CHADEMA wadai kuzuiwa msibani kwa mwanachama wao, kufuatia maagizo kutoka juu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamekasirishwa na kitendo kinachodaiwa kufanywa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi kuwazuia kushiriki kama chama kwenye msiba wa aliyekuwa mwanachama na Mweka Hakina wa chama hicho Jimbo la Mbagala, Bi Rose Ngangaji.

Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Temeke, Hermani Kiloloma amesema msiba ulipotokea wao kama chama walishiriki kikamilifu kwa michango na shughuli nyingine ila wameshangazwa kwa siku hiyo kuambiwa hawatakiwi kushiriki katika msiba huo kwani upo chini ya jeshi, huku bendera za CHADEMA zikiondolewa msibani.

VIDEO: Jambo Online TV

JW badala ya kuwashughulikia mafisadi walioko madarakani wanakubali kutumika katika siasa chafu hizi, Mzee Warioba alisihi sana kuwa JW isiingizwe kwenye siasa lakini CCM wanajifanya vichwa ngumu. DRC wanajeshi walianza kukimbia vitani wakavua magwanda na kujichanganya na raia sasa wanakimbia vitani wanajiunga na M 23, hata mbuyu ulianza kama mchicha.
 
Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamekasirishwa na kitendo kinachodaiwa kufanywa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi kuwazuia kushiriki kama chama kwenye msiba wa aliyekuwa mwanachama na Mweka Hakina wa chama hicho Jimbo la Mbagala, Bi Rose Ngangaji.

Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Temeke, Hermani Kiloloma amesema msiba ulipotokea wao kama chama walishiriki kikamilifu kwa michango na shughuli nyingine ila wameshangazwa kwa siku hiyo kuambiwa hawatakiwi kushiriki katika msiba huo kwani upo chini ya jeshi, huku bendera za CHADEMA zikiondolewa msibani.

VIDEO: Jambo Online TV

Lissu anasemaje?Lissu alisema ktk uongozi sio kama wa Mbowe, atakua mkali
 
Mbona unaongea kinyonge bado? Si utawala wa Mbowe huu. Ni wa Tundu Lissu
Toka uanze kudate na Mbowe hadi kubadili dini na kuwa mla nguruwe umekuwa wa hovyo sana, huwezi kuandika sentensi bila kutaja jina la Mbowe kwa jinsi anavyokupekea moto
 
Back
Top Bottom