CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

..mbona Magufuli naye amesema aombewe?

..tangu anachukua fomu Magufuli amekuwa akisema aombewe.

..kwanini hukulalamika wakati huo, unalalamika sasa hivi?
JokaKuu,

Ukweli utatuweka huru. Sikubalini kabisa na nadha ya kutumia 'dini' kama nyenzo ya kupata madaraka. Hilo moja.

Pili, kwa kumbukumbu zangu, hakuna siku hata moja Magufuli amehudhuria Ibada kanisani, akapanda madhahabuni, akachukua kipaza sauti na kuwaaambia waumini wengine kuwa wamuombee kwa sababu yeye ni wa 'dhehebu' lao. Na hakuna mahali Maguful amewachambua marais waliopita kwa dini zao ili kukazia 'sifa yake ya udini'.

Alichofanya Lowassa si kuteleza ni za mwizi 40 zimefika. Nitaeleza kwa kifupi sana.

Lowassa alikuwa kampeni meneja wa Kikwete 2005. Na Mkakati wake wa kutwaa madaraka kupitia kwa wanamtandao' ulijumuisha kwa kiasi kikubwa dhana ya udini. Lowassa alikuwa anazungukia majumba ya ibada kumnadi swahiba wake pamoja na kuchukua pesa (hasa temples za wahindi). Askofu Kilaini 'anasemekana' naye alikuwa mwanamtandao na ndio sababu akaja na ule msemo wake wa chaguo la mungu. Baada ya saga ya Richmond, Lowassa alianza kuunda mtandao upya kwa kutumia baadhi ya makanisa ya 'protestant' chini ya usimamizi za Gwajima.

Anachokifanya Lowassa sasa hivi ni 'activation' ya mtandao wake mpya ambao unafanana na kile alichofanya 2005. Na safari hii amekuja na sababu mahsusi, 'Ulutheri'. Na yeyote atakayejaribu kutia mchanga kitumbua chake atakutwa na kadhia ile ile iliyompata Dr Salim Ahmed Salim- character assassination.
 
Mkuu mnashangaa nyie lakini mimi hainishangazi kabisa. Na najua watu watasema mimi mdini lakini ndio hali halisi (Reality) na ndivyo Edo alivyo. Hakuomba aombewe tu ila kasema ni zamu ya Warutheli na ndio kauli yake!..Wengi wanamsikia tu hawajui ya Nigeria na Ujarumani..

Kama aliweza kurudisha shule na Hospital zilizojengwa na Mkoloni Mjarumani mikononi mwa kanisa lake atashindwa nini? Yeye Mrutheli, Mbowe sijui, Mtei sijui, Wakaskazini wengi sijui...kwa nini anapewa support kubwa hivyo sijui!. Panapofuka moshi kuna moto! Mimi ningependa tu kujua huyu Gwajima Askofu mzima ameingiaje katika uongozi wa Chadema au UKAWA hadi awe mshauri na msemaji wao?

- Unategema nini kitaandaliwa hapo? Nimeandika haya najua yatakuja mashambulizi ya hali ya juu kwa sababu watu hawatazami reality, wanataka kudanganyana na bikra ya ndimu! Udini upo mkuu wangu na hautakwisha kirahisi...

Mbowe, Sumaye wote Walutheri.
 
Twende taratibu ni sek. ya ngapi anasema hayo maneno yaani hapo kwenye nyekundu?
Tangazo la Serikali Na. 294 la tarehe 27/7/2015 chini ya kifungu cha 124A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, ukurasa wa 5 kifungu 2.1(k) kinasema:-

“Viongozi wa vyama vya siasa, wagombea au wafuasi wao wahakikishe kuwa majengo wanayotumia kufanya kampeni sio ya Ibada. Vile vile, vyama vya siasa vihakikishe kuwa havitumii viongozi wa dini kupiga kampeni kwa ajili ya vyama vya siasa au wagombea wao”.

Lakini katika maadili hayo hayo, ukurasa wa 7, kifungu 2.2(i) kinasema:-
“Vyama vya siasa au Wagombea hawaruhusiwi kuomba kupigiwa kura
kwa misingi ya UDINI, UKABILA, JINSIA AU RANGI.”

Ni wazi kampeni za Lowasa zinatakiwa zisitishwe mara moja, kazi ya kiongozi ni kuunganisha watu na sio kuwatenganisha, kesho wakiibuka pentekoste, Sabato, angalikana nao wakisema wanataka rais wao tutafika?
 
Unafikiri mahali muafaka pa kujisafisha dhidi ya tuhuma za ufisadi ni jukwaani na sio kwenye vyombo vya sheria?

Na hii ndio shida tuliyo nayo watanzania. Kashfa ya Richmond imekuwa ni gumzo kwa miaka 8 kwa sababu tumekuwa ni watu wa kupiga makelele tu majukwaani halafu inaishia hapo! Vyombo vya dola (DPP, Polisi, TAKUKURU, etc..) hawajachukua hatua yoyote kwa miaka 8 huku watu wakiendelea kupiga kelele mtaani kuwa na "nyaraka" za ufisadi za Lowasa! Yeye mwenyewe ameshasema mwenye ushahidi dhidi yake aende mahakamani mbona mpaka sasa hakuna aliyekwenda ikiwamo Dr Slaa mwenyewe?

Leo hii naweza kwenda kwenye press nikakutuhumu wewe Galaxy S3 kwamba ni mwizi na nina nyaraka, halafu nakwambia kama unabisha njoo ukanushe ili niibue madudu zaidi (tishia nyau). Vyombo vya dola vinafanya kazi gani?
Na huu ndio utamaduni wa hovyo tuliojijengea kuwa ni watu wa kupiga kelele majukwaani huku wenye wajibu wa kuchunguza na kushitaki wakiwa likizo ndio tunapaswa kuupiga vita kabisa.

Mwalimu,

Katika mazungumzo au majadiliano kuna kitu kinaitwa context. Ni muhimu sana katika kufikia muafaka.

FACT: Richmond ilifanyika chini ya serikali ya CCM, na kwa jinsi serikali ya CCM inavyoendeshwa hakukuwa na hatua za kisheria zilizochukuliwa.

CDM kwa kujua hiyo fact hapo juu, wakaenda kushitaki kwa wananchi. Ndio maana leo unaona yanayoitwa mafuriko kwenye mikutano ya CDM kuelekea uchaguzi mkuu. Ambaye alishtakiwa kwa wananchi na CMD akitaka kujibu mashtaka yake (kwa kipindi hiki ambacho bado CCM inaongoza), inabidi akajibu hayo mashitaka kwa wananchi ambako alishtakiwa. Sasa ukisema kuwa jukwaani sio sehemu ya kujisafisha bali ni kwenye vyombo vya sheria (which is true) katika muktadha huu tunaouongelea unakuwa out of context. Ni kama vile hujui hili suala lilianzia wapi na lipo katika mazingira gani. Hizo kauli za mwenye ushahidi aende mahakamani ni kauli za ki CCM CCM tu. Wewe unazisema kwa kebehi kelele za mitaani juu ya ufisadi kwa miaka 8 lakini najua unajua kuwa umaarufu wa kisiasa ambao upinzani unafaidi sasa hivi umetokana na hizo unazo ziita kelele za mitaani. Na sitaki kuamini kuwa katika all seriousness unahoji vyombo vya dola vinafanya kazi gani katika zama hizi za CCM katika kujenga hoja zako.

Na ili tusiende nje ya maada kidogo, naomba niseme nukta tunaizungumzia hapa, ni hoja yangu hapa ni kuwa Lowasa alipaswa sio kujieleza kwa kamati kuu peke yake, bali ilipaswa aidha akajieleza kwa wananchi ambao kwa miaka 8 waliambiwa taarifa ya uvundo wa Lowasa au kamati kuu ieleze Lowasa alitoa vielezo gani vilivyo fanya ushahidi waliotangaza kwa miaka 8 kuwa wanao juu yake uwe hauna msingi tena.

Na ili kuondoa kujirudia rudia kwa maswali na hoja zile zile, mimi ukinipa mjadala unaosema kwa nini CCM haiwezi kufanya mabadiliko yanayotangazwa na Magufuli katika kampeni zake, nitazungumza na kuzungumza kila ufisadi uliowahi kutokea katika serikali za CCM zilizopita kujenga hoja zangu. Katika mjadala huo sitakaa hata sehemu moja kwenye hoja zangu nikamtaja Lowasa eti alihusika na Richmondi. Kwa sababu hicho kitu japo ni kweli, kitakuwa kiko nje ya mada husika.
 
JokaKuu,

Ukweli utatuweka huru. Sikubalini kabisa na nadha ya kutumia 'dini' kama nyenzo ya kupata madaraka. Hilo moja.

Pili, kwa kumbukumbu zangu, hakuna siku hata moja Magufuli amehudhuria Ibada kanisani, akapanda madhahabuni, akachukua kipaza sauti na kuwaaambia waumini wengine kuwa wamuombee kwa sababu yeye ni wa 'dhehebu' lao. Na hakuna mahali Maguful amewachambua marais waliopita kwa dini zao ili kukazia 'sifa yake ya udini'.

Alichofanya Lowassa si kuteleza ni za mwizi 40 zimefika. Nitaeleza kwa kifupi sana.

Lowassa alikuwa kampeni meneja wa Kikwete 2005. Na Mkakati wake wa kutwaa madaraka kupitia kwa wanamtandao' ulijumuisha kwa kiasi kikubwa dhana ya udini. Lowassa alikuwa anazungukia majumba ya ibada kumnadi swahiba wake pamoja na kuchukua pesa (hasa temples za wahindi). Askofu Kilaini 'anasemekana' naye alikuwa mwanamtandao na ndio sababu akaja na ule msemo wake wa chaguo la mungu. Baada ya saga ya Richmond, Lowassa alianza kuunda mtandao upya kwa kutumia baadhi ya makanisa ya 'protestant' chini ya usimamizi za Gwajima.

Anachokifanya Lowassa sasa hivi ni 'activation' ya mtandao wake mpya ambao unafanana na kile alichofanya 2005. Na safari hii amekuja na sababu mahsusi, 'Ulutheri'. Na yeyote atakayejaribu kutia mchanga kitumbua chake atakutwa na kadhia ile ile iliyompata Dr Salim Ahmed Salim- character assassination.

..Lowassa ameshaomba radhi kwa suala hili.

..pia tume ya uchaguzi imemkemea kwa kitendo hicho.

..sasa tuondoke huko, turudi kwenye masuala yanayotuunganisha.

..humu JF wengine tumekuwepo kwa muda mrefu kidogo, hivyo tunajuana. kuna wenzetu ambao ni wadini kwelikweli and I can see kwamba wanataka mjadala wetu huu ukwame ktk hoja hii ya udini.

..CCM wako very efficient ktk hizi propaganda za udini, ukabila, na ukanda. angetokea mwana-CDM akafanya kile alichofanya Lukuvi kule kanisani chama hiki kingekuwa kimefutwa tayari. Lakini leo Lukuvi yuko ktk kampeni za Magufuli.

..I know what CCM are trying to achieve here. Lowassa put himself and Ukawa campaigns in a bad spot, he should have known better. But at the same time we are encouraged kwamba Lowassa ametoa tamko la kuomba radhi.

..I wish CCM na nyinyi mngekuwa waungwana kuomba radhi kwa kauli na matendo yenu. Kwa mfano kuomba radhi kwa kauli za Mzee Mkapa. Au kuomba radhi kwa umasikini, shida, na kero, ambazo zimesababishwa na utawala wenu mbovu wa miaka 35+.

NB:

Hii itakuwa ni post yangu ya mwisho kujadili hili tukio la Lowassa kanisani.
 
..Lowassa ameshaomba radhi kwa suala hili.

..pia tume ya uchaguzi imemkemea kwa kitendo hicho.

..sasa tuondoke huko, turudi kwenye masuala yanayotuunganisha.

..humu JF wengine tumekuwepo kwa muda mrefu kidogo, hivyo tunajuana. kuna wenzetu ambao ni wadini kwelikweli and I can see kwamba wanataka mjadala wetu huu ukwame ktk hoja hii ya udini.

..CCM wako very efficient ktk hizi propaganda za udini, ukabila, na ukanda. angetokea mwana-CDM akafanya kile alichofanya Lukuvi kule kanisani chama hiki kingekuwa kimefutwa tayari. Lakini leo Lukuvi yuko ktk kampeni za Magufuli.

..I know what CCM are trying to achieve here. Lowassa put himself and Ukawa campaigns in a bad spot, he should have known better. But at the same time we are encouraged kwamba Lowassa ametoa tamko la kuomba radhi.

..I wish CCM na nyinyi mngekuwa waungwana kuomba radhi kwa kauli na matendo yenu. Kwa mfano kuomba radhi kwa kauli za Mzee Mkapa. Au kuomba radhi kwa umasikini, shida, na kero, ambazo zimesababishwa na utawala wenu mbovu wa miaka 35+.

NB:

Hii itakuwa ni post yangu ya mwisho kujadili hili tukio la Lowassa kanisani.

Nakubaliana na sehemu kubwa ya maaelezo yako, lakini ninatofautiana na wewe mwishoni kwenye rangi.

1.nianze na Blue, Mkapa haogembei, na mkapa hajasimama kwenye eneo la ibada. Kama ni kauli za hovyo zinazotolewa na watu wengine mbali na wagombea nadhani pande zote mbili zina orodha ya kutosha. Lakini hapa tunajadili wagombea.


2. kwenye red: Ninapata shida sana kusikia CHADEMA/UKAWA yenye Lowassa wanapoongea kuhusu ufisadi. Kwangu mimi naona kama ni madharau kwa watanzania na ulaghai wa wazi wazi. CHADEMA/UKAWA ya sasa hawana moral authority kuongelea ufisadi. Hawana! Sumaye alisimamia sheria ya Takrima ikapitishwa bungeni! Lowassa ni sehemu ya CCM for the last 40 years, na jina lake limesheheni kwenye makaratasi na midomo ya CHADEMA/UKAWA wenyewe.

Out of principle, CHADEMA/UKAWA walitakiwa kwanza wawambie Watanzania kuwa kwa miaka yote 8+ walihubiri uwongo hivyo wanaomba radhi. Hili halijafinyika badala yake wanakuja na huu upuuzi wa kutuambua wanapambana na mfumo! Kumbuka ni hawa hawa CHADEMA waliotuambia kuwa walikuwa na ushahidi dhidi ya Lowassa, sasa ushahidi umeenda wapi? Nini kimetokea? Kwanini tunakubali wanasiasa wanatuyumbisha kila kukicha?

3. Ili hoja ya kuomba radhi isimame, ningetaka kusikia kutoka kwa Lowassa mwenyewe akisema hana uhusiano wowote (hata chembe) na ufisadi (catalogue nzima ya ufisadi) wa CCM. Awaambie Watanzania kwamba kwa miaka 40 aliyokaa CCM hakuwahi kuhusika na ufisadi wowote! Tumeambiwa CCM ni mafisadi, sasa kama mwananchi ningetaka kuhakikishwa CHADEMA na wapambe wake ni wasafi!

Twende kazi.
 
Nimesema hivi kama Richmond ilizaa Dowans kwa maana hiyo Richmond na Dowans ni mikataba ya kifisadi, na haya maneno yanasemwa na serikali (Serikali nikiwa na maana ya Dr. Mwakyembe na Sitta ambao ni mawaziri tena ni wanasheria)

Sasa swali langu kwako au kwa mtu yeyote yule ni kama Richmond ni Lowassa ambayo ilizaa Dowans, Dowans inalipwa mamilion ya shilingi je ni kwanini serikali isisitishe mkataba wa Dowans na kuwachukulia hatua viongozi wote waliohusika na mikataba hewa hiki kigugumizi ni cha nini?

Ningeomba kupata ufafanuzi kutoka kwako....
Alinda,

Ntakupa ufafanuzi wangu ila niseme tu kuwa hitimisho linalotakana na swali lako linahuzunisha sana. Kwanza niseme, kushindwa kwa serikali ya CCM kuchukua hatua stahili sio hoja ya kuhalalisha ufisadi uliofanyika au kuwasafisha mafisadi (WOTE) walioshiriki katika ufisadi huo. Hii sio hoja kabisa. Pili, labda niseme kitu ambacho masikio yako yatafurahi kukisikia. Serikali iliyopo madarakani kwa kushindwa kwake kuchukua hatua kunaonesha kuwa na yenyewe kuna kiasi ambacho imefaidika na hizi fisadi, sio Lowasa peke yake. Labda hapo tutakuwa sawa kidogo. Sio Lowasa peke yake. Na pia ufisadi ule mwingine nao pia ulikuwa ufisadi mkubwa na unapaswa kujadiliwa. Baada ya kusema hayo, nadhani tunaweza kurudi kwenye mjadala mkuu wa bango hili.

Swala la Magufuli na nyumba, halihitaji mpaka Magufuli aibuke na kusema hivi au vile kunahitaji mimi na wewe kuhoji ni kwanini aliuza nyumba kwa bei ya kupwa na ni kwanini walihonga nyumba hizo kwa wake zake na wadogo zake? na si nyumba tu kuna hata bil 265 zimepotea katika wizara ya ujenzi, kuna kivuko kibofu cha bil.8 haya ni mambo ambayo hatuwezi kusubiri mpaka Magufuli kuibuka na sema maaana hawezi kuyasema bali ni wajibu wangu mimi na wewe kuhoji na kupata majibu kutoka kwake.
Na kama ndvyo kwa tusubiri mtu mpaka ibuke ndio tumuweke kikaangoni, Je kama Lowassa angekaa kimya inamaana hili Richmond lingepita tu bila kuhojiwa?

Katika mjadala unasema CHADEMA/UKAWA Uwekekezaji usiotabirika. Ufisadi wa nyumba wa Magufuli (ambao sikatai kuwa ni kweli na unapaswa kuzungumzwa), unaingiaje kwenye mjadala huu? Sio kuwa mimi sitaki kusema kuwa Magufuli ni mchafu, najaribu kuchangia kile kilicholetwa kujadiliwa objectively. Akija mwingine akasema unajua na UDA pia ulikuwa ufisadi mkubwa sana katika majadiliano haya atakuwa amesema ukweli lakini hicho ndicho tunachokijadili jamani? Kuna tofauti kati ya mjadala kupanuka kwa jinsi hoja zinavyoongezeka na mjadala kuevolve into something else completely kwa sababu ya wachangiaji kudivert toka katika kile kilichokuwa kinajadiliwa awali.
 
FJM,

..I agree with u kwa mambo ambayo umependekeza CDM wawaombe radhi wa-Tz.

..Je, kwa upande wa CCM unadhani wanatakiwa kuwaomba radhi wa-Tz kwa masuala gani?

cc GalaxyS3, Nguruvi3, Alinda
 
Last edited by a moderator:
Out of Respect ya mjadala huu (mjadala mkuu), sitachangia chochote juu ya Lowasa na hiyo clip ya video. Ukiwepo uzi wa Dhana ya udini na Uchaguzi 2015 ntakuja huko kuchangia. Udini sio suala la kuwa sub-topic, ni suala zito ambalo halihitaji mihemko katika kujadiliwa. Na halijaanza leo kwa sababu hiyo clip ya Lowasa imeonekana.

Quality ya majadiliano inaondoka kukikosekana topic maalum inayojadiliwa. Ahsanteni.
 
Out of Respect ya mjadala huu (mjadala mkuu), sitachangia chochote juu ya Lowasa na hiyo clip ya video.

Ukiwepo uzi wa Dhana ya udini na Uchaguzi 2015 ntakuja huko kuchangia. Udini sio suala la kuwa sub-topic, ni suala zito ambalo halihitaji mihemko katika kujadiliwa. Na halijaanza leo kwa sababu hiyo clip ya Lowasa imeonekana.

Quality ya majadiliano inaondoka kukikosekana topic maalum inayojadiliwa. Ahsanteni.
Thank you
 
Wanajamvi

Kwanza nikubaliane kabisa na hoja za JokaKuu FJM GalaxyS3 kuhusu suala lililoingia la video

Nadhani linatuondoa katika hoja iliyopo mezani. Hii haina maana halijadiliki, hapana, linajadilika sana.

Ni issue kubwa inayohitaji uzi pekee ili kuwe na flow ya majadiliano hapa na huko kwenye uzi mwingine. Nadhani limeeleweka

Pili, kuna hili la asset na Liability

Nikimsoma Alinda na GalaxyS3 hoja zao zinapaingana kwasababu moja kuu.

Glaxy anasema Richmond ni liability pekee katika ujio wa Lowassa UKAWA.

Alinda anasemam si kweli, kwasababu hiyo si unique liability na kuendelea kuijadili ni kuikuza tukijua kuwa liabilities zipo nyingi na kwa maeneo tofauti.

Hivyo , kujadili inakuwa sehemu ya kampeni, jambo lisilo sahihi.
Nadhani nitakuwa sahihi na nasimama kusahihishwa kama nitakuwa nimeelewa vibaya kwa wote wawili

ASSET NA LIABILITY

Tunapoongela haya mawili lazima tuyaangalie kwa jicho pana.
Kwa mfano, Ujio wa Lowassa umesemwa kama asset kwa UKAWA.

Kisichoeleweka, ni kuwa hii ni asset kwa mtazamo upi? Kwa personality, kwa wafuasi au kwa timu anayokuaja nayo?

Na asset hiyo inatumiwaje katika mazingira yaliyopo.

Kwa mfano, watu wake wana nafasi za ubunge na udiwani? Kama hakuna, wafuasi wa watu wanasimama wapi leoo hii?

Impact ya asset ipo wapi. Haya ni baadhi ya maswali tunayoweza kujiuliza

Lakini pia tunashindwa kuiangalia hii asset kwa namna nyingine. Je, ujio wake umeunganisha UKAWA kama vyama au kama wanachama?

Je, kulikuwa na mkakati wa 'assimilation' kati ya kampeni yake na UKAWA?

Hapa ndipo hoja tunayozungumza na @Rev.Kishoka inapoingia.

Kwamba unaweza kuwa na asset lakini kama hujui namna ya kuzitumia ni sawa na hakuna.

Tukiangalia TeamLowassa na M4C ambazo ni vijana zote zinakuwa kama paralyzed.

Hakuna strategists walioona hilo na wanaoliona kwasasa

Watu waliopaswa kuunganisha nguvu zote mbili ni viongozi. Inapotokea kiongozi wa umoja wa vijana anayepaswa kuratibu shughuli za vijana anagombea ubunge na kuacha majukumu yake, hapo kuna tatizo.

Hapa hapakuwa na mkakati kutoka viongozi wa CDM/UKAWA kwa ujumla. Tunasikia Katambi anagombea ubunge, nani wa kuratibu shughuli za uhamasishaji huko mitaani? Nani atakuwa mwenyeji wa Team Lowassa/TeamCUF au NCCR i?

Kwa mtazamo huo, ujio unageuka kuwa liability kwasababu haujaweza ku 'harness and utilize' ujio effectively

LIABILITY

Kwamba, si suala la Richmond pekee. Ni suala la kutazama kama uwepo wake umeathiri au umeboresha hali ya upinzani?

Kwa bahati mbaya, inaonekana viongozi na timu za CDM/UKAWA wame back off pengine kwa nia njema inayotoa matokeo hasi.

Kudumaa kwa jitihada za makundi mengine bila sababu za msingi ni sehemu ya liability tunayoongelea

Kukosa 'common ground' ya kuongelea masuala ni sehemu nyingine

Kutokuwa na timu zinazofanya kazi kwa wepesi , umakini na uhodari ni sehemu kubwa ya tatizo

Hivyo, personality inaonekana ku 'override' institution in varies aspect of campaign.

Kwa hili kama hawakuwa makini, wanachosema ni asset inaweza kuwa liability, ni tatizo la timu nzima

Haina maana hawafanyi vema, wanatakiwa kuhakikisha kukabiliana na CCM yenye matawi muhimu ya nchi, chama na vyombo husika

Hivyo, tuangalie asset na liability kwa upana wake kama suala la fikra na si kudhani Richmond ndio itaamua hatima ya uchaguzi

Na mwisho, labda nimuulize swali GalaxyS3 . Hivi inawezekana kwa Lowassa kusimama na kueleza kila kitu kwa uwazi wake tukijua alikuwa katika cabinet na kuna mambo ya kisheria kama oath n.k. Hapa nisaidiwe naomba ushauri

Tunasema hivi kwasababu, mambo katika closed camera yanaweza kuwa na legal implication tofauti na outdoor

Tusemezane
 
Usemi wa those who expect moments of change to be comfortable and free of conflict have not learned their history, naweza kuutafsiri kwa Kiswahili changu cha ngumbaru kuwa, wanaotarajia kufanikisha mabadiliko kwa starehe bila migogoro si wanafunzi wazuri wa historia. Muda wa mabadiliko ukifika umefika na kwa taifa letu muda huo ni sasa ya yeyote anayedhani anaweza kuyazuia hana nia njema na hatma ya taifa hili...huyo mtu kwa pamoja bila kujali wadhifa wake katika jamii, tumuogope kama ukoma.

Mabadiliko tunayolilia wengi wetu nayafananisha na maamuzi ya kuachana na mfumo uliolididimiza na kulidumaza taifa kwa miaka mingi, kuachana na utawala ambao umechoka na kujawa kiburi usio tena na mbinu ya kutuondoa kwenye kambi ya umasikini na ufisadi na kuachana na timu iliyoshindwa kutuleta ushindi na kutusababishia fedheha baada ya fedheha. Mabadiliko tunayolilia nayafananisha na maamuzi ya kutoka gizani kwenye vitendo vya ulaghai na udanganyifu na kuingia kwenye mwanga kulipo na uwazi na uwajibikaji.

Wakati Lowassa amechukua uamuzi wa kuachana na genge la wezi lililolikamata taifa na kulifilisi, Dr. Slaa kwa upande wake ameamua kuungana na hilo genge. Jibu la nani kati ya Lowassa na Dr. Slaa katoka kwenye pango la wanyang'anyi na nani kahama na kujiunga na wadai mabadiliko nadhani halina mjadala. Wengi mnalichukulia tendo la Lowassa kuitosa CCM kimzaha mzaha, lakini naomba niwaambie kwamba maamuzi hayo hayakuwa rahisi, wako viongozi wengi wa zamani wangetamani kufanya hivyo ila ujasiri hawana.

Niongezeee kwa kusema kuwa mapenzi yangu kwa Dr. Slaa hayakunipofua kiasi cha kujifungia ndani ya box na kutupa funguo, hapana, kwa mawazo huru yalinipa changamoto kubwa. Vivyo hivyo chuki yangu kwa Lowassa haikunipofua, la hasha, badala yake nilitafakari kwa nini hawa watu wawili walilazimika kuchukua maamuzi waliyoyachukua. Je ujio wa Lowassa vs kutoka Dr. Slaa which holds more merit and between the two who risked losing what! Je uwekezaji upi unaoweza kusemwa umelipa?

Kilichojitokeza baada ya watu hawa wawili kuchukua hatua walizozichukua ndicho, kimepelekea mijadala kama hii tunayoishuhudia redioni, magazetini na mtandaoni. Ukweli ni kwamba ni matokeo ambayo hayakutegemewa, watu wanashangaa na kujiuliza imekuwaje walipanda nyanya wanavuna pili pili. Watu walikaa na kupiga mahesabu na kuamini UKAWA unasambaratika, kumbe! Ni kama vile badala ya kujadili ripoti ya mbwa kumng'ata binadamu, tumejikuta tukijadili ripoti ya binadamu kumng'ata mbwa.

Ujio wa Lowassa Chadema ulitakiwa ulete tafrani kubwa na machafuko ndani ya Chadema na UKAWA; badala yake umeleta utulivu na kuzidisha mshikamano. Kuondoka Dr. Slaa ndani ya Chadema kulipangwa kuleta hofu na mgawanyiko; badala yake kumeleta umoja na kuzidisha hamasa ya mabadiliko. Wahafidhina wamepigwa butwaa na kujawa hofu, wanajaribu kukamata kila jani katika harakati za kujiokoa wasizame, leo wanazua hiki, kesho wanazua kile lakini wapi, wakati ukifika umefika.

Wanaohangaika kupandikiza magugu kwenye shamba la UKAWA wanaumbuka kila siku na kila mbinu chafu inayoasisiwa na wapinga mabadiliko haifanikiwi. Wabaya wa UKAWA hawajakata tamaa na sasa badala ya kuelekeza nguvu zao kumnadi mgombea wao, wameamua kuwageukia wapiga kura na kuanza kuwatia hofu wakisahau kuwa Tanzania na dunia imebadilika na hawana uwezo tena wa kuturudisha tulikotoka. Tafadhali CCM, jiandaeni kisaikolojia kuachia madaraka kwa amani, hii nchi ni yetu sote.
 
Out of Respect ya mjadala huu (mjadala mkuu), sitachangia chochote juu ya Lowasa na hiyo clip ya video. Ukiwepo uzi wa Dhana ya udini na Uchaguzi 2015 ntakuja huko kuchangia. Udini sio suala la kuwa sub-topic, ni suala zito ambalo halihitaji mihemko katika kujadiliwa. Na halijaanza leo kwa sababu hiyo clip ya Lowasa imeonekana.

Quality ya majadiliano inaondoka kukikosekana topic maalum inayojadiliwa. Ahsanteni.
Hapana mkuu huyu ni mgombea Urais wa kwanza kutumia lugha hiyo kwa hiyo msitake kupotezea wakati hapa tunazungumzia mtu ambaye anaweza kuwa rais wa nchi hii..Tusiyafumbie macho mambo haya kwa kutaka kuyaweka kiporo kwa sababu Udini upo nchini lakini hatutegemei mgombea Urais kuwa kinara wa fikra hizo..
 
Hapana. We loved Slaa but his wife loved him more. That is why I said do not read too much into it. Remember the King who abdicated to be with the woman he loves?

No you don't love him. You CDM guys are practicing political prostitution, changing masters for fame. Well, we will see if that works in October.
 
Hapana mkuu huyu ni mgombea Urais wa kwanza kutumia lugha hiyo kwa hiyo msitake kupotezea wakati hapa tunazungumzia mtu ambaye anaweza kuwa rais wa nchi hii..Tusiyafumbie macho mambo haya kwa kutaka kuyaweka kiporo kwa sababu Udini upo nchini lakini hatutegemei mgombea Urais kuwa kinara wa fikra hizo..

Mkandara;

Napokea Facebook posts za Mzee Mwanakijiji. Kabla ya Lowassa kujiunga na CDM, karibu kila mtu alimuona Mwanakijiji anasema ya maana. Sasa hivi ana wapinzani wengi na wengine wanamuona kama hawezi tena uchambuzi kwa sababu ya kumpinga Lowassa.
 
FJM,

..I agree with u kwa mambo ambayo umependekeza CDM wawaombe radhi wa-Tz.

..Je, kwa upande wa CCM unadhani wanatakiwa kuwaomba radhi wa-Tz kwa masuala gani?

cc GalaxyS3, Nguruvi3, Alinda


Jokakuu;

Nilikuwepo Nyumbani Morogoro mwezi Julai na niliona matawi mengi ya CDM na wanachama waliojikita CDM. Miaka 10 iliyopita CUF ilikuwa na wanachama wengi kule kuliko CDM. Haya ni matokeo ya kazi nzuri iliyofanywa na watu. Lowassa anatakiwa azitambue kazi hizo na kuelewa makosa madogo yanaweza kufanya CDM another NCCR-mageuzi.
 
Ritz,
Nimemsikiliza EL akizungumzia suala nchi hii kutokuwa na rais Mluteri tangu kuasisiwa kwake na hivyo kuona umuhimu huo hivyo sasa! Kwa maoni yangu wala simuoni EL kama ni mdini sawa na inavyotangazwa ila nadhani ni one of the two if not both!

Mosi, EL ameanza kutumia nyumba za ibada muda mrefu sasa tangu akiwa ktk harakati zake za kuchaguliwa na CCM... na sina shaka hata chembe, kama angepata fursa ya kuingia msikitini vile vile angeenda kuomba kura huko! Hata hivyo, ingawaje kwangu sitafsiri kwamba ni mdini lakini ukweli unabaki pale pale kwamba it's too low for mtu kama EL! Hata CCM wenyewe wanafahamu kwamba EL sio mdini but this's politics... your opponents will always be there waiting for the right shot to hit you! Na wala EL au yeyote kwenye timu yake hawatakiwi kulalamika kwamba CCM wanasambaza propaganda... when you walk around the jungle where there's a sniper or two, you need to be good in hiding than running otherwise blame no one when you get a bullet into your neck! Star TV hivi sasa wanaitumia clip ya EL kanisani na hotuba ya Mwalimu Nyerere... kulalamika ni ujinga, ni ya kujitakia! Mahaba yake ya kungia Ikulu iwe kwa jua au mvua bila shaka ndiyo yaliyomfikisha EL hadi akafanya kosa la kijinga kabisa... kosa ambalo hatakiwi kumlaumu yeyote yule!

Alinda anaonekana kukataa kauli ya EL kwamba nchi hii haijapata kuwa na rais Mluteri! Alinda, mahaba kwa mgombea hayakatazwi na hapa JF watu tunatumia ID fake... wakati mwingine tunaowatetea ni watu wa nyumbani kwetu, jamaa zetu na hata wazazi! Lakini hii isitufanye kuukataa hata ukweli ulio dhahiri dhidi yao kwavile tu ukweli huo ni mchungu!!

Kwa upande mwingine, kilichotokea kwa EL ni kile Waingereza wanachosema, "a cornered rat will bite the cat!!" EL is a cornered rat... Magufuri is a cornered rat! Katika mazingira kama hayo, panya yupo tayari kutumia nguvu zake zote zilizobakia ili apambane na paka aliyembananisha ili apate kujinusuru! Hii wala haitamaanisha kwamba eti panya ni jasiri! Ni uoga wake ndio umemfanya ajitoe
muhanga!

JokaKuu, Nguruvi3, Mag3
 
Back
Top Bottom