CHADEMA waiangukia Jumuiya ya kimataifa wakipinga mashahidi kufichwa katika kesi ya uhaini ya Lissu

CHADEMA waiangukia Jumuiya ya kimataifa wakipinga mashahidi kufichwa katika kesi ya uhaini ya Lissu

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeiomba Jumuiya ya Kimataifa taasisi za haki za binadamu, ofisi za kidiplomasia, na mabunge ya kidemokrasia hasa Bunge la Marekani na mabunge ya washirika kuliangalia kwa dharura suala la mashahidi kufichwa katika kesi inayomkabili mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.

Agosti 4, Jaji Hussein Mtembwa wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam alikubali ombi la Serikali kwenye kesi hiyo la kuwalinda mashahidi wake baada ya kuwasilishwa hoja na Wakili wa Serikali Cuthibert Mbilingi ambaye alieleza kuwa mashahidi hao ni raia wa kawaida wanaoweza kuhatarishiwa usalama wao endapo taarifa zao zitafichuliwa wazi wakati wa usikilizwaji wa kesi.

Taarifa iliyotolewa leo Agosti 5, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, imesema suala hilolinakwenda kinyume na misingi ya sheria, na kuongeza ufuatiliaji wao juu ya mwenendo wa kisiasa na kimahakama nchini Tanzania.

“Hivyo basi, tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, taasisi za haki za binadamu, ofisi za kidiplomasia, na mabunge ya kidemokrasia hasa Bunge la Marekani na mabunge ya washirika wengine kuzingatia kwa dharura hali hii inayokwenda kinyume na misingi ya sheria, na kuongeza ufuatiliaji wao juu ya mwenendo wa kisiasa na kimahakama nchini Tanzania.”

Taarifa:
963e0563-995b-4223-bcd8-06130b70a974.jpg

96fdbb42-3a59-4a2e-abf9-163ad60aba94.jpg
 
Huyu bibi atengwe na Dunia nzima hata mbinguni. Kuwaficha mashahidi ni uovu uliopindukia. Tusimame tupaze sauti dhidi ya ushetani huu.
 
Bado hawajasema, mpaka ajinasue kwenye utando wa kisheria wa buibui sio leo, na buibui anaendelea kutandaza nyuzi tu. Tunaenda Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, maamuzi ya Mahakama ya Rufani ni mwakani Julai
 
Back
Top Bottom