CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

WAPINZANI WAPOTEZA MTAZAMO ‘FOCUS'

Tumesema huko nyuma, kati ya nyenzo muhimu zaushindi ni kutumia ‘shina' political base popote ilipo.

Hawa wanafahamu vyama kuanzia chini na ndio wajenzi.

Kupoteza political base ni jambo la hatari na madhara yake hayaonekani kwa haraka au kwa urahisi

Vikao vya UKAWA vimeendelea kwa siku nyingi. Mivutano ikiwa namna ya kupata majimbo na wagombea

Katika hali isiyokuwa ya kawaida kila chama kikatangaza ratiba ya kura za maoni, likatoa nafasi wanachama kugombea

Kura za maoni zina maana, kumpata anayekubalika atakayejenga mtandao katika ngazi husika. Kazi inahitaji muda/fedha

Katika mazingira ya kushangaza, majimbo yakagawanywa.

Zipo sehemu walioshinda kura za maoni wakaaachwa kupisha wagombea wa vyama vinginevya UKAWA

Yapo maeneo wanachama wameachwa kupisha waliohamia . Hili linafanyika bila kuangalia impact yake katika political base

Hayo mawili yameumiza Upinzani. Kuna matimbwili kama la Bunda, Sikonge ambapo Said Nkumba ghafla karudi CCM.

Haiwezekani wananchi wa react, makao makuu wasiwe na ufahamu

Kukiwa na sintofahamu hizo zinazogusa political base ya upinzani,wanafanya makosa, haionekani kuna anayetambua hilo

Kutokana na kuptoeza focus, na matumaini hewa UKAWA waliojazwa, hadi sasa wamepoteza majimbo 5.
Kabla hawajazindua kampeni kwa jinsi tulivyofauatilia, wameshapoteza

Huko kwingine kuna confusion, demoralization n.k. kwasababu hakuna mtu wa kuweka mambo sawa.

Hapa tunasema Dr Slaa alikuwa mtu aliyeweza kufuatilia kwa ukaribu. Alikuwa na ufahamu wa siasa kwa ujumla.
Ni ukweli lazima usemwe

Kwa viongozi waliopo, CUF haina uongozi unaoeleweka, CDM structure yao haijaziba pengo.
NCCR afadhali kidogo maana wao hawana cha kupoteza.

Uongozi wa juu wote umemzunguka Lowassa na kufanya maandalizi ya Lowassa bila kujua nini kinaendelea majimboni.

Yaani shauku kubwa ipo kwa mtu bila kujali huko mitaani nini kinaendelea.

Akina Tundu wanasema, wanajua walikuwa dhaifu sana katika baadhi ya maeneo ya nchi.

Hao hao akina Lissu sasa hivi hawana habari wamejikita katika Urais. This is wrong! Na kundi la ujio halionakani ku merge

CCM wakipata majimbo 2/3 mnatoa fursa kwa vyombo ''kufanya mambo yao''

Mnachotakiwa ni kushinda ili kuzuia kufinyangwa matokeo bilasababu.

Wapinzani mna disadvantage kwamba hamna vyombo vya kuwasaidia. Lazima mshinde kwa kishindo

Na kazi ya kushinda si ya mtu wala matumaini tu, ni kazi za wanachama waliojenga vyama hivyo, na kazi ya viongozi wanaoangalia ramani kwa ukubwa wake na si wingi wa mikutano.

Lipo tatizo upinzani, wasipoangalia CCM itawatokea kwa nyuma ikisaidiwa na vyombo vya umma.

Tunarudia lipo tatizo, hawajajipanga na wakiendelea na hali iliyopo watalipa gharama

Wamepoteza focus, wanamtazama mtu kama chama bila kujua ushindi ni suala la team !

Tusemezane
 
Nguruvi, umesema jambo moja ambalo watu sidhani kama wamelifikiria sana matokeo yake:

Mbowe anagombea Ubunge Hai
Mnyika anagombea Ubunge Kibamba
Tundu Lissu anagombea Ubunge Singida Mashariki
Peter Msigwa anagombea Ubunge Iringa Mjini
Godbless Lema anagombea Ubunge Arusha Mjini
John Heche - Tarime Mjini
Alphonse Mawazo - Busanda
Halima Mdee - Kawe
Mwita Waitara - Ukonga
Joshua Nassari - Arumeru Mashariki
Wilfred Lwakatare - Bukoba Mjini
Anthony Komu -

Viongozi walioachwa makao makuu - wote siyo wanasiasa hasa ukiondoa Naibu Katibu Mkuu Salum Mwalimu(Zanzibar).

Prof. Abdallah Safari
Prof. Mwesiga Beregu
Victor Kimesera.

Ni wazi basi kampeni ya Lowassa itaendeshwa ama na watu wengi wa CUF, wale wa "Ulipo Tupo" au na watu ambao kwa kweli siyo wanasiasa hasa.

Sasa hao hapo tunaweza kuwaita ndio wachezaji nyota wa CDM; lakini miezi hii miwili inayokuja wote watajikuta wanabanwa kwenye majimbo yao na siku ya uchaguzi kama ilivyokuwa 2010 hakuna hata mmoja wao atakayekuwa Makao Makuu kusimamia kura za Urais! Wote watabanwa majimboni! Siyo tu kwamba athari zake zitaonekana kwenye kura za Urais na majimboni lakini pia zimeanza kuonekana sasa hivi. Napenda sana kutumia mfano wa harakati za vita; majenerali wote kamwe hawaendi mstari wa mbele. Wanaoshinda vita siyo wale tu walioko katika mapambano bali hata walio mstari wa nyuma - wenye kuhakikisha walio mstari wa mbele wana kila kitu kinachohitajika kushinda vita. CDM wanarudia lile lile la 2010 - majemedari wake wakuu wote wako mstari wa mbele...

Viongozi walioach
 
Hata kama UKAWA wangefanya vile ambavyo mngependa wafanye, hivi kweli mnadhani yule Jaji Lubuva ana ubavu wa kumtangaza Edward Lowassa kuwa ndo mshindi wa nafasi ya urais?

Kwa nini hamlichukulii suala la tume ya uchaguzi ambayo imeteuliwa na mwenyekiti wa CCM kwa umaanani wake?

Hivi kweli kabisa mnadhani hiyo tume haikuundwa kulinda maslahi ya CCM? Tume ambaye imeteuliwa na mwenyekiti wa CCM?

Kuna mambo yaliyo ya msingi zaidi katika kuhakikisha tunakuwa na chaguzi zilizo za huru na haki lakini watu hata hamlioni hilo!

SMDH!!!!
 
WAPINZANI WAPOTEZA MTAZAMO ‘FOCUS'

Tumesema huko nyuma, kati ya nyenzo muhimu zaushindi ni kutumia ‘shina' political base popote ilipo.

Hawa wanafahamu vyama kuanzia chini na ndio wajenzi.

Kupoteza political base ni jambo la hatari na madhara yake hayaonekani kwa haraka au kwa urahisi

Vikao vya UKAWA vimeendelea kwa siku nyingi. Mivutano ikiwa namna ya kupata majimbo na wagombea

Katika hali isiyokuwa ya kawaida kila chama kikatangaza ratiba ya kura za maoni, likatoa nafasi wanachama kugombea

Kura za maoni zina maana, kumpata anayekubalika atakayejenga mtandao katika ngazi husika. Kazi hinahitaji muda/fedha

Katika mazingira ya kushangaza, majimbo yakagawanywa.

Zipo sehemu walioshinda kura za maoni wakaaachwa kupisha wagombea wa vyama vinginevya UKAWA

Yapo maeneo wanachama wameachwa kupisha waliohamia . Hili linafanyika bila kuangalia impact yake katika political base

Hayo mawili yameumiza Upinzani. Kuna matimbwili kama la Bunda, Sikonge ambapo Said Nkumba ghafla karudi CCM.

Haiwezekani wananchi wa react, makao makuu wasiwe na ufahamu

Kukiwa na sintofahamu hizo zinazogusa political base ya upinzani,wanafanya makosa, haionekani kuna anayetambua hilo

Kutokana na kuptoeza focus, na matumaini hewa UKAWA waliojazwa, hadi sasa wamepoteza majimbo 5.
Kabla hawajazindua kampeni kwa jinsi tulivyofauatilia, wameshapoteza

Huko kwingine kuna confusion, demoralization n.k. kwasababu hakuna mtu wa kuweka mambo sawa.

Hapa tunasema Dr Slaa alikuwa mtu aliyeweza kufuatilia kwa ukaribu. Alikuwa na ufahamu wa siasa kwa ujumla.
Ni ukweli lazima usemwe

Kwa viongozi waliopo, CUF haina uongozi unaoeleweka, CDM structure yao haijaziba pengo.
NCCR afadhali kidogo maana wao hawana cha kupoteza.

Uongozi wa juu wote umemzunguka Lowassa na kufanya maandalizi ya Lowassa bila kujua nini kinaendelea majimboni.

Yaani shauku kubwa ipo kwa mtu bila kujali huko mitaani nini kinaendelea.

Akina Tundu wanasema, wanajua walikuwa dhaifu sana katika baadhi ya maeneo ya nchi.

Hao hao akina Lissu sasa hivi hawana habari wamejikita katika Urais. This is wrong! Na kundi la ujio halionakani ku merge

CCM wakipata majimbo 2/3 mnatoa fursa kwa vyombo ''kufanya mambo yao''

Mnachotakiwa ni kushinda ili kuzuia kufinyangwa matokeo bilasababu.

Wapinzani mna disadvantage kwamba hamna vyombo vya kuwasaidia. Lazima mshinde kwa kishindo

Na kazi ya kushinda si ya mtu wala matumaini tu, ni kazi za wanachama waliojenga vyama hivyo, na kazi ya viongozi wanaoangalia ramani kwa ukubwa wake na si wingi wa mikutano.

Lipo tatizo upinzani, wasipoangalia CCM itawatokea kwa nyuma ikisaidiwa na vyombo vya umma.

Tunarudia lipo tatizo, hawajajipanga na wakiendelea na hali iliyopo watalipa gharama

Wamepoteza focus, wanamtazama mtu kama chama bila kujua ushindi ni suala la team !

Tusemezane
Mkuu huwezi kuamini haya yote niliyatazama mapema hata kabla ya kufi8kia hapa tulipo leo. Chadema ilitakiwa toka 2011 kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2015 baada ya mafanikio yake lakini wakajisahau wakalewa umaarufu mdogo walopata, kisha wakaanza kuogopeshwa wakaogopa wakaanza kuchambuana, wakageukana. Muda mwingi wakautumia kujisafisha wao wakati ni wasafi isipokuwa wameambiwa nyumba ina harufu kumbe harufu inatoka chooni sio wao!

Sasa wamefika pasipo weza tena kuzuilika. Unakumbuka nilikwambia hata Katiba mpya, CCM kuanza na ibara ya sita ya rasimu ilikuwa ujanja wao wakijua mtaanza kukosana na penngine katiba isiandikwe? Je unakumbuka kwamba JK aliisoma Katiba hata kabla haijaenda Bungeni akamwambia Warioba iko powa, kufika Bungeni akawageuka!..WHY?

Hii yote ilipangwa na CCM walitaka sana Uchaguzi huu ufanyike kwa katiba ya mwaka 1977 au yao ya Pendekezwa ambayo Tume ya uchaguzi sio huru, TISS sio Huru na hawawezi kupoteza nguvu ya rais na serikali kuu kabla ya uchaguzi huu. na kikubwa zaidi chama mbadala kimevurugika. Na wamefanikiwa yote sema liloongezeka ni kujisafishwa wao na Chadema ilopoteza mwelekeo baada ya kuvugwa kupokea makapi (magamba)..Kwao wametumia chekechea kuondoa makapi ya mpunga!

Nina hakika kati ya majimbo 265 (kama sikosei), Chadema wanayo 135, CCM itasimamisha kote majimbo 265 sidhani kama kuna ushindi hapa acha mbali kujipanga. Chadema ile ya mwaka 2010 ingesimama imara na kujiandaa vema kwa mwaka huu baada ya kuwasoma NCCR na CUF walivyosambaratika basi CCM ingekuwa na wakati mgumu zaidi leo hii.
 
Mkuu NN

Ukisoma mabandiko siku mbili zilizopita, tume waambia wapinzani wana disadvantage si ya tume tu, bali vyombo vyote

Tumeuliza vipi Polisi wakataze zomea zomea leo hii kulikoni?

Tukahoji msajili wa vyama anapokemea viongozi wa dini hilo limeanza lini wakati Lukuvi yupo katika video ya kanisani akiwakilisha kwa kauli za uchochezi za kidini?

Kuhusu tume, kosa hilo walifanya wapinzani kwa kupumbazwa. Kuna uzi wa Juisi ya maembe tumelizungumzia sana.

Lakini kuna ushahidi, wananchi majimboni wakiwa na usaidizi wa wenye weledi, uchakachuaji zuilika.

Maana yake, wapinzani wakipata wabunge z 2/3, hakuna namna uchakachuaji unaweza kuwana tija katika ngazi ya Urais

Hoja yetu, UKAWA wametumia muda mwingi sana, leo inawezekanaje saa chache za uzinduzi wa kampeni wameshapoteza majimbo 2 na mengine 3 huenda wakapoteza ?

Angalia focus ipo katika ngazi ya Urais. Na Mzee Mwanakijiji kasema uzuri hapo juu

Jiulize nani anayehoji majina ya watu kukosekana katika BVR? Nani anajua BVR inafanyaje kazi ?

Ukitaka kujua lipo tatizo, hakuna mtu aliyesimama ku-rebuttal ya jangwani, kisera au kimantiki.
Wapinzani wanasubiri muda wao, bilakujua kusubiri ni kutoa muda kwa CCM

Wangekuwa na focus habari inayotawala ingekuwa mkutano wao,nini wanatrajia kufanya
.

Wangeongelea matatizo yanayojitokeza majimboni, BVR n.k.yote ni kudhibiti CCM wenye vyombo vya umma. Hakuna!

Uchaguzi katika nchi za Afrika si sanduku au kura tu

Hii euphoric ya watu mikutanoni inawapa false impression , they have to change

CCM wakisema bao la mkono wana uhakika bao linapatikanaje.

Bila kuangalia mambo kwa mtazamo mpana, wapinzani watalipa gharama kubwa!
 
Nina hakika kati ya majimbo 265 (kama sikosei), Chadema wanayo 135, CCM itasimamisha kote majimbo 265 sidhani kama kuna ushindi hapa acha mbali kujipanga. Chadema ile ya mwaka 2010 ingesimama imara na kujiandaa vema kwa mwaka huu baada ya kuwasoma NCCR na CUF walivyosambaratika basi CCM ingekuwa na wakati mgumu zaidi leo hii.

Maneno mazito mkuu wangu; ila usije ukaambiwa ati sasa hutaki mabadiliko kwa vile hushabikii ngoma hii. Ila ni ukweli kabisa binafsi sijui ndio uwa too idealistic or what; sikufikiria in all my thinking kuwa CDM watamsimamisha Lowassa kama mgombea wao! I'm still in a state of utter disbelief.
 
Hata kama UKAWA wangefanya vile ambavyo mngependa wafanye, hivi kweli mnadhani yule Jaji Lubuva ana ubavu wa kumtangaza Edward Lowassa kuwa ndo mshindi wa nafasi ya urais?

Kwa nini hamlichukulii suala la tume ya uchaguzi ambayo imeteuliwa na mwenyekiti wa CCM kwa umaanani wake?

Hivi kweli kabisa mnadhani hiyo tume haikuundwa kulinda maslahi ya CCM? Tume ambaye imeteuliwa na mwenyekiti wa CCM?

Kuna mambo yaliyo ya msingi zaidi katika kuhakikisha tunakuwa na chaguzi zilizo za huru na haki lakini watu hata hamlioni hilo!

SMDH!!!!

NN, nitakuambia kitu kimoja. Mfumo wetu wa sasa wa Uchaguzi ulivyo tu bado kabisa unawezesha CCM kuanguka kwenye sanduku ka kura. Siyo tu kwenye Ubunge hata kwenye Urais wanaweza kuanguka. Siyo suala la tume tu ilivyo au kuteuliwa kwake. Tume ya Uchaguzi ya Nigeria haina tofauti na tume yetu kwa kiwango kikubwa tu; lakini hata wao hawakuweza kuzuia Buhari kushinda.

Nitakuambia mambo machache tu.

1. Matokeo yote ya Uchaguzi wa Wabunge Udiwani yanatangazwa majimboni. Hii ndio sababu ni rahisi sana kwa wabunge kushindwa na hakuna ubishi hasa.

2. Kinyume na fikra za watu wengi, matokeo ya Urais nayo yanatangazwa majimbo vile vile na kisheria ndiyo yanatangazwa kwanza kabla ya matokeo ya Urais. Yaani, yule Msimamizi wa Uchaguzi anaposimama anatakiwa kisheria - siyo suala la hiari - kusoma jumla ya matokeo ya Urais pale jimboni nani ameongoza. Hili halihitaji TUme ya Taifa ya Uchaguzi.

3. Katika majimbo yote zaidi ya 230 CDM kama chama kikuu cha upinzani kimesimamisha wagombea karibu 139 tu hivi. Ina maana kuna majimbo zaidi ya 100 ambayo CDM haina mgombea na kwa kiasi kikubwa haina wasimamizi isipokuwa wa vyama vigine vya upinzani. Kwangu mimi hiyo peke yake ilitosha kuwa kashfa. Yaani miaka mitano ya kelele zote CDM haikuweza kusimamisha wagombea kwenye majimbo yote. Unajua chama gani kinafuatia kwa kuweka wagombea wengi wa Ubunge kwenye kampeni hii - ACT! Go figure.

4. Nikirejea hiyo point ya 2 hapo juu, matokeo ya Urais yakishatangazwa kwenye jimbo na kusainiwa na wawakilishi na wahusika yanatumwa kwa TUme ya Taifa ya Uchaguzi. Hili nalo ni kwa mujibu wa sheria.

5. Tume ya Taifa ya Uchaguzi inachofanya ni kukusanya na kujumlisha (collecting and tallying) matokeo kutoka majimbo yote ya kura za Urais. Kumbuka kwenye Ubunge mgombea akishatangazwa ni mshindi na Msimamizi ndio imetoka hiyo; hausubiri Tume ya Uchaguzi. Ubishi wowote ni mahakamani lakini utakuwa ni ubishi dhidi ya mbunge mteule.

Sheria yetu imeweka utaratibu huu wa Tume na kura za Urais kwa sababu moja kubwa tu. Nchi yetu bado ni kubwa na haikuwa na nyenzo nzuri za kukusanya matokeo ya uchaguzi kutoka sehemu mbalimbali za nchi. Hivyo, ilipewa jukumu la kuhakikisha kuwa matokeo ya Urais lazima yawe yote yamekamilika na kujumlishwa na chombo kimoja kabla ya kutangazwa rasmi.

5. Kutokana na hilo la 4 wapo wanaodhani kuwa basi Tume itaweza kubadilisha matokeo tu hivi hivi. Hili si rahisi isipokuwa pale ambapo huna waangalizi wa kujua matokeo ya Ubunge kwenye majimbo yote yanayogombaniwa. Hata kwenye majimbo ya "wanaopita bila kuchaguliwa" huko pia lazima matokeo ya Urais yatangazwe jimboni. Sasa kama chama hakina mwakilishi kwenye majimbo yote, matokeo yakichakachuliwa nani alaumiwe wakati tulishaliangaliza hili tangu 2011?

Kimsingi basi, ukiweza kupata matokeo ya Urais kutoka majimboni - yale rasmi yanayotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi basi utaweza kumjua mshindi wa kiti cha Urais kabla matokeo rasmi hayajakusanywa toka nchi nzima. La maana ni kuangalia hasa majimbo gani yatachelewesha kutangaza kura za Ubunge na hivyo kuchelewesha matokeo ya kura za Urais.

Hili nililopigia mstari na kulibold lisome mara mbili. Clue. Likukumbushe jinsi gani Mrema alivyochezewa 1995 na majimbo ya Dar na jinsi gani Slaa naye alichezewa 2010.
 
NN, nitakuambia kitu kimoja. Mfumo wetu wa sasa wa Uchaguzi ulivyo tu bado kabisa unawezesha CCM kuanguka kwenye sanduku ka kura. Siyo tu kwenye Ubunge hata kwenye Urais wanaweza kuanguka.

Kama ni suala la uwezekano [possibility] tu hilo sina ubishi nalo sana kwani ni mengi tu yanayowezekana.

Hoja au wasiwasi wangu ni je, kwa sasa jinsi ambavyo mambo yalivyo [CCM kushikilia dola na kadhalika], uelekeo [likelihood] wa CCM kushindwa kwenye sanduku la kura kihalali upo?

Jibu ni hakuna.

Binafsi sioni CCM ikiachia madaraka kirahisi rahisi tu hivi kupitia sanduku la kura. Dola nzima wameishikilia wao. Tume nzima ya uchaguzi imeundwa na wao [na nahisi hao wajumbe kama si wote basi wengi wao watakuwa ni makada wa CCM tu kama tulivyoshuhudia kwa yule aliyekuwa jaji mkuu na makamu mwenyekiti wa hiyo hiyo tume ya uchaguzi alipotangaza nia ya kugombea uteuzi wa nafasi ya kugombea urais kupitia CCM. Kumbe miaka yote hiyo akiwa makamu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi huenda alikuwa kada wa CCM tu. Sasa unadhani hata huyo Damian Lubuva si mwanaCCM?].

Siyo suala la tume tu ilivyo au kuteuliwa kwake. Tume ya Uchaguzi ya Nigeria haina tofauti na tume yetu kwa kiwango kikubwa tu; lakini hata wao hawakuweza kuzuia Buhari kushinda.

Mzee, mazingira ya Nigeria ni tofauti sana na ya kwetu.

Kwanza, chama tawala cha People's Democratic Party [ambacho Goodluck Jonathan alitokea] hakikuwa chama tawala tokea Nigeria ipate uhuru wake zaidi ya miaka 50 iliyopita. PDP wameingia madarakani mwaka 1998 tu.

Sasa linganisha PDP na CCM! Watanzania tulio wengi hatujui chama tawala kingine zaidi ya CCM na madhila yote tuliyonayo sasa yamekua, yameshamiri, na mengine kuanza chini ya hao hao CCM.

Halafu, tofauti na Nigeria, sisi viongozi wetu wa tume wakishateuliwa na huyo mwenyekiti wa CCM ndo imetoka hiyo. Mambo ya kuidhinishwa sijui na bunge hakuna.

Sasa huko Nigeria, Prof. Attahiru Jega [aliyekuwa mwenyekiti wa INEC hadi mwezi Juni mwaka huu] aliteuliwa na rais Goodluck Jonathan lakini huo uteuzi ulikuwa ni lazima uthibitishwe/ uidhinishwe na bunge la seneti.

Licha ya hivyo, huo uteuzi wa Prof. Jega uliidhinishwa pia na 'National Council of State' ambao mkutano wake ulihudhuriwa na marais wa zamani wa Nigeria [akiwemo Muhammadu Buhari], rais wa seneti, spika wa bunge, magavana wa majimbo mengi ya Nigeria.

Na kwenye huo mkutano kulikuwa na 'unanimous approval' kwa Prof. Jega kuwa mwenyekiti wa hiyo tume huru ya uchaguzi ya Nigeria.

Sasa hebu linganisha jinsi Nigeria walivyompata mwenyekiti wa INEC na jinsi hawa wenyeviti wa NEC yetu wanavyopatikana.

Mimi nina uhakika hata wewe mwakani Magufuli akikuteua kuwa mwenyekiti wa NEC basi utakuwa tu maana baada ya uteuzi utakachobakiza ni kwenda Ikulu na kusimama mbele yake huku umeshikilia biblia yako sijui ya King James ile na kuapa mbele yake....tayari kitu na boksi.....Mzee Mwanakijiji ndo mwenyekiti mpya wa NEC.

Hahahaaaaaaa.......dude, we are not serious at all!!!!!
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji , bandiko lako 287 limenitoa wasiwasi kuhusu mtazamo wangu.

Nilidhani naona maruwe ruwe wasiyoona wenzangu.Bandiko linashadidia hoja ya kwamba, uchaguzi hauanzi na kuishia katika kura.

Yapo mengi yanayo influence ushindi au kushindwa hasa katika nchi zenye kubahatisha demokrasia kama yetu

Hoja yako namba 1

Unachosema ni kuwa uwezekano wa wapinzani kushinda au kushindw upo mikononi mwao.

Ni kwa msingi, tunasisitiza kuwa kukosekana kwa 1/3 au 2/3 kutahusishwa na uzembe. No more no less

Hoja namba 2
Ni kweli wengi hawafikirii matokeo ya Urais. Hii ni kwasababu matokeo ya ubunge yanachukua sehemu kubwa.

Kunapokuwa na frustration kidogo, watu wanapoteza focus ya kuwa kama mbunge wao kashindwa bado wana jukumu la kura za Urais

Endapo wangejipanga kama CCM kungekuwa na mawakala ''independent'' wa kura za urais tu ili wasiwe katika fukuto la ubunge kama tulivyoeleza

Hoja namba 3
Tunarudi pale pale kuwa katika majimbo 100 Chadema wasiyo namtu aliyesimama, wameacha wapinzani wasimamie kura za ‘mgombea' wao. Sijui hi iitafanya kazi kiasi gani. Suluhu ilikuwa kuwa na mawakala kutoka makuu
wa kushughulikia hayo.

Mawakala wangeweza kupatikana katika majimbo wakiwa responsible kwa makao makuu.

Katika majimbo 100 watafanyaje, inabaki kuwakitenda wili

Kuhusu kutokuwa na watu, Lissu alisema wamebaini ni dhaifu na ujio ungesaidia kuziba mianya hiyo.

Ujio wenyewe ni wa akina Said Nkumba.Lakini cha kujiuliza hivi miaka 5 walishindwaje kuwa na watu thabiti maeneo hayo?

Nakumbuka uzi wa Mwanakijiji tulisema, zile operation zisiihie mikutanoni, lazima zizae matunda.
Ndipo namuuliza Lissu miaka yote hawakuona udhaifu?

Hoja namba 5

Hili la kupita bila kupingwa lina disturb sana. Wapinzani wakijua wana upungufu hawakupaswa kuacha hali hiyo.

Hivi inakuwaje wagombea waCCM wapite tu UKAWA wakiwa hawajui nini kimetokea. Real!

Huko wanakopita bila kupingwa, ndiko tume na CCM wanaweza kuafikiana. Mana hakuna mtu wa kuhakiki.

Kumbuka CCM ilibadili sheria kuondoa 2/3 na mshindi ni kwa 50.1 .Jimbo zima likichakachuliwa 0.1 inapatikana bila tabu.

Haya yote yanatakiwa yawe mezani, yajadiliwe na kuundiwa mikakati.

Si kuendeleza euphoria ya nyomi katika mikutano. CCM wana utaalamu wakushinda.

Wao hawajui kura wanajua namna ya ‘kupata kura'

CCM wakisema goli lamkono, they mean it
 
Hahahaaaaaaa.......dude, we are not serious at all!!!!!

Right on! unajua ukweli ni kuwa hata Urais wakitaka kushinda wanaweza. Nigeria Tume ya Uchaguzi ilijaribu kudhibiti matokeo ya kura za Urais lakini walishindwa. Walishindwa kwa sababu upinzani wakisaidiwa na vyombo huru vya habari waliweza kukusanya na kutangaza matokeo toka kila State kabla hayajafikishwa rasmi NEC yao. Matokeo yake ni kuwa Buhari alionekana kushinda kwa zaidi ya kura milioni mbili wakati TUme bado haijapata matokeo yote... AP, BBC na wengine waliyaweka yale matokeo hadharani mapema tu kiasi kwamba NEC ilitakiwa itafute namna nyingine ya kuchezea kura na kwa vile macho ya kimataifa yalikuwa huko haikuwezekana. Na kilichosaidia sana ni kuwa Jonathan hakutaka sana kung'ang'ania kama marais wengine wa Afrika... hata jaribu la kutumia dola lilipokuja alilizima mapema tu kwa kukubali kushindwa (conceding defeat).

Sisi ukiondoa hayo mengine kuna uwezekano mkubwa sana wa kura zote kutokupigwa Oktoba 25. Tumeletewa hili dudu linaitwa BVR ambalo linasound kama DVD fulani hivi. Hadi leo hakuna mtu anayeweza kutuambia siku ya Uchaguzi BVR itatumika vipi. Inaonekana DVR inatumika sasa hivi tu kuhakiki majina ya walioandikishwa ila siku ya Uchaguzi sioni namna gani kila kituo nchi nzima kitaweza kutumia DVD hii kabla umeme haujaisha. Matokeo yake dalili ya kuahirishwa Uchaguzi (kama ilivyotokea Nigeria) ni mkubwa tu.

Nguruvi hapa chini kasema kitu ambacho wengine labda hawajakifikiria; CCM inahitaji asilimia 50.01 tu kushinda. Jamani imeshinda hivyo Zanzibar mara zote hizi wala haitokuwa kazi kushinda Bara. Upo uwezekano wa CDM kushinda lakini si kwa jinsi ambavyo wamefanya hadi hivi sasa. CDM wana underestimate CCM sana kwa sababu wanaamini wanapendwaaaa saaaana. Ingekuwa kweli Serikali za Mitaa mwaka jana zaidi ya asilimia 50 zingeenda upinzani. Hazikwenda.
 
Asante sana wanaduru wa michango yenu iliyoshiba.

Nianze kupingana na Mzee Mwanakijiji katika swala zima la utangazaji wa matokeo ya kura za urais.

Nafikiri ndugu yangu Mwanakijiji kama kumbukumbu zangu ziko sawa mwaka 2010 siku chache kabla la uchaguzi uliwahi kuja na "andishi lako moja" la kuondoa watu wasiwasi katika swala zima la wananchi kuibiwa kura zao/kutanganza matokeo ya uongo. Na katika andishi lile uliandika kama ulivyoandika leo kuwa "Matokeo ya kura za urais, ubunge na udiwani yatatangawa/kubandikwa katika kila kituo cha kupigia kura (yaani baada ya zoezi la kuhesabu kura kumalizika katika kituo hicho).

Lakini sote ni mashaidi, mwaka 2010 baada ya CCM/NEC kuona kuwa kila kituo Dr. Slaa alikuwa anaongoza kwa kura basi ilitolewa amri kuwa matokeo ya urais YASITANGAZWE PALE VITUONI BALI YATUMWE MOJA KWA MOJA DAR (Nec katika majumuisho ya pamoja) na kilichotokea baada ya hapo kila mtu humu ndani anakifahamu na mpaka leo pale NEC hakuna idadi halisi ya watanzania waliopiga kura za urais.

Hivyo basi ninapata wasiwasi kuwa kama waliweza kutumia hii mbinu "kuchakachua" (nasema hivyo maana kulikuwa hakuna uwazi ktk kura za urais) je watashindwa nini kutumia mbinu ile ile katika uchanguzi wa mwaka huu?

Na msingi huo ninaunga na Nyani Ngabu kuhusu kupata haki kwa tume iliyoundwa na Mweyekiti wa CCM.
Pia ninasikitika kwa wa viongozi wa upinzani kutolivalia njunga swala zima la tume ya uchanguzi kuhakikisha kuwa wanapata tume iliyobora na inayokubalika kwa vyama vyote.

Kuhusu Ukawa: pamoja na mapungufu ya hapa na pale aliyojitokeza katika mambo ya Ukawa hasa kuhusu wagombea wa ubunge na udwani lakini mpaka sasa niwapongeze wanachama wa vyama vyote vinne na viongozi wao kwa kuweza kupata mhafaka wa kusimamisha mbunge mmoja kwa kila chama.

Lakini ninashidwa kuelewa wale wote wanaobeza hiki kitu hali miaka yote nimekuwa nikisia malalamishi mengi, ushauri mwingi kuhusu umuhimu wa vyama vya siasa kuugana na kusimamisha mgombe moja kwa kila jimbo kwa nia ya kudondosha CCM. Tunaposema kuwa Chadema kiungane na vyama vingine na kusimamisha mtu moja na hapo hapo tunasema Chadema wamesimamsisha wagombea wachache hivi maana ya kuungana na vyama vingine ni nini? Yaani tunategemea kuwa Chadema kiugane na CUF, Nccr, Nld na hapo hapo Chadema kisimamishe wagombe kwa majimbo yote?kama ni hivi nini maana ya kuungana?
 
Last edited by a moderator:
Right on! unajua ukweli ni kuwa hata Urais wakitaka kushinda wanaweza. Nigeria Tume ya Uchaguzi ilijaribu kudhibiti matokeo ya kura za Urais lakini walishindwa. Walishindwa kwa sababu upinzani wakisaidiwa na vyombo huru vya habari waliweza kukusanya na kutangaza matokeo toka kila State kabla hayajafikishwa rasmi NEC yao. Matokeo yake ni kuwa Buhari alionekana kushinda kwa zaidi ya kura milioni mbili wakati TUme bado haijapata matokeo yote... AP, BBC na wengine waliyaweka yale matokeo hadharani mapema tu kiasi kwamba NEC ilitakiwa itafute namna nyingine ya kuchezea kura na kwa vile macho ya kimataifa yalikuwa huko haikuwezekana. Na kilichosaidia sana ni kuwa Jonathan hakutaka sana kung'ang'ania kama marais wengine wa Afrika... hata jaribu la kutumia dola lilipokuja alilizima mapema tu kwa kukubali kushindwa (conceding defeat).
Mkuu hapa napo kuna jambo. Unakumbuka CCM walipoona wananchi wanazidi kuichukia( sio lazima waliwapenda wapinzani) ikaleta miswada mitatu kwa hati ya dharura

1 Kwamba, ni tume ya uchaguzi peke yake yenye mamlaka yakutangaza matokeo.
Hawakusema kitaifa au katika jimbo, walichosema ni tumepekee.

2. Mswada wa takwimu, kwamba NBS ndiyo pekee inayoweza kutoa takwimu

3 Vyombo vya habari, na hapa walilenga TBC ili vyombo vingine vijiunge na TBC wakati tume inatangaza kutokana na takwimu za NBS kupitia TBC katika prime time. Mswada uligoma, of course CCM hawakupendele

Katika mazingira yetu, sijui kama mbinu za Nigeria zinaweza kufanya kazi.

Nachelea watu watafungwa hovyo na katika kamata kamata tume 'itafanya mambo' yake

Sijui hili una maoni gani nalo
 
Nguruvi hapa chini kasema kitu ambacho wengine labda hawajakifikiria; CCM inahitaji asilimia 50.01 tu kushinda. Jamani imeshinda hivyo Zanzibar mara zote hizi wala haitokuwa kazi kushinda Bara. Upo uwezekano wa CDM kushinda lakini si kwa jinsi ambavyo wamefanya hadi hivi sasa. CDM wana underestimate CCM sana kwa sababu wanaamini wanapendwaaaa saaaana. Ingekuwa kweli Serikali za Mitaa mwaka jana zaidi ya asilimia 50 zingeenda upinzani. Hazikwenda.

Hivi tumejiuliza kwanini vyama vya upinzani havikushinda kwa hiyo asilimia 50? Je uchanguzi ulikuwa wa uhuru na haki? je mpaka sasa kuna mitaa/vitongoji vingapi ambavyo mahakama ilitengua matokeo yake? Je tumejiuliza yale mapingamizi yalikuwa ni ya harali hivi mtu hasichangue kiongozi eti kwa vile kiongozi fulani ameandika CDM badala ya Chadema? Kweli watu tunawanyima haki yao ya msingi ya kuchagua viogozi wao kwa ajili ya kosa kama hili?

Hatuwezi kutegemea asilimia 50 kwa wapinzani kama kuna upendeleo wa wazi na kiasi hiki. Sikatai upinzani kushindwa lakini washindwe kwa hak.
 
Nitasema kweli daima, fitina kwangu ni mwiko!

Silisemi hili kama nimekula yamini ya CCM, bali ni kwa kutazama kwa kina jinsi gani tumefika hapa (hasa Chadema kuendelea kuwa mguu pande) na hata utata na hofu ya mizengwe ya kura kufanyika.

1. Kosa kubwa tulilofanya tangu 2005-2015, ni kuendelea kuamini kuwa Chadema ni chama kikubwa sana cha siasa kukabiliana na CCM.

2. Kosa la kwanza lilizaa kosa la pili la Chadema kutaka kuwa chama mbadala na pekee chenye haiba na uwezo wa kuwa chama tawala na hata kuwa kigumu kujenga ustawi mapema ambao leo hii tunauita Ukawa

3. Makosa hayo mawili ya kwanza, yalitokana na imani kuwa agenda ya Ufisadi pekee, ndio njia pekee ya kuleta mabadiliko Tanzania. Kasoro hii ilitokana na kujiamini sana kuwa Watanzania na unyonge wanaichukia rushwa na Chadema iliwekeza sana kutangaza Mafisadi na si kuelimisha umma madhara ya ufisadi, kuwasilisha miswaada au kutunga sheria Bungeni za kuleta maadili na kulikabili suala la rushwa na ufisadi (hapa hata wangeweza fanya kazi na Warioba na ripoti yake).

4. Kutokana na kujiegemeza sana na vita vya ufisadi (utajiri- nitalifafanua kadri ninavyoendela na hija yangu) mvuto huu wa kupiga vita Ufisadi (Utajiri) unatokana na msukumo wa kijamaa na wafuasi wa Chadema hasa kundi la Dr. Slaa ambao kudhulumiwa kwao ndani ya CCM, walijiondoa na kuja na ajenda ya Ufisadi kama njia ya kuwa ile sehemu ya kauli ya Mwalimu kuwa Upinzani makini utatoka ndani ya CCM. Hapa, kama tunavyomhoji Lowassa kuja na agenda yake, Wajamaa wa CCM wa Azimio la Arusha waliodiriki kuondoka CCM kutokana na kukatwa (Dr. Slaa na wafuasi), waliamini watakuwa ni watetezi wa wanyonge kupitia misingi ya Azimio la Arusha (miiko ya viongozi kuhodhi mali na kujihusisha na biashara wakiwa watumishi wa umma) kulipiga vita Azimio la Zanzibar ambalo ndilo lililozaa Ufisadi (hapa sizungumzi rushwa, bali ni utajiri na upatikanaji wa utajiri wa kupita kiasi kwa viongozi wa kiserikali na kichama-CCM: Lowassa na Voda, Mkapa na Kiwira, ambazo zilionekana kama conflict of interest na not necessarily wizi{ hata Richmond matokeo yake ni hasara ya uzembe na si wizi}, walichokosea na kukisahau kina Dr. Slaa na hata Zitto (including Mzee Mwanakijiji na Rev. Kishoka na wenginewe) ni kuwa Chadema ni chama cha Kibepari na si Kijamaa na hivyo mgongano wa kifalsafa, kiitikadi na hata mtazamo.

5. Mazao ya kipengele cha tano, ni ushirika na mshikamano wa kubahatisha uliofanywa ndani ya Chadema wakitafuta kupata dhamana ya kuongoza Taifa, kutegemea hoja ya Utakaso (vita vya ufisadi) kuwa ndio kitu cha msingi na sera na agenda kubwa masikioni mwa Watanzania na itasaidia kura (mchemko huu ulipotokea 1995 na Mtikila na Mrema, au hata wakati wa Sokoine na ulanguzi, ulikuwa ni nguvu ya soda) badala ya kujenga chama imara na hata kuwa na ushirikiano wa makini na wapinzani wenzao kabla ya BLK

6. Chadema kimepata mtu tajiri, mwenye mtazamo wa kibwanyenye, anajua kufanya kazi lakini anaupenda utajiri ingawa alikuwa CCM- Lowassa. Kitendo cha CCM kupitisha Azimio la Zanzibar, kilimpa Lowassa uhuru wa kujipatia mali (na inawezekana kwa kiasi kikubwa mali zake ni halali na kuwazidi ujanja na mbinu wenzake na ndio chanzo cha uhasama-speculation, kama si uhujumu ambao umebakia kuwa ni hadithi za kusadikika). Lowassa na hata Sumaye na utitiri wa Mabwanyenye wenye uthubutu kuondoka CCM ama kwa hiari au kwa "kudhulumiwa haki" ndani ya CCM na kukatwa, wamepata nyumba inayofanana nao: Chadema chama ambacho ni wazi kina falsafa ya kibepari na si kijamaa.

7. Kujimini sana kwa Chadema kutokana na Agenda ya Ufisadi na muonekano wa mapokeo ya wananchi wanaouchukia ufisadi kama washabiki halali wa Chadema, ulikifanya chama kujivisha joho la Upambanaji, na kupumbaa kujijenga kiitikadi (itikadi ya kibepari/kibwanyenye; somehow wimbi la chama kuwa na sura ya Uchagga, kinaashiria walioelewa somo kuwa Chadema ni mabepari ni Wachagga pekee). Kupumbaa huku kulifanya chama kidumae baada ya matokeo ya 2010 ambayo kulikuwa na dhuluma za wazi, lakini pia kulikuwa na uzembe wa hali ya juu kutokana na kukosekana na mfumo na uongozi thabiti kusimamia uchaguzi (angalia timu ya kusimamia uchaguzi wa CCM, walio wagombea ubunge watashinda kirahisi sana hawahitaji kampeni, lakini pia kuna watu makini kisiasa na utendaji kushikilia usukani na hata CCM kushinda kwa uhalali kabisa bila goli la mkono maana naamini inferiority complex seed kwa ukawa imeshapandwa kwa hii tamthilia ya goli la mkono au matumizi ya DOLA na NEC kubadilisha matokeo) na hivyo Kikwete kuweza kushidna Urais, CCM kuamua kubadilisha mfumo wa kutangaza matokeo na walichofanya Chadema pekee yao ni kukimbilia Ikulu kutaka katiba mpya badala ya kujipima kiuwezo na ustawi. Kumbuka Chadema iliwekeza sana uchaguzi mkuu 2005 na 2010 na kupuuzia Tamisemi 2004 na 2009 ambako huko wangeweza kuwa na grassroots leadership ambayo ingeweza kutumia sera na itikadi za Chadema kuleta maendeleo ya kuonyesha mfano na umakini wa Chadema huku CCM bado ikiwa chama Tawala.

8. Migongano ya kiitikadi, kutokuaminiana na upotofu ulisababisha Chadema kupoteza takriban miaka miwili na nusu wakiwa na mzozo wa kiuongozi uliofikia hatua ya hazina za chama (Zitto, Kitila Mkumbo na wengine) kufukuzwa chama na hata kukihama chama (ACT ina wagombea zaidi ya 100 na hakina zaidi ya miezi 7 tangu kiundwe, Zitto na KItila wamewezaje kujiimarisha haraka haraka na hata kuwa na itikadi inayoeleweka ya Azimio la Tabora? NYani Ngabu nisaidie hapa!). Chadema kimefarakana, na kimeshindwa kuendelea kujijenga kama chama. Aidha, kutokana na kumomonyoka kwa agenda ya Ufisadi, tangu 2011-2015, pamoja na Operesheni Sangara na M4C ambavyo vilisaidia uhamasishaji wa kujiandikisha kupiga kura na kutafuta kura, bado Chadema ilishindwa kujijenga Kichama kuwa na Semretarieti yenye nguvu, na mfumo wa kiuongozi kusimamia matawi na wanachama wake kwa ufanisi na ufasaha.

9. Fursa ya bunge la Katiba iliyozaa Ukawa, ilishindwa kuchangamka mapema kujijenga na kufanya mamuzi ya kujenga ilani moja, kuwa na fungamano linanoeleweka kwa wanachama wake ngazi zote na kuleta ushirikiano wa kweli ndani ya Ukawa. Hili linatokana na ama Chadema kuendelea kujiona kuwa chenyewe kuwa ni kambi kuu ya Upinzani, hivyo wanahitaji Lion's share ya kila kitu au kilichotokea leo hii kwa Lowassa kuhamia kilikuwa kimeanza kufanyiwa kazi kisirisiri (lakini, Chadema hata mgombea mwenza ni wa kuazimwa? hakuna uimara Zanzibar kuwa na mtu mwenye mvuto kama Duni, Jussa au Mzee Moyo?)

10. Ukawa kuacha kushinikiza mabadiliko madogo madogo ya kanuni, mfumo na sheria kabla ya kutaka kubadilisha kila kitu kupitia Katiba. Hili ni wazi, Ukawa walishindwa kubaini kuwa mwisho wa siku, CCM hukaa mstari mmoja wanaoopona maslahi ya CCM yanatishiwa. Ukawa wangeweza kuwasilisha muswaada na Sheria ya kutaka teuzi za kidola na mamlaka za Raisi zipitishwe na Bunge (mkuu wa Polisi, Takukuru, Mwenyekiti wa NEC, Msajili wa VYama), kuleta marekebisho madogo na ya kiasi ya utendaji wa Tume ya uchaguzi, ili kuanza kuifanya huru na hata suala la vitambulisho vya Taifa na BVR, viliachwa kushinikizwa baada ya November 2010, badala yake yalipuuzwa puuzwa mpaka kushtukizwa baada ya Tamisemi 2014.

11. Ukijumuisha hayo yote, na ukizingatia kuwa CUF wana sehemu ndogo sana ya kupigania tofauti na Chadema, NCCR, NLD, Ukawa wanajikuta wanategemea kubahatisha (EL/Duni/"makapi") wanaokatwa CCM kuja kuongeza nguvu na kutegemea ushindi.

Hivyo basi, kwa kuwa kila kitu ni short term na hakuna deep thought strategy tangu awali, bahati ya mtende kwa Ukawa inaweza isiwe wanayoitegemea na hata utegemezi wa CCM kupasuka yenyewe ili wao UKawa (Chadema) wanufaike, itakuwa ni ualinacha.

Bado tuna miezi miwili kabla ya uchaguzi, umakini ukiwepo unaoandamana na uwazi, basi UPinzani (Ukawa, ACT na wengine) wanaweza kupata nusu ya Bunge na kulazimisha Serikali ya Mseto na hata Lowassa ambaye amekuwa muwazi kuwa la Urais aachiwe yeye, anaweza kushinda.

Lakini hii ni kamari tatu, hujui winning number iko kwenye kikombe kipi? funua unachoamini ubahatishe!
 
Asante sana wanaduru wa michango yenu iliyoshiba.

Nianze kupingana na Mzee Mwanakijiji katika swala zima la utangazaji wa matokeo ya kura za urais.

Nafikiri ndugu yangu Mwanakijiji kama kumbukumbu zangu ziko sawa mwaka 2010 siku chache kabla la uchaguzi uliwahi kuja na "andishi lako moja" la kuondoa watu wasiwasi katika swala zima la wananchi kuibiwa kura zao/kutanganza matokeo ya uongo. Na katika andishi lile uliandika kama ulivyoandika leo kuwa "Matokeo ya kura za urais, ubunge na udiwani yatatangawa/kubandikwa katika kila kituo cha kupigia kura (yaani baada ya zoezi la kuhesabu kura kumalizika katika kituo hicho).

Lakini sote ni mashaidi, mwaka 2010 baada ya CCM/NEC kuona kuwa kila kituo Dr. Slaa alikuwa anaongoza kwa kura basi ilitolewa amri kuwa matokeo ya urais YASITANGAZWE PALE VITUONI BALI YATUMWE MOJA KWA MOJA DAR (Nec katika majumuisho ya pamoja) na kilichotokea baada ya hapo kila mtu humu ndani anakifahamu na mpaka leo pale NEC hakuna idadi halisi ya watanzania waliopiga kura za urais.

Nitakusahihisha jambo moja na ambalo labda halikueleweka. Katika andiko langu lile nilieleza jinsi gani ilivyo ngumu kuchakachua kura za Ubunge. Nilieleza na sheria haijabadilika kuwa kura za Ubunge zinahesabiwa na kutangazwa kituoni; hata kura za Urais ni hivyo hivyo na ndivyo ilivyotokea mwaka 2010. Kitu ambacho kilitokea ni kuwa agizo/amri haikutolewa kuzuia kutangazwa matokeo ya kura za Urais hadi yapelekwe NEC. Amri iliyotolewa ni kwa vyombo vya habari kutokutangaza matokeo ya Urais hadi yatakapotangazwa "rasmi" na NEC. Kwa maneno mengine, matokeo ya Urais yalitangazwa majimboni kama sheria inavyotaka - wasingeweza kutuma bila kuyatangaza ila vyombo vya habari havikuweza kutangaza hadharani kabla ya NEC. Hivyo, maripota wa TV au radio kina Ufoo Saro, George Marato na wenzao walipopewa nafasi ya kutangaza matokeo walikuwa na matokeo ya Urais mkononi lakini mabosi wao wa ITV waliwaambia wasiwaambie yale ya Urais bali yale ya Ubunge kwanza.

Kwanini? kwa sababu matokeo ya awali ya Urais yaliyokuja kutoka sehemu ambayo tayari yalikuwa yametangazwa na yale ya Ubunge yalionesha Dr. Slaa alikuwa anaongoza. Ilibidi wazuie hadi mikoa ya Lindi, Mtwara, Tabora na Tanga ilipoanza kuleta kura zake ndiyo Tume ilipokuwa inatangaza kura za Urais ikaanza na mikoa ile ya ngome ya CCM. Hawakuanza na kura ambazo tayari wengine walikuwa nazo za mikoa ambayo wapinzani (CDM) walikuwa tayari wamepata kama Arusha, Musoma Mjini, Mbeya mjini n.k.

Ukilielewa hili utaelewa kwanini walijitahidi sana kupitisha sheria ya Cybercrime na kudhibiti takwimu. Kama siyo rasmi siyo sahihi hata kama ni sahihi.
 
[/COLOR]

Hivi tumejiuliza kwanini vyama vya upinzani havikushinda kwa hiyo asilimia 50? Je uchanguzi ulikuwa wa uhuru na haki? je mpaka sasa kuna mitaa/vitongoji vingapi ambavyo mahakama ilitengua matokeo yake? Je tumejiuliza yale mapingamizi yalikuwa ni ya harali hivi mtu hasichangue kiongozi eti kwa vile kiongozi fulani ameandika CDM badala ya Chadema? Kweli watu tunawanyima haki yao ya msingi ya kuchagua viogozi wao kwa ajili ya kosa kama hili?

Hatuwezi kutegemea asilimia 50 kwa wapinzani kama kuna upendeleo wa wazi na kiasi hiki. Sikatai upinzani kushindwa lakini washindwe kwa hak.

Lakini mbona walishinda vile vile na sehemu nyingi tu. Hata 2010 Ukerewe, Mbozi, n.k na kwingine walishindwa kwa utaratibu ule ule. Haya matatizo mengine ukianglaia wala yasingebadili sana matokeo. Kwa mfano, leo unaambiwa kuna mbunge wa CCM kapita bila kuchaguliwa utalaumu CCM? Mbona hatupati wabunge wa upinzani wakipita bila kuchaguliwa? Asilimia ya kura za Urais siyo ngumu sana kufikiwa na CCM; ni ngumu zaidi kufikiwa na upinzani. Zinaweza kufikiwa hata hivyo, ila siyo rahisi kama watu wanavyoamini kwa kuangalia picha tu au hamasa. Tofauti ya upinzani kushinda inaweza kutokea kwa kura za DAR tu. Bila Dar Lowassa haendi popote.
 
Lakini ninashidwa kuelewa wale wote wanaobeza hiki kitu hali miaka yote nimekuwa nikisia malalamishi mengi, ushauri mwingi kuhusu umuhimu wa vyama vya siasa kuugana na kusimamisha mgombe moja kwa kila jimbo kwa nia ya kudondosha CCM. Tunaposema kuwa Chadema kiungane na vyama vingine na kusimamisha mtu moja na hapo hapo tunasema Chadema wamesimamsisha wagombea wachache hivi maana ya kuungana na vyama vingine ni nini? Yaani tunategemea kuwa Chadema kiugane na CUF, Nccr, Nld na hapo hapo Chadema kisimamishe wagombe kwa majimbo yote?kama ni hivi nini maana ya kuungana?

Hili la mwisho naomba nilijibu peke yake. Sijui kwanini unafikiria UKAWA ni Muungano. UKAWA siyo muungano wa vyama vya upinzani nchini, siyo umoja wa vyama vya upinzani nchini. UKAWA kwa kweli kabisa - na hili nimelisema mara nyingi huko nyuma - ni kitu kilichoharibu mikakati ya CDM kuliko watu wanavyoweza kufikiria. Ni ushirikiano mwepesi (loose cooperation) wa viongozi wa vyama vya siasa. Ni ushirikiano tu ambao haukuwa na lengo la kuongoza nchi au kutawala; uliundwa kama Pressure group ya kushinikiza mswada wa Katiba ya Warioba. Thats all. Jinsi gani watu wameamini ni muungano hadi leo sijaelewa.

Labda ni kuuliza swali: kwanini unaamini ni Muungano wa vyama vya upinzani Tanzania?
 
Hahahaaa hapo umefanya makusudi au ulikuwa unawaza cha kuangalia kwenye DVR yako [ya Comcast, maybe]?

Aisee niliachana na haya madude siku nyingi kweli; miye natumia over the air tu. Ila Tanzania kwa vifupisho vyake hadi unaweza kutunga wimbo,, BVR and BRN, MKUKUTA NA MKURUBITA, MMEM NA MMEP sijui na madudu gani mengine.. ndio maana BVR wangeita DVD tu ingenoga.
 
Back
Top Bottom