sababu muungano wao ni very Fragile!
JokaKuu nadhani umemfahamisha ZeMarcopolo kwa ufasaha kabisa
Ili serikali za nchi ziwe effective ni muhimu kuwa na 'majority' ya bunge
Kwa miaka mingi CCM wametumia mwanya huo si kuleta hali nzuri kwa wananchi bali ku-abuse
Wamefikia mahali serikali haina ushawishi isipokuwa kutumia bunge kutunga sheria kama zile za mtandao
Ili kuzuia kiburi na ujinga huo, matokeo yoyote yatakayobadilisha 'nguvu' za upande mmoja, na hapa ni CCM,yanatakiwa
Hilo litawarudisha katika mstari wa kukaa meza moja na wapinzani kujadili masuala kwa weledi na manufaa kwa ujumla
Hapa napo lipo tatizo. Ukiangalia kwa darubini wapinzani wameelekeza nguvu zao katika Urais bila kuliona hilo
Kuvunja mgongo wa ngamia, kutasaidia sana hili taifa. Kuendelea kuwapa CCM majority kutawafanya Watanzania kuongelea maendeleo ya majirani zetu. Hali ndivyo ilivyo sasa
JokaKuu nadhani umemfahamisha ZeMarcopolo kwa ufasaha kabisa
Ili serikali za nchi ziwe effective ni muhimu kuwa na 'majority' ya bunge
Kwa miaka mingi CCM wametumia mwanya huo si kuleta hali nzuri kwa wananchi bali ku-abuse
Wamefikia mahali serikali haina ushawishi isipokuwa kutumia bunge kutunga sheria kama zile za mtandao
Ili kuzuia kiburi na ujinga huo, matokeo yoyote yatakayobadilisha 'nguvu' za upande mmoja, na hapa ni CCM,yanatakiwa
Hilo litawarudisha katika mstari wa kukaa meza moja na wapinzani kujadili masuala kwa weledi na manufaa kwa ujumla
Hapa napo lipo tatizo. Ukiangalia kwa darubini wapinzani wameelekeza nguvu zao katika Urais bila kuliona hilo
Kuvunja mgongo wa ngamia, kutasaidia sana hili taifa. Kuendelea kuwapa CCM majority kutawafanya Watanzania kuongelea maendeleo ya majirani zetu. Hali ndivyo ilivyo sasa
..hoja yako ni ya msingi.
..nadhani ukawa walikuwa wanajaribu kujibu kiu na kilio cha muda mrefu cha wananchi kutaka vyama vya siasa viungane.
..kwa mtizamo wangu ukawa wamefanya kile kinachowezekana kwa kuzingatia matakwa ya sheria zilizopo.
..wakati wote wa majadiliano haya viongozi walikuwa wakisisitiza suala la MARIDHIANO. kwa maana nyingine walijaribu kuangalia maslahi ya kila chama kilichoko ktk ukawa.
..YES, kuna uwezekano mkubwa kwamba CDM wanaweza wasipate majority itakayowawezesha kuteua Waziri Mkuu.
..ikiwa hilo litatokea basi upinzani utakuwa na wakati mgumu. Kimbilio la mwisho katika mazingira hayo ni CCM ikose 2/3 ya wabunge na hivyo kutokuwa na uwezo wa kupitisha bajeti wao wenyewe.
..CCM wakikosa hiyo 2/3 basi watalazimika kuteua wabunge toka ukawa kuingia ktk baraza la mawaziri. Katika mazingira hayo EVERY BODY WINS na tutakuwa tumefungua ukurasa mpya ktk demokrasia ya nchi yetu.
NB:
..wakati mwingine tusiangalie tu kwamba wameshinda CCM, au wameshinda UKAWA. How about a situation where these two sides have to meet somewhere in the middle? Wouldn't that be better for the country/wananchi?
cc Rev. Kishoka, NasDaz, Mkandara, Alinda, GalaxyS3, Mchambuzi