Ombi kwa ndugu yangu
Nguruvi3kama utaweza tunaomba uchambuzi wa wagombea urais hasa Lowassa na Magufuli maana kati yao mmoja wapo ndiye rais..
Ningependa kuwafahamu kwa undani zaidi wa hawa wagombea katika mambo ya maamuzi magumu lakini ambayo si hasara kwa Taifa, maono yao katika kumsaidia mtanzania wa hali ya chini, utendaji wao, mapenzi yao kwa mama yetu Tanzania, Ilani zao, je zinatekelezeka? na mwisho katika maono yao wanataka kuona Tanzania ya aina gani katika miaka 5 ijayo..
Na nafikri kama itawezekana basi tunaomba
Invisible apeleke ombi wa hawa wagombea kwa ajili ya mahojiano humu JF inaweza kuwa kama ilivyokuwa kwa Mh. Kagesheki (video) au maandishi kama iliyokuwa kwa Mh. Zitto..