CHADEMA walikosea kukubali kuichoma nchi wanayotaka kuiongoza

Sasa waliotawala nchi wamechukua hatua stahiki za kulinda miundombinu yake, na tumeiona faida yake juzi 77 hakuna kima alojaribu kutoa pua yake

Miundombinu haiwezi kulindwa kwa mtutu nyie mlikua mnalinda madaraka mliyopata kwa
Kupora
Watanzania wameona ajabu Oct29 2026, kumbe kuna watu hawawezi kutofautisha kati ya mali za umma za watanzania wote wakiwemo wao na mali za Samia Suluhu Hassani, kati ya mali ya CCM na mali ya watanzania wote. wao Walichoma jumlajumla hata mabasi yao wanayotumia kwenda kariakoo kununua ngogwe. Mtu anatangaza maandamano siku ya 77 wakidhani kuwa wanawakomoa CCM na Samia ambae baada ya miaka 4 ijayo anaondoka zake nyumbani kwake Kizimkazi na kutuachia nchi yetu. Watu wa hivyo tutakuwa mataahira kama tukiwakabidhi nchi kwa hiari yetu.

Walidhani watu wataichukia serikali kumbe wanaichukia chadema.

Hebu ona sasa wanarudi kulekule walikokosea. Heche anafaidi

View: https://youtu.be/2kfIBqqcQTY?si=TAVh_VVgYbTx8Upu
 
Exactly!!! kwasababu tunaangalia tulipojikwaa sio tulipoangukia. Wakati SSH ni Makamu wa Rais hakuna mtu alimpinga na kusema hapana; ujio wake kwenye kiti cha uMakumu ulikuwa na baraka zote za JPM na ulifuata misingi ya Kikatiba. Shida ilikuja mara tu JPM kufariki na nani azibe nafasi yake Kikatiba. Hapo ndipo yakajitokeza makundi ya wanasiasa ndani ya CCM, makundi ya dini ya Kikristu, hasa Wakatoliki na Kanisa la Ufufuo ambalo mkuu wake ni msukuma kama JPM na chadema wakaiona na kutaka kuitumia fursa kwenye mnyukano huo wa wanaCCM wafuasi wa JPM, makanisa, wanaCCM wafuasi wa SSH, wadau walioapa kuilinda Katiba ya nchi na chadema ambao wanatumika tu kama farasi wa vita. Ndio maana Mh. Lissu kanasa kwenye mtego ambao sio wake kindakindaki, na waliomfanya anase kwenye mtego wanahangaika sana huku na huko ndani na nje kutafuta njia za kumnasua baba wa watu waliomwingiza mkenge.

Sisi wenye akili timamu tunajua shida ya SSH haitokani na kutuongoza vibaya kama Rais, bali shida nyingine tu za maslahi ya kifisadi, ulaji na kupoteza fursa mbalimbali ambazo walikuwa wakizipata chini ya JPM ama kama Rais, kama rafiki, kama mkristo, kama Mkatoliki, kama msukuma au kama Rais mtanganyika. Hatudanganyiki ng'oo.

..kila Rais mpya anapoingia lazima kuna kundi litapata, na kuna kundi litakosa.

..Na kundi litakalokosa lazima litaleta mashinikizo fulani fulani.

..Na kila Rais lazima afanye mabadiliko na kuleta ahueni ktk mapungufu ya mtangulixi wake.

..Mzee Mwinyi alipoingia alikuta nchi ipo ktk mkwamo wa kiuchumi, na uhaba mkubwa wa bidhaa muhimu.

..Mzee Mwinyi alichukua hatua sahihi za kupunguza makali ya kiuchumi aliyoyakuta wakati anakabidhiwa usukani.

..Mama Abduli naye aliingia nchi ikiwa imekwama kisiasa, na ikiandamwa na matukio ya kidhalimu na kinyama dhidi ya wakosoaji wa serikali.

..Sasa kilichopaswa kufanyika ni kuchukua hatua sahihi kurekebisha makosa ya mtangulizi wake.

..Kwa kusema ukweli Mama Abduli alitoa kauli na kuchukua hatua ambazo zilileta matumaini.

..Ni bahati mbaya kwamba kabla hatujaanza kupata matokeo chanya akarudisha mambo machafu ya mtangulizi wake, na wakati mwingine hata kuzidisha udhalimu.

..Mama Abduli alicheza na amani ya nchi yetu, matokeo yake akasababisha mauaji mabaya ya kihistoria OCT 29.
 
Hawa wamekwamba, vyama hivi vikikosa ruzuku habari yao imekwisha

View: https://youtu.be/p1WUnOlWjUc?si=zHks_nUOSCmgJZvE
 
..Chadema hawana ruzuku, lakini wana HOJA / AGENDA inayogusa hisia za watu.

..makosa ya Mama Abduli ndiyo yanayofanya Chadema waungwe mkono.

..kama Mama Abduli asingeiga udhalimu wa Jpm, na kuuwa watu Oct 29, Chadema wangekosa hoja.
Samia ndiye alieshupaza shingo alipoonywa na wanaCCM wenzake asifungulie vyama vya siasa vilivyofungiwa na Magufuli mapema hivyo. Samia alikuwa akitafuta umaarufu kimataifa kama mtu wa demokrasia. Bahati mbaya SAMIA anakubwa na hasira za Lissu kupigwa risasi. Baada ya risasi zote zile, ulemavu aliosababishiwa na familia yake kuwepo nje ya nchi Lissu anajikuta na kujiona hana thamani tena wala cha kupoteza hapa nchini, bora tukose wote. Hata Nchi ikochomwa moto yote hana cha kupoteza.
 
..Ni kweli mwanzoni Ssh alikubali kuachana na itikadi za Jpm akaleta 4R.

..hali ilielekea kutulia na kuleta matumaini.

..baadae Ssh akabadili muelekeo na kuanza kuteka, kupoteza watu, na kukataa mabadiliko.

..muelekeo huo mpya wa Ssh ndio ukasababisha mauaji ya OCT 29.

..Ssh amekwenda mbali zaidi ya Jpm kwa kuuwa mpaka WATOTO, halafu anadai ilitumika nguvu sahihi.
 
Hakuna chama kipya kinakuja madarakani pamoja na ofisi zake za serikali, majeshi, polisi, mahakama, barabara, hospitali, mahakama na majaji wake wapya. Watatumia miundombinu hiihii na rasilimali watu iliyopo, maana miundombinu hii sio mali ya chama kilichoko madarakani wala Rais, ni mali ya watanzania hata wale ambao hawajazaliwa. Kuichoma moto na kuiharibu sio sawa na kosa kubwa sana.

Hakuna mahali popote nimesikia chama cha chadema kimekerwa na kuharibiwa kwa mali/kodi za watanzania katika vurugu za Octoba 29, 2025 na siku zilizofuata siku hiyo. Hii ni kuonyesha kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya wachomaji na chadema, la sivyo, walifurahishwa na uchomaji ule.

Hayati Reginald Mengi (RIP) alikuwa miongozi mwa watu wa kwanza nchini kumiliki vyombo vya habari. Kila wakati unapokaribia uchaguzi mkuu alikuwa akitumia vyombo vyake vya habari kutuonyesha watanzania ubaya wa kuvunjika kwa amani kunakoweza kuletwa na vurugu za uchaguzi na vyama vya upinzani. Nadhani alikuwa mwanaCCM lakini alifanyahivyo kwa kusukumwa na umuhimu wa amani na utulivu katika uwekezaji wake nchini. Kwenye vurugu mitaji inapotea.

Mzee Mengi alikuwa anatuonyesha vita na mauaji ya Rwanda, Burundi na Somalia kwenye kituo chake cha TV. Wapinzani walimlaumu sana kuwa anawatisha watanzania wasivichague vyama vya upinzani. Leo Mengi hayupo lakini nchi ilichomwa moto na watanzania wenzetu wamepoteza maisha wakati wa uchaguzi sawasawa na hofu na tahadhali yake.

Kuchoma au kuunga mkono kuchoma nchi/malalo yetu ni kosa la kiufundi ambalo chadema walilifanya katika harakati zao za kisiasa. Wamekirudisha chama kilometa nyingi sana nyuma. Leo hii chadema kinaogopwa na wananchi kama chama kisichowatakia mema wananchi na taifa. Mwananchi ambae amepoteza mtoto wake kwenye vurugu zile anawalaumu chadema, waliokosa matibabu wakati wa vurugu wanailaumu chadema, waliokosa usafiri wa mwendokasi kwakuwa umechomwa moto wanailaumu chadema, waliokosa ajira kwakuwa sheli na malori waliyokuwa wameajiliwa yamechomwa moto wanailaumu chadema; watoto waliokosa masomo kwa kule kufungwa kutokana na vurugu wanailamu chadema; walioshindwa kutoka nje kujitafutia riziki kwasababu ya vurugu wanailamu chadema, waliofilisika kwasababu maduka yao yaliporwa kwenye vurugu wanailaumu chadema na viongozi wao akina heche; wanaokosa huduma kwenye ofisi za serikali za mitaa na kata zilizochomwa wanailaumu chadema; chadema, chadema, chadema.

Matokeo yake ni nini, leo hii ni rahisi sana kuyazuia maandamano ya chedema kuliko wakati mwingine wowote. Wakiitisha maandamano wananchi wooote wenye akili timamu wanabaki majumbani mwao na biashara zote zinafungwa kupisha maandamano ya chadema. Barabara na mitaa inabaki tupu, na hata wanaojitafutia riziki zao kwa kutoka kila siku kama bodaboda, daladala, mama lishe na wauza mboga wanakubali kukaa ndani na njaa ili kunusuru roho zao dhidi ya chadema na polisi. Chadema Wakiendelea kufanya hivi kwa muda mrefu watanzania hawa waliozoea amani wataifuta chadema vichwani mwao na kuwalinganisha na magaidi au watia hasara au wapenda vurugu au wapenda vita.

chadema kitabakia kuwa chama cha watu na vijana wapenda vurugu/wabwia unga, wavuta bangi na wasiokuwa na chakupoteza. Hata kwenye vurugu zile ni watoto wasiokuwa na chakupoteza tu ndio waliathirika; hakukuwepo na watoto wa wanasiasa, wafanyabiashara, viongozi, maprofesa wala watumishi. Wengi wao walikuwa ni watoto wa masikini kabisa waliotolewa kafara na watu wanaowaamini na kuwaheshimu sana kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiroho. Watu ambao walikuwa wanajua kuwa vijana wale kwa kuchoma mali za umma na hata zile zinazolindwa kwa bunduki lazima wangeuliwa na kujeruhiwa kwa wingi. Hesabu zao zilikuwa wangeuliwa wachache tu na wengine watafanikisha lengo lao kwakuwa walijua kuwa polisi wengi walikuwa kwenye malindo ya kulinda uchaguzi. Bahati yao mbaya ni kwamba mikoa mingi na watanzania wengi hawakujitokeza kuunga mkono vurugu zao kama walivyokuwa wamekusudia. Hii ilisababisha Vijana waleta vurugu wakaminywa wote na kunyanyua mikono, bila hivyo serikali na watanzania wote tungekuwa tunashuhudia magofu kila kona. Yaani tungerudi nyuma miaka 50 kimaendeleo.

Chadema imetumika tu kama mtu wa mwisho/loud speaker nyuma ya wapanga mipango wakubwa wenye maslahi ya kibiashara nyuma ya pazia. Vurugu tunazoziona msingi wake mkuu sio demokrasia, bali biashara haramu ambazo zilivurugwa na utawala mpya wa Rais samia. Mpango ambao ulianza kwa kumnyang'anya Mbowe chadema ili kitumike kama jukwaa lao la kufanikisha kile wanachokidai/maslahi.

Samia amevuruga biashara zao haramu nyingi sana. Kulikuwa na mipango kabambe ambayo ilikuwa inafanyika wakati wa JPM, ambayo ghafla iliingia hitilafu baada Rais JPM kufa ghafla ambayo hawakuwa na uhakika kama Samia angeruhusu waendelee nayo kama ilivyo au Samia angehamia kwa watu wengine kama Rostam, nk.

Vita hii sio ya kidemokrasia hata kidogo, ni vita ya maslahi.
Nguo chakavu unazichoma moto ili ununue mpya.
 
..Ni kweli mwanzoni Ssh alikubali kuachana na itikadi za Jpm akaleta 4R.

..hali ilielekea kutulia na kuleta matumaini.

..baadae Ssh akabadili muelekeo na kuanza kuteka, kupoteza watu, na kukataa mabadiliko.

..muelekeo huo mpya wa Ssh ndio ukasababisha mauaji ya OCT 29.

..Ssh amekwenda mbali zaidi ya Jpm kwa kuuwa mpaka WATOTO, halafu anadai ilitumika nguvu sahihi.
Chadema ilikosea sana tena sana kukubali chama chao kutumiwa na watu wa dini, wafanyabiashara haramu, wanaCCM wenye agenda zao, wanaharakati na magaidi. Chadema ilipoteza udhibiti wa kuwa chama cha siasa na kikavaa sura ya kigaidi kiasia na kukubaliana na watu wenye ugomvi wao binafsi na SSH, Kikwete na Rostam na magaidi wenye agenda zao za kupata rasilimali za tz.

Chadema baada ya kuingiwa na pepo hilo baya la kidini, ugomvi wa wanaCCM wenyewe, wanaharakati, wafanyabiashara haramu, vibaraka na magaidi ikasahau na kuachana na ahueni zoote walizopewa na SSH, na wakazitupilia mbali 4Rs za SSH kwasabu waliahidiwa na wamepata njia nyingine fupi na haraka ya kuiondoa CCM na SSH. Ukweli njia hii waliingizwa mkenge, maana ni njia hatari sana iliyofeli vibaya sana ambayo inahatarisha hata uhai wa chama chenyewe.

Chadema hawakuchanganya na akili zao pale walipoambiwa tuchome mali za wananchi wenzao zilizotokana na kodi zao, misaada, mikopo na juhudi binafsi. Walichoma huduma na ajira za watanzania wenzao kama njia ya wao kwenda Ikulu. Yaani strenthening the weakest by weakening the strongest.

Kuna watanzania ambao wanakosa huduma, ajira, na mitaji kwakuwa chadema na wenzao wamezichoma, kupora na kuziharibu. Kuna watanzania walipoteza maisha kwasababu tu walishindwa kutoka kwenda kutibiwa au walikuwa hoapitalini lakini hakukuwa na watumishi wa afya waliozuliwa na vurugu. Viwanda na taasisi kama shule na vyuo vilifungwa kutokana na chadema kuleta fujo. Hasara ilikuwa huge huge huge.

Hebu chadema iitishe maandano waone wangapi watawaunga mkono, kimekufa. Hakiwezi kutumia maandamano tena kama njia ya kisiasa.
 
..wananchi wanauliza Ssh wa 4R amekwenda wapi?

..wananchi hawamtaki Ssh anayeteka, kutesa, na kupoteza watu.

..Maraisi wote wa Tanzania hakuna aliyesababisha mauaji ya WATOTO.

..Ssh ametukosea sana Watanzania.
 
Hakuna chama kipya kinakuja madarakani pamoja na ofisi zake za serikali, majeshi, polisi, mahakama, barabara, hospitali, mahakama na majaji wake wapya. Watatumia miundombinu hiihii na rasilimali watu iliyopo, maana miundombinu hii sio mali ya chama kilichoko madarakani wala Rais, ni mali ya watanzania hata wale ambao hawajazaliwa. Kuichoma moto na kuiharibu sio sawa na kosa kubwa sana.

Hakuna mahali popote nimesikia chama cha chadema kimekerwa na kuharibiwa kwa mali/kodi za watanzania katika vurugu za Octoba 29, 2025 na siku zilizofuata siku hiyo. Hii ni kuonyesha kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya wachomaji na chadema, la sivyo, walifurahishwa na uchomaji ule.

Hayati Reginald Mengi (RIP) alikuwa miongozi mwa watu wa kwanza nchini kumiliki vyombo vya habari. Kila wakati unapokaribia uchaguzi mkuu alikuwa akitumia vyombo vyake vya habari kutuonyesha watanzania ubaya wa kuvunjika kwa amani kunakoweza kuletwa na vurugu za uchaguzi na vyama vya upinzani. Nadhani alikuwa mwanaCCM lakini alifanyahivyo kwa kusukumwa na umuhimu wa amani na utulivu katika uwekezaji wake nchini. Kwenye vurugu mitaji inapotea.

Mzee Mengi alikuwa anatuonyesha vita na mauaji ya Rwanda, Burundi na Somalia kwenye kituo chake cha TV. Wapinzani walimlaumu sana kuwa anawatisha watanzania wasivichague vyama vya upinzani. Leo Mengi hayupo lakini nchi ilichomwa moto na watanzania wenzetu wamepoteza maisha wakati wa uchaguzi sawasawa na hofu na tahadhali yake.

Kuchoma au kuunga mkono kuchoma nchi/malalo yetu ni kosa la kiufundi ambalo chadema walilifanya katika harakati zao za kisiasa. Wamekirudisha chama kilometa nyingi sana nyuma. Leo hii chadema kinaogopwa na wananchi kama chama kisichowatakia mema wananchi na taifa. Mwananchi ambae amepoteza mtoto wake kwenye vurugu zile anawalaumu chadema, waliokosa matibabu wakati wa vurugu wanailaumu chadema, waliokosa usafiri wa mwendokasi kwakuwa umechomwa moto wanailaumu chadema, waliokosa ajira kwakuwa sheli na malori waliyokuwa wameajiliwa yamechomwa moto wanailaumu chadema; watoto waliokosa masomo kwa kule kufungwa kutokana na vurugu wanailamu chadema; walioshindwa kutoka nje kujitafutia riziki kwasababu ya vurugu wanailamu chadema, waliofilisika kwasababu maduka yao yaliporwa kwenye vurugu wanailaumu chadema na viongozi wao akina heche; wanaokosa huduma kwenye ofisi za serikali za mitaa na kata zilizochomwa wanailaumu chadema; chadema, chadema, chadema.

Matokeo yake ni nini, leo hii ni rahisi sana kuyazuia maandamano ya chedema kuliko wakati mwingine wowote. Wakiitisha maandamano wananchi wooote wenye akili timamu wanabaki majumbani mwao na biashara zote zinafungwa kupisha maandamano ya chadema. Barabara na mitaa inabaki tupu, na hata wanaojitafutia riziki zao kwa kutoka kila siku kama bodaboda, daladala, mama lishe na wauza mboga wanakubali kukaa ndani na njaa ili kunusuru roho zao dhidi ya chadema na polisi. Chadema Wakiendelea kufanya hivi kwa muda mrefu watanzania hawa waliozoea amani wataifuta chadema vichwani mwao na kuwalinganisha na magaidi au watia hasara au wapenda vurugu au wapenda vita.

chadema kitabakia kuwa chama cha watu na vijana wapenda vurugu/wabwia unga, wavuta bangi na wasiokuwa na chakupoteza. Hata kwenye vurugu zile ni watoto wasiokuwa na chakupoteza tu ndio waliathirika; hakukuwepo na watoto wa wanasiasa, wafanyabiashara, viongozi, maprofesa wala watumishi. Wengi wao walikuwa ni watoto wa masikini kabisa waliotolewa kafara na watu wanaowaamini na kuwaheshimu sana kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiroho. Watu ambao walikuwa wanajua kuwa vijana wale kwa kuchoma mali za umma na hata zile zinazolindwa kwa bunduki lazima wangeuliwa na kujeruhiwa kwa wingi. Hesabu zao zilikuwa wangeuliwa wachache tu na wengine watafanikisha lengo lao kwakuwa walijua kuwa polisi wengi walikuwa kwenye malindo ya kulinda uchaguzi. Bahati yao mbaya ni kwamba mikoa mingi na watanzania wengi hawakujitokeza kuunga mkono vurugu zao kama walivyokuwa wamekusudia. Hii ilisababisha Vijana waleta vurugu wakaminywa wote na kunyanyua mikono, bila hivyo serikali na watanzania wote tungekuwa tunashuhudia magofu kila kona. Yaani tungerudi nyuma miaka 50 kimaendeleo.

Chadema imetumika tu kama mtu wa mwisho/loud speaker nyuma ya wapanga mipango wakubwa wenye maslahi ya kibiashara nyuma ya pazia. Vurugu tunazoziona msingi wake mkuu sio demokrasia, bali biashara haramu ambazo zilivurugwa na utawala mpya wa Rais samia. Mpango ambao ulianza kwa kumnyang'anya Mbowe chadema ili kitumike kama jukwaa lao la kufanikisha kile wanachokidai/maslahi.

Samia amevuruga biashara zao haramu nyingi sana. Kulikuwa na mipango kabambe ambayo ilikuwa inafanyika wakati wa JPM, ambayo ghafla iliingia hitilafu baada Rais JPM kufa ghafla ambayo hawakuwa na uhakika kama Samia angeruhusu waendelee nayo kama ilivyo au Samia angehamia kwa watu wengine kama Rostam, nk.

Vita hii sio ya kidemokrasia hata kidogo, ni vita ya maslahi.
Haya umeandika kutupa taarifa sisi tusio na vyama au umeandika kuwapa taarifa wakina nani?
 
..wananchi wanauliza Ssh wa 4R amekwenda wapi?

..wananchi hawamtaki Ssh anayeteka, kutesa, na kupoteza watu.

..Maraisi wote wa Tanzania hakuna aliyesababisha mauaji ya WATOTO.

..Ssh ametukosea sana Watanzania.
Samia kazima uasi, dunia nzima inampongeza mwanamke shupavu aliyejaribiwa na wahuni akawashinda. Wanaomlau ni wale walioshindwa kuiangusha serikali na waliofadhili uangushaji huo. Kama serikali ingeanguka waliokufa mngewaita mashujaa wenu. Sasa mnajilaumu kwa kuwatoa kafara bure vijana wa watu. YOU feel guilty.
 
..wananchi wanauliza Ssh wa 4R amekwenda wapi?

..wananchi hawamtaki Ssh anayeteka, kutesa, na kupoteza watu.

..Maraisi wote wa Tanzania hakuna aliyesababisha mauaji ya WATOTO.

..Ssh ametukosea sana Watanzania.
4Rs zipo palepale. Kama hakuna maridhiano hakuna Katiba, fullstop!! Serikali haitishiwi nyau, kasomeni Katiba.
 
..4R aliziacha akahamia kwenye ubabe.

..Na ubabe ndio uliosababisha akajikuta ameuwa mpaka watoto Oct 29.
 
Mbona mnapenda kuifananisha Tz nchi iliyoko Afrika na Marekani, Canada, UK, Oman, Bangaladesh,....? Linganisha tz na nchi za Afrika tena chini ya Jangwa la Sahara. Mnaonesha wazi kuwa tz iko mbele sana Afrika. INA ligi bora Afrika, ina reli ya umeme, ina amani na utulivu, umeme kila kitongoji, hospitali kila kijiji, shule kila kitongoji, sekondari kila Kata, maji yanaenda kila kona, barabara bwerere. Ukiichoma nchi yetu tutakula sahani moja na wewe. Hutana mchezo kwenye hili, tutakutosa majini uliwe na papa badala ya kutuzamisha wote.
Leteni katiba mpya na tume huru , nitapigia hata mti kura yangu siwezi ielekeza mboga mboga

Kinazungumzwa kwasababu 2 kuu. Kwanza kilichoma mali ya umma na binafsi, pili kimetumika kumpora Mbowe, KKKT chama chake na kukitumia vibaya kupin serikali.
 
Kama alikumbia wewe tu na yeye chumbani sawa, na tutahoji mlikuwa mnafanya nini, ila kama ni majukwaani tulisikia No reform no election
Endelea kusikia hivyo ila wengi tuliona na kusikia hivyo
 
Back
Top Bottom