CHADEMA wakitaka washinde yanayoendelea hawana budi kuwasamehe wabunge 19 Kwa masharti haya

CHADEMA wakitaka washinde yanayoendelea hawana budi kuwasamehe wabunge 19 Kwa masharti haya

Siasa si uadui!

Mdee kuwa bungeni si kosa kisheria ila njia alizotumia zaweza kuwa si sahihi,

Kwakuwa Mamlaka ya Bunge imeonekana kuwatambua basi vema hata CHADEMA ikaachana nao ila Kwa Mashrt haya

1. Kutangazia Umma kwamba alikosea na sasa wanaomba msamaha wala si kushindana na CHADEMA Kwenda kwenye mahakama Au kutunishiana msuli na Chama kilichowalea!

2. Watoe michango Kwa Utaratibu wa CHADEMA , wabunge wanachangia kila mwezi hivo watozwe faini ama ya 150M kila mmoja Ambayo ilipwe Kwa awamu Au Kwa mkupuo

3. Hatma yao ya kugombea mwaka 2025 iwe Siri ya Kamati kuu ya Chama

CHADEMA HII NDO TURUFU YA KUONESHA UKOMAVU

Then sina uhakika Kama Mdee wana Courage Hiyo ya kufoji Kwenda Bungeni, tunajua mengi na hatuyasemi

Britanicca
Daaaah hata ww....nadhan lile fungu la Mdee limekufikia...hongera mkuu

Sent from my TECNO R6 using JamiiForums mobile app
 
Pascal Mayalla ameshasema kina Mdee hawakujipeleka wenyewe kuapishwa ila kuna kiongozi mkubwa wa Chadema alitoa ruhusa ( green light), sema Cdm hawataki kuwa wakweli.

JokaKuu Nguruvi3 Behaviourist Tindo Yodazitto junior Daudi Mchambuzi THE BIG SHOW
Erythrocyte
Cha kushangaza DPP alimuachia Nusrat Ili awahi kuapishwa kesho yake asubuhi tena aliachiwa usiku mzito. Wote tunajiuliza Mbowe ana mamlaka gani hadi kumuagiza DPP amtoe haraka Nusrat awahi kuapishwa??

Okay tufanye ni kweli Mbowe aliwapa ruhusa, je Sheria Ina ruhusu viti maalum kuchaguliwa bila minutes za Kamati kuu iliyowateua na bila barua ya Katibu Mkuu? Au ndio kusema Mwenyekiti ndio anapeleka majina NEC?? Kanuni Gani inaruhusu Hilo.

Tuachane na Hilo..... Kamati kuu ikawavua uanachama na waliokata rufaa ni 6 tu out of 19!! Kwanini CCM iwalinde ilihali Sofia Simba alipovuliwa ubunge ama Lipumba alipowavua wabunge wa CUF hukumi ilitekelezwa na spika ndani ya saa 24 pekee why kwa CHADEMA Inakua ngumu ama Mbowe ana mamlaka kuliko spika hadi azuie hiyo hukumu??

Kwa tafakuri hii ni wazi uwepo wao bungeni ni zao la CCM na sio Mbowe otherwise NEC wangeshavujisha hii issue Ili kukipasua chama kwamba Mbowe kasaliti maamuzi ya Kamati kuu!!
 
Then sina uhakika Kama Mdee wana Courage Hiyo ya kufoji Kwenda Bungeni, tunajua mengi na hatuyasemi
Hii hoja nyepesi sana, kama alimleta Lowassa angeshindwa kuitisha press na kuwasafisha hao wabunge 19?? Yaani kitu Gani kilikua kigumu kama kumleta Lowassa?? Kama aliweza angeshindwa kujustify kupeleka wabunge 19??

Angeweza sana tu kusema tumetolewa bungeni ila tumetumia wabunge 19 Ili wakapiganie mabadiliko ya Sheria za uchaguzi!!! Ingeisha hiyooo!! Eti Mwenyekiti aogope hadi atumie forgery wakati yeye ndio mwenye maamuzi ya mwisho??

Illogical kabisa
 
Ni aibu kubwa chama kushindana na wanawake 19.
Jiwe alipomtimua Madam Jesca na Sofia Simba ubunge wa viti maalum hawakuwa wanawake?? Tena siku hiyo hiyo walifutiwa ubunge!!! Ila mkamuita chuma. Wakifanya CHADEMA inaonekana wivu!!

Nakukumbusha tu CHADEMA ilisimamisha wagombea ubunge wanawake 70.... Ikiwa na maana tungekua na wabunge wengi Wanawake wa majimbo kuliko wanaume!!! Sasa chama kama hiko kinakuaje kinapambana na wanawake??

Tokea uhuru hakuna chama hapa Africa mashariki na kati kimewahi simamisha wagombea wengi wa uchaguzi wanawake kuliko CHADEMA 2020!!!
 
Hapo umezungumzia mtu mmoja.

Ila mimi nazungumzia Chama kizima kushindana na wanawake 19.

Ni aibu kubwa mno.

Wawapotezee tu.

Kwani kuna ubaya gani hao kina mama wakiwa Bungeni. Hakuna madhara yeyote.
 
Inaonekana wewe ni miongoni mwao,unaumia ukiwa wapi?Halima na wenzake ni wasaliti na hivyo hawawezi kustahili msamaha bila wao wenyewe kuueleza umma nani aliwapeleka Bungeni,walipewa kitu gani na CCM hadi watende hayo?
Hata wakitubu hawa hawastahiri msamaha waende wakaunge mkono juhudi za Samia!! Chawa mtahangaika sana lakini hukumu ya hawa covid 19 iliishaandikwa!! Do not uxhaust your oxygen.
 
Hapo umezungumzia mtu mmoja.

Ila mimi nazungumzia Chama kizima kushindana na wanawake 19.

Ni aibu kubwa mno.

Wawapotezee tu.

Kwani kuna ubaya gani hao kina mama wakiwa Bungeni. Hakuna madhara yeyote.
Hoja ya kijinga kudhani jinai ina jinsia
Mbona ccm haikufanya hivyo kwa Sofia Sinba.
Chama kizima kikamuadhimia mwanamke mmoja?
 
Chadema chini ya utawala wa kaskazini hautasonga mbele. Wawaachie wasukuma n.k muone itakavyonawiri 😁
 
Nimeangalia calendar mara tatu kujiridhisha sio siku ya wajinga duniani...
Wasamehewe kwa lipi?
You are joking ama?

Hii nchi ina watu na viatu
19 wasamehewe how why
 
Kwahiyo kauli ya paskali mgombea wa ccm ndio ushahidi?

Nimeshangaa eti bado jamaa anamuamini Paskali Mayalla Huyo jamaa ni mzushi anayeaandika kwa kusoma upepo, ili ikitokea kama alichosema ajifanye alishasema. Kama angekuwa na uwezo wa kujua mambo hayo, alipaswa kujua kuwa angepata kura 2 alipoenda kwenye kura za maoni za ccm.
 
Mwandishi wa habari mwenye kufuata maadili ya kazi, hawezi leta habari za kutunga.

..hili suala lilitakiwa lichunguzwe na DCI na Takukuru.

..kuna hotuba ambayo Mbowe anadai kuna jinai ktk namna ambayo Mdee na wenzake wameingia bungeni.

..pia kuna barua ya Katibu Mkuu kwenda kwa Spika ikieleza kwamba Mdee na wenzake hawana baraka cha Cdm kuwa bungeni.

..Na barua ya Katibu Mkuu inatokana na maamuzi ya kikao cha kamati kuu ya Cdm.

..Haitoshi kusema Mdee na wenzake waliruhusiwa na kiongozi fulani kwenda bungeni. Maamuzi ya kupeleka wabunge wa viti maalum hufanywa na vikao, hayafanywi na kiongozi mmoja wa chama.
 
Siasa si uadui!

Mdee kuwa bungeni si kosa kisheria ila njia alizotumia zaweza kuwa si sahihi,

Kwakuwa Mamlaka ya Bunge imeonekana kuwatambua basi vema hata CHADEMA ikaachana nao ila Kwa Mashrt haya

1. Kutangazia Umma kwamba alikosea na sasa wanaomba msamaha wala si kushindana na CHADEMA Kwenda kwenye mahakama Au kutunishiana msuli na Chama kilichowalea!

2. Watoe michango Kwa Utaratibu wa CHADEMA , wabunge wanachangia kila mwezi hivo watozwe faini ama ya 150M kila mmoja Ambayo ilipwe Kwa awamu Au Kwa mkupuo

3. Hatma yao ya kugombea mwaka 2025 iwe Siri ya Kamati kuu ya Chama

CHADEMA HII NDO TURUFU YA KUONESHA UKOMAVU

Then sina uhakika Kama Mdee wana Courage Hiyo ya kufoji Kwenda Bungeni, tunajua mengi na hatuyasemi

Britanicca
CDM wako mtegoni
 
Back
Top Bottom