CHADEMA waikosoa vikali kauli ya Rais Samia ya "kukamatwa na kuwachapa mikwaju wanaharakati"

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesikitishwa na kauli ya ndugu Samia Suluhu Hassan aliyoitoa hivi karibuni kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa William Samoei Ruto.

Ndugu Samia alimtaka Rais Ruto awakamate na kuwachapa mikwaju wanaharakati mwanaotoka Tanzania na akasema kuwa yeye atawachapa mikwaju wanaharakati wanaotoka Kenya kuja Tanzania.

Chadema inapenda kumkumbusha ndugu Samia kuwa anachofikiria au kutamani kifanyike ni kinyume cha Katiba hii mbovu ya Tanzania Ibara ya 16, 17 na 18 inayotoa haki ya kujieleza na kutoa maoni, haki ya kutoka na kuingia nchini na haki ya kupata hifadhi.

Ikumbukwe Serikali ya Tanzania chini ya Baba wa Taifa Mheshimiwa Julius Nyerere ilishawahi kuwapa hifadhi wanaharakati na wanasiasa wengi kutoka nchi mbalimbali za Afrika akiwemo Mheshimiwa Nelson Mandela wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Joachim Chisano wa Msumbiji, Mheshimiwa Laurent Kabila wa Kongo na wengine wengi ambao walipewa mpaka ardhi ya kuweka kambi zao nchini Tanzania.

Pia Tanzania iliwahi kumpa hifadhi Mheshimiwa Raila Odinga na kumpa pasi ya kusafiria ya Tanzania ili aende nchi za Ulaya.

Chadema inasikitika kuona heshima hiyo iliyoasisiwa na kujengwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ikizikwa kwenye kaburi refu na watu waliojipachika madarakani wanaopambana kufuta heshima hiyo kwa taifa letu ambalo lilikuwa kimbilio la wanaharakati na wanasiasa waliokuwa wanaonewa kwenye nchi zao.

Soma Pia: Samia: Nimeongea na Rais Ruto, wale watoto wetu watovu wa adabu, wakija kwako chapa mikwaju, wakija kwangu nachapa mikwaju

Kwa uzito mkubwa Chadema inaitaka Serikali ya Kenya isikubali kuingizwa kwenye mtego wa kujichafua kwenye macho ya jumuiya ya kimataifa kwa kuonekana inakiuka haki za binadamu.
Imetolewa leo Jumatano, tarehe 06 Mei, 2026 na;

Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi
photo_2026-05-06_21-18-40.jpg
 
Halafu wakati mwingine ccm acheni kuteua wagombea wenu kwa mihemko au nguvu ya mitandao yenu haramu! Angalieni watu waliokamilika uptairs.

Yaani kama mtu ana utambulisho wa Dr. basi awe ni DR. kweli. Nyerere alikuwa na Masters, lakini unaona ni kwa namna gani alikuwa vizuri upstairs. The same to BEN, na yeye alikuwa vizuri. Hawa wengine siwezi kuwasemea.

Viongozi pia watambue hii nchi imeridhia mikataba mingi ya Kimataifa, ikiongozwa na Unilateral Declaration of Human Rights (UDHR) ya mwaka 1948, na Conventions mbalimbali. Hii mikataba inahusu haki za binadamu kwa ujumla wake. Hivyo wakati fulani viongozi waambiwe ukweli kuhusu matamko yao.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesikitishwa na kauli ya ndugu Samia Suluhu Hassan aliyoitoa hivi karibuni kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa William Samoei Ruto.

Ndugu Samia alimtaka Rais Ruto awakamate na kuwachapa mikwaju wanaharakati mwanaotoka Tanzania na akasema kuwa yeye atawachapa mikwaju wanaharakati wanaotoka Kenya kuja Tanzania.

Chadema inapenda kumkumbusha ndugu Samia kuwa anachofikiria au kutamani kifanyike ni kinyume cha Katiba hii mbovu ya Tanzania Ibara ya 16, 17 na 18 inayotoa haki ya kujieleza na kutoa maoni, haki ya kutoka na kuingia nchini na haki ya kupata hifadhi.

Ikumbukwe Serikali ya Tanzania chini ya Baba wa Taifa Mheshimiwa Julius Nyerere ilishawahi kuwapa hifadhi wanaharakati na wanasiasa wengi kutoka nchi mbalimbali za Afrika akiwemo Mheshimiwa Nelson Mandela wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Joachim Chisano wa Msumbiji, Mheshimiwa Laurent Kabila wa Kongo na wengine wengi ambao walipewa mpaka ardhi ya kuweka kambi zao nchini Tanzania.

Pia Tanzania iliwahi kumpa hifadhi Mheshimiwa Raila Odinga na kumpa pasi ya kusafiria ya Tanzania ili aende nchi za Ulaya.

Chadema inasikitika kuona heshima hiyo iliyoasisiwa na kujengwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ikizikwa kwenye kaburi refu na watu waliojipachika madarakani wanaopambana kufuta heshima hiyo kwa taifa letu ambalo lilikuwa kimbilio la wanaharakati na wanasiasa waliokuwa wanaonewa kwenye nchi zao.

Soma Pia: Samia: Nimeongea na Rais Ruto, wale watoto wetu watovu wa adabu, wakija kwako chapa mikwaju, wakija kwangu nachapa mikwaju

Kwa uzito mkubwa Chadema inaitaka Serikali ya Kenya isikubali kuingizwa kwenye mtego wa kujichafua kwenye macho ya jumuiya ya kimataifa kwa kuonekana inakiuka haki za binadamu.
Imetolewa leo Jumatano, tarehe 06 Mei, 2026 na;

Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi
View attachment 3584915
No dhahiri kuwa dhamira inamtesa na kumsuta kwa kile alichowafanyia wanaharakati wawili kutoka Kenya na Uganda waliokuja kusikiliza kesi ya uhaini ya Lissu ikiwa katika committal stage pale mahakama ya Kisutu.

Matendo ya ufedhuli waliyofanyiwa, na serikali yake, na kuwekwa wazi na vyombo vya habari nchini Kenya vilimfaya akose kitu cha maana cha kuongea mbele ya Rais Ruto, na kuishia kubwajabwaia tu kauli ya hovyo kama hiyo
 
We don't have Prezoo here 🚮🚮🚮🚮🚮🚮
 
A
atakae kosa adabu na utii atachapwa ipasavyo,
na hakuna atakachofanya wala hakuna atakapoenda.

Lazima kuacha tabia mbaya ili kuepuka viboko.
laasivyo utalazimishwa kuacha kiburi kwa viboko, upende usipende.
liyekosa adabu ni yule MWIZI, WEZI WA RIPOTI YA CAG ,WATEKAJI, WAUAJI WA 29 OCTOBER 🤔🤔🤔
 
Back
Top Bottom