CHADEMA Wajitafakari: Siasa za Kudandia hoja haziwajengi wala kujenga Taifa

Joined
Nov 23, 2018
Posts
97
Reaction score
205
Katika historia ya vyama vya upinzani nchini Tanzania, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimejipambanua kama sauti mbadala ya kisiasa. Hata hivyo, miaka ya hivi karibuni imeonesha mwelekeo unaotia shaka: chama hiki kimegeuka kuwa jukwaa la kila anayepinga serikali—bila kujali dhamira, malengo wala maslahi ya taifa.

Katika kipindi cha utawala wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, CHADEMA walikuwa mstari wa mbele kupinga juhudi za Rais huyo marehemu kupambana na ubadhirifu na uzembe katika utumishi wa umma. Walibeza juhudi za kujenga miundombinu mikubwa kama reli ya kisasa (SGR), mradi wa umeme wa Mwalimu Nyerere (JNHPP), na uboreshaji wa huduma za afya na elimu. Kila hatua ya utawala huo ilionekana kwao kama ina doa, hata kama ilikuwa yenye manufaa kwa taifa.

Cha kushangaza na kusikitisha ni kuwa sasa chama hicho hicho kimegeuka na kujifanya wapambanaji dhidi ya kile wanachokiita "ufisadi wa Serikali ya Rais Samia." Hili ni jambo la kushangaza kwa sababu wanakikosoa chama kile kile walichokipinga wakati kikichukua hatua kali za kupambana na ubadhirifu. Hii inazua maswali: Je, msimamo wao ni wenye msingi au wa kisiasa tu kwa ajili ya kutafuta umaarufu wa muda?

Mbaya zaidi, CHADEMA wamekuwa tayari kuungana na kila anayeipinga serikali, hata kama ni wageni au taasisi zenye ajenda za kikoloni au za kuhatarisha usalama wa nchi. Katika baadhi ya matukio, sauti zao zimekuwa zikilingana na zile za baadhi ya mashirika ya kimataifa ambayo yamekuwa yakishutumiwa kwa kupenyeza ajenda zisizo na maslahi kwa Watanzania. Kwa hili, CHADEMA wanajitokeza si kama chama kinachojali maslahi ya taifa, bali kama genge la kisiasa linalotafuta namna ya kujipatia umaarufu kwa gharama yoyote ile.

Wakati kijana aliyefahamika kama Hamza alipowafyatulia risasi askari jijini Dar es salaam, kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii za makada wa CHADEMA zilijaa kejeli kwa polisi na kumtambua Hamza kama shujaa.

Rais wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete alikemewa hadharani na viongozi wa CHADEMA wakidai kwa wakati huo , nchi inahitaji rais mkal- sio wa kaliba ya Kikwete ambaye mara nyingi uso wake ulikuwa umepambwa na tabasamu. Mara alipoingia madarakani hayati Magufuli na kuanzisha kampeni dhidi ya mafisadi, CHADEMA iliungana na makundi ya waliominywa na utawala wa Magufuli ili kuharibu taswira ya utawala huo kitaifa na kimataifa. Mathalan, Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA, Mhe. Lissu aliwahi kunikuliwa akimwita Hayati Magufuli "dikteta uchwara." Aidha Mhe. Lissu alisema,

"Hatujawahi kupata rais wa ajabu kama huyu..."

Upinzani wa kweli ni ule unaojengwa juu ya hoja, kanuni, na msimamo wa dhati wa kulinda haki za wananchi na kuhimiza utawala bora. Ni upinzani unaokosoa pale inapobidi na kupongeza pale inapostahili. CHADEMA wanapaswa kuwa mfano wa chama kinachojifunza kutoka katika historia, kinachojitathmini na kurekebisha mkondo wa siasa zake kwa ajili ya maendeleo ya taifa, si kudandia hoja zinazopigiwa kelele mitandaoni au kupokea mashinikizo kutoka nje.

Watanzania wanahitaji vyama vya upinzani vyenye dira na misimamo ya kweli—si vyama vinavyotegemea mihemko ya kisiasa au misukumo ya wageni. Kama CHADEMA wanataka kuaminika tena, wanapaswa kurejea kwenye msingi wa hoja, kujenga sera madhubuti, na kujiepusha na siasa za kuchochea bila suluhisho.

Siasa si mteremko wa kusaka huruma kwa kila anayepinga. Ni kazi ya kujenga taifa kwa hoja, misimamo na dhamira. CHADEMA bado wana nafasi ya kujisahihisha, lakini si kwa staili hii ya kudandia hoja—bali kwa kusimamia misingi. Wakitaka kuaminika tena, waanze kwa kutafakari walikosea wapi, na waamue kusimama kama chama cha hoja, si chama cha kelele.
 
Wanaipinga Serikali kwa mazuri iliyofanya au mabaya iliyofanya? Jibu maswali haya
1. Watu wanatekwa na kuuwawa, wakae kimya?
2. Bandari, mbuga, mpaka uwanja wa ndege wa KIA wamepewa waarabu, wakae kimya?
3. Nyaraka zinavuja zikionesha ufisadi mkubwa wa fedha unaofanywa na viongozi wa juu, wakae kimya?
5. Umesahau kashfa ya Tegeta Escrow?
6. Unafahamu Seth aliingizia taifa hasara kiasi gani? Alifungwa na Magufuli, sasa hivi yuko wapi?
Nadhani Akili zako zipo kwenye visigino na sio Ubongo
 
Back
Top Bottom