CHADEMA wachemka tena, wapeleka barua ya hukumu kusiko

CHADEMA wachemka tena, wapeleka barua ya hukumu kusiko

Verrazanno

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2021
Posts
454
Reaction score
1,011
SALUM Mwalimu anatuambia wamepeleka barua kwa Spika kumweleza hukumu ya mahakama iliowapiga chini kina Mdee na kwa sasa awatoe bungeni.

Wamechemka tena.

Anaemtangazia Spika, na anaeitangazia nchi, nani ni mbunge wa wapi kutoka chama gani sio Salum Mwalimu bali ni Tume ya Taifa Uchaguzi.

Salum Mwalimu aelekeze barua yake kwa Tume ya Uchaguzi.

Spika hawezi kufanyia kazi barua ya Salum Mwalimu au ya John Mnyika halafu kesho kutwa ikaja barua ya Freeman Mbowe imeamua kuwasamehe kina Mdee.
 
Huu uchafu uliopo bungeni uliyosababishwa na uchafuzi wa 2020 unamdhalilisha rais Samia, spika wa bunge na taifa kwa ujumla. Siyo suala la kufurahia.

Kwann spika alipowakingia kifua hakusubiri barua ya tume lkn kwenye kuwaondoa ndiyo anasubiri barua ya tume?
 
😁😁😁
16554546876670.jpg
 
We ni mwanasheria?au mburula?fatilia mahojiano start,usikie mwanasheria anatolea maelezo
Mwanasheria sio msemaji wa CHADEMA.

CHADEMA imetoa tamko kupitia Salum Mwalimu kwamba wamemweleza Spika matokeo ya hukumu hivyo awaondoe kina Mdee.

Spika haambiwi hata na mahakama nani mbunge nani sio mbunge.

Sembuse Salim Mwalimu.
 
Mwanasheria sio msemaji wa CHADEMA.

CHADEMA imetoa tamko kupitia Salum Mwalimu kwamba wamemweleza Spika matokeo ya hukumu hivyo.

Spika haambiwi hata na mahakama nani mbunge nani sio mbunge.

Sembuse Salim Mwalimu.
Ficha umbulula. Punguza ujuaji mavi unajidhalilisha
 
Kwann spika alipowakingia kifua hakusubiri barua ya tume lkn kwenye kuwaondoa ndiyo anasubiri barua ya tume?
Kwa sababu tayari anayo taarifa ya Tume ya Uchaguzi ya mwaka 2020 inayowatambua kina Mdee, deservedly or otherwise, kama wabunge.

Taarifa hiyo, whether ilitengemezwa kwa kughushi au vinginevyo, itatenguliwa na taarifa rasmi nyingine kutoka Tume kwenda kwa Spika.

Salum Mwalimu, cover your bases, peleka barua TUME.
 
Maisha Ni Vita babu .hayo Ni maisha ya kisiasa Ni akili yako na ushapu wako kungamua wapi utapata pesa kwa mbinu zozote ulitaka Nani waende bungeni

Hata hao wa bunge wa ccm wengi wako pale isivyo halali hili hawalisemi hkn mbunge pale hata tulia Yuko pale isivyo halali jaribu kulitazama hili kwa wabunge wengi jins walivyo ingia kimazabe so wakina mdee wapambane maisha Ni vita
 
Yote yanafanyika kisa ni Chadema. Tangu Nyerere aondoke nchi haona mwenyewe kila mtu na lake.
 
Mleta mada ni bure kabisa

Kwani Tundu Lisu alifukuzwa ubunge na NEC?
Tundu Lissu alifukuzwa na parliamentary rules. Spika ndio arbiter wa parliamentary rules, kwa hiyo Spika akaiambia TUME,na TUME ikaitangazia dunia kwamba jimbo la Tundu Lissu liko wazi.

Mdee na wenzake wamefukuzwa na constitutional rules. CHADEMA inapaswa kuelekeza hoja zao za kikatiba kwa TUME, TUME itaitangazia nchi na Spika nani ni mbunge wapi kutoka chama gani kuanzia lini.
 
Wale Wabunge 8 wa CUF walifukuzwaje?

Cecil Mwambe baada ya kujivua uanachama wa Chadema na kuitaarifu Tume ya Uchaguzi ni nani aliyemrejesha bungeni?
 
Kwa sababu tayari anayo taarifa ya Tume ya Uchaguzi ya mwaka 2020 inayowatambua kina Mdee, deservedly or otherwise, kama wabunge.

Taarifa hiyo, whether ilitengemezwa kwa kughushi au vinginevyo, itatenguliwa na taarifa rasmi nyingine kutoka Tume kwenda kwa Spika.

Salum Mwalimu, cover your bases, peleka barua Tume.
Msingi wa Tulia kusema anasubiri hukumu ni upi?Kwanini hakusema yeye anasubiri tume ya uchaguzi?Nijuavyo Mimi,mbunge akifukuzwa uanachama,Spika huiandikia tume kuijulisha kuwa Kuna nafasi Iko wazi baada ya mbunge kupoteza sifa za kuendelea na ubunge!Tume ndio hapo hushughulikia namna ya upatikanaji wa mbadala na baada ya mchakato,humpa taarifa Spika juu ya nafasi iliyowazi itajazwa na nani!
Rejea wabunge wa CUF waliofukuzwa na Lipumba,mtiririko ulikuwa hivi,Lipumba alimuandikia Spika kuwa imewafukuza uanachama wabunge wa viti maalumu,Spika Ndugai(wakati huo akiwa kwenye matibabu India) alimuandikia tume kuwa Kuna nafasi ziko wazi baada ya wabunge kukosa sifa za kuendelea,Tume ikashughulikia kujaza nafasi zilizowazi na kupeleka barua Kwa Spika juu ya majina Mapya yatakayoingia bungeni!
Punguza ujuaji Kwa mambo usitokuwa na taarifa nayo sahihi!
 
Acha uongo nakala wamepewa NEC na ofisi ya msajili
NEC haiwezi kufanyia kazi nakala. Salum Mwalimu kasema.kapelela nakala Tume

TUME inajibuje nakala ya barua ambayo sio yao ?

Cover all your bases, peleka direct letter TUME.

Salim Mwalimu was goofy on the podium. Anatuambia wananchi tuwe watulivu. Kwani lini tumefanya fujo?

Don't lecture us. Do your job. Peleka barua TUME!
 
Back
Top Bottom