mbegubora29
JF-Expert Member
- Mar 14, 2015
- 513
- 338
Ha hqnhqnhabah chadema huwa wanaota saana yaan mambo yao Kama abunuasi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo shida za maccm zinatatuliwa kt yale mabanda??Kwa hiyo wananchi wakiwa na shida watakuwa wanakuja nyumbani kwenu? Au ndio Yale mliyowaambiaga watanzania wakasome ilani mtandaoni? Yaani nyie wanachadema hamjaanza ubabaishaji Leo Wala Jana, mmeanza muda Sana ubabaishaji Hadi Sasa watanzania wamewashitukia na kuamua kuwapuuza mambo yenu.
Dunia ya sasa ya kidigitali inaondoa ulazima wa kuwa na liofisi likubwa. Wazee ndio wanaamini kuwa na ofisi. Matokeo ya kuwa na maofisi mengi kama CCM, hizo ofisi zimegeuka kuwa sehemu ya majobless, wapika majungu, washirikina, kupanga mipango haramu ya kudhuru wapinzani nk.
Wewe hizi habari umezipata ofisini au nyumbani kwake?Kwa hiyo wananchi wakiwa na shida watakuwa wanakuja nyumbani kwenu? Au ndio Yale mliyowaambiaga watanzania wakasome ilani mtandaoni? Yaani nyie wanachadema hamjaanza ubabaishaji Leo Wala Jana, mmeanza muda Sana ubabaishaji Hadi Sasa watanzania wamewashitukia na kuamua kuwapuuza mambo yenu.
Sasa hilo swali uliloliuliza, linahusiana vipi na hayo maazimio yaliyotolewa na Chadema?Lini wanajenga ofisi ya chama?
Wametumia shs ngapi kufanya kikao kwenye hoteli ya kitalii?
CHADEMA waliamua kuwekeza kwanza kwa watu na sio majengo na ndio maana imekuwa tishio sana kwa CCM kwa sababu ina watu wengi sana. Pia dunia ya kisasa haihitaji maofisi makubwa kama hakuna lengo la kuyafanya kuwa vitega uchumi.Lini wanajenga ofisi ya chama?
Wametumia shs ngapi kufanya kikao kwenye hoteli ya kitalii?
Ccm ikiwa na ofisi inatosha.maana pamoja na kya na ofisi bado hakuna kikubwa cha maana nchi hii.Yaliyofanyika hata somalia wanaweza kuyafanya.Lini wanajenga ofisi ya chama?
Wametumia shs ngapi kufanya kikao kwenye hoteli ya kitalii?
kwani ofisi za chama nikwaajili yakupokea shida za wananchi?.ikiwa hivyo na ofisi za serikali zitakua zinafanya kazi gani sasa.Kwa hiyo wananchi wakiwa na shida watakuwa wanakuja nyumbani kwenu? Au ndio Yale mliyowaambiaga watanzania wakasome ilani mtandaoni? Yaani nyie wanachadema hamjaanza ubabaishaji Leo Wala Jana, mmeanza muda Sana ubabaishaji Hadi Sasa watanzania wamewashitukia na kuamua kuwapuuza mambo yenu.
Hapana. Ila naona kama haya maazimio yamekaa kama kelele za chura zisizomzuia ng'ombe kunywa maji. Ama kelele za mlango zisizomzuia mwenye nyumba kuingia ndani kwakeHili nalo ulitaka/ulitegemea waliweke kwenye "maazimio"?
Aiseee, ukijua maudhi ya "mlango wenye kelele" kamwe usingetumia mfano huu.Hapana. Ila naona kama haya maazimio yamekaa kama kelele za chura zisizomzuia ng'ombe kunywa maji. Ama kelele za mlango zisizomzuia mwenye nyumba kuingia ndani kwake
Napenda sana tuipate katiba mpya lkn hofu yangu ni kwamba ccm hawako tayari kunoa kisu cha kujichinjia wenyewe.Aiseee, ukijua maudhi ya "mlango wenye kelele" kamwe usingetumia mfano huu.
Hizi kelele za CHADEMA sasa CCM haipuuzi tena.
Hatua hiyo ilikwishapita siku nyingi sana; ndiyo maana unaona wanatumia mbinu zote wanazoweza kujaribu kuzisikiliza na kuzitafutia njia za kuzipunguza.
Ni kelele hizo hizo zilizompa wazimu Magufuli, na kufanya kila awezalo kuimaliza CHADEMA lakini wapi.
Sasa wewe hapa leo unakuja na kusema "kelele za chura"?
Kumbe baso Saccos hii bado ipo?Mzungumzaji kuu ni Mhe. Salimu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho ambaye anaelezea maamuzi ya kamati kuu iliyoketi Septemba 17-18, 2022
Pamoja na hayo, Kamati kuu ilipokea taarifa za uchaguzi wa Kenya ambapo imeona moja kati ya jambo kubwa ambalo watanzania tunaweza kujifunza ni kuwa na katiba imara inayoweza kutoa nafasi ya kuwa na uchaguzi wa huru, haki na wazi.
- Kamati kuu imeitaka Serikali kupeleka muswada wa kufuta sheria mpya ya tozo ambayo imekuwa mzigo mkubwa kwa watanzania.
- Serikali ije na mpango madhubuti wa kuhakikisha chakula kinapatikana kwa uhakika na kudhibiti kupanda kwa gharama zake.
- Serikali ipunguze utitiri wa kodi na tozo kwenye mafuta ili bei yake ipungue nchini.
- Kamati kuu imemtaka CAG kufanya ukaguzi maalumu kwenye mfuko wa bima ya Taifa (NHIF) ili aje na majibu kwa Umma juu ya mwenendo wa michango ya wanachama. Serikali itoe muda wa kutosha kwa wananchi kujadili sheria mpya ya bima kwa afya kwa wote, CHADEMA inapinga mchakato unaopanga kuipitisha sheria hii kwa hati ya dharura.
- Ripoti ya CAG upande wa Zanzibar imebaini matumizi mabaya ya fedha za umma. Kamati kuu inataka hatua stahiki kwa wahusika zichukuliwe dhidi yao.
- Vyombo vya ulinzi vya Zanzibar vimekuwa vinapewa kandarasi bila uwazi. Mikataba lazima iwekwe wazi kwa umma.
- Mazungumzo ya maridhiano ya kisiasa nchini yaendelee. Ili mazungumzo haya yaendelee pasipo kukwama, Kamati kuu imeitaka Serikali kuondoa haraka zuio haramu kwa vyama vya siasa juu ya uhuru wao wa kufanya mikutano bila masharti yoyote. Muswada wa sheria unaofufua mchakato wa katiba mpya upelekwe bungeni kabla ya mwezi novemba. Aidha, Serikali iwaondoe bungeni wabunge 19 wa viti maalumu kabla ya mwezi novemba.
- Kamati za vyama nchi nzima zianze kujipanga kuanza kwa mikutano ya hadhara.
- Kamati kuu inalaani uondolewaji wa wamasai Loliondo pamoja na kuhamishwa kwa fedha zao za miradi ya maendeleo, pia inaitaka Serikali kusitisha zoezi hili pamoja na kuwalipa fidia waathirika wote.
Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kufahamu juu ya sharti la kuwatoa wabunge 19 Bungeni huku kesi ikiwa mahakamani, Mhe. Mwalimu amesema Serikali na Chama cha mapinduzi wanajua ni jinsi gani wabunge hao waliwaruhusu waingie bungeni hivyo wao wenyewe wataona namna gani wafanye ili kuwatoa.
Kuhusu kikosi kazi, wao kama CHADEMA bado hawakitambui na hawahusiki kwa namna yoyote na mambo wanayofanya.
======
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA KILICHOFANYIKA SEPTEMBA 17-18, 2022 JIJINI DAR ES SALAAM.
Kamati Kuu ya Chadema ilikutana kwa siku mbili Jijini Dare es salaam katika kikao chake cha kawaida kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mheshimiwa Freeman Mbowe.
Kamati Kuu ilikuwa na ajenda kadhaa zikiwemo kupokea na kuijadili taarifa ya hali ya Siasa na Uchumi nchini, pia ilihusisha taarifa ya hali ya siasa Zanzibar, Mwenendo wa mazungumzo ya Maridhiano baina ya Chadema, CCM na Serikali, Bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/23 na madhara yake kwa wananchi, Hatari ya Mfuko wa Bima ya Afya kufilisika na kutungwa Kwa sheria Mpya ya bima ya Afya kwa wote. Hali ya upatikanaji na bei kubwa ya chakula nchini. Bei kubwa ya Mafuta na nyinginezo kadhaa.
Katika kikao hicho Wajumbe walijadili kwa kina taarifa hizo na kufikia maamuzi mbalimbali kama ifuatavyo;
1. Bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/23 na tozo za miamala ya kieletroniki.
Kamati Kuu imeitaka Serikali kupeleka Muswada wa marekebisho ya sheria ya fedha ya mwaka 2022/23 kufuta kifungu kilichoingiza tozo kwenye miamala ya kieletroniki nchini kutokana na tozo hizo kuwa mzigo mkubwa kwa Mwananchi.
Kamati Kuu imetaka Muswada huo wa marekebisho ya sheria ufute kifungu cha Sheria ya fedha ya mwaka 2022/23 kilichoanzisha Tozo Mpya ya Vingamuzi ambayo bado haijaanza kutozwa ili kumpunguzia mwananchi gharama kubwa za maisha.
2. Gharama kubwa za chakula nchini.
Kamati Kuu imeitaka Serikali kuja na mpango madhubuti wa uhakika wa upatikanaji wa chakula na kuthibiti kasi ya ukuaji wa bei za chakula nchini.
3. Bei ya Mafuta Nchini.
Kamati Kuu imeitaka Serikali kupunguza msururu wa Kodi na Tozo kwenye Mafuta ili kupunguza bei kubwa ya mafuta nchini.
4. Kufilisika kwa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) na kutungwa kwa Sheria Mpya ya Bima ya Afya kwa Wote.
Kamati Kuu inamtaka Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum kwenye mfuko wa Bima ya Afya nchini na kutoa taarifa yake kwa Umma kuhusu mwenendo wa hali ya Fedha za wanachama wa mfuko huo ikiwa ni pamoja na madeni yake.
Kamati Kuu imeitaka Serikali kutoa Muda wa kutosha kwa wananchi kuijadili Sheria Mpya ya Bima ya Afya Kwa Wote badala ya kutumia utaratibu wa Hati ya Dharura kuwasilisha Muswada Bungeni. Serikali itumie utaratibu wa kawaida katika kutunga sheria hiyo.
5. Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali Zanzibar
Ripoti ya mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2020/21 kama ilivyo kwa miaka iliyotangulia zimebainisha Ubadhirifu, Ufisadi, Uzembe na matumizi mabaya kwa ujumla ya Fedha za Umma.
Chadema haijaridhishwa na hatua ambazo zimechukuliwa na SMZ mpaka hivi sasa hivyo inataka hatua zaidi zichukuliwe kwa wahusika na taarifa ya hatua hizo iwekwe wazi kwa umma. Hatua hizo ziambatane pia kwa upande mwingine kuweka wazi kandarasi zilizopewa vyombo vya usalama na kushughulikia walioshindwa kutekeleza matakwa ya kandarasi hizo."
6. Kuhusu Maridhiano
Kamati Kuu inaazimia kwamba mazungumzo kati ya Chadema na Serikali/CCM kuhusu Maridhiano ya Kisiasa nchini yaendelee kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
Kuondolewa haraka iwezekanavyo na bila masharti yoyote zuio haramu la mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa vya upinzani nchini.
Ratiba ya mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya na hatua zake zote inakubaliwa kwa pamoja na pande zote na kuandaliwa kwa muswada wa sheria ya utekelezaji wake kabla ya kikao cha Bunge cha mwezi Novemba mwaka huu.
Kamati ya Pamoja ya Wataalamu wa Sheria yenye Wajumbe wa pande zote mbili iundwe kwa lengo la kuandaa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria mbalimbali yanayohitajika ili kutengeneza mazingira bora ya kupatikana kwa Katiba Mpya. Kamati hiyo iundwe na kuanza kazi kabla ya kikao cha Bunge cha Novemba mwaka huu.
Serikali/CCM inachukua hatua za kuwaondoa Bungeni wale wanaoitwa “Wabunge wa Viti Maalum wa Chadema” kabla ya kikao cha Bunge cha mwezi Novemba mwaka huu.
7. Maandalizi ya Mikutano ya Hadhara
Kamati Kuu inaazimia kwamba Chama, katika ngazi zake zote, kianze maandalizi ya kuanza kwa mikutano ya hadhara nchi nzima kwa wakati na muda utakaoelekezwa na uongozi wa Chama kwa kufuata Katiba, sheria na Kanuni za nchi.
8. Kuhusu kufukuzwa kwa Wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro.
Kamati Kuu inapinga na kulaani vikali vitendo vya Serikali ya CCM kuwaondoa kwa nguvu na kinyume cha Katiba, Sheria na Mikataba ya Kimataifa ya Haki za Binadamu wananchi wanaoishi maeneo ya Hifadhi ya Ngorongoro hususani Tarafa ya Loliondo.
Kamati Kuu inapinga na kulaani vikali vitendo vya Serikali ya CCM vya kuhamisha fedha za maendeleo na huduma za jamii zilizotengwa na Bunge kwa ajili ya wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro na kuzipeleka Wilaya ya Handeni kama njia ya kuwashinikiza wananchi hao kuondoka katika ardhi na maeneo yao ya jadi na wanayoyamiliki kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.
Kamati Kuu inaitaka Serikali ya CCM kusitisha vitendo hivi haramu dhidi ya wananchi wa Ngorongoro pamoja na kuwafidia wale wote ambao wameathiriwa kwa namna mbali mbali na vitendo hivyo.
9. Uchaguzi Mkuu wa Kenya
Kamati Kuu imepokea taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Kenya na imepongeza uwepo wa Katiba Imara ya Kenya Kwa kuweka mifumo na taasisi imara za kusimamia na kuendesha Chaguzi zilizo Wazi na Huru na kuwataka Watanzania kuendelea kupigania upatikanaji wa Katiba Mpya nchini ambayo pamoja na mambo mengine itaweka bayana Mifumo na Taasisi imara za kusimamia na kuendesha Chaguzi Huru, Wazi na za Haki nchini mwetu.
Ninakubaliana nawe moja kwa moja.Napenda sana tuipate katiba mpya lkn hofu yangu ni kwamba ccm hawako tayari kunoa kisu cha kujichinjia wenyewe.
Watafanya janja ya mama asiyekuwa na chakua ya kuchemsha mawe na kuendelea kuyachochea mpk watoto walale. Hayo maridhiano ni mawe ili chadema wapumbazike (walale).
Mzungumzaji kuu ni Mhe. Salimu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho ambaye anaelezea maamuzi ya kamati kuu iliyoketi Septemba 17-18, 2022

sasa ndugu hao wamewapeleka wenyewe wana tuzuga tu ndiyo maana hawawezi kuwatoa na kinachofuata ni kuumbuka kwa katibu mkuu tu hapoCHADEMA bhana,kutakua na shida ya uongozi,hao Covid19 bado wamo bungeni,na hatujaona chochote kinachofanyika,haya mambo bhana.