Wanajamvi
Kwanza nikubaliane kabisa na hoja za
JokaKuu FJM GalaxyS3 kuhusu suala lililoingia la video
Nadhani linatuondoa katika hoja iliyopo mezani. Hii haina maana halijadiliki, hapana, linajadilika sana.
Ni issue kubwa inayohitaji uzi pekee ili kuwe na flow ya majadiliano hapa na huko kwenye uzi mwingine. Nadhani limeeleweka
Pili, kuna hili la asset na Liability
Nikimsoma
Alinda na GalaxyS3 hoja zao zinapaingana kwasababu moja kuu.
Glaxy anasema Richmond ni liability pekee katika ujio wa Lowassa UKAWA.
Alinda anasemam si kweli, kwasababu hiyo si unique liability na kuendelea kuijadili ni kuikuza tukijua kuwa liabilities zipo nyingi na kwa maeneo tofauti.
Hivyo , kujadili inakuwa sehemu ya kampeni, jambo lisilo sahihi.
Nadhani nitakuwa sahihi na nasimama kusahihishwa kama nitakuwa nimeelewa vibaya kwa wote wawili
ASSET NA LIABILITY
Tunapoongela haya mawili lazima tuyaangalie kwa jicho pana.
Kwa mfano, Ujio wa Lowassa umesemwa kama asset kwa UKAWA.
Kisichoeleweka, ni kuwa hii ni asset kwa mtazamo upi? Kwa personality, kwa wafuasi au kwa timu anayokuaja nayo?
Na asset hiyo inatumiwaje katika mazingira yaliyopo.
Kwa mfano, watu wake wana nafasi za ubunge na udiwani? Kama hakuna, wafuasi wa watu wanasimama wapi leoo hii?
Impact ya asset ipo wapi. Haya ni baadhi ya maswali tunayoweza kujiuliza
Lakini pia tunashindwa kuiangalia hii asset kwa namna nyingine. Je, ujio wake umeunganisha UKAWA kama vyama au kama wanachama?
Je, kulikuwa na mkakati wa 'assimilation' kati ya kampeni yake na UKAWA?
Hapa ndipo hoja tunayozungumza na
@Rev.Kishoka inapoingia.
Kwamba unaweza kuwa na asset lakini kama hujui namna ya kuzitumia ni sawa na hakuna.
Tukiangalia TeamLowassa na M4C ambazo ni vijana zote zinakuwa kama paralyzed.
Hakuna strategists walioona hilo na wanaoliona kwasasa
Watu waliopaswa kuunganisha nguvu zote mbili ni viongozi. Inapotokea kiongozi wa umoja wa vijana anayepaswa kuratibu shughuli za vijana anagombea ubunge na kuacha majukumu yake, hapo kuna tatizo.
Hapa hapakuwa na mkakati kutoka viongozi wa CDM/UKAWA kwa ujumla. Tunasikia Katambi anagombea ubunge, nani wa kuratibu shughuli za uhamasishaji huko mitaani? Nani atakuwa mwenyeji wa Team Lowassa/TeamCUF au NCCR i?
Kwa mtazamo huo, ujio unageuka kuwa liability kwasababu haujaweza ku 'harness and utilize' ujio effectively
LIABILITY
Kwamba, si suala la Richmond pekee. Ni suala la kutazama kama uwepo wake umeathiri au umeboresha hali ya upinzani?
Kwa bahati mbaya, inaonekana viongozi na timu za CDM/UKAWA wame back off pengine kwa nia njema inayotoa matokeo hasi.
Kudumaa kwa jitihada za makundi mengine bila sababu za msingi ni sehemu ya liability tunayoongelea
Kukosa 'common ground' ya kuongelea masuala ni sehemu nyingine
Kutokuwa na timu zinazofanya kazi kwa wepesi , umakini na uhodari ni sehemu kubwa ya tatizo
Hivyo, personality inaonekana ku 'override' institution in varies aspect of campaign.
Kwa hili kama hawakuwa makini, wanachosema ni asset inaweza kuwa liability, ni tatizo la timu nzima
Haina maana hawafanyi vema, wanatakiwa kuhakikisha kukabiliana na CCM yenye matawi muhimu ya nchi, chama na vyombo husika
Hivyo, tuangalie asset na liability kwa upana wake kama suala la fikra na si kudhani Richmond ndio itaamua hatima ya uchaguzi
Na mwisho, labda nimuulize swali
GalaxyS3 . Hivi inawezekana kwa Lowassa kusimama na kueleza kila kitu kwa uwazi wake tukijua alikuwa katika cabinet na kuna mambo ya kisheria kama oath n.k. Hapa nisaidiwe naomba ushauri
Tunasema hivi kwasababu, mambo katika closed camera yanaweza kuwa na legal implication tofauti na outdoor
Tusemezane