Pre GE2025 CHADEMA walia na rafu kuelekea Uchaguzi wa Mwenyekiti. Team Lissu waliwa vichwa ili kumpa ushindi Mbowe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Mambo yanakuwa matamu huko, Hilda ameweka bandiko kupitia account ya X kuwa mpaka CHADEMA yanatokea mambo ya hovyo ambayo kila wakati wanayapinga wakifanya CCM. Katika orodha hii inasemekana team Lissu kabakishwa mmoja tu, je tutegemee matokeo tofauti hapo kesho.

Kama wao kwa wao wanafanyiana haya kuna mwanga wa kuwa na upinzani wa kweli unaokicheki kweli chama tawala?

 
Aliyeelewa tafadhari anieleweshe wakuu...
 
Hamna chama cha upinzan hapa! Hili ni genge la wasaka tonge🚮🚮
 
CHADEMA lazima kilindwe kwa hali yoyote ile hatuwezi kuachia wahuni waingie na kuharibu CHAMA kilichojengwa kwa jasho la damu.
 
Aliyeelewa tafadhari anieleweshe wakuu...
Ni majina ya watia nia kugombea ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA. Inasemekana watia nia walioonyesha kuwa upande wa Lissu wote wamefyekelewa mbali isipokuwa mmoja tu (Pambalu). Kwa hivyo Kamati Kuu itajaa watu wa Mbowe peke yake. Ndiyo maana kelele zinapigwa kila upande kwamba hata huo uchaguzi hapo kesho si ajabu ukagubikwa na mauzauza ya wazi kama yaliyotokea kwenye uteuzi wa wagombea wa Kamati Kuu.

Chama cha DEMOKRASIA na maendeleo indeed! 🚮
 
Mnyika naye anafanya mambo kama ya TAMISEMI kuengua wagombea.

Hapo CHADEMA in the future haiwezi kuwa na moral authority ya kulalamikia uenguaji pindi serikali ya CCM itakapokuwa inawaengua kwenye kugombea serikali za mitaa n.k
Labda wamepewa maagizo 😄 toka juu

Ova
 
Nimeshangaa sana Mbowe kawaje, sasa unamuacha Rose Mayemba alafu unweka random women tu ambao hata kwenye struggle za chama hatujawahi kuwaona.

Mfano unamkata Twaha Mwaipaya alafu unamuweka Assenga? Hivi Mbowe nani atakayempigia kampeni za urais 2025 kama ndio watu anaojaza ni liabilities.

Bora angekua anaweka watu wenye uwezo zaidi kuliko kujaza liabilities ili tu kukomoa upande wa Lissu.

Yaleyale ya kumteua Mashinji ili kumkomoa Mnyika kisa alimpinga Lowassa!!
 
Mbali na siasa Mnyika ana shughuli gani?

Au na yeye ni miongoni mwa wanaolishwa na Mbowe kwa kupitia ruzuku?
 
Chama Cha ovyo, naona mzee wa Machame kikimfia rasmi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…