CHADEMA walikosea kukubali kuichoma nchi wanayotaka kuiongoza

Hamuwezi kutatua tatizo kwa kujidanganya kwamba halipo.
Kama wewe hujatejwa basi waliotekwa wote wana shinda zao. Baki hivyohivyo kaka kutekwa sio kuzuri, jilinde.

Nitakusaidia baadhi ya sababu zinazoweza kusababishwe utekwe na kupotea ili uviepuke:
1. Ushirikina. Kuna watu wanatafuta viungo vya binadamu kwasababu za kishirikana
2. Wivu: kuna watu wanapotea kwasababu za mapenzi. acha kugombania wapenzi.
3. Biashara: Mkidhulumiana mnaweza mkatekana kama kulipizana
4. Uongizi: unaweza kutekwa kama mkigombea nafasi ya uongozi kwenye chama chenu au uongozi mwingine.
5. Kinyongo: Mafanikio yako yanaweza kuwakera watu.
6. Afya ya akili: Kuna watu wanajiteka wenyewe au kupotea kwa ukosefu wa afya ya akili
7. Kutafuta sababu: Unamteka mtu ili ionekane mpinzani wako ndiye kamteka ili apate matatizo kutoka kwa watu wengine baada ya wewe kumshindwa.
8. Usalama: unaweza kutekwa kwasababu za kiusalama wako au wa mtu mwingine
9. Vibaraka wakigundulika hawaponi
10. Visasi: Ukimteka ndugu yangu nitakuteka au kumteka ndugu yako.
11. Kufichua siri muhimu: kutoa nje siri za jando kwakuwa unazifahamu na umeasi.

OGopa sana mambo haya hapo juu
 
Hivi unaelewa dhana ya katiba bora ni nini?
Demokrasia na haki ni vitu ghali sana, hakuna taifa la Afrika linaloweza kuzimudu gharama zake. HATA chadema wanadhani demokrasia ni chama tawala kushindwa uchaguzi na chama cha upinzani kushinda. Looo

Hebu fikiria taifa masikini linatumia 700b kugharania uchaguzi, pesa ambayo ingetosha kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wasomo vyuoni. Halafu chama kimoja cha siasa kinakwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi na mahakama inakipa ushindi na kufuta matokeo na uchaguzi urudiwe baada ya miezi 3 na kutumia 700b nyingine kurudia uchaguzi. Nchi hiyo itadumaa tu hata iweje.

NYERERE hakuwa mjinga kuja na Katiba ya hivi ya 1977. Anaetaka kuibadili atafakari sana na sana ili aone alipokosea Nyerere na wenzake kuandika katiba ya hivi. Hawakuwa wajinga hata kidogo.

Demokrasia pana inaruhusu watu kuandamana kila siku badala ya kuzalisha kila siku. Demokrasia na haki itakutaka uwe na majaji wengiii na mahakama nchi nzima, polisi wengiii wa upelelezi, magereza mengii na wafungwa wengiii
 
Naomba majina ya hawa na utueleze huko CHADEMA wana vyeo gani.
20260522_144752.jpg
 
Yaani ndiyo hamnazo kabisa. Nchi gani kila kitu kiko sawasawa kabisa? Exposure zenu zina mashaka. Mimi kazi yangu ni fundi wa kuchomelea vyuma, Lissu akiwa Rais ataniongezea nini kwenye kazi yangu?

Mnadanganywa kama mazuzu
Hujui hata Impact ya siasa kwenye maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida halafu unaita watu hamnazo. Kazi kweli kweli.
 
Kama wewe hujatejwa basi waliotekwa wote wana shinda zao. Baki hivyohivyo kaka kutekwa sio kuzuri, jilinde.

Nitakusaidia baadhi ya sababu zinazoweza kusababishwe utekwe na kupotea ili uviepuke:
1. Ushirikina. Kuna watu wanatafuta viungo vya binadamu kwasababu za kishirikana
2. Wivu: kuna watu wanapotea kwasababu za mapenzi. acha kugombania wapenzi.
3. Biashara: Mkidhulumiana mnaweza mkatekana kama kulipizana
4. Uongizi: unaweza kutekwa kama mkigombea nafasi ya uongozi kwenye chama chenu au uongozi mwingine.
5. Kinyongo: Mafanikio yako yanaweza kuwakera watu.
6. Afya ya akili: Kuna watu wanajiteka wenyewe au kupotea kwa ukosefu wa afya ya akili
7. Kutafuta sababu: Unamteka mtu ili ionekane mpinzani wako ndiye kamteka ili apate matatizo kutoka kwa watu wengine baada ya wewe kumshindwa.
8. Usalama: unaweza kutekwa kwasababu za kiusalama wako au wa mtu mwingine
9. Vibaraka wakigundulika hawaponi
10. Visasi: Ukimteka ndugu yangu nitakuteka au kumteka ndugu yako.
11. Kufichua siri muhimu: kutoa nje siri za jando kwakuwa unazifahamu na umeasi.

OGopa sana mambo haya hapo juu
Unanichukulia mimi ni mtoto wa kindergarten? Huu ukasuku mliokaririshwa huko CCM shirikishaneni wenyewe huko lumumba. Hata Polepole alikuwa ana hoja kama hizi zako jee leo hii yuko wapi? Kama mamia ya watu waliotekwa na kupotezwa ni kwa sababu hizo ulizotaja ambazo zote hizo ni jinai lakini hakuna hata moja ambayo polisi wamewakamata wahusika basi hatuna jeshi la polisi bali tuna makada wa CCM wanaovaa crown tu.
 
Naomba majina ya hawa na utueleze huko CHADEMA wana vyeo gani.
View attachment 3629739
Hata sijui unataka kusema nini, lakini inafahamika kuwa kocha hachezi uwanjani. Baafa ya kupanga, kuhamasisha, kufundisha na kulipa wachomaji viongozi wakajivunja ili wasionekane eneo la tukio. Walilopoka, kutukana, kutamka na kusonya ili wakamatwe ili wasiwepo huru siku ya tukio wao na wapendwa leo. Ndio maana leo unaona marundo ya makaratasi na vitabu vya sheria vya kutafutia tundu (technicalities) za kujitenga na tukio la uchomaji. It is too late, hatukubali upuzi wa kiufundi wa kukwepa hatia utumike hapa wakati mazingira yote yako wazi kuwa ni chadema imechoma.
 
Hamna akili ya kuendesha nchi. Huwezi kuleta maisha bora kwa kuchoma nchi na kuwatishia wananchi. Kila unapotishia kuandamana wananchi wanaacha shughuli zao zote za kujiingizia kipato, safari, starehe na hata kuingilia ratiba za masomo za wanafunzi mashuleni na vyuoni. Nani anakubali watu wapuuzi kama nyie. Mnadhani mnamkomoa Samia kumbe mnakomoa wananchi na mnapoteza imani kwa wananchi wenye akili timamu.

Kila mkiitisha maandamano watanzania wanajificha uvunguni kuepuka magaidi na upotevu wa maisha na mitaji yao. Akili hamna, tafuteni mbinu nyingine kuliko hii ya kipuuzi.
 
Hata sijui unataka kusema nini, lakini inafahamika kuwa kocha hachezi uwanjani.
Huwezi kujua sababu ni zezeta.
Baafa ya kupanga, kuhamasisha, kufundisha na kulipa wachomaji viongozi wakajivunja ili wasionekane eneo la tukio.
Nani aliyepanga?

Nani aliyefundisha?

Walifundisha /walifundishwa nini?

Ushahidi wa hayo mafunzo wa picha, sauti , video upo wapi?

Ushahidi wa matukio hayo kwenye maeneo uliyotaja upo wapi?

Kwanini tume iliyoitwa ya kuchunguza ilifanya uchunguzi kwa umma ila ripoti ikafichwa kwa umma?
Walilopoka, kutukana, kutamka na kusonya ili wakamatwe ili wasiwepo huru siku ya tukio wao na wapendwa leo.
Kulopoka ni nini??

Kutukana nini?

Kusonya nini?

Unamkamata mtu bila uthibitisho au kosa?

Unazifahamu taratibu za kumkamata mtu kwa mujibu wa PGO?
Ndio maana leo unaona marundo ya makaratasi na vitabu vya sheria vya kutafutia tundu (technicalities) za kujitenga na tukio la uchomaji.
Hayo marundo yako wapi?

Hebu weka hapa picha za hayo marundo?

Kwanini "findings" za ile iliyoitwa tume ya kuchunguza vurugu waliishia kusoma tu hizo "findings" na ripoti halisi imefichwa ilhali ilitumia pesa za walipa kodi?

Hayo marundo ya vitabu aliyokuja nayo Lissu ulitaka afanye rejea kutoka wapi na gerezani hakuna internet?

Ulitaka asije na rundo la vitabu wakati mnamnyima haki yake kisheria kuwasiliana faragha na mawakili wake?
It is too late, hatukubali upuzi wa kiufundi wa kukwepa hatia utumike hapa wakati mazingira yote yako wazi kuwa ni chadema imechoma.
Too late kwa nani? too late kwa Samuya muuaji aliyesema amechaguliwa kwa 98 % halafu bado anaomba maridhiano?

Too late kwa matokeo ya kura ambayo hayajawekwa kwenye tovuti ya tume kama sheria inavyotaka?

Too late kwa mtu muongo aliyesema uchaguzi watu wamepiga kura milioni 32 katikati ya mabomu, risasi na damu ilhali chaguzi zote ambazo hazikuwahi kuwa na vurugu haziikufikia viwango vingi vya wapiga kura?

Too late kwa mtu aliye katika rada za Senatw ya US , Bunge la Ulaya , na sasa Commonwealth?

Too late kwa mtu anayeteka , kuua, kupoteza wakosoaji wake.?

Too late kwa muuaji anayetumia dola kukandamiza vyombo na uhuru wa habari?

Huo ushahidi wa CHADEMA kuchoma ndio ninaoutaka uweke hapa..
 
Tunachofanya ni kuendelea kuboresha huduma kwa watanzania na kuilinda nchi, watu na mali zao. Tutaongeza askari, technolojia na risasi zaidi. Vibaraka hawatashinda kanwe. Tumejifunza kutoka Kenya, Somalia, Libya, DRC, Iraq, Mali, Niger, Burkina Faso na kwingineko ambako vijana walihadaiwa na wahuni. Kwetu ni kata funua kwa cheche za moto zote kabla hazichoma taifa lote.
Hayo yote fanyeni lkn msipoacha kuiba chaguzi, kubambika kesi, kuteka na kuua. Juhudi zenu ni sawa na kujilisha upepo. Sisi hatutapoa, hakuna kuchelewa wala kuwahi.
 
Unanichukulia mimi ni mtoto wa kindergarten? Huu ukasuku mliokaririshwa huko CCM shirikishaneni wenyewe huko lumumba. Hata Polepole alikuwa ana hoja kama hizi zako jee leo hii yuko wapi? Kama mamia ya watu waliotekwa na kupotezwa ni kwa sababu hizo ulizotaja ambazo zote hizo ni jinai lakini hakuna hata moja ambayo polisi wamewakamata wahusika basi hatuna jeshi la polisi bali tuna makada wa CCM wanaovaa crown tu.
Mnatulazimisha watanzania tuione katiba ndio chanzo cha shida zetu, wazembe sana. Katiba hiihii ndiyo iliyotuunganisha makabila yote na dini zote tuweze kuishi pamoja. Katiba imewapatia haki makabila mengine kumiliki ardhi za makabila mengine bila kipingamizi, Katiba ambayo imejenga vijiji, shule kila kijiji, barabara na Kiswahili kama lugha ya taifa.

Katiba mbaya eti kwakuwa imebana njia kwa wehu kwenda Ikulu bila sera zinazoeleweka zaidi ya kuorodhesha kero za watanzania ambazo bado kupewa majibu kutokana ukosefu wa misuli minene ya fedha. Unadhani watanzania ni weupe vichwani kiasi hicho?
 
Tatizo ni CCM kukoma kuwa chama cha siasa na kuwa genge masilahi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendekeza utawala wa kifisadi na kidhalimu. CCM imeshindwa kufanya siasa za ushindani kwa hoja badala yake kutumia polisi kuteka na kuua wote wenye mitazami tofauti na watawala. CCM itaondoka madarakani kwa aibu kubwa.
 
Hakuna chama kipya kinakuja madarakani pamoja na ofisi zake za serikali, majeshi, polisi, mahakama, barabara, hospitali, mahakama na majaji wake wapya. Watatumia miundombinu hiihii na rasilimali watu iliyopo, maana miundombinu hii sio mali ya chama kilichoko madarakani wala Rais, ni mali ya watanzania hata wale ambao hawajazaliwa. Kuichoma moto na kuiharibu sio sawa na kosa kubwa sana.

Hakuna mahali popote nimesikia chama cha chadema kimekerwa na kuharibiwa kwa mali/kodi za watanzania katika vurugu za Octoba 29, 2025 na siku zilizofuata siku hiyo. Hii ni kuonyesha kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya wachomaji na chadema, la sivyo, walifurahishwa na uchomaji ule.

Hayati Reginald Mengi (RIP) alikuwa miongozi mwa watu wa kwanza nchini kumiliki vyombo vya habari. Kila wakati unapokaribia uchaguzi mkuu alikuwa akitumia vyombo vyake vya habari kutuonyesha watanzania ubaya wa kuvunjika kwa amani kunakoweza kuletwa na vurugu za uchaguzi na vyama vya upinzani. Nadhani alikuwa mwanaCCM lakini alifanyahivyo kwa kusukumwa na umuhimu wa amani na utulivu katika uwekezaji wake nchini. Kwenye vurugu mitaji inapotea.

Mzee Mengi alikuwa anatuonyesha vita na mauaji ya Rwanda, Burundi na Somalia kwenye kituo chake cha TV. Wapinzani walimlaumu sana kuwa anawatisha watanzania wasivichague vyama vya upinzani. Leo Mengi hayupo lakini nchi ilichomwa moto na watanzania wenzetu wamepoteza maisha wakati wa uchaguzi sawasawa na hofu na tahadhali yake.

Kuchoma au kuunga mkono kuchoma nchi/malalo yetu ni kosa la kiufundi ambalo chadema walilifanya katika harakati zao za kisiasa. Wamekirudisha chama kilometa nyingi sana nyuma. Leo hii chadema kinaogopwa na wananchi kama chama kisichowatakia mema wananchi na taifa. Mwananchi ambae amepoteza mtoto wake kwenye vurugu zile anawalaumu chadema, waliokosa matibabu wakati wa vurugu wanailaumu chadema, waliokosa usafiri wa mwendokasi kwakuwa umechomwa moto wanailaumu chadema, waliokosa ajira kwakuwa sheli na malori waliyokuwa wameajiliwa yamechomwa moto wanailaumu chadema; watoto waliokosa masomo kwa kule kufungwa kutokana na vurugu wanailamu chadema; walioshindwa kutoka nje kujitafutia riziki kwasababu ya vurugu wanailamu chadema, waliofilisika kwasababu maduka yao yaliporwa kwenye vurugu wanailaumu chadema na viongozi wao akina heche; wanaokosa huduma kwenye ofisi za serikali za mitaa na kata zilizochomwa wanailaumu chadema; chadema, chadema, chadema.

Matokeo yake ni nini, leo hii ni rahisi sana kuyazuia maandamano ya chedema kuliko wakati mwingine wowote. Wakiitisha maandamano wananchi wooote wenye akili timamu wanabaki majumbani mwao na biashara zote zinafungwa kupisha maandamano ya chadema. Barabara na mitaa inabaki tupu, na hata wanaojitafutia riziki zao kwa kutoka kila siku kama bodaboda, daladala, mama lishe na wauza mboga wanakubali kukaa ndani na njaa ili kunusuru roho zao dhidi ya chadema na polisi. Chadema Wakiendelea kufanya hivi kwa muda mrefu watanzania hawa waliozoea amani wataifuta chadema vichwani mwao na kuwalinganisha na magaidi au watia hasara au wapenda vurugu au wapenda vita.

chadema kitabakia kuwa chama cha watu na vijana wapenda vurugu/wabwia unga, wavuta bangi na wasiokuwa na chakupoteza. Hata kwenye vurugu zile ni watoto wasiokuwa na chakupoteza tu ndio waliathirika; hakukuwepo na watoto wa wanasiasa, wafanyabiashara, viongozi, maprofesa wala watumishi. Wengi wao walikuwa ni watoto wa masikini kabisa waliotolewa kafara na watu wanaowaamini na kuwaheshimu sana kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiroho. Watu ambao walikuwa wanajua kuwa vijana wale kwa kuchoma mali za umma na hata zile zinazolindwa kwa bunduki lazima wangeuliwa na kujeruhiwa kwa wingi. Hesabu zao zilikuwa wangeuliwa wachache tu na wengine watafanikisha lengo lao kwakuwa walijua kuwa polisi wengi walikuwa kwenye malindo ya kulinda uchaguzi. Bahati yao mbaya ni kwamba mikoa mingi na watanzania wengi hawakujitokeza kuunga mkono vurugu zao kama walivyokuwa wamekusudia. Hii ilisababisha Vijana waleta vurugu wakaminywa wote na kunyanyua mikono, bila hivyo serikali na watanzania wote tungekuwa tunashuhudia magofu kila kona. Yaani tungerudi nyuma miaka 50 kimaendeleo.

Chadema imetumika tu kama mtu wa mwisho/loud speaker nyuma ya wapanga mipango wakubwa wenye maslahi ya kibiashara nyuma ya pazia. Vurugu tunazoziona msingi wake mkuu sio demokrasia, bali biashara haramu ambazo zilivurugwa na utawala mpya wa Rais samia. Mpango ambao ulianza kwa kumnyang'anya Mbowe chadema ili kitumike kama jukwaa lao la kufanikisha kile wanachokidai/maslahi.

Samia amevuruga biashara zao haramu nyingi sana. Kulikuwa na mipango kabambe ambayo ilikuwa inafanyika wakati wa JPM, ambayo ghafla iliingia hitilafu baada Rais JPM kufa ghafla ambayo hawakuwa na uhakika kama Samia angeruhusu waendelee nayo kama ilivyo au Samia angehamia kwa watu wengine kama Rostam, nk.

Vita hii sio ya kidemokrasia hata kidogo, ni vita ya maslahi.

..kwa hiyo genge la Jpm ndilo linalosaidia Chadema?

..Na kinachoendelea ni vita kati ya genge la Ssh dhidi ya genge la Jpm?
 
Kaka unaandika kitu ambacho hakina uhalisia. Ni kweli CCM imekoma kuwa chama cha siasa au hujui siasa ni kitu gani?

CCM ina uhusiano wa moja kwa moja na ujenzi wa barabara unazopita kwenda kwenu, usambazaji wa umeme mpaka kijijini kwenu, ujenzi wa vivuko na madaraja, usambazaji wa maji, shule, zahanati, pembejeo, sera za biashara, umiliki wa ardhi ulinayonayo sasa, elimu bure, reli na mwendokasi. Chama kilichokoma kuwa chama cha siasa kisingewahudimia wananchi wake kiasi hiki. Kingeacha majambazi yawanyime watu uzingizi; yaani yangekubaka hata wewe mbele ya mkeo na wanao.

Hata hivyo, hakuna mtanzania mwenye akili timamu atashangilia kuona vyama vya upinzani vinadhoofika na kupotea nchini; mtu kama huyo hajui siasa na haitakiwi mema nchi hii. Vyama vya upinzani lazima viwepo tena vyenye nguvu ya muundo, watu, uongozi bora, hoja na sera safi bora pengine kuzidi chama tawala. Hii itasaidia vyama vinavyotawala kuwa macho muda wote na kero za wananchi, kutumia rasilimali za nchi vizuri kwa maendeleo ya watu na vitu. Hata Mwl. Nyerere alitulazimisha kukubali uwepo wa vyama vingi nchini kwasababu hiyo; kukikosoa na kukitia jambajamba chama tawala kisilale na kubweteka. Ndiyo maana Nyerere alivisihi vyama vya upinzani vianze kwa kuwa na wabunge wengi bungeni kunakopitishwa hoja za wananchi kuliko kukimbilia Ikulu bila kuwa na wabunge wengi kwanza.

Shida ya vyama vya upinzani ni kuwa vyenyewe havina demokrasia ndani ya vyama lakini vinadai demokrasia kutoka CCM; vinapinga kila kitu badala ya kukosoa na kuja na njia mbadala za uhakika na zinazowezekana za kuyaendea mambo ambayo CCM haifanyi vizuri.

Huwezi kulazimisha wananchi wabadilike, mabadiliko yanakuja yenyewe baada ya wananchi 75% kufikishwa mwisho wa kuvumilia jambo. Hali ikifikia hapo mabadiliko yanatokea kama jipu linalopasuka baada ya kuiva sana. Huwezi kuleta madiliko kama embe za kupepea na ndizi za kuvundika kwanza ili ziive. Wananchi wa sasa bado hawaelewi nini wapinzani wanataka, wateleta ambacho ni tofauti na CCM kinachowapa. Sasa Mmasai anatoka Arusha anakwenda kumiliki ardhi Kisarawe bila bughuza yoyote, Mchaga kapora ardhi nje ya Kilimanjaro bila shida yoyote, Mpemba yuko Mvomero analima bila shida, watanganyika wako Zanzibar wanafanya umachinga kule; hakuna shida ya kuwafanya ikibidi wafe ili wafanye mabadiliko.
 
Kitendo cha kutumia polisi kupambana na Chadema ni dhahiri CCM siyo chama cha siasa tena kwani kimekabidhi majukumu yake kwa jeshi la polisi. Bila mbeleko ya vyombo vya dola hasa polisi , kwenye uwanja sawa wa kisiasa CCM ni kama Chauma tu.
 
Hakuna chama kipya kinakuja madarakani pamoja na ofisi zake za serikali, majeshi, polisi, mahakama, barabara, hospitali, mahakama na majaji wake wapya. Watatumia miundombinu hiihii na rasilimali watu iliyopo, maana miundombinu hii sio mali ya chama kilichoko madarakani wala Rais, ni mali ya watanzania hata wale ambao hawajazaliwa. Kuichoma moto na kuiharibu sio sawa na kosa kubwa sana.

Hakuna mahali popote nimesikia chama cha chadema kimekerwa na kuharibiwa kwa mali/kodi za watanzania katika vurugu za Octoba 29, 2025 na siku zilizofuata siku hiyo. Hii ni kuonyesha kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya wachomaji na chadema, la sivyo, walifurahishwa na uchomaji ule.

Hayati Reginald Mengi (RIP) alikuwa miongozi mwa watu wa kwanza nchini kumiliki vyombo vya habari. Kila wakati unapokaribia uchaguzi mkuu alikuwa akitumia vyombo vyake vya habari kutuonyesha watanzania ubaya wa kuvunjika kwa amani kunakoweza kuletwa na vurugu za uchaguzi na vyama vya upinzani. Nadhani alikuwa mwanaCCM lakini alifanyahivyo kwa kusukumwa na umuhimu wa amani na utulivu katika uwekezaji wake nchini. Kwenye vurugu mitaji inapotea.

Mzee Mengi alikuwa anatuonyesha vita na mauaji ya Rwanda, Burundi na Somalia kwenye kituo chake cha TV. Wapinzani walimlaumu sana kuwa anawatisha watanzania wasivichague vyama vya upinzani. Leo Mengi hayupo lakini nchi ilichomwa moto na watanzania wenzetu wamepoteza maisha wakati wa uchaguzi sawasawa na hofu na tahadhali yake.

Kuchoma au kuunga mkono kuchoma nchi/malalo yetu ni kosa la kiufundi ambalo chadema walilifanya katika harakati zao za kisiasa. Wamekirudisha chama kilometa nyingi sana nyuma. Leo hii chadema kinaogopwa na wananchi kama chama kisichowatakia mema wananchi na taifa. Mwananchi ambae amepoteza mtoto wake kwenye vurugu zile anawalaumu chadema, waliokosa matibabu wakati wa vurugu wanailaumu chadema, waliokosa usafiri wa mwendokasi kwakuwa umechomwa moto wanailaumu chadema, waliokosa ajira kwakuwa sheli na malori waliyokuwa wameajiliwa yamechomwa moto wanailaumu chadema; watoto waliokosa masomo kwa kule kufungwa kutokana na vurugu wanailamu chadema; walioshindwa kutoka nje kujitafutia riziki kwasababu ya vurugu wanailamu chadema, waliofilisika kwasababu maduka yao yaliporwa kwenye vurugu wanailaumu chadema na viongozi wao akina heche; wanaokosa huduma kwenye ofisi za serikali za mitaa na kata zilizochomwa wanailaumu chadema; chadema, chadema, chadema.

Matokeo yake ni nini, leo hii ni rahisi sana kuyazuia maandamano ya chedema kuliko wakati mwingine wowote. Wakiitisha maandamano wananchi wooote wenye akili timamu wanabaki majumbani mwao na biashara zote zinafungwa kupisha maandamano ya chadema. Barabara na mitaa inabaki tupu, na hata wanaojitafutia riziki zao kwa kutoka kila siku kama bodaboda, daladala, mama lishe na wauza mboga wanakubali kukaa ndani na njaa ili kunusuru roho zao dhidi ya chadema na polisi. Chadema Wakiendelea kufanya hivi kwa muda mrefu watanzania hawa waliozoea amani wataifuta chadema vichwani mwao na kuwalinganisha na magaidi au watia hasara au wapenda vurugu au wapenda vita.

chadema kitabakia kuwa chama cha watu na vijana wapenda vurugu/wabwia unga, wavuta bangi na wasiokuwa na chakupoteza. Hata kwenye vurugu zile ni watoto wasiokuwa na chakupoteza tu ndio waliathirika; hakukuwepo na watoto wa wanasiasa, wafanyabiashara, viongozi, maprofesa wala watumishi. Wengi wao walikuwa ni watoto wa masikini kabisa waliotolewa kafara na watu wanaowaamini na kuwaheshimu sana kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiroho. Watu ambao walikuwa wanajua kuwa vijana wale kwa kuchoma mali za umma na hata zile zinazolindwa kwa bunduki lazima wangeuliwa na kujeruhiwa kwa wingi. Hesabu zao zilikuwa wangeuliwa wachache tu na wengine watafanikisha lengo lao kwakuwa walijua kuwa polisi wengi walikuwa kwenye malindo ya kulinda uchaguzi. Bahati yao mbaya ni kwamba mikoa mingi na watanzania wengi hawakujitokeza kuunga mkono vurugu zao kama walivyokuwa wamekusudia. Hii ilisababisha Vijana waleta vurugu wakaminywa wote na kunyanyua mikono, bila hivyo serikali na watanzania wote tungekuwa tunashuhudia magofu kila kona. Yaani tungerudi nyuma miaka 50 kimaendeleo.

Chadema imetumika tu kama mtu wa mwisho/loud speaker nyuma ya wapanga mipango wakubwa wenye maslahi ya kibiashara nyuma ya pazia. Vurugu tunazoziona msingi wake mkuu sio demokrasia, bali biashara haramu ambazo zilivurugwa na utawala mpya wa Rais samia. Mpango ambao ulianza kwa kumnyang'anya Mbowe chadema ili kitumike kama jukwaa lao la kufanikisha kile wanachokidai/maslahi.

Samia amevuruga biashara zao haramu nyingi sana. Kulikuwa na mipango kabambe ambayo ilikuwa inafanyika wakati wa JPM, ambayo ghafla iliingia hitilafu baada Rais JPM kufa ghafla ambayo hawakuwa na uhakika kama Samia angeruhusu waendelee nayo kama ilivyo au Samia angehamia kwa watu wengine kama Rostam, nk.

Vita hii sio ya kidemokrasia hata kidogo, ni vita ya maslahi.
Uchawa unawadhalilisha sana hata watu tuliodhani ni great thinkers wa humu!

Ni nani aliyekwambia maandamano na vurugu za 29 Oct ziliandaliwa na Cdm?

Au ndiyo haya ya kusema:'ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya'?

Tuwekee ushahidi wenye vigezo vya kuibeba hoja yako hii, vinginevyo utakuwa ni uzushi kama ulivyo uzushi mwingine na upuuzwe.
 
..kwa hiyo genge la Jpm ndilo linalosaidia Chadema?

..Na kinachoendelea ni vita kati ya genge la Ssh dhidi ya genge la Jpm?
Exactly!!! kwasababu tunaangalia tulipojikwaa sio tulipoangukia. Wakati SSH ni Makamu wa Rais hakuna mtu alimpinga na kusema hapana; ujio wake kwenye kiti cha uMakumu ulikuwa na baraka zote za JPM na ulifuata misingi ya Kikatiba. Shida ilikuja mara tu JPM kufariki na nani azibe nafasi yake Kikatiba. Hapo ndipo yakajitokeza makundi ya wanasiasa ndani ya CCM, makundi ya dini ya Kikristu, hasa Wakatoliki na Kanisa la Ufufuo ambalo mkuu wake ni msukuma kama JPM na chadema wakaiona na kutaka kuitumia fursa kwenye mnyukano huo wa wanaCCM wafuasi wa JPM, makanisa, wanaCCM wafuasi wa SSH, wadau walioapa kuilinda Katiba ya nchi na chadema ambao wanatumika tu kama farasi wa vita. Ndio maana Mh. Lissu kanasa kwenye mtego ambao sio wake kindakindaki, na waliomfanya anase kwenye mtego wanahangaika sana huku na huko ndani na nje kutafuta njia za kumnasua baba wa watu waliomwingiza mkenge.

Sisi wenye akili timamu tunajua shida ya SSH haitokani na kutuongoza vibaya kama Rais, bali shida nyingine tu za maslahi ya kifisadi, ulaji na kupoteza fursa mbalimbali ambazo walikuwa wakizipata chini ya JPM ama kama Rais, kama rafiki, kama mkristo, kama Mkatoliki, kama msukuma au kama Rais mtanganyika. Hatudanganyiki ng'oo.
 
Uchawa unawadhalilisha sana hata watu tuliodhani ni great thinkers wa humu!

Ni nani aliyekwambia maandamano na vurugu za 29 Oct ziliandaliwa na Cdm?

Au ndiyo haya ya kusema:'ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya'?

Tuwekee ushahidi wenye vigezo vya kuibeba hoja yako hii, vinginevyo utakuwa ni uzushi kama ulivyo uzushi mwingine na upuuzwe.
unaongea kile mahakamani wanachokiita kunyima mtu haki kwasababu tu za kiufundi za kisheria. Yaani unatenda kosa lakini umeacha mwenyewe au unatafuta au kutafutiwa tundu la kutokea ili kulikwepa kosa. Nchi imechomwa, wananchi wameingizwa hasara ya kupoteza mali na uhai; na wapo watu walisema watavuruga uchaguzi kwa kukinukisha vibaya sana. Kwavyovyote vile lazima yupo aliyechoma, aliyepanga na aliyegharamia; woote manzenyange, tunawatafuta wote.
 
Sasa waliotawala nchi wamechukua hatua stahiki za kulinda miundombinu yake, na tumeiona faida yake juzi 77 hakuna kima alojaribu kutoa pua yake
Miundombinu haiwezi kulindwa kwa mtutu nyie mlikua mnalinda madaraka mliyopata kwa
Kupora
 
Back
Top Bottom