Chadema: Wabunge 19 wa viti maalumu waondolewe Bungeni kabla ya mwezi Novemba, 2022

Chadema: Wabunge 19 wa viti maalumu waondolewe Bungeni kabla ya mwezi Novemba, 2022

Kwa hiyo hayo ndio walikaa wakawa wanajadili kwa siku mbili? Ndio maana nikasema Hawa wamebaki wanakusanyika kupiga soga tu kupoteza muda, Ndio sababu ya kupuuzwa na watanzania.

Sasa hayo ndo manini waliyojadili? Kwani kipi kipya na kisichofanyiwa kazi na serikali hii pendwa ya mh mama Samia suluhu Hassani? Ndio maana watanzania wameendelea kuwa na matumaini na serikali hii ya mama was nguvu
Kwako hayana umuhimu kwa vile huna akili,kwa wenye akili wameelewa.
 
Kuagiza Wabunge 19 wa Chadema akina Halima Mdee waondolewe bungeni kabla ya November ni kuingilia Uhuru wa Mahakama, CC ya Chadema lazima ikemewe

Chadema kuagiza Serikali ifute Tozo wakati Kamati kuu ya CCM imeshatoa agizo hilo ni dhahiri Chadema ni tawi la CCM

Nategemea Wakili msomi Kibatala atawaomba radhi akina Halima Mdee kwa niaba ya mteja wake( Chadema)
Kwani Tanzania tuna mahakama? Au unaongelea idara ya Rais anayoitumia kama mahakama kuwapofusha wananchi?
 
Wakati Chadema ikiendelea na mazungumzo na Serikali na CCM, Kamati Kuu ya chama hicho imetoa masharti manne ya kuzingatiwa ili kiendelee na mazungumzo hayo.

Masharti hayo ni kuondolewa kwa zuio la mikutano ya hadhara kwa vyama vya upinzani, kukamilishwa kwa mchakato wa katiba mpya, kuondolewa kwa wabunge 19 wa Viti Maalum bungeni na kuundwa kwa kamati ya pamoja ya wataalamu wa sheria ili iandae maboresho ya kisheria yatakayohusishwa katika mabadiliko ya Katiba.

Masharti hayo yametolewa kupitia Kikao cha Kamati Kuu iliyoketi Septemba 17 na 18, 2022 jijini Dar es Salaam.

Akitoa taarifa ya kikao hicho leo Jumanne Septemba 20, 2022, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu amesema kuhusu Katiba mpya, kamati hiyo imeazimia kuandaliwa kwa muswada wa sheria ya utekelezwaji na upelekwe bungeni kabla ya kikao cha bunge cha Novemba,2022.

“Muswada huo unatakiwa kutolewa wazi sio kinyemela, ili watu waone na watoe maoni yao,” amesema Mwalimu.

Sharti lingine lililotolewa na Kamati Kuu hiyo ni kuondolewa bungeni kwa wabunge 19 wa viti maalum wa chama hicho, akisisitiza hilo lifanyike kabla ya kikao cha bunge cha Novemba, 2022.

Hata hivyo wabunge hao akiwemo Halima Mdee na wenzake wamefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.

Mdee na wenzake wamevuliwa uanachama wa chama hicho Novemba 27, 2020 kwa sababu wamekiuka katika na kanuni za chama hicho kwa uamuzi wao wa kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila chama hicho kuwapitisha.

Kulingana na Mwalimu, sharti lingine ni kuondolewa kwa zuio la mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa vya upinzani, bila masharti.

Kadhalika, kimetaka kuundwa kwa kamati ya pamoja ya wataalamu wa sheria ili iandae maboresho ya kisheria yatakayohusishwa katika mabadiliko ya Katiba.

Hata hivyo, amesema chama hicho kimeshatoa maelekezo kwa viongozi wa ngazi za chini kuandaa mikutano ya hadhara itakayofanyika nchi nzima kwa kufuata kanuni na sheria zilizopo sasa.

CHANZO: Mwananchi
 
Kwa hiyo wananchi wakiwa na shida watakuwa wanakuja nyumbani kwenu? Au ndio Yale mliyowaambiaga watanzania wakasome ilani mtandaoni? Yaani nyie wanachadema hamjaanza ubabaishaji Leo Wala Jana, mmeanza muda Sana ubabaishaji Hadi Sasa watanzania wamewashitukia na kuamua kuwapuuza mambo yenu.
.
IMG_20211011_195427.jpg


Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Justice delayed,is Justice denied.Niwe nakuita wakili msomi au WAKILI tu inatosha?
huyo jamaa ni wakili wa hovyo sana, anaona kabisa justice inakuwa delayed na yeye anaunga mkono pumbavu kabisa huyo mzee
 
Kenya maamuzi ya kisiasa ni wiki mbili tu Tza uchukua miaka 5
 
Lini wanajenga ofisi ya chama?

Wametumia shs ngapi kufanya kikao kwenye hoteli ya kitalii?
Ofisi ni nini kwa uelewa wako ni jengo au ni watu, Kama unadhani kuwa ni jengo nakushauri nenda ukawaze upya.
 
Back
Top Bottom