CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Lakini, si Dk Slaa alikuwa CCM. Yeye liwezajekubadilika

Wengi tu walikuwa CCM wamebadilika

Usisahau mwananchi aliyeipigia CCM kura miaka 50 anaweza kupigia upinzani. Je, hajabadilika!

Kwa hoja yako hii, watakaobadilisha Tanzania lazim awatoke nchi jirani kama si mbinuni

Senti sumuni tu
Nguruvi3, hivi hapa mtu anahukumiwa kwavile tu alikuwa CCM anahukumiwa kutokana na matendo yake alipokuwa CCM? Katika hili, utampa Dr. Slaa ujiko wa chee coz', kwa huo muktadha, Dr. Slaa na EL ni sawa na mbingu na ardhi! Nchi hii, kwa rika la akina Slaa; CCM ilikuwa ni kama Yanga na Simba! Na kama tatizo ni kuwa CCM basi kansa ya CCM kwa EL imeenea kila mahali compared na huyo Slaa!
 
Mwalimu,

Lowasa alishutumiwa kwa hard evidence, zikiwemo barua and memo zinazoonesha involvement yake kwenye Richmond. CDM ilitangaza jina lake kuwa ni fisadi ikidai ina hard evidence za ushiriki wake. Kusema alijielezea kwenye kamati kuu bila kutoa specifics sio fair kwa kweli. Hii habari eti somebody told him, that some on top said he should proceed, does not make any sense.

Tuseme tu kuwa, hata CCM wako mafisadi and that should not be an agenda kwa Lowasa ila tusidanganye kuwa Lowasa alitoa maelezo. Kama kungekuwa kuna maelezo ya maana tusingekuwa tunazungumzia Richmond leo. Tukianza kukubali haya mambo ya eti alijieleza kwenye kamati kuu, kwani aliowafanyia ufisadi ni kamati kuu. Slippery Slope.

Mimi ndio nasema sitaki kuweka mayai yangu kwenye kapu moja, tutarudi kule kwa CCM, maswali yanapewa majibu marahisi halafu tunakubali. Kama upande mmoja utapewa serikali, it is in the best interest ya Tanzania upande huo usipewe na bunge. Tutaepusha haya mambo ya alijieleza kwenye kamati kuu ya chama wakati tunazungumzia nation interest.
^1

Hivi Tanzania ufisadi umefanyika katika swala la Richmond tu?

Halafu kitu ambacho sijapata ufafanuzi wa kutosha ni Richmond (ufisadi wa Lowassa) ilizaa Dowans na Dowans ni mkataba wa kifisadi lakini mpaka sasa serikali inaendelea kulipa Dowans pamoja na kujua kuwa Dowans imetokana na Richmond ambayo ni ufasadi wa Lowassa.. Sasa swali ambalo hata wewe nafikiri utakuwa nalo kichwani Je kwanini serikali iendelee kulipa Dowans hali wanafahamu ni mkataba wa kifisadi na ulitoka kwa fisadi Lowassa? Hiki kigugumizi cha nini?

Swali la pili hivi Tanzania tatizo la ufisadi ni Richmond tu? Kama kuna matatizo mengine ambayo ni makubwa zaidi ya Richmond tena ambayo hata Magufuli anahusishwa, ni kwanini haya hayaongelewi linaloongelewa ni Richmond tu?
Je hatufahamu kuwa katika wizara ya Ujenzi bil.265 zimetoweka bila maelezo yeyote?

Na je tunamaelezo gani kuhusu nyumba za serikali pamoja na kuuzwa kwa bei ya kutupwa lakini nyingine ziligawiwa kwa nyumba ndogo?

Tunapojadili ufisadi wa Lowassa ambaye ni mgombea rais kupita Ukawa, basi tujadili hata ufisadi wa Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM.. hama sivyo tutakuwa tunapendelea upande mmoja na upande wa pili kuufanya kuwa mtakatifu wakati sivyo..
 
Kwani tunafahamu maswali aliyoulizwa mbele ya kamati kuu ni yepi? Au ulitaraji Lowasa ajieleze kwa njia ipi na wapi ili kuweka mambo sawa na kuondoa mashaka? Kama ni kuwa fair let us be fair on both sides. Hatuwezi kusema kwamba haturidhiki na majibu yake kule kamati kuu wakati hatuna uhakika wa kilichotokea huko ndani, au maswali yepi yaliuliza na yalijibiwa vipi. Ukweli unabaki kwamba alijieleza na maelezo yake yalikubaliwa na wajumbe wa kikao kile...
 
JokaKuu,

MABADILIKO TOWARDS TANGANYIKA! Hapa EL ameshafahamu kwamba Watanzania ni rahisi kuwateka akili! Narudia, EL hana ubavu wa ku-engineer mabadiliko ya katiba itakayojali maslahi mapana ya wananchi na kupunguza nguvu dola! Ili kuwateka zaidi CHADEMA na CUF, sana sana ninachoona anaweza kufanya ni ku-revive tu Rasimu ya Katiba Ya Jaji Warioba na kurudisha suala la serikali tatu ambalo sichelei kulisema hata kidogo kwamba ndio pekee ambalo linaimarisha ushirikiano huu wa UKAWA, husani kati ya CHADEMA na CUF... huku CHADEMA wanataka Tanganyika yao, na kule CUF wanataka Zanzibar yao yenye mamlaka kamili!

Je Magufuli ana ubavu wa kubadilisha katiba ya Sitta na kuwa ni katiba yenye maoni ya wananchi? Ukichukua Lowassa ambaye yuko katika chama kingine chama ambacho kimeunda umoja wa kutetea katiba ya wananchi, na Magufuli aliyeko katika chama ambacho kiliamua kwa wingi wao kukandamiza maoni ya wananchi, nani anayeweza kukupata matumaini ya kupata katiba walau yenye kubeba maoni ya wananchi?..

Tukija katika ufisadi, Pamoja na kutulisha propoganda kuhusu Lowassa na ufisadi wake, je kama serikali ilifahamu kuwa Lowassa ni fisadi walishindwa nini kumchukulia hatua? na kama walishindwa basi wafunge midomo wananchi tuamue nani tunamtaka kuwa rais wetu.

Pia nafikiri kwa sasa wananchi hawana shida na ufisadi wanachotaka ni wapate ajira kitu ambacho serikali imeshindwa kutengeneza mazingira ya vijana kujiajiri na kuwajiriwa, watu wapate madawa hospitali serikali imeshindwa, elimu bora mashuleni serikali imeshindwa na wewe leo nikikuuliza kuwa uchumi wa Tanzania unategemea nini (ukitoa madini na gesi) sijuia kama utanijibu. Haya ndio matatizo ya watanzania ambayo wanataka yapatiwe majibu.. Maana wanafahamu kama ufisadi basi si Lowassa peke yake bali viongozi karibia wote wa vyama vya siasa.

Na kuwa kudhibitisha ninachokisema Mwaka 2010 wakati wa ndio Richmond na list of shame ikiwa moto tuliona Lowassa alirudi bungeni na Rais Kikwete alishinda uchaguzi. Pia mwaka huu pamoj na kashfa ya Escrow na watu kukubali kupata mgao, lakini wabunge karibia wote waliohutumiwa na kula rushwa wanagombea ubunge na kuna uwezekano wa kurudi tena bunge na hata kama watashindwa basi watashindwa kwa sababu nyingine lakini si sababu ya Escrow..

Labda swali kujiuliza tunategemea nini kutoka kwa Magufuli na tunategemea nini kutoka kwa Lowassa..
Kwangu mimi sina mategemeo yeyote tofauti na haya kutoka kwa Magufuli maana ni chama kile kile chenye watu wale wale itakuwa maajabu kuleta kitu tofauti.
 
^1

Hivi Tanzania ufisadi umefanyika katika swala la Richmond tu?

Halafu kitu ambacho sijapata ufafanuzi wa kutosha ni Richmond (ufisadi wa Lowassa) ilizaa Dowans na Dowans ni mkataba wa kifisadi lakini mpaka sasa serikali inaendelea kulipa Dowans pamoja na kujua kuwa Dowans imetokana na Richmond ambayo ni ufasadi wa Lowassa.. Sasa swali ambalo hata wewe nafikiri utakuwa nalo kichwani Je kwanini serikali iendelee kulipa Dowans hali wanafahamu ni mkataba wa kifisadi na ulitoka kwa fisadi Lowassa? Hiki kigugumizi cha nini?

Swali la pili hivi Tanzania tatizo la ufisadi ni Richmond tu? Kama kuna matatizo mengine ambayo ni makubwa zaidi ya Richmond tena ambayo hata Magufuli anahusishwa, ni kwanini haya hayaongelewi linaloongelewa ni Richmond tu?
Je hatufahamu kuwa katika wizara ya Ujenzi bil.265 zimetoweka bila maelezo yeyote?

Na je tunamaelezo gani kuhusu nyumba za serikali pamoja na kuuzwa kwa bei ya kutupwa lakini nyingine ziligawiwa kwa nyumba ndogo?

Tunapojadili ufisadi wa Lowassa ambaye ni mgombea rais kupita Ukawa, basi tujadili hata ufisadi wa Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM.. hama sivyo tutakuwa tunapendelea upande mmoja na upande wa pili kuufanya kuwa mtakatifu wakati sivyo..

Alinda,

I think you are missing the point here. Hakuna mjadala wa kusema eti Lowasa ndio fisadi peke kwenye nchi hii, wala hakuna mjadala wa kuwa Dowans, Meremeta, Escrow, EPA, kuuza nyumba za serikali sio ufisadi. Au kuwa upi ulikuwa ufisadi mkubwa zaidi. Sidhani kuwa kuna anaesema hivyo, atleast i know i am not saying that. Ukiwa katika kundi la kunguru halafu ukajitangaza kuwa wewe ni njiwa lazima utegemee watu watakao uhoji huo u'njiwa wako. Sasa ukiianza kujitetea kwa kuwauliza mbona hamuwaulizi wale kunguru wengine kama vile unaonewa unakuwa unatia mashaka kwenye huo u'njiwa wako unaouhubiri.

Leo hii Magufuli akijidai kuibuka na kusema eti zile nyumba alipata amri toka juu, nae pia atakuwa kikaangoni kama alivyo Lowasa. Nasikitika kuwa kwenye mjadala huu unataka kujadili ufisadi wa Magufuli, labda kama sijaelewa huu mjadala unahusu nini au somehow ume evolve into something else completely. Huu mjadala unasema CHADEMA/UKAWA na uwekezaji usiotabirika. Naelewa ni kwa sababu gani issue ya Dr. Slaa imekuwa valid kuongelewa humu kwa sababu yeye ni matokeo ya mwanzo kabisa ya huo uwekezaji unazungumziwa.

Dada angu labda uniambie unataka tu uwasikie wadau wakimkaanga Magufuli na madudu yake, lakini sidhani kama ndio mada hasa inayozungumziwa hapa. Nimeona sehemu umemshauri Nguruvi aanzishe mada ya kuwalinganisha Lowasa na Magufuli kwenye uchaguzi huu, sasa kwenye huo mjadala wadau wakiendelea tu kuongelea Richmond bila kusema hivyo vingne na mimi ntaungana na wewe kukemea huo ubaguzi wa kihoja.
 
Mkuu,

Unachosema ni kweli, humu kinachoendelea ni kampeni na propaganda na sio mjadala huru wa great thinkers.

Hata hivyo sio Alinda tu anayetoka nje ya mada, hata aliyeanzisha mada anataka tumjadili Samwel Sitta. Sasa sijui Samwel Sitta kwenye mada ya uwekezaji wa Chadema/Ukawa anaingiaje.

Nadhani ili kulitendea haki jukwaa la great thinkers ni vema wachangiaji wakafanya declaration of conflict of interest. Mtu kujifanya neutral huku yuko kwenye kampeni ni utovu wa maadili. Ni sawa na Gwajima anajifanya mtabiri ameoteshwa na Mungu kumbe yuko kwenye kampeni. Jukwaa hili tukatae kwenda huko.
 
Kwa mujibu wa Tundu Lisu, Lowasa alijieleza mbele ya kamati kuu kuhusiana na tuhuma zinazomkabili hususan Richmond ambapo alimtaja mhusika mkuu. Ukiondoa Dr Slaa hatujasikia mjumbe mwingine yoyote wa kamati kuu alieonyesha kutoridhika na maelezo ya Lowasa.

Bado swali la msingi linabaki kwa Dr Slaa kwamba pingamizi lake kwa Lowasa linatokana na tuhuma za ufisadi au kutotimiza "masharti" ikiwemo kuingia na wabunge na wenyeviti wa CCM wa mikoa?

Mwalimu;

Desperation isn't a good policy for change. Ukiondoa Richmond, bado jamaa si msafi. Tundu Lissu anafanya kazi ya kuzima moto. Hana jipya.

Dr. Slaa sio pingamizi. Ungekuwa katika nafasi ya Dr. Slaa, ungesema hayohayo. Hivyo kabla ya kumshutuma Dr, jaribu kuwa kwenye viatu vyake.
 
Unaweza kuwa sahihi, lakini unapoona Mbowe na Lissu ni sawa kuwa na urafiki mpya na Lowassa unaweza vipi kuona Slaa kuwa karibu na Mwigulu na Mwakyembe ni tatizo?

..wako wazee ktk taifa hili ambao tarbia na mienendo yao siyo ya mashaka-mashaka.

..hapa nazungumzia watu kama dr.salim salim, mzee sinde joseph warioba, na wengine.

..ingependeza kama dr angejiweka karibu na wazee hao kuliko watu wa ajabu-ajabu kama dr.mwakyembe, mwigulu nchimba, na wengine wa aina hiyo.

..hivi umesahau mwakyembe alivyokuwa anadai al shabaab wanataka kumuua? Au alivyodai amewekewa sumu? Huyu unafikiri anaaminika na kuheshimika?
 
Je Magufuli ana ubavu wa kubadilisha katiba ya Sitta na kuwa ni katiba yenye maoni ya wananchi? Ukichukua Lowassa ambaye yuko katika chama kingine chama ambacho kimeunda umoja wa kutetea katiba ya wananchi, na Magufuli aliyeko katika chama ambacho kiliamua kwa wingi wao kukandamiza maoni ya wananchi, nani anayeweza kukupata matumaini ya kupata katiba walau yenye kubeba maoni ya wananchi?..

Tukija katika ufisadi, Pamoja na kutulisha propoganda kuhusu Lowassa na ufisadi wake, je kama serikali ilifahamu kuwa Lowassa ni fisadi walishindwa nini kumchukulia hatua? na kama walishindwa basi wafunge midomo wananchi tuamue nani tunamtaka kuwa rais wetu.

Pia nafikiri kwa sasa wananchi hawana shida na ufisadi wanachotaka ni wapate ajira kitu ambacho serikali imeshindwa kutengeneza mazingira ya vijana kujiajiri na kuwajiriwa, watu wapate madawa hospitali serikali imeshindwa, elimu bora mashuleni serikali imeshindwa na wewe leo nikikuuliza kuwa uchumi wa Tanzania unategemea nini (ukitoa madini na gesi) sijuia kama utanijibu. Haya ndio matatizo ya watanzania ambayo wanataka yapatiwe majibu.. Maana wanafahamu kama ufisadi basi si Lowassa peke yake bali viongozi karibia wote wa vyama vya siasa.

Na kuwa kudhibitisha ninachokisema Mwaka 2010 wakati wa ndio Richmond na list of shame ikiwa moto tuliona Lowassa alirudi bungeni na Rais Kikwete alishinda uchaguzi. Pia mwaka huu pamoj na kashfa ya Escrow na watu kukubali kupata mgao, lakini wabunge karibia wote waliohutumiwa na kula rushwa wanagombea ubunge na kuna uwezekano wa kurudi tena bunge na hata kama watashindwa basi watashindwa kwa sababu nyingine lakini si sababu ya Escrow..

Labda swali kujiuliza tunategemea nini kutoka kwa Magufuli na tunategemea nini kutoka kwa Lowassa..
Kwangu mimi sina mategemeo yeyote tofauti na haya kutoka kwa Magufuli maana ni chama kile kile chenye watu wale wale itakuwa maajabu kuleta kitu tofauti.
Kwamba ni nani ana ubavu wa kuileta katiba ya wananchi kati ya EL na Magufuri; hakuna hata mmoja kati yao and at least kwa Magufuri, yeye hana sababu ya kufanya hivyo! Hana sababu ya kufanya hivyo si kwamba katiba ya Sitta ni mzuri bali si miongoni mwa agenda ya chama chake wala yeye mwenyewe... na katika hili, hana wa kumfurahisha tofauti na EL!

Kwamba ikiwa EL ni fisadi mbona serikali haikumchukulia hatua ni hoja ya ajabu kwa kweli na ni hoja ambayo hivi sasa imepata mashiko ile mbaya! Kimsingi hoja ya kwamba mbona serikali haikumchukulia hatua ni hoja isiyo na mashiko unless kama unataka kusema nchi haina mafisadi! Ni nani miongoni mwa wengi waliotuhumiwa ufisadi wamechukuliwa hatua? Itoshe tu kusema kwamba hoja ya kwamba mbona hakuchukuliwa hatua wala haiwezi kumfanya mtuhumiwa wa ufisadi kuwa hana hatia unless kama tunataka kusema wale wote wanaotuhumiwa ufisadi nao ni wasafi!!!

Wananchi hawana shida ya ufisadi... anyway, am speechless! Binafsi mara zote nimekuwa nikisimamia jambo moja kwamba jamii yetu ni ya hovyo, imeoza kila mahali! Hata hivyo sikutarajia kama hali ni mbaya kiasi hiki cha kufikia kusema wananchi hawana shida ya ufisadi! Are you serious? Au ili mradi tu tunayemtaka ashinde urais! Lakini kwa upande mwingine unashangaza unaposema wananchi hawana shida ya ufisadi na wanachotaka ni ajira na huduma bora za kijamii!! Hizo ajira na huduma bora za kijamii zitatoka wapi ikiwa no body cares about corruptions?

Kwamba ukiniuliza nitajibu nini kuhusu uchumi wa Tanzania unategemea nini zaidi ya madini na gesi; labda nikuulize wewe hiyo gesi ni gesi ipi unayoisema wewe? Tangu lini Tanzania imeanza kutegemea uchumi wa gesi? Hiyo gesi inauzwa nchi zipi? Na hata hayo madini unayosema wewe mapato yake hayafikii ya mapato kutoka sekta ya utalii

Kwamba, pamoja na kashfa ya Richmond na EPA kuwa hot bado JK na chama chake waliweza kurudi madarakani bado haiwezi kuwa sababu ya kusema kwamba wananchi hawajali issues za ufisadi unless kama unataka kusema pia hawajali issue za umaskinim ukosefu wa huduma bora kijamii, ajira na kadhalika! Kabla ya uchaguzi wa 2010 hayo mambo yalikwepo... je, unataka kuniambia wananchi na hayo hawayajali?

Wakati wewe hutegemei chochote kutoka kwa Magufuri, mimi sitegemei chochote kutoka kwa yeyote kati ya hao mafahari wawili! Na kama umenisoma vizuri tangu mwanzo, ingawaje wengi wenu huwa mnajishitukia sana; mara zote hoja yangu imejikita kwenye suala la EL na kauli mbio ya mabadiliko! Mimi si leo wala si jana; mara zote msimamo wangu haujabadilika kwamba CCM na upinzani wote ni wale wale tu...!! Na sio CCM na upinzani tu, bali sehemu kubwa ya jamii ya Kitanzania ni corrupt community na ndio maana hata wakati wa mchakato wa katiba maoni yangu ilikuwa ni kuachana na what's the so called good governance... ingawaje lengo na misingi ya mfumo wa utawala bora ni mzuri lakini huwezi ku-practice good governance kwenye corrupt community! Na viongozi wetu wamekua wakiupigia chapuo sana huu mfumo coz' unasaidia kuficha uovu wao... ni sawa tu na ulivyosema wewe; kama EL ni fisadi mbona hajafikishwa mahakamani...
 
Kwani tunafahamu maswali aliyoulizwa mbele ya kamati kuu ni yepi? Au ulitaraji Lowasa ajieleze kwa njia ipi na wapi ili kuweka mambo sawa na kuondoa mashaka? Kama ni kuwa fair let us be fair on both sides. Hatuwezi kusema kwamba haturidhiki na majibu yake kule kamati kuu wakati hatuna uhakika wa kilichotokea huko ndani, au maswali yepi yaliuliza na yalijibiwa vipi. Ukweli unabaki kwamba alijieleza na maelezo yake yalikubaliwa na wajumbe wa kikao kile...

Mwalimu,

Nilikuwa sijaona hii reply yako. Sijui kama umenielewa nilivyosema Slippery Slope. Namaanisha haya mambo ya kusema mambo yenye national interest yameongelewa ndani ya kamati kuu wamekubaliana bila kutoa specific details ni mteremko wa kuteleza sana. Hiyo ndio tabia ya CCM inayokataliwa sasa hivi. Wamefanya hivi kwenye mikataba mbali mbali, hawataki kutoa details za content ya mikataba wanaishia tu kusema tumesaini mkataba!

Nikisema majibu hayaridhishi ni kweli kuwa hayaridhishi and that is being fair to both sides kwa sababu hiyo ni FACT. List of Shame haikutangazwa kwenye kamati kuu. Iitangazwa hadharani, kujisafisha toka kwenye list of shame ni lazima kufanyike hadharani. Kama kweli kuna hard evidence Lowasa ametoa to convince kamati kuu kwa nini isiwe wazi tuachane na hizi mambo ya Lowasa na Richmond ibaki CCM na Richmond. Ugumu uko wapi kwani??

Haya mambo yanakuwa repeatative mpaka yanachosha. Point sio kuwa Lowasa anachukiwa sana na wenye maoni kama yangu, HAPANA. Tatizo CCM bado kuna mafisadi wengi sana, hii ya Lowasa bila kuhojiwa inaset a loop hole huko mbeleni watu wezi waachie tu kwa sababu wamejieleza kwenye kamati kuu bila kutoa maelezo ya maana nini hasa kimesemwa huko kamati kuu. Na huko kamati kuu kuna watu sio malaika. Jamani kwa nini hamni lioni hili suala!

Wanasema "The End, justify the Means"! But in politics there are no Ends, there are just Means. Watanzania tuwe makini, we are setting precedence kwenye serikali ijayo on how mafisadi wa EPA, Meremeta, Escrow etc will be dealt with!! Again SLIPPERY SLOPE.
 
Ombi kwa ndugu yangu Nguruvi3kama utaweza tunaomba uchambuzi wa wagombea urais hasa Lowassa na Magufuli maana kati yao mmoja wapo ndiye rais..

Ningependa kuwafahamu kwa undani zaidi wa hawa wagombea katika mambo ya maamuzi magumu lakini ambayo si hasara kwa Taifa, maono yao katika kumsaidia mtanzania wa hali ya chini, utendaji wao, mapenzi yao kwa mama yetu Tanzania, Ilani zao, je zinatekelezeka? na mwisho katika maono yao wanataka kuona Tanzania ya aina gani katika miaka 5 ijayo..

Na nafikri kama itawezekana basi tunaomba Invisible apeleke ombi wa hawa wagombea kwa ajili ya mahojiano humu JF inaweza kuwa kama ilivyokuwa kwa Mh. Kagesheki (video) au maandishi kama iliyokuwa kwa Mh. Zitto..
Alinda hilo la Invisible kuwaalika mtandaoni nadhani wengi wanaliafiki.

Wote wapewe nafasi sawa, atakayekataa hilo litakuwa juu yake

Kuhusu mada inayoongelea issue za kitaifa kwa ujumla, hilo tulishaliona na kulifanyia kazi, tunamaalizia ni suala la muda tu

Ni kweli kuwa sasa ni wakati tujadili hawa watu kwa upana wao kama ulivyodokeza.

Update Sept 12

https://www.jamiiforums.com/great-t...zi-ni-juu-ya-ilani-sera-na-hatma-ya-nchi.html

cc Alinda
 
Last edited by a moderator:
Mwalimu,

Nilikuwa sijaona hii reply yako. Sijui kama umenielewa nilivyosema Slippery Slope. Namaanisha haya mambo ya kusema mambo yenye national interest yameongelewa ndani ya kamati kuu wamekubaliana bila kutoa specific details ni mteremko wa kuteleza sana. Hiyo ndio tabia ya CCM inayokataliwa sasa hivi. Wamefanya hivi kwenye mikataba mbali mbali, hawataki kutoa details za content ya mikataba wanaishia tu kusema tumesaini mkataba!

Nikisema majibu hayaridhishi ni kweli kuwa hayaridhishi and that is being fair to both sides kwa sababu hiyo ni FACT. List of Shame haikutangazwa kwenye kamati kuu. Iitangazwa hadharani, kujisafisha toka kwenye list of shame ni lazima kufanyike hadharani. Kama kweli kuna hard evidence Lowasa ametoa to convince kamati kuu kwa nini isiwe wazi tuachane na hizi mambo ya Lowasa na Richmond ibaki CCM na Richmond. Ugumu uko wapi kwani??

Haya mambo yanakuwa repeatative mpaka yanachosha. Point sio kuwa Lowasa anachukiwa sana na wenye maoni kama yangu, HAPANA. Tatizo CCM bado kuna mafisadi wengi sana, hii ya Lowasa bila kuhojiwa inaset a loop hole huko mbeleni watu wezi waachie tu kwa sababu wamejieleza kwenye kamati kuu bila kutoa maelezo ya maana nini hasa kimesemwa huko kamati kuu. Na huko kamati kuu kuna watu sio malaika. Jamani kwa nini hamni lioni hili suala!

Wanasema "The End, justify the Means"! But in politics there are no Ends, there are just Means. Watanzania tuwe makini, we are setting precedence kwenye serikali ijayo on how mafisadi wa EPA, Meremeta, Escrow etc will be dealt with!! Again SLIPPERY SLOPE.
Nakumbuka tuliwahi kusema ili Lowassa afikiendoto ya matumaini ni lazima asimame kukabaliana na hili la Richmond perfectand square
Nakubaliana nawe kuhusu utamaduni wa kuwekamambo wazi.

Hili ni jambo lenye masilahi mapana. Maelezo ndani ya kamati kuu hayawezikuwafikia wengine wenye mashaka ambao huenda walikuwa tayari kumuunga mkonokama wangeelewa.

Lakini pia lina set bad precedent kama ulivyosema
na linafuata model ya CCM.

Kwa upande mwingine, tutakuwa tunafanya sualahili kama ndilo tatizo pekee la kitaifa.

Kwa mfano, tukimtaka ajieleze sishie hapo tutamtaka Magufuli ataueleze yakehata kama yamezungumzwa katika kamati kuu

Hatutaishia hapo, tutarudi kwa akina Sittawalio ‘obstruct justice' tunayoidai leo Lowassa atueleze.

Hapa ndipo akina zeMarcopolo wasipotaka na wanaita propraganda.

Kwamba tunatakiwa tuzungumzie Lowassa na Richmond tu tufumbe macho madudumengine yaliyoamabatana na hilo. Hapana! Tutaweka wazi na kila mtu kwa nafasiyake bila kuomba radhi

Na mwisho, hapa kuna grey line, taujuiLowassa ana umbali gani anaoweza kwenda kuhusu mambo mengine tukizingatiaalikula ‘oath' Mwenye ujuzi na hili atusaidie

Lakini pia, tunakuwa na upungufu mkubwa sana.Kwanini CCM wadhani Richmond ni tatizo la wapinzani tukijua kuna vidonda vyaEscrow ambavyo baadhi ya wahusika wapo CCM

Ili kutenda haki ni lazima jamvi lifumuliwena kila kitu kionekane.

Tunawezakuongelea uwekezaji usiotabirika tukiwa na kila jambo wazi.

Mimi ndio nasema sitaki kuweka mayai yangu kwenye kapu moja, tutarudi kule kwa CCM, maswali yanapewa majibu marahisi halafu tunakubali. Kama upande mmoja utapewa serikali, it is in the best interest ya Tanzania upande huo usipewe na bunge. Tutaepusha haya mambo ya alijieleza kwenye kamati kuu ya chama wakati tunazungumzia nation interest.

Sidhani kama jambo unaloliongelea linaweza kuwa applicable kwenye siasa zetu hasa siasa za kiafrika na Tanzania kwa ujumla.
Haitakaa itokee kwa Tanzania rais na bunge kuwa na utofauti kulingana na vyama.
Watanzania wanapiga kura kwa mtindo wa "full suti", wanachagua chama hawachagui mtu.
Hivi kwa mfano unataka kuniambia nikienda kwenye kupiga kura nimchague Magufuli kuwa Rais na Mnyika awe Mbunge na diwani atoke Cuf/Chadema/NLD?
Au nimpige Lowasa kuwa Rais, Fenala Mkangara kuwa Mbunge nimuache Mnyika na Diwani awe chama tofauti na hapo juu?
Hata dhamiri yangu itanisuta sana, nadhani nitakuwa nimeisaliti nafsi yangu.
Una hoja nzuri na yenye mantiki nzuri kwa mustakabali wa taifa letu, hata mimi natamani iwe hivyo kuweka serikali inayowajibika ila kwa watanzania tunaoishi nao mtaani sio wa aina hiyo.
Hiyo theory yako inafaa kuwa applied nchi ambazo zimeshaendelea.
Na pia kwenye huo muundo wa serikali naona wazi kuwa serikali itakuwa inaangushwa na bunge mara kwa mara.
 
Labda swali kujiuliza tunategemea nini kutoka kwa Magufuli na tunategemea nini kutoka kwa Lowassa..
Kwangu mimi sina mategemeo yeyote tofauti na haya kutoka kwa Magufuli maana ni chama kile kile chenye watu wale wale itakuwa maajabu kuleta kitu tofauti.

Nadhani hapa ndio umezungumzia hoja muhimu kuliko zote. Ingekuwa vyema wana GT tujikite hapa, tuumize vichwa vyetu kujua ni nini hawa wagombea watatupa kwenye uchaguzi huu.
Wimbo wa ufisadi hautaisha kama tukiamua kuuimba zaidi tutazidi kubadili chorus na kuongeza mashairi.
Je, Magufuli atatuletea nini akiwa ndani ya CCM?
Je, Lowasa atatuletea nini akiwa kwenye mrengo tofauti na aliouzoea?
Je, serikali ya nani kati ya hao wawili itakuwa na na 'impact' kwenye maisha ya kila siku ya wananchi?
Je, kati ya Lowasa na Magufuli nani ataondoa na kufuta ufisadi ulioishika nchi yetu?
Karibuni wana jamvi.
 
Nakumbuka tuliwahi kusema ili Lowassa afikiendoto ya matumaini ni lazima asimame kukabaliana na hili la Richmond perfectand square
Nakubaliana nawe kuhusu utamaduni wa kuwekamambo wazi.

Hili ni jambo lenye masilahi mapana. Maelezo ndani ya kamati kuu hayawezikuwafikia wengine wenye mashaka ambao huenda walikuwa tayari kumuunga mkonokama wangeelewa.

Lakini pia lina set bad precedent kama ulivyosema
na linafuata model ya CCM.

Kwa upande mwingine, tutakuwa tunafanya sualahili kama ndilo tatizo pekee la kitaifa.

Kwa mfano, tukimtaka ajieleze sishie hapo tutamtaka Magufuli ataueleze yakehata kama yamezungumzwa katika kamati kuu

Hatutaishia hapo, tutarudi kwa akina Sittawalio ‘obstruct justice’ tunayoidai leo Lowassa atueleze.

Hapa ndipo akina zeMarcopolo wasipotaka na wanaita propraganda.

Kwamba tunatakiwa tuzungumzie Lowassa na Richmond tu tufumbe macho madudumengine yaliyoamabatana na hilo. Hapana! Tutaweka wazi na kila mtu kwa nafasiyake bila kuomba radhi

Na mwisho, hapa kuna grey line, taujuiLowassa ana umbali gani anaoweza kwenda kuhusu mambo mengine tukizingatiaalikula ‘oath’ Mwenye ujuzi na hili atusaidie

Lakini pia, tunakuwa na upungufu mkubwa sana.Kwanini CCM wadhani Richmond ni tatizo la wapinzani tukijua kuna vidonda vyaEscrow ambavyo baadhi ya wahusika wapo CCM

Ili kutenda haki ni lazima jamvi lifumuliwena kila kitu kionekane.

Tunawezakuongelea uwekezaji usiotabirika tukiwa na kila jambo wazi.

Nguruvi,

Kuna suala moja, nadhani mifano yangu ya picha sijui sio mizuri au ni mimi uandishi wangu sio mzuri. Nimetoa mfano wa kunguru kujitangaza kuwa amekuwa njiwa. Ni hivi, madudu ya CCM yanajulikana. Yamekuwa yanasemwa for the last 10 years and counting. Hawa tunawajua ni kunguru through and through. Huyu anayesema sio kunguru amekuwa njiwa anahitaji speacial attention, ndio maana hata wewe mkuu ukaanzisha huu mjadala kwa sababu uliliona hili. Hii hoja ya tukimaliza kwa huyu tuende kusema na yale mengine, kwani ni lini tuliamua kuwa yale mengine yameisha? Ni lini tuliamua Escrow, Meremeta, EPA mjadala wake umefungwa? Issue ni kuwa hiyo mijadala haijapata information mpya za kujadili, kuzungumzia hiyo mijadala ni kurudia yale yale. Leo hii kukiibuka habari mpya kuhusu zile pesa za Escrow zilizotoka Stanbic, unadhani kuna mtu atakuwa anajadili Richmond?

Mnaposema tuwajadili na kina Sitta, Mwakyembe tunajadili nini. Hao ni kunguru, na hawajasema chochote kupinga au kinachopingana na ukunguru wao. Ndio maana mna mpa nafasi ZeMarcopolo kusema kuhusu propaganda. Kwamba Lowasa amesemwa kwenye mjadala basi ili huo mjadala uwe fair basi ni lazima Magufuli au CCM wengine nae asemwe hapo hapo. Kufanya mjadala objectively kuhusu either Magufuli au Lowasa, si lazima uwazungumzie wote kwa pamoja. Unaweza kuwa objective na ukaongea objectively kuhusu mtu yoyote kwa kuangalia hoja za ukweli na zenye mashiko kuhusu huyo mtu. Lazima tuweze kama learned people, tukiamua kuongelea perfomance ya Magufuli katika wizara zote alizopitia, tuweze kuufanya huo mjadala objectively bila kuanza kulinganisha au kuulizana mbona Lowasa alifanya hivi na vile.

Na mwisho kabisa, kama comparison ni makunguru wa CCM sasa who is replacing who? Mtu akizungumzia mabadiliko, sauti kubwa kabisa anayosema ni kuwa mimi bora zaidi. I AM BETTER AND I CAN DO BETTER. Sasa ikitokea umekuwa questioned kidogo baada ya kutokea information mpya unaanza kufanya reference kwa wale unataka kuwa replace unaondoa ule u ' BETTER wako.
 
Sidhani kama jambo unaloliongelea linaweza kuwa applicable kwenye siasa zetu hasa siasa za kiafrika na Tanzania kwa ujumla.
Haitakaa itokee kwa Tanzania rais na bunge kuwa na utofauti kulingana na vyama.
Watanzania wanapiga kura kwa mtindo wa "full suti", wanachagua chama hawachagui mtu.
Hivi kwa mfano unataka kuniambia nikienda kwenye kupiga kura nimchague Magufuli kuwa Rais na Mnyika awe Mbunge na diwani atoke Cuf/Chadema/NLD?
Au nimpige Lowasa kuwa Rais, Fenala Mkangara kuwa Mbunge nimuache Mnyika na Diwani awe chama tofauti na hapo juu?
Hata dhamiri yangu itanisuta sana, nadhani nitakuwa nimeisaliti nafsi yangu.
Una hoja nzuri na yenye mantiki nzuri kwa mustakabali wa taifa letu, hata mimi natamani iwe hivyo kuweka serikali inayowajibika ila kwa watanzania tunaoishi nao mtaani sio wa aina hiyo.
Hiyo theory yako inafaa kuwa applied nchi ambazo zimeshaendelea.
Na pia kwenye huo muundo wa serikali naona wazi kuwa serikali itakuwa inaangushwa na bunge mara kwa mara.

Bavaria,

Ukipata bunge jingine ya "Wanaokubali, waseme Ndio" NDIYOOOOOOOO , ukaja kulalamika hapa. Ntakuja kukumbusha uhai ukiwepo mungu akipenda. It begins with you.
 
Mkuu GalaxyS3

Niombe wanajamvi tuweke baadhi ya hoja katika mstari ulioonyooka.
Hii hoja ya propaganda inapotosha. Inawezekana baadhi ya wachangiaji hawafuatilii majadiliano kutoka nyuma

Wakati tunaongelea ujio wa Lowassa na UKAWA kwa ujumla kila jambo ‘lilionekana' kuwa sawa.
Mabandiko matano yaliyohusu Lowassa na hotuba yake ya babu Seya ‘ilikuwa sawa'.

Mjadala unapopanuka unagusa CCM, hapo ni propaganda!

Uzi unaosema UKAWA nauwekezaji usiotabirika kwa maana ya UKAWA/CDM/ Lowassa wanavyobadilisha hali ya kisiasa kiasi cha kutoweza kutabirika, ukilenga hatma ya UKAWA/CDM kutokana na ujio

Ndipo hoja ya Asset or liability ilipoingia. Haya mawili ni mapana.
Kwa mfano, ujio wa Lowassa umegawa viongozi wa CDM na wanachama kwa mitazamo tofauti.

Kila kundi lina hoja ,wengine wakisema ni vema au vibaya na wapo wenye na shaka

Hivyo basi, uwekezaji usiotabirika ni jambo la jumla na pana tofauti na inavyodhaniwa ni Richmond.
Hiyo ni sehemu ndogo sana ya hoja zinazohusiana na ujio wa Lowassa.

Mag3 katika bandiko lake namba 568 ameuliza maswali 4 bila majibu.
Aliongelea kwa ujumla ujio wa Lowassa, hali ya kisiasa nchini, nyuma na twendako.

Hata kama hatukubaliani, lazima tukubaliane ujenzi wa hoja zake ulizingatia ujio wa Lowassa

Mjadala wa Richmond ulioanzaI mikutano ya nje umeingizwa katika hoja kwamba uwekezaji usiotabirika ni Richmond.

Tunarudia hiyo ni sehemu tu. Walioleta mjadala wamekuja na tuhuma za utajiri , ufisadi n.k.

Ni maoni yao tunayaheshimu sana na wala si facts unless watuwekee facts

Richmond haikuangauka kama kimondo kutoka space. Kusema kuwa uwekezaji usiotabirika uzungumzie Lowassa/Richmond tu ni kuingiza kampeni wanazozituhumu.

Huwezi kuzungumzia Richmond bila kumgusa Mwakyembe tume ya Bunge au Sitta, Spika aliyezuia suala hilo kuongelewa

Kuzungumzia Lowassa /Richmond tu ni kampeni tu kwasababu katika nyakati za uchaguzi hilo linaweza kuwa kampen

Jambo tunalodhani si sahihi katika mijadala kama hii.
Haina maana watu wasijadili kwa maono na maoni yao, hapana!

Maana yake tusichukue upande mmoja wa kampeni kwa njia za upendeleo

Na wala Richmond si sehemu kuu ya mada bali inachomekwa. Kwamba, uzuri wa mada ni kumsema Lowassa tu!

Hiyo si haki na kuikubali ni kutotenda haki. Haonewi wala hahurumiwi mtu ni motto yetu

Kwa mukatadha huo, pengine tujadili uwekezaji usiotabirikakwa upana wake tukitoka nje ya na kubaki withini the topic.

Tuongelee uwekeaji usiotabirika bila limitations, kwa ukweli bila kuficha jambo na kwa dhati yetu

Je, ujio wa Lowassa UKAWA una impact gani positive ornegative kwa Upinzani na taifa kwa ujumla.

Je, umeunganisha wapinzani au umedhoofisha wapinzani?

Nini athari zakekatika siasa za Tanzania? Je,nchi itanusurika na matatizo ya miaka 30 au zaidi?

Haya ndiyo ya kujadili na si Richmond tukimbebesha Lowassa mzigo,tukiwaficha wengine kwasababu si sehemu ya mada.

Hapana, ikibidi kila mmoja atabeba mzigo wake, bila kuonewa au kuhurumiwa

Kuwa, objective ni kuichambua mada kwa mapana yake, si kusingle out Lowassa/Richmond ili tumshindilie tuhuma, eti tukipanua mjadala ni kampeni, kwasababu tu hatutaki tuguse maeneo nyeti.

Hahurumiwi haonewi mtu, ni hoja tu

Tusemezane
 
Sidhani kama jambo unaloliongelea linaweza kuwa applicable kwenye siasa zetu hasa siasa za kiafrika na Tanzania kwa ujumla.
Haitakaa itokee kwa Tanzania rais na bunge kuwa na utofauti kulingana na vyama.
Watanzania wanapiga kura kwa mtindo wa "full suti", wanachagua chama hawachagui mtu.
Hivi kwa mfano unataka kuniambia nikienda kwenye kupiga kura nimchague Magufuli kuwa Rais na Mnyika awe Mbunge na diwani atoke Cuf/Chadema/NLD?
Au nimpige Lowasa kuwa Rais, Fenala Mkangara kuwa Mbunge nimuache Mnyika na Diwani awe chama tofauti na hapo juu?
Hata dhamiri yangu itanisuta sana, nadhani nitakuwa nimeisaliti nafsi yangu.
Una hoja nzuri na yenye mantiki nzuri kwa mustakabali wa taifa letu, hata mimi natamani iwe hivyo kuweka serikali inayowajibika ila kwa watanzania tunaoishi nao mtaani sio wa aina hiyo.
Hiyo theory yako inafaa kuwa applied nchi ambazo zimeshaendelea.
Na pia kwenye huo muundo wa serikali naona wazi kuwa serikali itakuwa inaangushwa na bunge mara kwa mara.
Mkuu Bavaria nadhanimuhimu ni kubadili mind set za watu.

Nakubaliana na GalaxyS3 kuwa lazima watu watambue umuhimu wa viongozi wao pale walipo

Kama unadhani haliwezekani labda ungejiuliza lini katika historia ya nchi hii mawaziri wakuu wawili wameondoka chama tawala? Kwanini unadhani ni impossible na lini unadhani utakuwa mwanzo wa kubadilika kama si leo hii?
 
Hivi ni akina nani wanaunda 'Genge' la Lowassa?...

Kuna yeyote anaweza kunisaidia kuwataja kwa majina?...

Pia si vibaya mkuu wangu ukaanza na hao aliowaacha CCM...
Ni kundi kubwa , wengine wameondoka wenginewamebadili mawazo
Ni ngumu kuelewa kama wapo naye ‘kiroho’ au ipoje
Ndio maana ya kusema ‘uwekezaji usitabirika’’
 
Back
Top Bottom