Kuna haja ya kuhakikisha kuwa tunailewa Katiba, taratibu na Sheria pamoja na Barua ya Chadema. Barua ya Chadema, kama nimeilewa vizuri, siyo ya kuomba ruhusa kwa Polisi ili kufanya maandamano. Inailitaarifu jeshi kuwa inatarajia kufanya maandamano ya amani. Je kuna mahali kwenye Katiba na Sheria za nchi yetu ambapo Jeshi la Polisi linabidi liombwe ruhusa ya kufanya maandamano? Au liombwe kuandaa maandamano?