Hata kama kuna kiongozi alitoa hiyo 'green light' je, hiyo peke yake inatosha kuwafanya wawe Wabunge?
Kuna taratibu za kuzingatiwa na si takwa la mtu au watu. Walikwendaje Bungeni na Form zikabaki Ufipa?
Hakuna mtu anayeweza kupeleka mtu Bungeni, ingalikuwa rahisi hivyo tusingekuwa na sheria.
Hoja ni je hawa ni Wanachama halali wa chama cha siasa?
Hii ndiyo hoja yao , walifukuzwa bila kuzingatia taratibu.
Hoja yao si kwamba walikwenda vipi Bungeni, ni uhalali wao Bungeni kupitia uanachama.
Kuna mwanasheria mmoja anayejitambulisha kama Baba Mwita, ameandika hoja nzuri sana. Mwita anasema Mahakama iliacha wajibu wake wa kutazama katiba ikaingia katika kutafuta mapungufu ya Katiba.
Mahakama ilitakiwa kuhakikisha je Katiba ya Chadema imefuatwa? Kumbuka katiba imeridhiwa na Msajili
Hoja za akina Halima Mdee ni kutosikilizwa na Baraza kuu, hawakupewa muda wa kufika na upuuzi wa namna hiyo.
Jaji anaposema wajumbe wa CC hawakupaswa kuingia Baraza kuu ni kituko, akina Halima hawakuomba tafsiri ya suala hilo. Mahakama yetu inatia shaka sana na sijui hawa Majaji hupatikana kwa utaratibu gani.
Prof angepisha wengine , amefeli
JokaKuu Pascal Mayalla